Monday, 31 October 2016

Ziara Ya Kwanza Ya Rais Magufuli Kenya

Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili nchini Kenya.
V 2
Rais Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili nchini Kenya.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli leo amewasili nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Akiwa nchini Kenya Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, na baadae atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Mheshimiwa Rais pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini Nairobi.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi na pia kuzindua barabara mchepuko (Southern By­pass) iliyopo Jijini humo. Barabara hiyo ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini.

Bomoa Bomoa Yazidi Kushika Kasi Mbezi Louis


Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la uboamoji wa nyumba maeneo ya mbezi Luis.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia zoezi la ubomoaji wa nyumba maeneo ya mbezi Louis.
Wakala wa Barabara Tanzania(Tanroad) wiki hii umeendesha zoezi la kubomoa nyumba, vibanda pamoja na mabango ya biashara yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya Barabara katika maeneo ya Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam.
Zoezi la ubomoaji limefanyika chini ya Ulinzi mkali kutoka kwa Jeshi la Polisi waliokuwa na silaha za moto.
Hata hivyo wakati wa zoezi la ubomoaji likiendelea baadhi ya Polisi walizuia watu waliokuwa wanapiga picha tukio hilo kupitia simu na vifaa vingine vya kigitali.Moja ya Ghorofa lililobomlewa nje ya kituo kikuu cha Daladala Mbezi luis.Moja ya Ghorofa lililobomlewa nje ya kituo kikuu cha Daladala Mbezi luis.Moja ya Ghorofa lililobomolewa nje ya kituo kikuu cha Daladala Mbezi louistTinga tinga likivunja moja ya nyumba katika eneo la Mbezi Louis jijini Dar es salaam

COSTA, HAZARD WACHEKA NA NYAVU CHELSEA IKIITULIZA SOUTHAMPTON MBILI MTUNGI

V 2


SOUTHAMPTON (4-3-3-): Forster 6.5; Martina 5, Fonte 6, Van Dijk 6.5, Bertrand 6 (McQueen 78); Romeu 6, Clasie 5 (Boufal 61), Davis 6; Redmond 6, Tadic 5 (Hojbjerg 78), Austin 5
SUBS NOT USED: Taylor, Yoshida, Ward-Prowse, Olomola
 MANAGER: Claude Puel 6

CHELSEA (3-4-3): Courtois 6; Azpilicueta 7, Luiz 7, Cahill 6.5; Moses 7.5 (Ivanovic 87), Kante 7 Matic 7.5, Alonso 6; Pedro 6.5 (Willian 78), Costa 8.5 (Batshuayi 88), Hazard 8
SUBS NOT USED: Begovic, Oscar, Terry, Chalobah
GOALS: Hazard 6, Costa 55
MANAGER: Antonio Conte 7 
REFEREE: Mike Jones 6
ATTENDANCE: 31,827
MAN OF THE MATCH: Diego Costa

* Ratings by Matt Barlow




Sunday, 30 October 2016

Bondia Thomas Mashali Auawa Kikatili


Marehemu Bondia, Thomas Mashali.
Marehemu Bondia, Thomas Mashali.
Bondia Mtanzania wa ngumi za kulipwa, Thomas Mashali ‘Simba asiyefugika’ ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo baada ya kuitiwa kele za mwizi.
Mashali ambaye jina lake kamili ni, Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara Jijini Dar es Salaam wakati akinywa pombe, ambapo ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi ndipo watu wakaanza kumshambulia.
Kwa mujibu wa ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi na kupelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako umauti ulimkuta.
Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa (TPBO), Yassin Abdallah ‘Ustadh’ amesema kuwa ni kweli Mashali amefariki dunia baada ya kupokea habari hizo muda mfupi uliopita na yupo njiani akielekea Muhimbili.
Inadaiwa kuwa hadi nyakati za jioni, marehemu alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

Bodi Yafafanua Vigezo Vya Mikopo Na Waliokosa Mikopo Elimu Ya Juu

1
V 2

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017.

Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu.

Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na 25,717 wa mwaka wa kwanza.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana (Jumapili, Oktoba 30, 2016), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul­Razaq Badru alisema vigezo vikuu vinavyotumika mwongozo uliotangazwa na Bodi hiyo wakati ilipotangaza kuanza kupokea maombi mwezi Juni mwaka huu ambao unataja makundi makuu matatu ya watakaopata mikopo.

