Wednesday, 31 August 2016

Viongozi Chadema Kuripoti Polisi Septemba Mosi.

Tarehe August 31, 2016
lowassa_mboweV 1

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho, Edward Lowassa na viongozi wengine waandamizi wameitwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuripoti kesho Septemba Mosi.

Hatua hiyo inatokana na viongozi hao kukamatwa juzi, baada ya kufanya kikao cha ndani cha Kamati Kuu, katika Hoteli ya Giraffe, Jijini Dar es Salaam na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati ambapo walihojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Mbali na Mbowe na Lowassa, viongozi wengine wa Chadema waliokamatwa na kutakiwa kwenda Polisi kesho ni Katibu Mkuu, Vincent Mashinji, Naibu wake, John Mnyika na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Said Issa Mohammed.

Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene amesema ni kweli wametakiwa kwenda polisi Septemba Mosi kuripoti baada ya kukamatwa na kuhojiwa wakituhumiwa kukiuka maagizo ya polisi.

“Maandamano yatakuwepo kama yalivyopangwa hapo awali kwani maandalizi yote yamekwishakamilika lakini viongozi hao wanaweza kwenda polisi kwanza au wakaanzia kwenye maandamano kisha wakaenda Polisi kuripoti,” amesema Makene.

Kigogo CHADEMA Ajivua Uanachama, Achoshwa Na Siasa Za Uchochezi.

Tarehe August 31, 2016
Aliyekuwa Katibu wa Chadema, Mkoa wa Mwanza, John NzwalileV 1
Aliyekuwa Katibu wa Chadema, Mkoa wa Mwanza, John Nzwalile

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo baada ya Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza, John Nzwalile kujivua nyadhifa zake tatu alizokuwa akizishikilia ikiwa ni pamoja na uanachama kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa na ubabaishaji.

Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu CHADEMA, amesema chama hicho kimekuwa kikiwachonganisha wananchi na Serikali yao jambo ambalo halikubaliki.

“Nimefikia uamuzi huu mgumu wa kujivua nyadhifa zangu zote na uanachama wa Chadema baada ya kuchoshwa na siasa za uchochezi, majungu na uchonganishi zinazofanywa na chama hiki kikubwa cha upinzani nchini,” amekaririwa akisema Nzwalile.

Ameongeza kuwa amechoshwa na siasa hizo baada ya kuona kila mara viongozi wa Chadema wakijifungia ndani kwenye vikao vyake ni kuhusu maandamano na uchochezi tu, “kwanini tusifanye shughuli za maendeleo badala ya kuhamasisha vurugu na uvunjifu wa amani,” amehoji.

Kada huyo anajivua uanachama ikiwa imebaki siku moja tu kuanza kwa ‘operesheni’ Ukuta iliyoandaliwa na Chadema. 

Tuesday, 30 August 2016

Majaliwa Alia Na Wafanyabiashara Ulipaji Wa Kodi

Tarehe August 31, 2016
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohamed Dewji, ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.V 1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohamed Dewji, ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi wanaiathiri Serikali katika juhudi zake za kuboresha maisha ya Watanzania.

Amesema Serikali haina mgogoro na wafanyabiashara bali inawataka walipe kodi na kama kuna wanaonewa na watendaji wa chini kwa kubambikiziwa kodi watoe taarifa juu ya jambo hilo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), Mohamed Dewji, ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali imedhamiria kuwaunga mkono wafanyabiashara katika shughuli zao ili waweze kulipa kodi itakayoifanya imudu kuwahudumia wananchi katika huduma mbalimbali za jamii.

 “Sisi msisitizo wetu ni ulipaji kodi, wakwepa kodi wanatuathiri. Sekta nyingine zinashindwa kuendelea kwa sababu hazina mtaji na kodi hazipatikani vizuri,” amesema.

“Ninyi timizeni wajibu wenu kwa kulipa kodi stahiki, tutawasaidia katika kufanya biashara zenu. Tutawasaidia katika kusimamia mambo yenu ila mjue kwamba nchi hii bila viwanda hatuwezi kwenda,” amesema.

Pia amewataka wafanyabiashara kwenda kujenga viwanda katika maeneo ambayo malighafi zinazalishwa ili kuwahamasisha wakulima kuzalisha zaidi na kuwapunguzia mzigo wa kusafirisha malighali hizo.

Kwa upande wake Dewji amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wafanyabiashara wanaiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano na hawana mpango wowote wa kuhamishia mitaji yao nje ya nchi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

“Huu ni uongo na uzushi tu ambao watu wameamua kuusambaza, mfano mimi mwenyewe nimeanza kuongeza mitaji katika biashara zangu. Nimefufua kiwanda cha kuchambua pamba cha Chato. Nafungua biashara zingine mpya kubwa ikiwemo ya kufufua kiwanda cha nguo cha Musoma ambacho kitakuwa kinatengeneza jeans za kuuza nje ya nchi,” amesema.

