Wednesday, 9 August 2017

POLISI WAMTWANGA RISASI MKE WA M / KITI SERIKALI YA MTAA

bastola
IMG-20170426-WA0006
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa Polisi Jijini Mwanza wamemfyatulia risasi ya mguuni mke wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mabatini, Majengo Mapya Jijini humo.
Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo ambapo hadi sasa, sababu na taarifa zaidi kuhusiana na tukio zitatolewa na mamlaka husika.
Majeruhi huyo, Editha Ntobi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya kuvuja damu nyingi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema uchunguzi zaidi unaendelea kufahamu chanzo cha tukio hilo. 

clouds stream