Vigezo vilivyotumika kutoa mikopo

Kwa mujibu wa Bw. Badru, kundi la kwanza linajumuisha wanafunzi waombaji wa mikopo wenye uhitaji maalum kama wenye ulemavu uliothibitishwa na Waganga Wakuu wa Wilaya na yatima ambao katika maombi yao waliwasilisha nakala za vyeti vya vifo zilizothibitishwa na makamishna wa viapo.

“Kundi la pili linajumuisha waombaji wa mikopo ambao baada ya uchambuzi wa taarifa zao walizowasilisha na baada ya kulinganisha na gharama za jumla za masomo yao ya sekondari, wamebainika kuwa wana uwezo mdogo wa kugharamia masomo yao ya elimu ya juu na hivyo kuwa na uhitaji zaidi wa mikopo,” amesema Bw. Badru.

Badru ametaja kundi la tatu na la mwisho kuwa linajumuisha waombaji wa mikopo ambao wenye ufaulu wa juu katika matokeo yao ya kidato cha sita na wamechaguliwa kujiunga na fani za kipaumbele kwa taifa.

Fani hizo ni Sayansi za Tiba, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi wa Kilimo, Mafuta na Gesi na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

Makundi ya wanafunzi waliopata mikopo

“Hivyo basi, hadi sasa tumetoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 wakiwemo wanafunzi yatima 4,321, wenye ulemavu 118, wanafunzi wenye uhitaji waliosomeshwa na taasisi mbalimbali katika masomo ya sekondari (87), wanafunzi wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na wanafunzi wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele lakini wanaotoka kwenye familia duni 9,498,” amefafanua Bw. Badru.

Sababu za kukosa mikopo

Katika mkutano huo, kiongozi huyo wa HESLB pia ameeleza kwa kina sababu nyingine za waombaji 27,053 ambao hawajapangiwa mikopo.

Ametaja sababu hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya waombaji (90) kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30, waombaji mikopo waliopata udahili kwa sifa linganishi (equivalent qualifications) na waombaji waliomaliza masomo ya kidato cha sita zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Kundi jingine la waombaji waliokosa mikopo katika awamu ya kwanza ni waombaji waliopata nafasi katika vyuo kwa ufaulu wa mitihani waliyofanya kama watahiniwa binafsi (Private Candidates) na waombaji ambao hawakurekebisha fomu zao za maombi ingawa waliitwa kufanya hivyo.

Nafasi ya rufaa na uhakiki wa wanafunzi wanaoendelea na masomo

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo pia amewataka waombaji ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo unaotangazwa, kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao utakaofunguliwa kuanzia katikati ya wiki hii.

“Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamekosa mkopo kwa kutowasilisha baadhi ya nyaraka ingawa tuliwaomba kufanya hivyo, hawa na wengine wenye sababu za msingi, watapata fursa ya kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao na nakala kuzituma kwa utaratibu tutakaoutangaza wiki inayoanza kesho(leo),” amesema Bw. Badru.

Aidha, Bw. Badru amesema bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kazi kuhakiki taarifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wanapata mikopo ya elimu ya juu kwa lengo la kubaini kama ni wana uhitaji wa mikopo hiyo kwa mujibu wa vigezo au hapana.

Katika zoezi hili linalotarajiwa kufanyika kwa siku 30 kuanzia mwezi ujao (Novemba, 2016), wanafunzi wote ambao ni wanufaika watalazimika kujaza dodoso maalum litakalokusanya tarifa za kiuchumi za wazazi na walezi wao ili kuweza kupata uhalisia wa sasa.

“Wanafunzi watakutana na dodoso katika akaunti zao katika mtandao wetu wa maombi ya mikopo (OLAMS) na watapaswa kujaza. Wale ambao hawatajaza dodoso hili kwa njia ya mtandao tutasitisha mikopo yao na wale ambao baada ya uchambuzi tutabaini hawana uhitaji, nao tutasitisha mikopo yao na watapaswa kuanza kurejesha fedha walizokopokea,’ amefafanua.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka 2005 kwa lengo la kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji waliopata nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wadaiwa walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994.

Ajali:Basi La Abiria na Lori la cement Yateketea kwa Moto Dar.



