Thursday, 31 March 2016

Gary Nevile ‘Out’ Valencia


Gary Nevile ‘Out’ Valencia


Tarehe March 31, 2016
kocha wa Valencia Gary Neville
kocha wa Valencia Gary Nevillekocha wa Valencia Gary Neville
Beki wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Gary Neville amefutwa kazi na klabu ya Valencia ya Uhispania baada ya kuhudumu kama meneja wao kwa chini ya miezi minne.
Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 41, ambaye yumo kwenye benchi la kiufundi la Uingereza, alipewa kazi Desemba.
Valencia walishinda mechi tatu pekee kati ya 16 walizocheza ligini chini ya Neville, na mechi 10 kati ya 28 kwa jumla katika mashindano yote.
Neville amesema alitaka sana kukaa Valencia lakini matokeo hayakufikia kiwango chake na viwango vinavyohitajika na klabu hiyo.
Ameongeza kwamba anafahamu wazi kwamba “tumo katika biashara ya kuangalia matokeo”.
Ndugu yake mdogo, Phil, amekuwa kwenye benchi ya kiufundi Valencia na ataendelea na kazi yake.
Neville alianza kutakiwa ajiuzulu baada ya klabu hiyo kucharazwa 7-0 na Barcelona mechi ya kwanza ya nusu Copa del Rey mwezi Februari

Picha: Ronaldo,Pepe Wakirudi Hispania Baada Ya Kuitungua Ubelgiji


Picha: Ronaldo,Pepe Wakirudi Hispania Baada Ya Kuitungua Ubelgiji


Tarehe March 30, 2016
Mshambuliaji wa Ureno Christiano Ronaldo akiwa katika ndege akirudi nchini Hispania akiwa na Pepe
Mshambuliaji wa Ureno Christiano Ronaldo akiwa katika ndege wakirudi nchini Hispania akiwa na Pepe

Ubingwa Bado Kitendawili Msimbazi


Ubingwa Bado Kitendawili Msimbazi


Tarehe March 30, 2016
Kocha wa Simba Jackosn Mayanja
Kocha wa Simba Jackosn MayanjaKocha wa Simba Jackosn Mayanja
Jackson Mayanja anayekinoa kikosi cha Simba ambacho kipo kileleni katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara amekuwa akisita kuzungumzia suala la ubingwa.
Mayanja ambaye ana kibarua kizito cha kuhakikisha Simba inarudisha heshima baada ya kukosa ubingwa kwa miaka minne amekuwa akishindwa kujibu swali hilo kama Simba inaweza kubeba kikombe hicho.
Kocha huyo kila alipoulizwa suala hilo amekuwa akijibu kuwa ni mapema sana kuzungumzia suala la ubingwa ambao kila timu unautolea macho.
“Kuongelea suala la ubingwa sahivi unajidanganya maana kuna timu zina pointi ambazo zinaweza kuchukua ubingwa pia,”amesema Mayanja


