Tuesday, 31 January 2017

Watford wailaza Arsenal 2-1

Mara ya mwisho Watford kuifunga Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa 1988

Mara ya mwisho Watford kuifunga Arsenal katika uwanja wake wa nyumbani ilikuwa 1988
img-20161130-wa0008

Matumaini ya klabu ya Arsenal kutwaa ubingwa wa England yanaanza kufifia baada ya kuchapwa na Watford 2-1 na hii ni Emirates.

Mlinzi wa zamani wa Tottenham Younes Kaboul alianza kuiandikia Watford goli la kwanza dakika ya 10 baada ya kuachia shuti kali lililomgonga Aaron Ramsey na kutinga nyavuni.

Dakika mbili na sekunde 57 baadaye Troy Deeney akaiandikia goli la pili Wtaford baada ya mpira uliopigwa na Etienne Capoue kupanguliwa na mlinda mlango Petr Cech na kisha kumkuta Troy aliyendika bao safi.

Kipindi cha pili Arsenal walianza kwa kasi na kujipatia goli la kufutia machozi kutoka kwa Alex Iwobi baada ya kupanda pande safi lililochongwa na Alexis Sanchez.

Kwa mara ya mwisho Arsenal kushinda kikombe cha ligi kuu England ilikuwa msimu wa mwaka 2003-04 na kwa sasa wapo nyuma kwa alama tisa dhidi ya vinara Chelsea ambao wametoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Liverpool.

Trump amteua jaji wa mahakama kuu Neil Gorsuch

Rais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama kuu

Rais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama kuu
img-20161130-wa0008

Rais Donald Trump amemteua Neil Gorsuch kujaza nafasi katika mahakama kuu kwa mwaka mmoja .

Bw Gorsuch mwenye umri wa miaka 49 ni jaji katika mahakama ya rufaa mjini Denver.

Jaji huyo hatarajiwi kutoa hukumu juu ya utoaji mimba na ndoa za wapenzi wa jinsi moja.

Hata hivyo uteuzi wake unasubiri kuidhinishwa na bunge la Seneti.

Maseneta wa Democratic wametishia kumfungia nje mgombea yeyote atakayeonekana kuwa mhafidhina.

Waandamanaji wapinga uteuzi wa Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama ya juuWaandamanaji wapinga uteuzi wa Neil Gorsuch kuwa jaji wa mahakama ya juu

Awali maseneta hao walipinga uteuzi wa watu watatu uliofanywa na rais kuchukua wadhifa wa waziri.

Walisusia vikao vya kuwaidhinisha mawaziri wa fedha na afya waliopendekezwa na kuchelewesha upigaji kura wa kumuidhinisha Jeff Sessions aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria mkuu.

AU kujiondoa katika mahakama ya ICC

Jengo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC

Jengo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC
img-20161130-wa0008

Umoja wa Afrika umeunga mkono mpango wa kujiondoa kwa pamoja katika mahakama ya ICC ambayo mataifa mengi ya Afrika yanahisi inawalenga viongozi wa bara la Afrika pekee.

Uamuzi huo uliochukuliwa katika kikao cha faragha haujahalalisha hatua hiyo.

Viongozi wa Afrika wanasema kuwa mahakama hiyo ilikosea kumlenga rais wa Sudan Omar El Bashir kwa mauaji ya Darfur na Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Afrika katika kikao chao katika makao makuu ya Umoja wa Afrika AU
Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Afrika katika kikao chao katika makao makuu ya Umoja wa Afrika AU

Mpango huo unapendekeza kwamba mataifa ya Afrika yanafaa kuimarisha mahakama zake na kupanua uwezo wa mahakama ya Afrika kuhusu haki na haki za binaadamu.

Sunday, 29 January 2017

Liverpool kumsafirisha Mane kwa ndege ya kibinafsi

Sadio Mane ameifungia Livepool mabao 8 msimu huu

Sadio Mane ameifungia Livepool mabao 8 msimu huu
img-20161130-wa0008

Liverpool wamepanga kumsafirisha kwa ndege ya kibinafsi mshambuliaji Sadio Mane, kutoka michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon, ili kumpa nafasi ya kushiriki mechi na viongozi wa Ligi Chelsea.

Mane atasafirishwa baada ya Senegal kupoteza tena kwa mabao 5-4 ilipocheza na Cameroon wakati wa mechi ya robo fainali siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 24, alipoteza penalti muhimu wakati wa mechi hiyo.

Liverpool imeshinda mechi moja tu tangu aondoke kushiriki mechi za kimataifa.

