Tuesday, 29 August 2017

Korea Kaskazini yaichokoza Japan

Kiongozi wa Korea kaskazini na makamanda wake

Kiongozi wa Korea kaskazini na makamanda wake.
IMG-20170426-WA0006

Korea kaskazini imerusha makombora yake ambayo yalipita Japan kabla ya kudondokea baharini.

Makombora hayo yalisafiri kuelekea mashariki karibu kilomita elfu moja juu ya kisiwa cha Japan cha Hokkaido.

Tukio hilo limechochea tahadhari ya hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.

Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa ardhini.

Wanajeshi wa Marekani na Japan wanafanya zoezi la pamoja katika eneo hilo la Hokkado, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in aliagiza uwezo wa utumiaji wa nguvu ili kujibu shambulio hilo.

Ndege nne za Korea Kusini zilifanya zoezi la kurusha makombora siku ya Tuesday.

Bwana Abe alisema kuwa amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote wamekubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.

Katika mfululizo wa majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta wasiwasi mkubwa.

Waziri mkuu wa japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.
Waziri mkuu wa japan Shinzo Abe amesema urushwaji huo wa makombora ambao haujawahi kutokea , umeleta kitisho kikubwa kwa taifa lake.

Katika siku za hivi karibuni Pyongyang ilijaribu kombora lake lililopata mafanikio kutokana na uwezo wake wa kuweza kuifikia Marekani na kuonyoa kuwa inasimamia mipango yake ya kushambulia kwa makombora eneo la Marekani la Guam, kilomita elfu mbiili kusini mashariki mwa Japan.

clouds stream