Ban Ki-moon akamilisha muhula wake katika Umoja wa Mataifa ambapo amehudumu kama katibu mkuu
Saturday, 31 December 2016
CHELSEA YAENDELEA KUMFUKUZA MWIZI KIMYAKIMYA, YAITWANGA STOKE CITY 4-2 NA KUJISHINDILIA KILELENI
Chelsea: Courtois 6, Azpilicueta 6, Luiz 6, Cahill 6.5, Moses 5 (Ivanovic 82, 5), Kante 6, Fabregas 8 (Matic 73, 6), Alonso 6, Willian 8.5 (Chalobah 84), Hazard 8, Costa 7.5
Subs: Begovic, Zouma, Loftus-Cheek, Batshuayi.
Goals: Cahill 34, Willian 57, 65, Costa 85.
Booked: Moses, Fabregas, Alonso.
Stoke City: Grant 8, Johnson 6, Shawcross 6, Martins Indi 7, Diouf 5, Allen 6, Adam 7, Pieters 7, Afellay 4(Bojan 6.5), Crouch 7, Shaqiri 5(Imbula 6)
Subs: Bardsley, Whelan, Bony, Imbula, Given, Krkic, Sobhi.
Goals: Martins-Indi 46, Crouch 64.
Booked: Diouf, Adam.
Referee: Robert Madley 6
Ban Ki-moon akamilisha muda wake UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayestaafu, Ban Ki-moon, ameondoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa , kwa mara ya mwisho baada ya muhula wake wa mwongo mzima.
Bwana Ban Ki-moon anamaliza kazi rasmi, mwaka mpya unapoingia.
Alisema atakuwako Medani ya Times mjini New York, kuukaribisha mwaka, na kuadhimisha kumaliza kazi.
Alifanya mzaha kwamba mamilioni ya watu watakuwa wakiangalia wakati akipoteza kibarua chake.
Pahala pake panachukuliwa na waziri mkuu wa zamani wa Ureno, Antonio Guterres.
Bwana Ban anatarajiwa kurudi Korea Kusini, ambako kuna tetesi, kwamba huenda akagombea nafasi ya Rais Park Geun-Hye, ambaye anashtakiwa.
Makubaliano ya kisiasa nchini DR Congo yakwama
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila
Makubaliano ya kisiasa kati ya serikali na upinzani nchini DR Congo ili kumaliza mgogoro wa kisiasa yamekwama katika dakika ya mwisho.
Muhula wa rais Joseph Kabila ulikamilika mapema mwezi huu ,lakini uchaguzi umeahirishwa huku makumi ya watu wakipoteza maisha yao katika maandamano.
Wapatanishi kutoka kanisa Katoliki awali walikuwa wamesema kwamba pande hizo mbili zilikuwa zinakaribia maafikiano ambapo rais Kabila atasalia mamlakani hadi uchaguzi utakapoandaliwa mwishoni mwa 2017 .
Hatahivyo baadhi ya makubaliano hayakuafikiwa hivyobasi kuahirisha sherehe ya kutia kandarasi makubaliano hayo huku mazungumzo yakiendelea.
Wednesday, 28 December 2016
ULIISIKIA HII YA MAMBO KUMUENDEA POA IBRAHIM AJIBU KULE MISRI?
Kiungo Ibrahim Ajibu sasa ana hadi nafasi ya asilimia 70 kupata nafasi ya kuitumikia Haras El Hodood ya Misri.
Ajibu amepasi vipimo vya afya, maana yake nafasi ya kukipiga nchini Misri ni kubwa kama ambavyo taarifa zimeeleza.
Amepewa muda wa wiki moja na nusu wa majaribio na unaisha Desemba 31.
Abdel Haidar anayejishughulisha na masuala ya afya katika timu hiyo ya Jeshi la Misri, amezungumza na Championi kutoka Alexandria Misri na kusema hiyo ni hatua kubwa kwa Ajibu.
“Amefuzu vipimo vya afya. Hii ni hatua kubwa zaidi, sasa yamebaki masuala baadhi ambayo yanamhusu kocha.
“Kocha sasa anaendelea naye na mwisho atatoa maelezo kuhusiana na suala la vipimo vya afya,” alisema Haidar.
Wakati Haidar anasema hivyo, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema wanasubiri kuhusiana na Ajibu hadi Desemaba 31.
“Taarifa za maendeleo yake tunazifuatilia kwa karibu kabisa. Tunajua hilo la vipimo vya afya lakini sisi hatutalizungumzia kwa kuwa anaendelea na majaribio hadi Desemba 31.