Walishindwa na klabu ya zamani ya Mane kwenye kombe la EFL siku ya Jumatano na kuondolewa kutoka kombe la FA walipocheza na Wolves.

Westham:Payet alikosa nidhamu

Payet alijiunga na Westham akitokea Marseille June 2015

Payet alijiunga na Westham akitokea Marseille June 2015
img-20161130-wa0008

Klabu ya Westham imesema kuwa aliyekuwa kiungo wake Dimitri Payet amekosa nidhamu na upendo kwa timu hiyo baada ya kujiunga na klabu ya Marseille ya Ufaransa kwa Euro milioni 25.

Wagonga nyundo hao wa London wamesema kuwa hawakutaka kumuuza Payet huku mwenyekiti wa klabu hiyo David Sullivan akiongeza kuwa walitamani kuendelea kubaki nae.

Sullivan amesema kuwa sababu ya kumuuza ni ili kutokuondoa umoja wa wachezaji jambo ambalo ni muhimu zaidi.

Payet amejiunga na Marseille kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

Treni Ya Abiria EXPRESS Yapata Ajali Ikitokea Kigoma



IMG-20170129-WA0022
img-20161130-wa0008

Treni ya abiria ya EXPRESS imepata ajali na kupinduka ikiwa inatokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam jana katika maeneo ya Ruvu, Mkoa wa Pwani ikiwa ni kilometa kadhaa kabla ya kufika Jijini Dar es Salaam.

Mabehewa zaidi ya kumi yalipinduka na kulazimu abiria kupitia madirishani nili kunusuru maisha yao huku kukiwa bado hakuna kifo kilichoripotiwa kutokea.

IMG-20170129-WA0020IMG-20170129-WA0017 (1)IMG-20170129-WA0016IMG-20170129-WA0015

Trump ajitetea kuhusu sera ya usafiri aliyoianzisha Ijumaa

Trump amekosolewa vikali kwa sera hiyo

Trump amekosolewa vikali kwa sera hiyo
img-20161130-wa0008

Rais wa Marekani Donald Trump ametetea marufuku yake ya muda ya kusafiri kwa watu wanaotoka katika nchi saba ambazo ni za kiislamu baada ya watu kuukosoa uamuzi huo huku wengine wakiandamana.

Katika taarifa ya maandishi, bwana Trump amevilaumu vyombo vya habari kwa kupotosha taarifa kwamba marufuku hiyo ni kwa waislamu.

Amesema viza zitatolewa kwa wasafiri kutoka nchi zote ndani ya siku tisini.

Katika hali inayoonekana kulegeza msimamo wa amri ya kiutendaji iliyopitishwa siku ya Ijumaa, Reince Priebus, ambae ni kiongozi wa wafanyakazi wa serikali amesema marufuku hiyo haitawahusu wenye kuhodhi kadi za green, ambao wana haki ya kisheria kuishi nchini Marekani.

Mhariri wa BBC kaskazini mwa marekani amesema ikulu ya marekani imekosolewa vikali kwa sera hiyo.

Mamia ya watu wameandamana kupinga hatua hiyo
Mamia ya watu wameandamana kupinga hatua hiyo

Wakati huo huo, maelfu ya waandamanaji wanaopinga amri hiyo ya Trump kwa mara nyengine wameandamana katika viwanja vya ndege na sehemu nyinginezo nchini Marekani.

Waandamanaji wamepita katika miji ya Boston, New York na karibu na ikulu mjini Washington.

Mwanasiasa mwandamizi wa Republican ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya senate ya mambo ya nje, Bob Corker, amesema amri hiyo ya Rais utekelezaji wake haukuwa na ufanisi,hivyo kutaka mabadiliko ya haraka kufanywa.

Washauri wakuu wa masuala ya sheria kutoka majimbo kumi na sita nchini Marekani wameshutumu marufuku hiyo ya kusafiri na kusema haiko kisheria, imekiuka maadili ya kimarekani na imekiuka katiba ya nchi.

Kwa upande wake, Hakeem Jeffries kutoka chama cha Demokrat, alikuwa ni miongoni mwa walioandamana katika uwanja wa ndege wa JFK mjini New York.

Amesema idadi kubwa ya watu wanazuiwa kinyume cha sheria katika uwanja wa ndege.

Wednesday, 25 January 2017

Ghana, Misri zasonga mbele Afcon

Misri

Wachezaji wa Misri wakishangilia goli lililofungwa na Mohamed Salah
img-20161130-wa0008

Michezo miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya Afcon 2017 imemalizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana na hivyo kuongoza kundi D kwa alama 7 huku Ghana wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Bao la ushindi la mafarao wa Misri lilifugwa na nyota wao Mohamed Salah, katika dakika ya 11 ya mchezo kwa mkwaju mkali wa mpira wa kutenga uliokwenda moja kwa moja nyavuni.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya Uganda walitoshana nguvu na Mali kwa kufungana bao 1-1.