Amesema yuko tayari kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda cha sukari katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kununua miwa tani milioni 1.2 zitakazozalisha tani 120,000 za sukari kwa mwaka.

Mkurugenzi huyo amesema amepanga kuwekeza shilingi bilioni 40 kwa ajili ya kukuza uzalishaji katika mashamba yake ya mkonge kwenye mikoa ya Pwani, Tanga na Morogoro.

Pia amewekeza shilingi bilioni 70 katika viwanda vya kusaga unga wa ngano na sembe na anatarajia kununua tani laki moja za mahindi katika msimu wa mwaka huu. 

JWTZ Kufanya Usafi Wa Mazingira Jijini Dar Es Salaam

Tarehe August 30, 2016
KanaliNgemelaV 1
Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga

Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), limesema kuwa litashirikiana na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam Septemba mosi mwaka huu.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia maandalizi ya shughuli ambazo jeshi hilo litazifanya siku hiyo ambapo Jeshi hilo litakuwa linafikia kilele cha maadhimisho ya miaka 52 tangu kuanzishwa kwake.

Kanali Lubinga anasema pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali shughuli nyingine zitakazofanywa na wanajeshi hao ni za kijamii ikiwemo kushiriki katika zoezi la uchangiaji damu kwenye vituo mbalimbali pamoja na kufanya mazoezi ya ndege za kijeshi. 

Monday, 29 August 2016

Mbwana Samatta Afunika Ligi Za Ulaya

Tarehe August 29, 2016
mbwana-samatta_2nx5mzohoms410k2eiy1i42znV 1
Nahodha wa Taifa stars na Straika wa Ubelgiji,Mbwana Samatta,ameonekana kuuanza msimuu huu kwa nguvu na kasi kwa kuonekana kufunika baadhi ya mastaa katika ligi za Ulaya .
Mchezaji huyo Samatta aliyekuwa amejiunga na dirisha dogo msimu uliopita akitokea katika timu ya TP Mazembe ya Congo , kabla ya mechi iliyo chezwa jana Jumaapili alikuwa akionekana kuwafunika wachezaji wenzake akiwemo Wayne Rooney pamoja na Ibrahimovic wakiwa wote ni wachezaji wa Manchester United.
Pia Samatta anaongoza kwa mabao yapatayo manne ,hali ya kuwa Ibrahimovic akiwa na jumla ya mabao yapatayo matatu huku Mchezaji Rooney kuonekana akiwa hana ata bao moja .
Licha ya Mbwana Samatta kuonekana kuwa kidedea kati ya wachezaji hao ,ameonekana kupigwa bao na mchezaji anaye waniwa na kocha wa Arsenal,Arsene Wenger,Alexandre Lacazette anayekipiga Olympique Lyon ya Ufaransa mwenye mabao sita.
Huu ni mwanzo mzuri wa mchezaji Samatta kwani kuonekana kwake kuwa bigwa dhidi ya wachezaji wakogwe ni moja ya hatua kwa upande wake .
Pia Mbwana Samatta ameonekana akifunga mabao yake kwa kiwango cha juu tofauti na wachezaji wengine wa Tanzania kwani yeye huonekana akitumia ufundi wake kama Mastraika wakubwa.

PICHA: Lema Alazwa Baada Ya Kutokula Kwa Saa 48

Tarehe August 29,2016
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa hospitali alikolazwa baada ya mwili kudhoofu kutokana na kutokula kwa saa 48.V 1
 Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akiwa hospitali alikolazwa baada ya mwili kudhoofu kutokana na kutokula kwa saa 48.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amelazwa katika hospitali mojawapo Jijini humo kufuatia mwili wake kudhoofu baada ya kugoma kula kwa saa 48 tangu alipokamatwa juzi na Jeshi la Polisi.

Mbunge huyo anatarajiwa kupandishwa mahakamani leo kujibu tuhuma za kufanya uchochezi kwa njia ya mtandao.

UDOM Kuziazima Wizara 4 Majengo Yake

Tarehe August 29, 2016
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).V 1
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Idris Kikula akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

Hatimaye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimekubali kutoa majengo yake kutumiwa na wizara nne kama ofisi za muda wakati wakiendelea na ujenzi wa ofisi za kudumu Mkoani humo.

Hivi karibuni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alikaririwa akisema kuwa suala hilo lisingewezekana kwani utaratibu huo ungeingiliana na taraibu za wanafunzi na kuvuruga hadhi ya elimu chuoni hapo.

Profesa Kikula amezitaja wizara hizo kuwa ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya majadiliano marefu na kukubaliana kuwa majengo mapya ambayo yalijengwa kwa ajili ya ofisi lakini kwa sasa hayatumiki ndio yatakayotumiwa na wizara hizo.