Tuesday, 22 March 2016

Mabasi Yaendayo Kasi Kuanza Majaribio Ndani Ya Wiki Moja-Majaliwa

Tarehe March 22, 2016
10262227_717689465039977_2529648417247638500_n
10262227_717689465039977_2529648417247638500_n
Wazir Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mabasi yaendayo kasi (DART) yataanza kufanyiwa majaribio ndani wiki moja kuanzia sasa ili madereva waanze kuzoea njia na taa za kuongozea magari.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa majiko ya gesi sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha soko hilo na mabasi yaendayo kasi.
Amesema wataanza na mabasi kati ya 30 – 50 ambayo yatapita kwenye njia zote za mradi huo na zoezi hilo litafanyika ili watumiaji wengine wakiwemo waendesha daladala, bodaboda na watembea kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya mabasi yaendayo kasi si ya kwao hivyo waanze kuzoea.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea soko hilo kuanzia saa 5:10 hadi saa 5:54, alitoa jibu hilo wakati akijibu maombi ya mfanyabiashara mmoja, Bw. Sharifu Ramadhani ambaye alisema wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya usafiri kwa vile mabasi mengi yanaishia Mnazi Mmoja.
“Mabasi yanaishia Mnazi Mmoja na huku ni mbali kwa hiyo tunalazimika kutembea kwa miguu kwa sababu kukodi taxi ni gharama kubwa,” alisema Ramadhani.
Akifafanua kuhusu hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu amesema hivi sasa wanakamilisha ufungaji wa mitambo ya kukatia tiketi ambapo abiria atakuwa na kadi kama za benki ambayo anaijaza fedha halafu anapita kwenye mashine, kiasi cha nauli kinakatwa halafu anaingia kwenye basi, hakutakuwa na muda wa kukata tiketi.”
Amesema tatizo la usafiri kwa wafanyabiasha wa feri litakwisha hivi karibuni baada ya mabasi hayo kuanza.

Zitto Kabwe Ajiuzulu Kamati Ya Bunge Kisa Tuhuma Za Rushwa

Zitto Kabwe Ajiuzulu Kamati Ya Bunge Kisa Tuhuma Za Rushwa

Tarehe March 22, 2016
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ametoa taarifa rasmi ya kujiuzulu kutoka kwenye kamati aliyokuwa akihudumu ya Huduma za Maendeleo ya Jamii kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha uliotokana na rushwa.
Kupitia mtandao wa kijamii Zitto Kabwe, ameandika ujumbe kutoa taarifa hiyo, na kusema kuwa pia ameamua kufanya hivyo ili kupisha uchunguzi kufanyika.
Capture
Sambamba na hilo amedai kuwa amemuandikia barua spika wa bunge ili uchunguzi huo ufanyike kwa haraka dhidi ya tuhuma hizo na ikiwezekana hatua kali dhidi ya yeyote atakayehusika na vitendo vy rushwa ichukuliwe.
“Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya kamati mbalimbali za Bunge, ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika kuomba uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa, nimejiuzulu ujumbe wa kamati ili kutoa nafasi ya uchunguzi husika”, aliandika Zitto
Mapema mwaka huu wabunge waliteuliwa kuhudumu kwenye kamati mbali mbali, na Zitto Kabwe, alipangwa kwenye kamati ya Huduma na maendeleo ya jamii, ambapo awali alikuwa akihudumu kwenye kamati ya hesabu za serikali (PAC).

UKAWA Yaibuka Kidedea Uchaguzi Meya Jiji La Dar Es Salaam

UKAWA Yaibuka Kidedea Uchaguzi Meya Jiji La Dar Es Salaam

Tarehe March 22, 2016
tanzania2011_0106_dar_askarimonument
tanzania2011_0106_dar_askarimonument
Diwani Isaya Mwita kupitia Vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es salaam baada ya kuishinda CCM iliyopata kura 67, huku UKAWA wakipata kura 84, ambapo kura 7 ziliharibika.
Uchaguzi huo ulifanyika Machi 22 kuanzia saa 4.00 asubuhi ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Uchaguzi huo uliahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio batili la mahakama lililowekwa na makada wa CCM likidaiwa kutolewa na Mahakama Hakimu Mkazi wa Kisutu.
Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Magufuli aliingilia kati mvutano wa Umeya katika Jiji la Dar es Salaam na kuwaomba wanachama wa CCM kukubali uchaguzi kufanyika na kwamba yeyote atakayeshinda apewe kwani watanzania hawahitaji chama bali maendeleo bila kujali yanatoka chama gani au upande gani.

