Thursday, 31 August 2017

Kamanda Mambosasa Akemea Kauli Ya ‘Order’ Kutoka Juu

21078448_1321690834608554_4419939277427757950_n (1)
IMG-20170426-WA0006

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa katika uongozi wake hakutakuwa na kauli ya ‘order’ kutoka juu kutoka kwa askari polisi.

Kamanda Mambosasa amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na IGP, Simon Sirro kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam akitokea Dodoma alipokuwa Kamanda wa Polisi Mkoani humo.

Amesema mtu yeyote atakayesikia kauli ya ‘order’ kutoka juu, aikatie rufaa kwa kumpigia simu na kumueleza kuwa kuna mtu anataka kuchezea uhuru wake.

“Ukisikia askari anasema ‘order’ kutoka juu, ujue huyo hajiamini na pengine ni mbabaishaji asiyejua kile anachotenda,” amesema.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni na miongozo inayoongoza jeshi hilo.

clouds stream