“Sasa wanaweza kutumia majengo hayo yaliyo mbali kidogo kwa muda wakati wakijenga ya kwao ya kudumu na hili halitaleta athari kwa wanafunzi kama ukosekanaji wa utulivu kwa wanafunzi kwakuwa yapo mbali kidogo,” amesema.

Ameongeza kuwa katika kufikia maamuzi hayo, wamezingatia pia umuhimu wa taasisi za Serikali kuunga mkono agizo la Rais Magufuli la kuhamia Mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuzingatia uwezekano wa majengo hayo kuharibika kutokana na kutotumiwa kwa muda mrefu kwa ajili ya shughuli za chuo.

Ameyataja majengo hayo kuwa ni pamoja na Kituo cha Utafiti cha Asha­Rose Migiro, na yale yaliyopo katika Chuo cha Sayansi ya Jamii (College of Humanities and Social Sciences).

Tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza kuhamia Mkoani Dodoma ifikapo Septemba 1, mwaka huu ambapo alishaunda kikosi kazi kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ambacho kimebaini kuwa asilimia 70 tu ya majengo ya ofisi yataweza kupatikana huku asilimia 75 tu ya nyumba za kuishi watumishi ndizo zitakazopatikana.

Waumini Waingia Na Mabango Kanisani Kumpinga Askofu

Tarehe August 29, 2016
DSCN0546V 1

Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kusini Mashariki, Kanisa Kuu la Mtwara wameingia katiba ibada na mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali za kumpinga Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Lucas Mbedule kwa tuhuma za kukiuka Katiba, Unyanyasaji wa watumishi na ubadhirifu wa fedha za Ushirika wa Dayosisi hiyo.

Pamoja na mabago hayo, Umoja wa Wazee katika Kanisa hilo ulitoa tamko ndani ya kanisa hilo kutokana na tuhuma zinazomkabili askofu huyo huku wakimtaka asijihusishe na mambo yanayohusu usharika wa dayosisi hiyo ili kuweza kupisha uchunguzi.

Wazee hao wamemuomba Askofu Mkuu wa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo aunde tume itakayoweza kuchunguza tuhuma hizo.

Akisoma tamko la Wazee hao ndani ya Kanisa, Amon Mkocha amesema kuwa wanapinga uamuzi uliofanywa na kikao cha halmashauri kuu huku akidai ukiukwaji wa katiba uliofanyika ni pamoja na kumsimamisha msaidizi wa Askofu, Yeriko Ngwema na kumpangia kuwa mchungaji wa Ushirika wa Kilwa Masoko ambako hakuna jengo la kuabudia huku akitakiwa kukabidhi ofisi maramoja.

“Kwa kuwa mojawapo ya wajibu wa Mzee wa Kanisa kama ilivyotajwa katika Kanuni ya Katiba, Dayosisi ya Kusini Mashariki, inatutaka kuhakikisha kanuni, sheria na miongozo ya dayosisi inafuatwa na Wakristo na ndiyo maana tumelazimika kupinga uamuzi huo,” amesema.

Wazee hao pia wamedai kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu za ajira kwa watumishi wa kanisa hil kutopewa taarifa zinazohusu maslahi yao kama zinavyotajwa kwenye sheria ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa mishahara.

Naye Mtuhumiwa, Askofu Mbedule alipotafutwa kwa njia ya simu alidai kuwa asingependa kuyazungumzia kwa sababu walikaa kikao.

“Kimsingi tulikaa katika kikao, kwa hiyo nisingependa kulisemea sana. Nilifuata taratibu za kikao,” amesema.

Monday, 15 August 2016

Olimpiki : Bolt Aibuka Na Dhahabu Mita 100 Huko Rio.

Tarehe August 15, 2016
Usain Bolt akiwa kaziniV 1
Usain Bolt akiwa kazini.

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda nishani ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio za mita mia moja, kwenye michezo ya olimpiki ya Rio 2016.

Bolt, 29, amechukua muda wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika michezo ya olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya olimpiki mjini Beijing 2008, na London 2012.

Gatlin, ambaye amepigwa marufuku mara mbili kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli, alimaliza sekunde 0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.

“Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda,” Bolt ameiambia BBC.

Mwanariadha wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake.

Bolt anatazamia kuondoka Rio na nishani zaidi za dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi ilivyokuwa katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.

Mwanariadha huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa dunia mwaka 2017.

Sababu Ya Mgosi Kustaafu Mapema Hii Hapa.

Tarehe August 15, 2016
Mussa Hasan Mgosi akiwa na mwanae mara baada ya kuwaaga rasmi mashabiki wa Simba FcV 1
Mussa Hasan Mgosi akiwa na mwanae mara baada ya kuwaaga rasmi mashabiki wa Simba Fc.