4V 2
Basi lenye namba za usajili T990 AQF mali ya kampuni ya Safari Njema liililokuwa likitokea Dodoma kuja jijini Dar es Salaam, jana liliteketea kwa moto maeneo ya Kimara Stop Over­Suka, baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake za usajili hazikujulikana mara moja).
Imeelezwa kuwa mali zote zilikuwemo katika basi vimeteketea kabisa kwa moto.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.125896

Wednesday, 26 October 2016

Serikali Yapiga Marufuku Michakato Ya Kubadili Umiliki Simba Na Yanga

mabasi1V 2

Serikali kupitia Baraza la Michezo Tanzania (BMT) imetoa agizo la kusitishwa kwa michakato ya kubadilisha umiliki wa timu za Simba na Yanga.

Inataka klabu hizo zibaki kwa wanachama kama ilivyo sasa na kwa muda mrefu tangu kuanza kwa vilabu hivyo.

Hivi karibuni kumekuwa na malumbano kuhusu umiliki wa vilabu hivyo baada ya wafanyabiashara wawili wakubwa Yusuph Manji (Yanga) na Mohamed Dewji ‘MO’ (Simba) ambapo Manji anataka kukodishiwa klabu ya Yanga kwa muda wa miaka kumi huku MO akitaka kuwa na hisa zaidi ya 51 katika klabu hiyo.

NSSF Yakiri Kuingizwa Mkenge Bilioni 270

profesa-godius-kahyarara
V 2

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limekiri mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa linaweza kupoteza kiasi cha Sh bilioni 270, zilizoingizwa kwenye mradi wa ubia baina yake na Kampuni ya Azimio Housing Estates (AHEL), kama shirika hilo lisipokuwa makini.

Pamoja na hayo, kamati hiyo baada ya kubaini madudu kadhaa katika hesabu za shirika hilo, imemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu wa mikopo yote iliyotolewa na NSSF kwa vyama vya akiba na mikopo.

Akijibu hoja za wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mradi huo ambao ni ujenzi wa mji wa kisasa katika eneo la Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara amesema kwa sasa kinachoangaliwa kwenye mkataba huo ni athari za kupoteza fedha hizo.

Profesa Kahyarara amesema pamoja na shirika hilo kuwepo kwenye ubia huo, lakini limegundua ekari zilizopo kwenye mkataba si za uhalisia.

Amesema kwa mujibu wa mkataba zilitakiwa ziwe ekari 20,000 lakini kiuhalisia baada ya kufanya tathmini zipo ekari zaidi ya 3,500.

Aidha, alifafanua kuwa bei iliyothaminiwa kwenye ekari hizo pia ni tofauti kwani mwekezaji huyo alithaminisha ardhi hiyo kwa Sh milioni 800, lakini baada ya NSSF kufanya uchunguzi wake ikabaini kuwa ekari moja thamani yake ni Sh milioni 25.

Kwa mujibu wa taarifa za CAG zinaeleza kuwa NSSF iliingia ubia na kampuni hiyo na kuanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Builders Limited.

Katika mkataba huo, Azimio Housing Estates itatakiwa kuendeleza ekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa mji mpya wa kisasa wa Kigamboni kupitia mradi uliopo eneo la Dege.

Hata hivyo, mradi huo umesimama utekelezaji wake tangu Februari, mwaka huu kutokana na mwekezaji kutokuwa na fedha huku NSSF tayari ikiwa imeshaingiza Sh bilioni 270.

Katika ubia huo, NSSF inamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estates inamiliki asilimia 55 ya hisa na jumla ya gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 653.44.

Mashabiki Yanga Wamlilia Pluijm

plujin
V 2

Siku moja baada ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Pluijm, kuandika barua ya kujiuzulu kuwafundisha mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kundi la mashabiki wa timu hiyo wameonesha kutoridhishwa na uamuzi huo na kuutupia lawama uongozi kwa kusababisha kuondoka kwa mpendwa wao huyo.

Pluijm ameifundisha timu hiyo kwa misimu miwili na kuipa mafanikio makubwa ikiwemo kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu hatua ambayo ilikuwa haijafikiwa na timu hiyo kwa kipindi cha miaka 18 nyuma.

Baadhi ya mashabiki wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa uongozi wao wa juu na wengine kudai hawatoona ajabu kwa timu hiyo kushindwa kutetea ubingwa wake kutokana na kubadilisha kocha wakati ligi ikiendelea.