Mkuu Wa Wilaya Amuomba Rais Magufuli Asimteue Katika Nafasi Hiyo

Mkuu Wa Wilaya Amuomba Rais Magufuli Asimteue Katika Nafasi Hiyo

Tarehe March 22, 2016
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais Dkt. John Magufuli asimteue katika orodha ya Wakuu wa Wilaya wapya anaotarajiwa kuwateua hivi karibuni kwa madai kuwa anahitaji apate fursa zaidi ya kusimamia biashara zake zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya Ukuu wa Wilaya.
Mayenga aliweka wazi ombi hilo kwa Rais Magufuli hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika kikao cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mkoani Shinyanga ikiwa ni siku chache tu tangu Rais Magufuli aweke bayana vigezo vitakavyotumika katika kuwateua wakuu wa wilaya.
“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi ili isitafsiriwe kwamba nimeogopa lasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano lakini nimeona ni vyema nibakie na ubunge na biashara zangu,” amesema Mayenga ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM).
Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

Majaliwa Amtaka CAG Kukagua Mchezo Kati Ya TPA Na CRDB

Majaliwa Amtaka CAG Kukagua Mchezo Kati Ya TPA Na CRDB

Tarehe March 22, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki.
Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao.
Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesema kuna kila dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyokuwa yakifanyika kibenki lakini fedha hazionekana na wakaati huohuo wakala anaambiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia.
“Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha,” alisema Majaliwa.
Majaliwa pia amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Injinia Aloyce Matei kuandaa dispatch zote walizotumia kupokelea malipo ya kuanzia mwaka 2015 na ikibidi aandae za kuanzia mwaka 2014 ili CAG atakapozipitia aweze kupata picha halisi.
Vilevile, Waziri Mkuu alimwagiza Injinia Matei kuhakikisha wananunua mashine ya photocopy ili iwekwe kwenye chumba cha kupokelea stakabadhi za malipo ya benki (bank pay in slip) ili mteja anapoleta nakala ya benki aweze kutolewa photocopy na kubakia na nakala ya malipo aliyofanya.
Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua bandari ni eneo nyeti katika kuinua uchumi na mapato ya nchi lakini pia ni eneo muhimu katika kutengeneza ajira.
“Ninapenda niwahakikishie kuwa bado tutaendelea kukagua bandari hadi pawe safi kwasababu hii bandari ni yenu na mtafanya kazi kama kawaida,” alisema.
Mapema, akizumgumza kwa niaba ya mawakala hao, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha nchini (TAFFA), Bw. Stephen Ngatunga alieleza matatizo mbalimbali ambayo wao kama mawakala wa forodha wamekuwa wakikumbana nayo kuanzia ulipaji, utoaji wa mizigo na kuitaka Serikali iongeze nguvu katika kuikabilia sekta hiyo.
Alizikosoa baadhi ya sheria ambazo zinaruhusu wamiliki wa bandari kavu kumiliki pia makampuni ya uwakala wa forodha, sheria kadhaa zinazochangia kukwamisha utoaji wa mizigo bandarini, ukaguzi hafifu wa kwenye scanner na uwepo wa vituo vinane vya mizani kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa wasafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.
Wakati huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Injinia Edwin Ngonyani amesema Serikali imeamua kuyafungulia makampuni zaidi ya 150 ambayo yalikuwa yamefungiwa kufanya kazi za uwakala wa forodha kutokana na madai ya kuhusishwa na ukwepaji wa kodi.

