Uchaguzi Wa Meya Dar Wakumbwa Na Vurugu
Tarehe February 27, 2016
Uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam umeahirishwa tena leo kufuatia kuibuka kwa vurugu kubwa wakati tangazo la kuahirishwa uchaguzi huo lilipotolewa.
Chanzo cha vurugu hizo Katika ukumbi huo wa Karimjee kinadaiwa kuwa ni mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani.
Suala hilo limewakasirisha madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia.
Wakati UKAWA wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo wenyewe, Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini, jambo lilowachukiza tena na kuibua vurugu ndani ya ukumbi.
Uchaguzi huo leo umeahirishwa kwa mara ya nne huku kukiwa na dalili ya figisu figisu inayoedelea kuwamisha uchaguzi huo.
Uchaguzi huo leo umeahirishwa kwa mara ya nne huku kukiwa na dalili ya figisu figisu inayoedelea kuwamisha uchaguzi huo.