Nahodha wa Simba, Mussa Hassan Mgosi aliyetangaza kustaafu amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya astaafu mapema ni kutokupenda hadi mashabiki wa mzomee uwanjani.

Amesema aliamua kustaafu akiwa anaheshimika, anahitajika na ndiyo maana amefurahi kuondoka katika kipindi hiki.

“Nimeondoka katika kipindi ninahitajika, ninafurahi kwa kuwa bado nitaendelea kubaki ndani ya kikosi cha Simba na kutoa msaada wangu,” alisema.

“Bora kuondoka mapema wakati unahitajika kuliko kusubiri kipindi cha malumbano, au mashabikikuanza kulalamikia.

“Niwashukuru sana Wanasimba wote kwa ushirikiano wao, naomba waiunge mkono timu yao katika kipindi kigumu au kile cha furaha,” alisisitiza.

Mgosi sasa anachukua nafasi ya Meneja wa kikosi cha Simba na ataendelea kushirikiana na wachezaji.

Mgosi alipata nafasi ya kuichezea timu hiyo mara ya mwisho katika kikosi hicho.

Taarifa Ya Dkt.Shein, Mazishi Ya Rais Mstaafu Wa Z’bar.

Tarehe August 15, 2016
Aliyekuwa Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, Mheshimiwa Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.V 1
Aliyekuwa Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, Mheshimiwa Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, Mheshimiwa Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi.

Katika taarifa hiyo aliyoitoa jana kupitia vyombo vya habari, Alhaj Dk. Shein kwa masikitiko makubwa aliwaarifu wananchi kuwa jana tarehe 14 Agosti 2016, Mzee Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia, msiba ambao umetokea nyumbani kwake Mji Mwema, Dar es Salaam.

Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa Marehemu Mzee Aboud Jumbe ni Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Pili, ambaye vile vile alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Marehemu Mzee Aboud Jumbe amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na umri wake.

Kwa mujibu wa kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ya Zanzibar imebainisha kuwa maziko ya marehemu yatafanyika leo tarehe 15 Agosti 2016 saa 7.00 mchana ambapo maiti yake itasaliwa katika Masjid Mshawar, Mwembeshauri na kuzikwa nyumbani kwake Migombani.

Aidha, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa kufuatia mchango na juhudi kubwa ambazo Marehemu Mheshimiwa Aboud Jumbe Mwinyi alizichukua katika uhai wake kwa kuitumikia, kuiongoza na kuijenga Zanzibar pamoja na nafasi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nchi yetu imekabiliwa na msiba mkubwa kwa kifo cha kiongozi huyu mahiri”alieleza Alhaj Dk. Shein katika taarifa hiyo.

Kutokana na msiba huo mkubwa Alhaj Dk. Shein alitangaza rasmi siku saba za maombolezo, kuanzia leo tarehe 15 Agosti 2016 ambapo katika kipindi hicho chote bendera zote zitapepea nusu mlingoti.

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein alieleza kuwa utaratibu wa maziko utafuata wasia ambao mwenyewe marehemu aliutoa wakati wa uhai wake.

“Tunaungana na Wanafamilia wote katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Naomba kutumia nafasi hii kutoa mkono wa pole kwa wafiwa wote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie kauli thabit marehemu mzee wetu na amlaze pahala pema peponi, Amin. Inalillahi wainnailaihi rajiun”Alieleza Alhaj Dk. Shein katika Taarifa hiyo.

Saturday, 13 August 2016

Bonge La U-Turn, Messi Arejea Timu Ya Taifa.

Tarehe August 13, 2016
Lionel Messi.
Lionel Messi.

Nguli wa Soka na Mshindi wa mara 5 wa FIFA Ballon d’ Or, Lionel Messi amepiga bonge la U­turn na kutangaza rasmi kurejea katika timu ya Taifa ya Argentina ikiwa ni miezi michache tu imepita tangu atangaze kustaafu kuicheza timu hiyo baada ya kuvunjika moyo kufuatia kushindwa katika fainali ya Copa America, 2016.

Akiwa tayari amekwishaongea na Kocha mpya wa timu ya Argentina, The Albiceleste Boss, Edgardo Bauza, Messi amefanya uamuzi wa kuiwakilisha nchi yake tena.

“Tayari naona kuna matatizo kibao katika mpira wa Argentina na hivyo basi nisingependa kutengeneza tatizo lingine tena,”amesema Messi katika taarifa maalum aliyoitoa siku ya Ijumaa. 

 Amesema kuwa hataki kusababisha tatizo lolote kwani siku zote amekuwa akifanya kinyume na hilo na kuisaidia timu pale anapoweza.

“Tunatakiwa kurekebisha mambo mengi sana katika mpira wa Argentina lakini ningependa kufanya hivyo nikiwa ndani na sio kupinga nikitokea nje,” amezidi kufunguka Messi.