Thursday, 17 March 2016

Bayern Wachomokea Kwenye Extra Time Washinda 4-2 Dhidi Ya Juventus

Bayern Wachomokea Kwenye Extra Time Washinda 4-2 Dhidi Ya Juventus

Tarehe March 17, 2016
Thomas Muellar
Thomas Muellar
Baryen wametinga robo fainali ya mabingwa ulaya baada ya kukomaa na kuitandika miamba ya soka italia Juventus magoli manne kwa mawili katika mchezo uliomalizika hivi punde.
mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya magoli mawili kwa mawili hivyo ushindi wa leo Bayern anakuwa na jumla ya magoli 6-4
Juventus walianza kuichapa Bayern wakimtumia Pogba dakika ya 5 na Juan Cuadrado dakika ya 28 magoli yalidumu hadi mapuziko lakini hali ilibadilika dakika ya 73 ambapo Robert Lewandowski alipatia Bayer goli la kusawazisha na  dakika ya 90 Mjerumani Thomas Muellar akaipeleka Juventus katika muda wa ziada.
Dakika 30 za nyongeza Bayern walionekana kucheza kwa kujiamini na dakika ya 108 Thiago Alcantara alitingisha nyavu na kuwaachaJuventus wakiduwaha lakini matumaini ya Juventus yalimalizwa na Kingsley Coman dakika ya 10 baada ya kuambaa na mpira huku mabeki wa Juventusi wakimshangaa na kumruhusu kupiga mkwaju uliomshonda kipa wa Juve.

Hii Ndio Barcelona Bwana,Watinga Robo Fainali Waipiga Arsenal 3-1

Hii Ndio Barcelona Bwana,Watinga Robo Fainali Waipiga Arsenal 3-1

Tarehe March 17, 2016
Neymar na Messi wakimpongeza Luis Suarez mara baada ya kuifungia Barcelona goli
Neymar na Messi wakimpongeza Luis Suarez mara baada ya kuifungia Barcelona goli
Barcelona wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa ya dunia kwa kuitandika Arsenal magoli matatu kwa moja.
Katika mchezo wa awali Barcelona walishinda magoli mawili kwa bila huko uingereza na kwa ushindi wa leo Barcelona wanafuzu kwa jumla ya magoli matano kwa moja.
Magoli ya leo yalifungwa na Neymar dakika ya 8,Luis Suarez akapiga Tik-Tak dakika ya  65 na Messi dakika ya 88 huku goli la kufutia machozi la Arsenal likifungwa na  Mohamed Elnen dakika ya 51

JWTZ Wakana Kutuma Kikosi Uchaguzi Wa Marudio Z’bar

JWTZ Wakana Kutuma Kikosi Uchaguzi Wa Marudio Z’bar

Tarehe March 17, 2016
Baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania.
Baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania.
Jeshi la Wananchi wa Tanzania limekanusha vikali taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa limepeleka wananjeshi wengi Visiwani Zanzibar kwa lengo la kudhibiti usalama kwenye uchaguzi wa marudio utakaifanyika machi 20,2016.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano Makao makuu ya Jeshi hilo  Upanga jijini Dar es salaam imebainisha kuwa  habari  hizo sio za kweli na zina lengo la kupotosha umma.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa JWTZ linao wanajeshi Visiwani Zanzibar ambao wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ni pamoja na  Ulinzi  wa nchi.
Jeshi hilo limesisitiza kuwa  hakuna mwanajeshi  yeyote aliyeongezwa zaidi ya wale  waliopo visiwani humo.