Michezo ya hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa jumamosi ya terehe 28 kwa Burkina Faso kucheza na Tunisia huku Senega wakicheza na Cameroon.

Jumapili kutacheza michezo miwili ya robo fainali ya pili kwa DR Congo kuchuana na Ghana nao Misri wakipimana ubavu na Morroco.

Southampton yatinga fainali EFL

Saint

Wachezaji wa Southampton wakishangilia goli
img-20161130-wa0008

Timu ya Southampton ama watakatifu wametinga katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL).

Watakatifu hao wametinga hatua hiyo baada ya kuichapa Liverpool kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili mchezo ulifanyika katika dimba la Anfield .

Bao pekee lililoipa timu hiyo ushindi liliwekwa kambani na mshambuliaji Shane Long katika dakika za lala salama za mchezo huo.

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Liverpool walifungwa kwa bao moja kwa bila hivyo Southampton wanawaondosha kwa jumla ya mabao 2-0.

Nusu fainali nyingine ya pili inachezwa leo hii ambapo Hull City watakua wenyeji wa Manchester United katika mchezo wa kwanza United walishinda kwa mabao 2-0 .

Mchezo wa fainali utafanyika tarehe 26/2 mwaka huu katika uwanja wa Wembley.

Southampton yatinga fainali EFL

Saint

Wachezaji wa Southampton wakishangilia goli
img-20161130-wa0008

Timu ya Southampton ama watakatifu wametinga katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL).

Watakatifu hao wametinga hatua hiyo baada ya kuichapa Liverpool kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili mchezo ulifanyika katika dimba la Anfield .

Bao pekee lililoipa timu hiyo ushindi liliwekwa kambani na mshambuliaji Shane Long katika dakika za lala salama za mchezo huo.

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Liverpool walifungwa kwa bao moja kwa bila hivyo Southampton wanawaondosha kwa jumla ya mabao 2-0.

Nusu fainali nyingine ya pili inachezwa leo hii ambapo Hull City watakua wenyeji wa Manchester United katika mchezo wa kwanza United walishinda kwa mabao 2-0 .

Mchezo wa fainali utafanyika tarehe 26/2 mwaka huu katika uwanja wa Wembley.

Marekani kujenga ukuta mara moja kati yake na Mexico


Marekani kujenga ukuta kuidhibiti MexicoMarekani kujenga ukuta kuidhibiti Mexicoimg-20161130-wa0008

Rais wa Marekani Donald Trump amesema serikali yake itaanza mara moja kushughulikia ujenzi wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi yake kubwa aliyoiweka wakati wa kampeni za uchaguzi.

Akizungumza na wafanyakazi wanaohusika na usalama wa taifa, Donald Trump amesema ukuta huo utazuia wahamiaji haramu na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, kwa kuongeza kuwa siku zao zimekwisha wao kuishi na kufanya uharibifu.

Amesisitiza kauli yake ya kutaka Mexico kulipia ukuta huo, licha ya Mexico kukataa kufanya hivyo.

Wakati Marekani ikiweka msimamo wake huo, serikali na raia wa Mexico nao wameingilia kati kutetea nchi yao.

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto naye anashinikizwa kufuta mkutano wake na Rais Trump unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Washngton, ikiwa kama ni kujibu uamuzi huo wa Marekani kujenga ukuta.

Meya wa mji wa Mexico City Miguel Espinosa amesema kujengwa kwa ukuta huo, Marekani itajitenga yenyewe sio tu na Mexico bali na Amerika ya kusini yote.

Wakati huohuo, Rais wa Marekani amesema kuwa ana amini kwamba njia ya mateso inayotumika kuwahoji washukiwa wa ugaidi inafanya kazi vilivyo.

Akihojiwa na kituo cha Televisheni cha ABC, amesema Marekani inapaswa kupambana kwa nguvu zote katika kujibu mateso yaliyofanywa na kundi la Islamic State kwenye eneo la mashariki ya kati.

Mtangulizi wake Rais Barack Obama alipiga marufuku njia hiyo ya kutumia maji kuwahoji washukiwa kutokana na kuleta mabishano, mbinu hiyo ilikuwa ikitumika wakati wa utawala wa George Bush.