Hamisi Abdallah mwanachama wa Yanga kutoka tawi la Buguruni, amesema, binafsi angependa Kocha Pluijm aendelee kuifundisha timu hiyo kwa sababu bado hajaona mabaya aliyoyafanya na hasa ukizingatia mafanikio aliyowapa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Abdallah amesema, kama uongozi ulitaka kumbadilisha kocha huyo ungesubiri wakati wa dirisha dogo na siyo kipindi hiki, ambacho ligi ipo kwenye ushindani na wapinzani wao Simba wameonekana kujipanga kuwapoka ubingwa wao.

Naye Emmanuel Mgamilo, shabiki wa Yanga kutoka Magomeni amesema, kitendo wanachokifanya viongozi wa Yanga kinaweza kuitafuna timu hiyo kushindwa kupata taji lolote msimu huu, kwani kumbadilisha Kocha Pluijm na kuleta kocha mpya ni sawa na kuwachanganya wachezaji.

Mgamilo, alisema kwa mafanikio ambayo wameyapata chini ya Pluijm kocha huyo alikuwa na nafasi ya kuendelea kuifundisha timu hiyo na sababu ambazo uongozi wao umezichukua hata kumtimua kocha huyo hazina mashiko kwani ni sawa na kumdhalilisha kwani rekodi zake zinajieleza wazi.

Kocha Pluijm aliamua kuandika barua ya kuacha kazi muda mfupi baada ya kupata taarifa ya kuwasili Kocha wa Zesco United, Mzambia George Lwandamina, ambaye kwa muda wa wiki sasa taarifa zake zilizagaa nchini kuja nchini kuziba nafasi ya Mdachi huyo ambaye alitua Yanga kwa mara ya kwanza mzunguko wa pili wa msimu wa 2013/14 akichukua mikoba ya Mholanzi mwenzake Ernie Brandts na aliweza kumaliza nafasi ya pili nyuma ya waliokuwa mabingwa wa msimu huo Azam.

Kabla ya msimu wa 2014/15 kuanza kocha huyo aliomba kuvunja mkataba wake na kuondoka baada ya kupata timu ya kufundisha nchini Saudi Arabia ‘Al Shaola FC’ na alimchukua aliyekuwa msaidizi wake Boniface Mkwasa, lakini hawakudumu sana alitimuliwa huko na kuamua kurudi Ghana anapoishi wakati huo Yanga ikimchukua Mbrazil Marcio Maximo aliyeziba nafasi yake lakini baada ya uongozi wa Yanga kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao kwenye ligi uliamua kuachana na Maximo karibu na mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.

 Msimu uliofuata wa 2015/16 Pluijm aliiwezesha Yanga kutetea ubingwa huo akiwa ameanza nayo mwanzo na kusajili yeye nyota kadhaa akiwemo Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Hajji Mwinyi na nyota wengi ambapo mbali na kutetea ubingwa pia walibeba Kombe la FA lililofanyika kwa mara ya kwanza baada ya kusimama kwa muda na pia aliweza kuifikisha timu hiyo raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa kwa mabao 2­1 na Al Ahly ya Msri na kuangukia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya makundi.

Pluijm mwenyewe amesema kilichomfanya aandike barua ya kujiuzulu ni dharau aliyooneshwa na viongozi wa Yanga kwa kumleta nchini kocha mpya bila kumtaarifu yeye na amewaomba radhi mashabiki na wanachama wa timu hiyo.

Asilimia 90 Wanafunzi Elimu Ya Juu Kupata Mikopo Kesho

kassim3
V 2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia kesho asilimia 90 ya wanufaika mikopo ya elimu ya juu watakuwa wameshapata fedha zao.
Maliwa ameyasema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kudai kuwa kwa taarifa aliyonayo aliyoipata jana asubuhi wachache sana walikwishaanza kulipwa tangu juzi na kuwa ulipaji huo utaendelea hadi siku ya kesho ambapo asilimia 90 ya wanaopaswa kulipwa watakuwa wamepata fedha hizo.
“Serikali haitavumilia tena ucheleweshwaji wa makusudi wa malipo ya fedha za mikopo ya chuo. Kama kuna tatizo taarifa lazima zitolewe haraka ili kuzuia migogoro kati ya wanafunzi na Serikali yao,” amesema.
Wakati huohuo Majaliwa amesema Serikali itaendelea kutafuta fedha za mafunzo kwa ajili ya wahadhiri wa vyuo vikuu nchini ili kuziba pengo la wahadhiri waandamizi lililopo hivisasa.
Amevitaka vyuo hivyo viweke utaratibu wa kuachiana nafasi ama kurithishana kazi (succession plan).
Amesema yeye binafsi anatambua upungufu uliopo umesababishwa na masharti ya ajira za mkataba kwa wahadhiri waandamizi kuwa miaka 65 na maprofesa kuwa miaka 70.
“Ninatambua kuwa katika vyuo vya umma kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri waandamizi na maprofesa na hivyo kuathiri hali ya utoaji wa taaluma kwa fani za ‘Post­Graduates’. Ninajua kuwa pamoja na sababu nyingine, hali hii inachangiwa pia na masharti ya ajira za mikataba kwa wahadhiri waandamizi kuwa miaka 65 na maprofesa kuwa miaka 70,” amesema.