Mwapachu Atoa Siri Ya Lowassa, Arejea Rasmi CCM

Mwapachu Atoa Siri Ya Lowassa, Arejea Rasmi CCM

Tarehe March 16, 2016
Balozi Juma Mwapachu akirejea chama cha Mapinduzi leo jijini Dar es salaam.
Kada mkongwe Balozi Juma Mwapachu aliyetangaza kukihama chama cha Mapinduzi kwa mbwembwe tarehe 13 Oktoba 2015 leo amerejea nyumbani katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufuatia chama chake kuteua mgombea ambaye ni Rais Magufuli aliyeibadilisha nchi kwa kipindi cha muda wa miezi 3 na siku kadhaa.
Kada huyo aliyetangaza kuihama CCM na kurejesha kadi yake ya uanachama katika ofisi ya CCM Kata ya Mikocheni leo amerudi katika tawi hilo la CCM na kuichukua kadi yake.
Akizungumza baada ya kuchukua kadi yake amesema kwamba hapo mwanzo aliamini kuwa CCM imepoteza mwelekeo kwa kuamua kumnyima haki ya kugombea mcha mungu Edward Lowassa ambaye yeye alikuwa rafiki yake wa karibu.
“Baada ya miezi miwili ya uongozi wa Magufuli nataka niseme nilikosea sana. Nililewa mahaba ya Lowasa na nilipotezwa na ahadi ya Lowasa ya kunipa uwaziri wa mambo ya Nje.” Amesema Mwapachu.
Ameongeza kuwa aliamini mafuriko ya Lowasa ambayo yalimfanya aamini kabisa anachukua nchi na kunyetisha kuwa walikubaliana na wenzake kwamba wiki mbili za mwisho tuihame CCM kwa wimbi kubwa ili kuitikisa na kukitoa madarakani chama kikongwe cha Mapinduzi CCM, ambapo baadhi waliogopa na hadi sasa bado wamebaki CCM na wana vyeo.
Mwapachu amesema ameamua kurudi CCM kwasababu ameona kazi nzuri ya Magufuli na kujutia kosa kubwa alilolifanya katika siasa la kuihama CCM na kuwasihi vijana walio kwenye siasa wasilifanye.
“Nilihama kwa kwasababu ya mtu (Lowassa). Nimerudi kwasababu ya mtu (Magufuli). Nataka niwaahidi kwamba CCM ikiweka mtu hovyo baada ya Magufuli, sitahama,”Ameongea Mwapachu 
Ameomba radhi familia ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere kwa kuitumia kisiasa siku aliyokufa (tar 14 Octoba) na kutumia msiba wake kutoa kauli za kisiasa dhid ya chama chake alichokiunda na ambacho hadi anakufa alikuwa mwanachama.

Magufuli Aitumbua IPTL , Ataka Ndoa Yake Na TANESCO Ife


Magufuli Aitumbua IPTL , Ataka Ndoa Yake Na TANESCO Ife

Tarehe March 16, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuhusu ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi I nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL iliingia mkataba wa hovyo na Serikali na hivyo Serikali yake haitaendelea nao.
Rais John Magufuli amesema hayo leo wakati akizindua ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa Megawati 240 cha Kinyerezi II Jijini Dar es salaam ambapo katika kipindi cha siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani kampuni hiyo tayari imeshalipwa kiasi cha shilingi Bilioni 36.
Kampuni hiyo ya IPTL ambayo inamilikiwa na Habirnder Seth Singh inalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) shilingi milioni 40 hadi shilingi milioni 104 kwa siku kama gharama ya kuuziana umeme kati ya kampuni hizo mbili.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni hiyo Joseph Makandege, malipo hayo yanahusisha gharama za uwekezaji ambazo ni senti mbili kwa unit moja ya umeme na senti 28  kama gharama za uzalishaji.
Amesema “IPTL inaiuzia TANESCO zaidi ya megawati 85 kwa siku na malipo yote yanakatwa kodi ya Ongezeko la Thamani yaani VAT.
Naye Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe hivi karibuni alimtaka Rais Magufuli kumaliza kile alichodai kuwa ni ufisadi wa TANESCO wa kuilipa kampuni hiyo kiasi hicho kikubwa cha fedha ambapo ni takribani bilioni 36 zimeshalipwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani.
Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini.

Monday, 14 March 2016

Picha: Ronaldo Ajiunga Na Mwanae Kumpa Sapoti Dogo Ayman Wa Syria

Picha: Ronaldo Ajiunga Na Mwanae Kumpa Sapoti Dogo Ayman Wa Syria

Tarehe March 14, 2016
Ronaldo akiwa na mtoto wake Christiano jr wakiwa wameshika picha ya mtoto Raia wa Syria anayejulikana kwa jina la Ayman mwenye umri wa miaka mitano
Ronaldo akiwa na mtoto wake Christiano jr wakiwa wameshika picha ya mtoto Raia wa Syria anayejulikana kwa jina la Ayman mwenye umri wa miaka mitano
Kuonyesha ushirikiano katika suala la kupinga vita vnavyoendelea nchini Syria,Winga matata wa klabu ya Real Madrid na Ureno Christiano Ronaldo amepost picha katika matandao wake wa kijamii akiwa na mwanae huku wakiwa wameshika picha ya mtoto mwenye umri wa miaka mitano  aliyejulikana kwa jina la Ayman ambaye anapenda kucheza soka.