Nahodha huyo ameweka wazi kuwa ni mapenzi yake kwa Argentina ndio yaliyomshawishi kurudi katika timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia lijalo.

“Mambo mengi sana yalikuwa ndani ya kichwa changu siku ya fainali ya mwisho na kiukweli kabisa nilifikiria kuachana na timu ya Taifa, lakini nalipenda Taifa hili na Jezi ya Argentina,” amesema Mkali huyo anayekiwasha katika klabu ya Barcelona.

JPM Aahidi Kurudisha CCM Ya Mwl. Nyerere.

Tarehe August 13, 2016
Mwenyekiti wa kwanza wa CCM na Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Mwenyekiti wa kwanza wa CCM na Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais, Dkt. John Magufuli amesema anataka kuona CCM mpya na kuahidi kukirudisha chama katika maadili kama kilivyoachwa na Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amaan Karume.

Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi waliojitokeza kumshuhudia wakati akiingia katika Ofisi Ndogo za CCM Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo wa Uenyekiti Julai 23, mwaka huu, Mjini Dodoma.

Amewataka wanachama wa chama hicho kumvumilia wakati atakapokuwa akifanya kazi ya kukirudisha kwenye maadili, kwani katika kuifanya kazi hiyo mahali atakapoamua kunyoosha, atanyooshea hapo hapo hata kama kuna kigogo ataondoka.

“CCM tumepanga tuanze kujisahihisha, kwa sababu ni chama ninachokipenda nimekulia humu, kilikuwa kimeanza kupoteza dira na hili lazima niliseme wazi bila unafiki,” alikiri Rais Magufuli.

Mrema Awaonya Tena Chadema, Maandamano Ya UKUTA

Tarehe August 13, 2016
Mwenyekiti wa chama cha TLP Auguustino Mrema.V 1

Mwenyekiti wa chama cha TLP Auguustino Mrema. Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Mrema amewaonya Viongozi pamoja na wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuachana na maandamano ya Ukuta ifikapo septemba 1,mwaka huu.

Akizungumza kwenye mahojiano na moja ya kituo cha redio hapa nchini Mrema alisema wapinzani wanatakiwa kufanya siasa kama anayoifanya yeye ya kuwa mpinzani mstaarabu ambaye anaunga mkono kazi zinazofanywa na Rais Magufuli. “Mimi ni mpinzani mstaarabu, upinzani wa kijinga siutaki kama wewe ni mpinzani wa kweli inatakiwa ukae bungeni ili kutoa matatizo ya watanzania lakini sasa wao wanatoka, niwashauri tu wakae wafanye kazi,” alisema Mrema.

Mrema amewataka wanachama wa Chadema na Ukawa kuacha maandamano hayo na badala yake waende shambani kulima au kusaidia kutatua tatizo la madawati kama wamekosa kazi ya kufanya.

Chama cha Chadema hivi karibuni kimetangaza tarehe 1septemba kuwa ni siku ya kufanya mikutano kisiasa hapa nchini kwa madai ya kuchoshwa na utawala wa awamu ya tano uliopiga marufuku mikutano ya kisiasa ya upinzani.

Friday, 12 August 2016

Sikia Kauli Ya Kifukwe Kuhusu Manji,Pia Jua Kinachosubiriwa Sasa.

Tarehe August 12, 2016
Yusuf Manji akifungua mkutano pamoja na kuwasilisha ajenda za mkutanoV 1
Yusuf Manji akifungua mkutano pamoja na kuwasilisha ajenda za mkutano .

Wazo la mfanyabiashara Yusuf Manji kutaka kukodishiwa klabu ya Yanga kwa miaka kumi limeendelea kushika vichwa vya habari katika magazeti na baadhi ya wadau wa michezo.

Moja ya watu waliongelea suala hilo ni Mjumbe wa baraza la wadhamini wa timu hiyo Francis Mponjoli Kifukwe ambaye amesisitiza kusubiri ombi hilo la Manji katika maandishi.

“Japo wanachama wamekubali 100% lakini tunasubiri mapendekezo yake rasmi katika maandishi, ili sisi (Baraza la Wadhamini) tuanze kuyafanyia kazi,tuone klabu klabu yetu itanufaika vipi katika muda huo wa miaka 10 chini yake”alisema Francis Mponjoli Kifukwe .

Shibuda Aifananisha UKAWA Na Mlenda, Amfagilia JPM.

Tarehe August 12, 2016
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda. V 1
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA­Tadea, John Shibuda.

 Katibu Mkuu wa Chama cha ADA­Tadea, John Shibuda amejitokeza katika mkutano wa Rais, Dkt. John Magufuli katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo anatatua kero za wananchi.

Akiwa mmoja wa maelfu ya wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani waliojitokeza kumsikiliza Rais Magufuli akihutubia katika viwanja vya Furahisha, amevitaka vyama vingine vya siasa nchini kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuwa kazi anayoifanya ni kwa ajili ya watanzania wote.