Saturday, 21 January 2017

Ivory Coast na DRC watoka sare ya mabao 2-2

Ivory Coast wakisherehekea bao lao la kwanza

Ivory Coast wakisherehekea bao lao la kwanza
img-20161130-wa0008

Mabingwa Ivory Coast walijikakamua na kutoka sare ya mabao mawili na DRC na kufufua matumaini yao ya kufika robo fainali ya kombe la taifa bingwa barani Afrika.

DRC ndiyo iliona lango kwanza kupitia mpira uliorushwa na Neesken Kebano lakini bao hilo lilisawazishwa baadaye na Wilfired Bony aliyefunga kwa njia ya kichwa.

DRC tena ilifanikiwa kufunga bao la pili dakika mbili baada ya Ivory Coast kusawazisha kupitia kwa Junior Kabananga.

Ivory Coast bila kusita kwa mara nyingine walisawazisha bao hilo kupitia mkwaju

Gambia: Jammeh atangaza ataondoka madarakani

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow
img-20161130-wa0008

Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.

Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya "hata tone moja la damu" kumwagika.

Alitoa tangazo hilo baada ya mazungumzo ya saa kadha kati yake na wapatanishi wa Afrika Magharibi.

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yaliyoafikiwa.

Bw Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Desemba na mrithi wake Adama Barrow tayari ameshaapishwa.

Bw Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.

Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua Bw Jammeh madarakani.

Bw Adama Barrow, aliapishwa kuwa rais katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal Alhamisi
Bw Adama Barrow, aliapishwa kuwa rais katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal Alhamisi

Uamuzi wa Jammeh kung'atuka aliufanya baada ya kufanya mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania waliofika mjini Banjul Ijumaa kujaribu kumshawishi kuondoka madarakani kwa amani.

"Nimeamua leo, nikiwa na dhamiri njema, kuachia uongozi wa taifa hili kubwa nikiwa na shukrani zisizo na kikomo kwa raia wa Gambia," amesema.

"Namuahidi Allah na taifa lote kwamba masuala masuala ambayo yanatukabili kwa sasa yatatauliwa kwa njia ya amani"

Muda mfupi kabla ya Jammeh kutoa hotuba yake kwenye runinga, Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz alisema kwamba maafikiano yalikuwa yamefikiwa na kwamba Bw Jammeh angeondoka nchini humo.

Hakutoa taarifa zaidi.

Bw Jammeh alikuwa amepewa makataa ya saa sita mchana kuondoka madarakani la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Makataa hayo yalimalizika saa sita mchana, wakati mazungumzo kati yake na Abdel Aziz na Rais Alpha Conde wa Guinea yakianza. Aliomba aongezewe muda hadi saa kumi saa za Gambia.

Map of The Gambia

Dalili za kwanza za kupatikana kwa maafikiano zilianza kuonekana baadaye Ijumaa wakati mmoja wa wasaidizi wakuu wa rais mpya alipomwambia mwandishi wa BBC Umaru Fofana kwamba Bw Jammeh amekubali kuachia madarakani.Bw Jammeh alikuwa awali amekubali kushindwa lakini baadaye akabadili msimamo wake na kusema hangeng'atuka akisema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu na kasoro nyingi.

Aliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo hayo na baadaye akatangaza hali ya tahadhari ya siku 90.

Baadaye, alihakikisha bunge la nchi hiyo linapitisha sheria ya kumruhusu kuendelea kuongoza kwa muda hadi mwezi Mei.

Tume ya uchaguzi ilikiri kwamba kulikuwa na kasoro kwenye baadhi ya matokeo yaliyotangazwa, lakini ikasema kasoro hizo hazingebadilisha ushindi wa Bw Barrow.

Bw Jammeh awali alikuwa ameappa kuendelea kuongoza hadi uchaguzi mpya ufanyike.

Mbona Senegal inaongoza kumkabili

Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.

Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh makataa ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.

Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.

Rais Macky Sall wa Senegal akiwa na Adama Barrow
Rais Macky Sall wa Senegal akiwa na Adama Barrow awali Ijumaa

Hii inaifanya vigumu kufikiria ni vipi wanaweza kuwashinda wanajeshi wa kanda hiyo, anasema mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama Afrika Tomi Oladipo.Nigeria imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.Ghana pia inachangia wanajeshi.