Picha: Ona Watanashati Azam Walivyotua Bongo

Picha: Ona Watanashati Azam Walivyotua Bongo

Tarehe March 14, 2016
Kikosi cha Azam kikiwa tayari kuondoka nchini Afrika ya Kusini
Kikosi cha Azam kikiwa tayari kuondoka nchini Afrika ya Kusini
Timu ya Azam FC ilipoondoka jijini Johannesburg na kuwasili Dar es Salaam leo saa 12.15 jioni ikitoka kufanya makubwa nchini Afrika Kusini kwa kuichapa Bidvest Wits mabao 3-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
wachezaji wa Azam wakiwa Airpot
wachezaji wa Azam wakiwa Airpot
wakiwa wamewasili Dar es Salaam
wakiwa wamewasili Dar es Salaam

Samatta Kafanya Kweli Genk,Yaitungua Oostende 4-1

Samatta Kafanya Kweli Genk,Yaitungua Oostende 4-1

Tarehe March 14, 2016
Mbwana Samatta
Mbwana Samatta
Mbwana Ally Samatta anayekipiga huko Genk ya Ubelgiji  ameifungia bao ikishinda 4-1 dhidi ya KV Oostende katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji, maarufu kama Pro League usiku huu Uwanja wa Cristal Arena mjini Genk.
Samatta aliyeanza kwa mara ya kwanza leo tangu asajiliwe Genk Januari kutoka TP Mazembe ya DRC, alifunga bao hilo dakika ya 24 kwa kichwa akiunganisha krosi ya mshambuliaji wa Jamaica, Leon Bailey.

PSG-9 Troyes-0 :Zlatan Ibrahimovic Atoa Mpya Na Mpira Wake Wa Hat-Trick Alivyoondoka Na Mpira Wake

PSG-9 Troyes-0 :Zlatan Ibrahimovic Atoa Mpya Na Mpira Wake Wa Hat-Trick Alivyoondoka Na Mpira Wake

Tarehe March 14, 2016
 Zlatan Ibrahimovic akiwa amelala na mpira wake
Zlatan Ibrahimovic akiwa amelala na mpira wake
Mshambuliaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic akiondoka na mpira baada ya kufunga mabao manne katika ushindi wa 9-0 ugenini dhidi ya Troyes kwenye mchezo wa Ligue 1 ya Ufaransa usiku wa leo Uwanja wa Aube. Mabao mengine ya PSG yamefungwa na Edinson Cavani, Adrien Rabiot, Dreyer na Saunier aliyejifunga.
Baada ya kupokea mpira wake Ibrahimovic alipost picha katika mtando wa kijamii wa facebook akiwa amekaa nao kwenye ndege huku ameufung mkanda kama abiria wa kawaida
 Zlatan Ibrahimovic
Zlatan Ibrahimovic

