Friday, 11 August 2017

Maagizo Ya JPM Yaanza Kuzaa Matunda Tanga

Image result for magufuliIMG-20170426-WA0006

Katika kuhakikisha wananchi wanasikilizwa na kutatuliwa kero zao kwa wakati,maagizo aliloyatoa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika ziara yake Mkoani Tanga yakumtaka Mkandarasi aliyejenga Mabwaya yakuhifadhia maji kurudia ujenzi huo kutokana na kuyajenga chini ya kiwango yameenza kuchukuliwa hatua.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema wakandarasi ambao wametakiwa kufika eneo la ujenzi kwa siku 14 tayali ameshawandikia barua kwa kutakiwa kufika eneo la kazi kwa siku tano kuanzia tarehe liyopangwa.

“Wakandarasi hawa,wale ambao wamepangiwa kufika katika site (eneo la kazi) kwa siku 14 kamanda wa polisi wa mkoa analifahamu hilo na tayari wameshamuelekeza Mkurugenzi na ameshawaandikia barua yakufika kuja kufanya kazi kamamheshimwa Rais alivyosema, na fedha zao bado tumezishikilia hadi pale watakapokuja kufanya kazi, na sisi turudishe taarifa kama tulivyagizwa” alisema Gondwe

clouds stream