Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Jiji la Arusha limeingia katika ‘headlines’ kuanzia siku ya jana baada ya kuripotiwa kwa matukio ya utekaji watoto wadogo huku watekaji wakidai pesa kiasi cha milioni 4 ili kuwaachia.
Inadaiwa kuwa tayari watoto wanne wametekwa, na watekaji hao wanatumia njia ya karatasi iliyoandikwa kwa kalamu na mkono kuwasiliana na wazazi wa watoto hao na kudai pesa ili kuwaachia.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahalifu hao na kuwatia nguvuni huku akiwataka wananchi kuwa watulivu.