JPM Atajwa Kuwania Tuzo Ya ‘Forbes’, Ingia Hapa Kumpigia Kura


personV 2
Rais Dkt John Pombe Magufuli ametajwa kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year.’ JPM atachuana na watu wengine wanne wakiwemo, Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda.
Zikiwa zimebaki siku 22 za kupiga kura, unaweza kumpigia kura Rais Magufuli ambaye hadi sasa anaongoza kwa asilimia nyingi (73%).
Mwaka huu tuzo hizo zitatolewa jijini Nairobi, Kenya November 17.
Wafuatao ni washindi wa tuzo hiyo kwa miaka ya nyuma
Mohammed Dewji (Tanzania)– 2015
Aliko Dangote (Nigeria)– 2014
Akinwumi Adesina (Nigeria) – 2013
James Mwangi (Kenya) – 2012
Sanusi Lamido Sanusi (Nigeria)- 2011

Tuesday, 25 October 2016

Rushwa Bilioni 8 Yawapandisha Vigogo Bandari Kizimbani


courthousedoorsV 2

Vigogo watatu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Ephraim Mgawe (62) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kujihusisha na rushwa ya Sh bilioni nane. 

Mbali na Mgawe, vigogo wengine katika kesi hiyo ni Mkurugenzi wa zamani wa Uhandisi wa TPA, Bakari Kilo (59) na aliyekuwa Meneja wa Mazingira wa TPA, Theophil Kimaro (54) pamoja na Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya DB Shapriya, Kishor Shapriya (60).

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Wakili Kishenyi alidai katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2009 na 2012, Mgawe, Kilo na Kimaro kwa kutumia nafasi zao, waliomba rushwa ya Dola za Marekani milioni nne ikiwa ni zaidi ya Sh bilioni nane.

Inadaiwa waliomba rushwa hiyo kutoka kwa Shapriya ili kumuwezesha ashinde zabuni iliyokuwa ikishindaniwa yenye namba AE/0116/2008­2009/10/59 kwa ajili ya ujenzi wa bomba la TPA katika RAS ya Mjimwema.

Aidha, inadaiwa katika tarehe tofauti kati mwaka 2008 na 2009 akiwa kama Mkurugenzi wa DB Shapriya alitoa rushwa ya Dola za Marekani milioni nne kwa vigogo hao, kwa ajili ya kuiwezesha kampuni yake ishinde zabuni. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa walikana kuhusika na kutenda makosa hayo.

Wakili Kishenyi alisema upelelezi wa kesi bado unaendelea, pia hawana pingamizi la dhamana endapo washtakiwa watatimiza masharti ya dhamana yatakayotolewa na mahakama.

Vigogo hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakaosaini hati ya dhamana ya Sh milioni 500 kwa kila mmoja.

Vigogo Wa Polisi Wakamatwa Na Magari Ya Wizi

car-theft-2
V 2

Wakazi wa Mji wa Himo, Wilayani Moshi wamelalamikia hatua ya Jeshi la Polisi kutowawajibisha maofisa wake wawili wanaohusishwa na mtandao wa wizi wa magari.

Taarifa kutoka ndani ya Polisi zinadai kuwa maofisa hao, ambao mmoja ni Mratibu wa Polisi huku mwingine akiwa Koplo walikamatwa na magari magari matatu ya wizi yaliyosafirishwa kutoka kutoka Mjini humo hadi Dar es Salaam.

Maofisa hao wanadaiwa kukamatwa na magari hayo mwezi uliopita na kikosi kazi maalum kutoka Dar es Salaam lakini hadi sasa wapo kazini.