Trump Ala Kiapo Rasmi Na Kuwa Rais Wa 45 Wa Marekani

C2oWeamWgAAI6im
Rais Obama na mkewe Michelle Obama wakimkaribisha Ikulu ya Marekani Rais mteule, DonaldTrump na mkewe Melanie TrumpRais Obama na mkewe Michelle Obama wakimkaribisha Ikulu ya Marekani Rais mteule, DonaldTrump na mkewe Melanie Trump
img-20161130-wa0008
Msafara wa Rais Obama na Rais mteule wa Marekani, DonaldTrump ukiwa umewasili CapitalHill ambapo shughuli ya kuapishwa Rais mteule imefanyika.
Msafara wa Rais Obama na Rais mteule wa Marekani, DonaldTrump ukiwa umewasili CapitalHill ambapo shughuli ya kuapishwa Rais mteule imefanyika.
Rais Mteule Donald Trump akila kiapo cha kuwa Rais wa 45 wa Marekani.
Rais Mteule Donald Trump akila kiapo cha kuwa Rais wa 45 wa Marekani huku familia ikishuhudia
C2oFyYQXAAEKUhU

Wednesday, 18 January 2017

Ghana yailaza Uganda

Nahodha wa kikosi cha Ghana Asamoah Gyan kulia aliyepata penalti

Nahodha wa kikosi cha Ghana Asamoah Gyan kulia aliyepata penalti
img-20161130-wa0008

Andre Ayew alifunga bao la pekee la mechi dhidi ya Uganda katika mechi ya ufunguzi ya kundi D katika michuano ya kombe la bara Afrika linaloendelea nchini Gabon.

Winga huyo wa klabu ya West Ham alifunga bao la penalti kunako dakika ya 32 baada ya nahodha Asamoah Gyan kuvutwa katika eneo la hatari.

Ghana pia ilitishia kupitia vichwa viwili vya Gyan ,huku Ayew na Christian Atsu wakimjaribu kipa wa Uganda Denis Onyango.

Uganda walikaribia lango la Ghana baada ya Faruku Miya kupiga mwamba wa goli lakini hawakuweza kusawazisha.

Mhubiri aliyetabiri kifo cha Mugabe akamatwa Zimbabwe

Rais Mugabe akihutubu Februari 27, 2016

Mugabe ameongoza Zimbabwe tangu 1980
img-20161130-wa0008

Maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Pasta Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi ameambia wanahabari.

Alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa

"Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo," Bw Mtisi aliambia AFP.

"Awali alishtakiwa kwa kudunisha na kukosea heshima mamlaka ya rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa kuwatusi watu wa asili fulani au dini fulani."

Pasta Mugadza, ambaye huhudumu katika mji wa Kariba kaskazini mwa nchi hiyo, aliandaa kikao na wanahabari wiki iliyopita ambapo alitabiri kwamba Mugabe angefariki Oktoba 17 mwaka huu.

Kumfanyia mzaha Rais Mugabe au kutoa unabii au ubashiri kumhusu ni jambo hatari nchini Zimbabwe.

Patrick MugadzaPATRICK MUGADZA
Patrick Mugadza amekamatwa mara kadha na polisi Zimbabwe

Nchini humo kuna sheria ambayo huharamisha "kudunisha mamlaka ya au kumtusi rais."

Mwaka 2015, Mugadza alikamatwa na kuzuiliwa kwa karibu mwezi mmoja baada ya kujitokeza hadharani na bango lililokuiwa na ujumbe uliomwambia Mugabe kwamba watu wamekuwa wakiteseka chini ya utawala wake.

Siku ya maadhimisho ya uhuru mwaka jana, alitoa mahubiri akiwa amejifungia kwenye boriti ya taa nje ya duka kubwa zaidi la kibiashara mjini Harare, akisema hiyo ilikuwa ishara ya raia kukandamizwa Zimbabwe.

Maandamano ya kupinga uongozi warais Mugabe Zimbabwe
Maandamano ya kupinga uongozi w arais Mugabe Zimbabwe

Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu 1980.

Kumekuwa na uvumi kuhusu afya yake na mara kwa mara husafiri mataifa ya Asia kwa matibabu.

Mawaziri watatu zaidi wajiuzulu Gambia

Yahya Jammeh

Yahya Jammeh
img-20161130-wa0008

Mawaziri watatu nchini Gambia wamajiuzulu wakati Rais Yahya Jammeh akipuuza wito wa kumtaka aondoke madarakani wakati muhula wake utakapokamilika siku ya Alhamisi.

Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni, fedha na biashara walijiuzulu kwa mujibu wa mtandao wa Fatu.

Wiki iliyopita waziri wa habari Sheriff Bojang na Alieu Jammeh wa michezo nao walijiuzulu.

Maelfu ya watu wamekuwa wakikimbia kwenda nchi jirani ya Senegal na hadi nchini Guinea-Bissau, kutokana na hofu kuwa huenda kukazuka ghasia, kufuatia hatua ya Rais Jammeh ya kukataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba.

Mfanyabiashara Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal ameapa kuchukua madaraka.

Barrow alimshinda Yahya Jammeh ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994.

clouds stream