Tuesday, 22 August 2017

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini

A map showing Estcourt, KwaZulu-Natal

Wanaume 4 washtakiwa kwa kula nyama ya binadamu Afrika Kusini
IMG-20170426-WA0006

Wanaume wanne wamefikishwa kwenye mahakama ya Afrika Kusini kujibu mashtaka ya ulaji nyama ya binadamu, baada ya madai kuwa mmoja wao alifika katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.

Alipohojiwa zaidi mwanamume huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu.

Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu zilipatikana.

Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.

Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini magharibi mwa mji wa Durban.

Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa kuna uwezekano kuwa wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge kubwa.

Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa zao wametowewa kujitokeza.

Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu kadhaa.

Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa daktari wa kitamadunia.

clouds stream