CCM yawataka wananchi ‘kuwalipua’ wavunjifu wa amani
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya CCM, Jakaya Kikwete akipiga makofi wakati alipowasili katika mkutano wa chama hicho hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mjumbe wa Halmsahuri ya Taifa ya CCM Ndugu January Makaba imebainisha kuwa chama hicho kinafuatilia kwa karibu zoezi zima la uchaguzi nchini kote.
Tarifa hiyo imeongeza kuwa Mwana-CCM yoyote anayeshuhudia au kusikia mipango ya kuvunja amani na kuhujumu au kuvuruga zoezi la uchaguzi atume ujumbe mfupi kwenda nambari 15016, akielezea mahali alipo, tukio husika na ikiwezekana wahusika. Ujumbe huu ni bure. CCM itazishughulikia taarifa hizo na kuzipeleka kwa mamlaka husika.
Chama hicho pia kimesisitiza uchaguzi wa amani huku hadi sasa, katika sehemu kubwa ya nchi dalili zote zinaonyesha kwamba upigaji kura umekuwa wa utulivu. Katika hatua nyingine chama hicho kimewataka viongozi wote wa CCM kuwa macho dhidi ya hujuma kwa CCM katika vituo mbalimbali vya uchaguzi nchini kulekea kuhesabu kura na kutangaza matokeo.