“Mheshimiwa Rais Magufuli endelea kuwahudumia watanzania na nikuambie sijawahi kuona mchongoma unang’olewa kwa upepo au sijawahi kuona utelezi wa mlenda unamwangusha mtu mzima,” amesema.

Shibuda ametoa rai kwa vyama vya siasa vinavyounda UKAWA kuwa vinapaswa kutambua kwamba Rais Dkt. Magufuli ni mtu mzuri ndiyo maana aliwasaidia kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam hivyo watambue mchango wake kwa Taifa .

Thursday, 11 August 2016

Bodi Ya Mikopo Yapata Bosi Mpya.

Tarehe August 12, 2016 
imagesV 1

Serikali imemteua Abdul­Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).

Badru anachukua nafasi iliyoachwa wazi na George Nyatage aliyefurumushwa kazi pamoja na vigogo wengine watatu ikiwa ni miezi sita tu tangu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako awatumbue vigogo hao kwa ufisadi katika bodi hiyo na kusababisha upotevu wa mamilioni ya fedha.

Uteuzi wa Bosi huyo mpya ulioanza tangu Julai 20, mwaka huu umetangazwa leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya HESLB, Prof. Anselm Lwoga na kudai kuwa kiongozi huyo mpya ameteuliwa kwa mujibu wa vifungu namba 10 (1) na 11 (1) na (2) vya Sheria ya HESLB namba 9 ya mwaka 2014.

Kifungu hicho kinampa mamlaka Prof. Ndalichako kumteua Mkurugenzi Mtendaji aliyependekezwa na Kamati Maalum ya Bodi ya Wakurugenzi.

Kabla ya uteuzi huo, Badru alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Ifakara.

Maalim Seif Awekwa Mtu Kati Kuhusiana Na Tuhuma Za Ufisadi

Tarehe August 11, 2016
Maalim Seif Sharif HamadV 1

Mamlaka ya Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA), imemhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufuatia kuhusishwa kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na tuhuma za ufisadi.

Afisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma cha ZAECA, Abubakari Mohamed Lunda, amesema kuwa Maalim Seif alihojiwa na Mkurugenzi wa ZAEC, Mussa Haji Ali, ili athibitishe tuhuma hizo nzito zilizotolewa dhidi ya watendaji na viongozi na kupelekea mamlaka hiyo kuamua kuchunguza ukweli wake kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake.

Amesema kazi kubwa ya mamlaka hiyo ni kuchunguza jambo lolote ambalo linahusu maslahi ya Zanzibar katika kupambana na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi na nia ya kumhoji Maalim Seif ilikuwa kupata ukweli wa tuhuma alizotoa dhidi ya viongozi na watendaji aliowatuhumu kwa kumiliki fedha chafu na mali nje ya nchi.

“Tayari mamlaka imemhoji Maalim Seif ili kutafuta ukweli juu ya tuhuma alizotoa za kuwapo viongozi wanaomiliki fedha chafu na mali nje ya nchi,” ameongeza.

Hata hivyo, Lunda amesema mpaka sasa hafahamu mkurugenzi amegundua kitu gani baada ya kufanyika kwa mahojiano hayo huku akisisitiza kuwa ZAECA imetimiza wajibu wake wa kupokea na kuchunguza taarifa mbalimbali wanazopata kupitia wanasiasa, vyombo vya habari na wananchi ambapo tayari kuna majalada 20 yamekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Ibrahim Mzee kwa ajili ya hatua za kisheria kuchukuliwa.

Amesema majalada hayo yanahusisha kesi mbalimbali zikiwamo za rushwa ya uchaguzi zilizotokea wakati wa kura ya maoni ya kuwapata wagombea wa ubunge na uwakilishi kupitia CCM mwaka jana.

Naye Maalim Seif, ambaye ni alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar alituhumu baadhi ya viongozi na watendaji wa visiwani humo kumiliki fedha chafu na mali nje ya nchi.

Amesema fedha hizo zilipatikana kwa njia za ufisadi na kutaka jumuiya ya kimataifa kufuatilia akaunti za vigogo hao na watendaji nje ya nchi kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake na kuongeza kuwa haihitajiki tochi kuwamulika viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi na kutaka mamlaka za dola kufanya uchunguzi dhidi ya vigogo hao na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Stendi Kuu Ya Mabasi Kuhamia Mbezi Mwisho, Kufanywa Ya Kimataifa

Tarehe August 11, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.V 1

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa Serikali ipo katika mpango wa mwisho wa kuihamishia stendi kuu ya mabasi kutoka Ubungo kwenda Mbezi Mwisho ili kuwa na stendi ya kimatatifa tofauti na ya sasa.