Treni Reli Ya Kati Yaanza Kupiga Mzigo Tena

Treni Reli Ya Kati Yaanza Kupiga Mzigo Tena

Tarehe March 14, 2016
reni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
reni ya Mizigo ikiwa tayari kuanza safari katika eneo la Kidete Wilayani Kilosa, kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa eneo hilo, uliodumu kwa takriban miezi miwili na hivyo kurudisha mawasiliano ya reli kati ya Mkoa wa Morogoro na Dodoma.
Huduma ya usafiri wa reli ya kati iliyokuwa imesimama kwa takribani miezi miwili sasa imerejea katika hali yake ya kawaida kufuatia kukamilika kwa ukarabati wa reli hiyo katika eneo la Kidete Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema hayo baada ya kukagua na kuridhika na ukarabati uliofanywa katika maeneo ya Magulu, Munisagara, Mzaganza na kidete Wilayani Kilosa.
“Hakikisheni mnailinda reli hii kwa manufaa yenu na ya Taifa, leo hii reli iko vizuri na treni ya kwanza kutoka Dar es Salaam kwenda bara itapita na kumaliza changamoto ya usafiri iliyokuwa inawakabili wananchi wanaotumiia reli hii,” amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo ya Kilosa, Magulu, Munisagara, Mzaganza, Kidete, Godegode na Gulwe ambao maeneo yao yanakabiliwa na mafuriko ya mto Mkondoa kuacha kilimo cha kuelekeza maji kwenye reli bali washirikiane na Serikali kudhibiti maji hayo kwenda kwenye hifadhi ya reli.
Amesema Shirika la Reli Tanzania (TRL) litaendelea kuhakikisha kuwa treni inayopita kwenye reli ya kati inapata mzigo mwingi wa kusafirisha kutoka bandarini za Tanga na Dar Es Salaam kuelekea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Mpanda na hivyo kuwataka wafanyabiashara watumie fursa hiyo ili kupunguza mzigo unaosafirishwa kwa njia ya barabara.
Pia Profesa Mbarawa ametembelea bwawa la Kidete linaloelezwa kuwa chanzo cha mafuriko pindi linapojaa wakati wa mvua za vuli na masika katika mikoa ya Dodoma na Iringa.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele amemhakikishia Profesa Mbarawa kuwa ofisi yake itafuatilia kwa karibu malalamiko ya wananchi wanaoishi karibu na reli ya kati ili kuyapatia ufumbuzi na kuwataka wananchi hao kuitumia fursa ya kuwa karibu na reli kunufaika kiuchumi.
Takribani Shilingi million 926 zimetumika katika ukarabati wa reli hiyo kufuatia uharibifu uliotokea mwezi Januari na kukata mawasiliano ya reli kati ya mikoa ya Dodoma na Morogoro na kusababisha safari za treni kutoka bara kuishia Dodoma.

Basi La Leina Tours Likitokea Kahama Lapata Ajali Dar

Basi La Leina Tours Likitokea Kahama Lapata Ajali Dar

Tarehe March 14, 2016
Basi la Leina Tours mara baada ya kupata ajali.
Basi la Leina Tours mara baada ya kupata ajali.
Watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa kufuatia basi la Leina Tours kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Kimara Bucha usiku wa kuamkia  leo jijini Dar es salaam.
Chanzo cha ajali hiyo bado  hakijafahamika hadi sasa  ambapo  Basi hilo lilikuwa likitokea Kahama kwenda Dar es Salaam.
Majeruhi katika ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala pamoja na wengine kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Jitihada za uokoaji zikiendelea baada ya basi hilo kupata ajali.
Jitihada za uokoaji zikiendelea baada ya basi hilo kupata ajali.

Yaliyojiri Wakati Katibu Mkuu Mpya Chadema Akitambulishwa Mwanza

Yaliyojiri Wakati Katibu Mkuu Mpya Chadema Akitambulishwa Mwanza

Tarehe March 14, 2016
Mafuriko ya wananchi katika mkutano wa Chadema.
Mafuriko ya wananchi katika mkutano wa Chadema.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kimemtambulisha  Katibu mkuu CHADEMA Dr Vicent Mashinji  kwenye viwanja  vya   Furahisha jijini  Mwanza.
Kwa matukio zaidi katika picha tazama hapa..
Aliyekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa (kulia) akiwa na Katibu mpya Dr.Vicent Mashinji.
Aliyekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa (kulia) akiwa na Katibu mpya Dr.Vicent Mashinji.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Baadhi ya wanachama wa Chadema katika mkutano huo.
Baadhi ya wanachama wa Chadema katika mkutano huo.
4
Dr.Mashinji akiwasalimia wananchi katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana.
Dr.Mashinji akiwasalimia wananchi katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza jana.

clouds stream