“Baada ya hapo, tunaamini timu hiyo itaanza mawasiliano nasi. Hivyo nafikiri mgevuta subira,” alisema Dewji maarufu mama Gwiji ambaye amewahi kuwa katibu mwenezi wa kikosi cha Simba kilichotinga fainali ya Caf mwaka 1993 na katibu mkuu wakati Simba ikiing’oa Zamalek Klabu Bingwa Afrika mwaka 2003.
Kama Ajibu atakuwa amefuzu vipimo vya afya maana yake ni sawa na kufuzu kuichezea timu hiyo kwa asilimia 80.
Hata hivyo, kama atafuzu na kujiunga nayo atakuwa na kazi ngumu kuhakikisha anapambana kuisaidia kurejea Ligi Kuu Misri baada ya kuwa imeshuka msimu uliopita.
Kwa Tanzania, Haras El Hood kwa kile kipigo cha mabao 5-1 ilichokitoa kwa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa.
Yanga Wailaza Ndanda 4-0 Shamba La Bibi
Domald Ngoma akiwahi kuupiga mpira mbele ya beki wa Ndanda, Bakari Mtama uwanja wa uhuru Dar es salaam.
Klabu ya Yanga leo imejipatia pointi tatu muhimu baada ya kuifunga Ndanda ya Mtwara mabao 40 katika mchezo wa ligi kuu Vodacom uliochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dares salaam.
Kufuatia ushindi huo Yanga SC inafikisha pointi 40 ikizidiwa pointi moja na watani wao, Simba SC ambao kesho watacheza na klabu ya Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo Mshambuliaji Donald Dombo Ngoma alifunga mabao mawili mfululizo, Amissi Joselyn Tambwe alifunga bao la tatu na beki Mtogo, Vincent Bossou akafunga la nne kipindi cha pili.
AZAM FC IMEWATIMUA MAKOCHA WAKE WOTE RAIA WA HISPANIA
Azam FC imemtimua Kocha wake Mkuu, Zeben Hernandez.
Zeben na makocha wengine raia wa Hispania, wametimuliwa kazi leo baada ya Azam FC kwenda mwendo wa kusuasua.
Azam FC iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17.
Katika mechi 17 za Ligi Kuu Bara, Azam FC imechinda mechi saba, imepoteza nne na sare sita, hali ambayo wazi inaonekana kutoufurahisha uongozi wa Azam FC hata kidogo.
Afariki dunia, siku moja baada ya kifo cha binti yake
Debbie Reynolds na binti yake Carrie Fisher
Msanii wa Hollywood Debbie Reynolds amefariki akiwa na umri wa miaka 84, siku moja tu baada ya kifo cha binti yake, Carrie Fisher.
Alikimbizwa hospital baada ya kushikwa na ugonjwa nyumbani kwa mtoto wake wa kume huko Beverly Hills.
Debbie Reynolds ama Mary Frances, umaarufu wake ulikuwa mwaka 52, wakati alipofanya tamasha sambamba na Gene Kelly katika wimbo uliojulikana kama ''..Singin' in the Rain..''
Alikuwa pia ni muigizaji wa sanaa ya vichekesho
Netanyahu aipinga hotuba ya Kerry kuhusu makazi
Ujenzi wa Makaazi ya Wayahudi
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani John Kerry ameutetea uamuzi wa nchi yake wa kuliwezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuupitisha uamuzi wa wiki iliyopita, kutangaza Makazi ya Wayahudi kuwa ni kitendo kilicho kinyume na sheria.
Waziri Kerry amesema hatua hiyo ina nia ya kulinda uamuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea.
Amesema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.
Lakini hata hivyo, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea kuvunjwa moyo na hotuba iliyotolewa na John Kerry kuhusiana na jambo hilo, ambayo ameielezea kuwa haijakaa sawa.
Amesema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubali uwepo wa Israel.
Kwa upande wake, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amesema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makaazi mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.
Tuesday, 27 December 2016
30 Wafa Maji Baada Ya Boti Kuzama
Polisi nchini Uganda wanasema takriban watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi mwa taifa hilo.
Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.
Mafisa wa polisi wamesema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupita kiasi huku abiria wakiimba na kupiga tarumbeta.