Kukamatwa kwa maofisa hao kulitokana na kutajwa na watuhumiwa muhimu wa mtandao wa wizi wa magari Jijini Dar es Salaam waliokuwa mikononi mwa polisi ambao walisafirishwa hadi himo na kupelekea kukamatwa kwa magari hayo.

Katika operesheni hiyo, mtuhumiwa mmoja alikamatwa nyumbani kwa Koplo akiwa na gari moja la wizi na vibao 70 vya namba za magari huku ASP huyo akidaiwa kukamatwa na gari aina ya RAV4 likiwa na namba bandia huku magari mengine mawili yakikutwa kwa Koplo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alikiri vigogo hao wa polisi kukamatwa na magari hayo na kudai kuwa hawawezi kupewa adhabu hadi pale itakapothibitika kuwa wamefanya uhalifu.

Rais Magufuli Ataja Vitu 3 Mfalme Wa Morocco Kuisadia Tanzania

pombe-j-m
Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
V 2
Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema Serikali ya Morocco inatarajia kuisaidai Tanzania vitu 3 katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza leo katika Hafla ya utiaji saini Ikulu jijini Dar es salaam leo Rais Magufuli alisema kwamba amemuomba Mfalme wa Morocco Mohammed VI kujenga Msikiti mkubwa katika Jiji la Dar es salaam amekubali kazi ya kuujenga Msikiti huo.
Rais Magufuli amemuomba Mfalme huyo kujenga uwanja mkubwa wa Mpira wa Kisasa Makao makuu ya nchi mjini Dodoma ambao utakuwa na thamani ya dola milioni 80 hadi 100 na Mfalme huyo pia ameahidi kuujenga uwanja huo.
Rais Magufuli amesema kwa mategemeo yake uwanja huo utakuwa mkubwa zaidi kuliko uwanja wa Mpira wa jijini Dar es salaam ambao ndio mkubwa kwa kuliko uwanja mwingine wowote hapa nchini.
Kwa upande wa mambo mengine Rais Magufuli amesema wamekubaliana kufanya mafunzo ya ulinzi kati ya nchi hizo mbili za Tanzania na morocco ambapo zaidi ya Maaskari 150 watakwenda nchini Morocco wiki ijayo kwenda kujifunza.
Katika ziara yake nchini Tanzania Mfalme wa Morocco na Mawaziri kutoka nchini humo wametiliana saini mikataba takribani 21.

Sunday, 23 October 2016

Matokeo EPL Mechi Za Leo Jumapili Man U Akigaragazwa

epl
V 2epl2

Maalim Seif Adai Kuna Njama Za Kumuua

maalim-2

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ametoa tuhuma nzito kuwa kuna njama za kumuua kwa kumkamata na kumpulizia sumu itakayochukua uhai wake taratibu.

Seif aliyezaliwa Oktoba 22, 1943 katika Kijiji cha Nyali Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba ameyasema hayo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Baraza Kuu, Viongozi, Watendaji na Wafuasi wa CUF alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 73.

Bila kutaja wanaotaka kumuua, amesema kuwa kuna taarifa za kuaminika kwamba zipo njama za kumkamata na kupelekwa Dar es Salaam kama walivyofanyiwa masheikh, waniweke kwenye chumba maalum kidogo kasha wanipulizie dawa ili afya yangu izorote polepole na mwisho nifariki dunia.

Amesema hujuma za kutaka kumuua zipo tangu zamani lakini ni Mwenyezi Mungu ndiye ameweza kumlinda, hivyo hajali wala kuogopa chochote.

Kiongozi huyo ambaye alikuwa pia Makamu wa Kwanza wa Rais kwa iliyokuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK) amesema kuwa kama ana makosa yoyote ni vyema sharia ikachukua mkondo wake kwa kumfikisha mahakamani.

Akizungumzia tuhuma hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Abood Mohamed amesema Serikali itatoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo.

“Waulizeni Jeshi la Polisi wanaweza kuwapa taarifa , lakini kwa upande wa Serikali ya Zanzibar itatoa taarifa rasmi kuhusu suala hilo,” amesema.

Naye Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Hamdan Onar Makame amesema hana taarifa zozote kuhusiana na suala hilo.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Salum Msangi pia amedai kutokuwa na taarifa za Maalim Seif kuzungumza maneno hayo lakini akaahidi kuzifanyia kazi ili kufahamu ukweli wa maneno hayo.