Amesema pamoja na mambo mengine sababu za kuhamishwa kwa stendi hiyo ni kuepuka kero ya kukutana na mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto kubwa katika stendi kuu ya mabasi Ubungo.

Mhe. Makonda aliyasema hayo katika ziara ya ghafla aliyoifanya katika stendi ya Ubungo kwa lengo la kujionea hali ya sasa na stendi hiyo kuu.

Aidha, amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo hadi hapo yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.

Amesema haiwezekani mawakala wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si sahihi wakati katika eneo hilo hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.

“Nataka maeneo rasmi yakishatengwa ndipo muanze kutoza faini, mmekuwa mkiwasumbua wananchi hawajui wapi ni sehemu ya maegesho na wapi si sehemu ya maegesho wekeni alama ndipo muanze kuwatoza,” ameongeza Makonda.

Wakati huohuo amemtaka Mkurugenzi wa Jiji kuhakikisha kituo hicho kinawekwa taa ili kuondoa usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi hasa wakati za usiku kabla ya kumalizika wiki hii na kuahidi kurejea baada ya siku 20 kujionea utekelezaji wa agizo hilo.

“Shahuku yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe na stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo halmashauri ya Jiji tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo.

Dokta Mwaka Ajisalimisha Polisi

Tarehe August 11, 2016 8/11/2016
IMG_20150510_185527V 1

 Hatimaye Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia nguvuni tabibu maarufu wa tiba asilia, Dokta Mwaka maarufu kama Dokta JJ Mwaka kufuatia agizo la Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamis Kigwangalla.

Dokta Mwaka ambaye alikuwa anatafutwa na polisi tangu juzi aliweza kujisalimisha polisi jana na kushikiliwa kwa mahojiano zaidi baina yake na Jeshi la Polisi.

Tabibu huyo wa Tiba Mbadala kutoka Foreplan Clinic alikuwa akisakwa na polisi kwa kile kilichodaiwa kukaidi uamuzi wa Serikali wa kufutia usajili kituo chake na badala yake akaendelea kutoa huduma hizo kama kawaida.

Hivi karibuni Dokta Mwaka alikuwa miongoni mwa matabibu wa tiba mbadala waliofutiwa usajili huku wengine wakisimamishwa kwa muda na tayari baadhi yao wamekwishakimbilia mahakamani ili kupewa ruhusa ya kufungua kesi dhidi ya Serikali kufuatia uamuzi wa kuwafutia leseni zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdani alisema jana kuwa baada ya kujisalimisha muda huo, alihojiwa na kuachiwa kwa dhamana lakini akatakiwa kuripoti leo kwa mahojiano zaidi.

“Kuhusu kupelekwa mahakamani, ni mpaka jeshi la Polisi litakapomaliza kukusanya ushahidi na kumkabidhi DPP ambaye atautumia kufungua kesi,” amesema.

Tuesday, 9 August 2016

Mfumuko Wa Bei Mwezi Julai Wapungua Hadi Asilimia 5.1

Tarehe August 10, 2016
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraimu Kwesigabo akielezea mfumuko wa bei kwa mwezi Julai, 2016.V 1
Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraimu Kwesigabo akielezea mfumuko wa bei kwa mwezi Julai, 2016.

Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) imesema kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwezi ulioishia wa Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji wa bidhaa hizo iliyokuwepo kwa mwezi ulioishia Juni, 2016.

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa kwa maana hiyo mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai 2016 umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 iliyokuwepo mwezi Juni mwaka huu. 

Amesema kuwa kupungua kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Julai 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2016 zikiwemo bidhaa za samaki kwa asilimia 6.6,mafuta ya kupikia asilimia 4.9 na maharage kwa asilimia 1.9 huku bei zisizo za vyakula zikihusisha ni gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni pamoja na bidhaa za gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

Aidha, ameeleza kuwa pamoja kupungua huko, kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kwenye baadhi ya bidhaa umeonesha kuongezeka katika kipindi hicho hasa kwenye kama mchele, mahindi, unga wa mahindi, vyakula kwenye migahawa na mkaa.

Bw. Kwesigabo amesema kuwa Fahirisi za Bei nazo zimeongezeka hadi kufikia 103.50 mwezi Julai, 2016 kutoka 103.47 za mwezi Juni 2016, ongezeko ambalo limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula zile zisizokuwa za vyakula.

Amesema ongezeko hilo la Fahirisi linahusisha kundi la bidhaa na huduma za vyakula na vinywaji baridi, Vinywaji vyenye kilevi na bidhaa za Tumbaku, Mavazi ya nguo na viatu, nishati, maji na Makazi pamoja na Samani, vifaa vya nyumbani na ukarabati wa nyumba.

Kundi lingine linahusisha gharama za Afya, usafirishaji, Mawasiliano, Utamaduni na Burudani, Elimu, hoteli na migahawa pamoja na bidhaa na huduma nyinginezo ambazo jumla ya Fahirisi za Bidhaa hizo kwa mwezi huo zimefikia 103.50.