Mkulima Apigwa Mshale Na Kutokea Shingoni Mikumi, Prof. Jay Atoa Tamko
Mkulima mmoja wa Kitongoji cha Upangwani Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata ya Masanze JImbo la Mikumi Morogoro aliyepigwa mkuki.(Tahadhari Picha zinatisha)
Migogoro ya Wakulima na Wafugaji isiyokwisha Mkoani Morogoro imepelekea mkulima aliyejulikana kwa jina la Augustino Mtitu kupigwa mshale mdomoni na kutokea shingoni na Mfugaji wa Kimasai jana.
Kwa mujibu wa tarifa ya Katibu Ofisi ya Mbunge Prof. Jay Bw. Robert A. Galamona imebainisha kuwa Kijana huyo Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng’ombe wasiharibu mazao shambani kwake.
Mkulima huyo kwa alikimbizwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae alipelekwa hospitali ya mkoa Morogoro ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na matibabu zaidi.
Aidha, Kipande cha mti kinachoonekana (pichani) mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali, Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi, Profesa Jay imetoa wito kwa Serikali kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa.
Mkuliwa aliyepigwa mshale mdomoni na kutokezea Shingoni
Mkulima huyo akipelekwa Hospitali.
Sunday, 25 December 2016
Msako mkali ndege ya Urusi waendelea
Rais Vladmir Putin wa Urusi
Msako mkali unaendelea kutafuta miili ya askari wa Urusi walio waliokuwemo kwenye ndege iliyopata ajali kwenye bahari nyeusi iliyoanguka na kuua askri wote tisni na mbili waliokuwemo .
Wafanyakazi zaidi ya elfu tatu, wakiwemo wazamiaji zaidi ya elfu moja wako kwenye harakati za utafutaji manusura ama maiti za askari hao katika eneo la tukio.
Ndege iliyokuwa imebeba askari hao ilianguka dakika tatu baada ya kuanza safari kutoka katika mji wa Sochi ikiwa njiani kuelekea nchini Syria.
Abiria walio wengi walikuwa ni askari wa Urusi waliokuwa katika shamra shamra za sherehe za tamasha la kimuziki la Alexandrov wanaojulikana kama kwaya ya jeshi jekundu.
Ibada ya kuwaombea marehemu hao imefanyika mjini Sochi na miji mingine tofauti tofauti kabla ya siku maalumu ya Jumatatu iliyotangazwa kuwa ya maombolezo.
Mamlaka nchini Urusi zimetoa tamko kuwa zinafahamu fika wapi ilipo ndege hiyo katika bahari nyeusi. Mpaka sasa miili saba ya askari imepatikana .Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kuwepo kwa manusura wa ajali hiyo.
Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Urusi, Igor Konashenkov, amesema kwamba zoezi la utafutaji linaendelea.
Gereza kuu la Kigali lateketea kwa moto
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana.
Shughuli za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
Hilo Ni gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi.
Bado Ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu ya Kigali.
Magari ya zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Papa Francis: Ataka amani baina ya Israel na Palestina
Papa Francis ametoa wito kufanywe juhudi mpya kuleta amani baina ya Waisraeli na Wapalestina
Papa Francis ametoa wito kufanywe juhudi mpya kuleta amani baina ya Waisraeli na Wapalestina.
Katika hotuba yake ya Krismasi, aliyotoa Vatikani, Papa alizihimiza pande mbili zinazohusika, kujaribu kuazimia kuandika ukurasa mpya, na kumaliza chuki na kulipizana kisasi.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki pia ametaka kumalizwa kwa vita nchini Syria akisema ni wakati wa silaha kunyamazishwa.
Katika ujumbe wake wa Krismasi kiongozi wa kanisa la Anglikana duniani Askofu mkuu Justin Welby amewataka raia kumuomba mungu ili kukabiliana na ugaidi.
Aidha amesema kuwa mengi yanapaswa kufanya ili kukabiliana na ukosefu wa usawa.
Thursday, 22 December 2016
Watu 34 wadaiwa kufariki katika maandamano DR Congo
Maandamano nchini DRC ambapo takriban watu 34 wanahofiwa kufariki kulingana na shirika la Human Rights Watch
Shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vikosi vya usalama ini DR Congo vimewaua takriban watu 34 wakati wa maandamano wiki hii.
Mazungumzo yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili kujaribu kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila ambaye alikataa kuondoka madarakani wakati muda wake ulipokamilika siku ya Jumatatu.
Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine 17 wameuawa kaskazini magharibi mwa Congo.
Maafisa wa polisi wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu linaloamini kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa dunia.
Wakati huohuo Mamlaka nchini DRCongo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Lubumbashi.
Meya wa mji huo anasema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu, japo wenyeji wa mji huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.
Subscribe to:
Posts (Atom)