CHADEMA Wasusia Uchaguzi Wa Meya

chadema1
V 2

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimegoma kushiriki katika uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na Ubungo uliopangwa kufanyika leo Jijini Dar es Salaam na kupelekea uchaguzi huo kuvugika.

Kwa mujibu wa Chadema, uamuzi huo umefikiwa baada ya wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuongezwa katika hali isiyoeleweka pamoja na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo, John Kayombo amekataakuzungumzia hatma ya uchaguzi wa Meya Ubungo na kuamua kuondoka eneo la uchaguzi.

Katika Manispaa ya Ubungo uchaguzi huo umeahirishwa baada ya UKAWA kujenga hoja kwamba wapo madiwani wasiohusika wametolewa Kinondoni na kuja Ubungo kupiga kura.

Katika Manispaa ya Kinondoni uchaguzi huo umeshindwa kufanyika baada ya madiwani wote wa UKAWA kuondoka ukumbini bila kujisajili kufuatia kile kilichodaiwa kuwa hujuma kubwa kutaka kutokea na hali hiyo ikasababisha madiwani wa CCM waliobakia kushindwa kufanya uchaguzi kutokana na kutofikia akidi yaani theluthi mbili.

Awali ulinzi uliiimarishwa katika eneo la uchaguzi ambapo ni wapiga kura tu ndio walioruhusiwa kuingia katika uzio wa eneo la uchaguzi.

Saturday, 22 October 2016

Shein: Hatutoi Mikopo Wanafunzi Elimu Ya Juu.

shein
V 2

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kusimamisha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, hadi hapo serikali itakapojiridhisha na utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo hiyo.

“Hatutatoa mikopo mwaka huu mpaka hapo tutakapokamilisha kazi ambayo tumeanza kuifanya ya kupitia upya utaratibu wa utoaji mikopo hiyo ili kuhakikisha inatolewa kulingana na mahitaji ya sasa ya nchi na kwa wanaostahili,” amesema Dkt. Shein.

Akizungumza katika hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofaulu daraja la kwanza katika mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne mwaka 2015 na Kidato cha Sita mwaka 2016, Dkt. Shein amesema kuwa katika utaratibu wa sasa wapo waliodanganya kupata mikopo na ambao wamekopeshwa lakini wamekuwa wagumu kurejesha mikopo hiyo.

Katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Usii Gavu, jumla ya wanafunzi 119 waliomaliza kidato cha nne na wengine 50 waliomaliza kidato cha sita, walipewa zawadi kwa kupata daraja la kwanza katika mitihani yao ya taifa.

“Wako waliokejeli matokeo yenu, lakini ukweli ni huo mko 50 wa kidato cha tano mliopata daraja la kwanza na wengine 119 mliofaulu daraja la kwanza mtihani wa kidato cha nne,” amesema Dkt. Shein na kuhoji msingi wa kukebehi matokeo hayo.

Bodaboda Iliyotelekezwa Yazua Maajabu, Yaogopwa Na Polisi,Raia

pikipiki
V 2
Boda boda yente maajabu ikiwa imepigwa vumbi kwa muda wa mwaka mmoja bila kuguswa na mtu yeyote.

Pikipiki aina ya Fekoni yenye namba za usajili T684 CJZ imeonekana kuwa ya maajabu kufuatia kutelekezwa na kuogopwa na watu katika kituo cha Waendesha Bodaboda cha Maganga Veterinary jijini Dar es salaam.

Wakizungumzia bodaboda hiyo waendesha Bodaboda wanaopaki katika kituo hicho wameiambia HivisasaBlog kuwa Bodaboda hiyo imeshakaa hapo kituoni zaidi ya mwaka mmoja sasa, haijulikani nani hasa mmiliki wa Bodaboda hiyo.

Bodaboda hiyo inadaiwa kuwa licha kukaa mwaka mmoja bila kuguswa, ukikaribia inajiwasha,hivyo Jeshi la Polisi na Raia kushindwa kuiondoa katika eneo ilipopaki.

“Mwandishi hii Bodaboda sio ya kawaida,yaani ipo hapa zaidi ya mwaka na hakuna wa kuigusa kutokana na kama ina mauza mauza vile maana ukiikaribia inajiwasha yenyewe wakati pale ilipo haina funguo na Mwenye funguo hajulikani yuko wapi”.Alisema mmoja wa wendesha Bodaboda.

clouds stream