“Baadhi ya bidhaa zilizo sababisha kuongezeka kwa Fahirisi ni pamoja na mafuta ya kupikia asilimia 1.1, samaki wabichi asilimia 6.0, matunda asilimia 4.9, maharage makavu kwa asilimia 2.7, ndizi za kupika asilimia 1.9 na mahindi kwa asilimia 1.5” Amesisitiza Kwesigabo.

Mbali na hilo ameeleza kuwa Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2016 umepungua hadi kufikia asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ya mwezi Juni 2016.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi ya 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 62 mwezi Julai 2016 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 65 ya mwezi Juni, 2016.

Aidha, hali ya Mfumuko wa Bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki imeonesha kuwa nchi ya Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Julai umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.39 kutoka asilimia 5.80 za mwezi Juni, 2016, Uganda ikiwa na Mfumuko wa Bei uliopungua wa asilimia 5.1 kwa mwezi Julai kutoka asilimia 5.9 za mwezi Juni, 2016.

TCRA Yawapiga Faini Ya Milioni 19 ITV, Cloudz Media

Tarehe August 10, 2016
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi.

Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi. Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo imevitoza faini ya jumla Shilingi milioni 19 vituo vya utangazaji vya luninga vya ITV, Clouds TV na Redio Clouds kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

Kwa mujibu wa TCRA, Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.

ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja, ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema “Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas,hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge.”

TCRA imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.

Magufuli Kutikisa Viwanja Vya Furahisha Mwanza.

Tarehe August 10, 2016
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.V 1

Rais Dkt.John Pombe Magufuli. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza anatarajia kuweka historia ya kuhutubia katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela amesema Rais Magufuli atawahutubia wananchi katika viwanja hivyo kesho na kuwataka wanachi kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo mkubwa wa kisiasa.

Viwanja vya Furahisha ni moja ya viwanja vilivyojipatia umaarufu mkubwa kutokana na wanasiasa pamoja na viongozi wa serikali kuvitumia kuwakuhutubia wananchi.

Monday, 8 August 2016

Supu Ya Pweza Yathibitika Kusaidia Nguvu Za Kiume.

Tarehe August 9, 2016
12472499_1138768596202399_1414658179980401994_nV 1

Wataalam na wanasayanzi wa ndani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na wa Kimataifa wamethibitisha kuwa supu ya pweza ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.

Wataalam hao wanadai kuwa supu hiyo inafanya kazi hiyo kwa asilimia kubwa tofauti na madawa mengine ya kemikali.

Taarifa hii ya wataalm hawa inakuja wakati kukiwa na majadiliano ya mara kwa mara juu ya uwezo wa supu hiyo ambayo ni maarufu sana katika viunga tofautitofauti katika Jiji la Dar es Salaam hasa nyakati za jioni.

Je ndugu msomaji nini maoni yako kuhusiana na taarifa hii ya wataalam wetu kuhusu pweza na supu yake?

Mwigulu Atangaza Kiama Kwa Wasafirishaji Wa Madawa Ya Kulevya

Tarehe August 9, 2016
Screen-Shot-2016-05-23-at-12.51.47-PMV 1

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya katika mpaka wa Tunduma, Mkoa wa Songwe, kuwakamata wahusika wa uvushaji wa dawa hizo kutoka nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.

Nchemba amesema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka kutokana na kutapakaa kwa dawa za kulevya.

Amesema kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani, wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa baadhi ya nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila atakayejitambulisha kuwa Mtanzania.

“Hatuwezi kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China Watanzania zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan wapo, India, Afrika Kusini ni Watanzania na hili linatuchafua sana,” amesema Nchemba.

Katika hatua nyingine, Nchemba aliutaja mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha dawa hizo na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako.

Saturday, 6 August 2016

Taarifa : Manara Atoa Bei Mpya Ya Jezi Simba Fc

Tarehe August 6, 2016
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Simba Fc,Haji ManaraV 1
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Simba Fc,Haji Manara Mkuu wa kitengo cha mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewasisitiza mashabiki wa Simba kuiunga mkono timu hiyo kwa kununua jezi ya timu hiyo ambayo itauzwa kwa shilingi 20,000 za kitanzania.
Manara amesema kuwa jezi hizo zipo katika ubora wa hali ya juu na zitapatikana uwanjani siku ya Simba Day.

Picha: Manji Ndani Ya Nyumba Mkutano Umeanza

Tarehe August 6, 2016
Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji akiingia katika ukumbini
Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji akiingia katika ukumbini. Yusuf Manji akifungua mkutano pamoja na kuwasilisha ajenda za mkutanoYusuf Manji akifungua mkutano pamoja na kuwasilisha ajenda za mkutano Manji 1manj 3

clouds stream