Tuesday, 29 August 2017

Zitto: Siwezi Kukubali Uteuzi Wowote Wa Rais Magufuli

Rais Dkt John Magufuli (kushoto) akiwa na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.
Rais Dkt. John Magufuli (kushoto) akiwa na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe (kulia).
IMG-20170426-WA0006

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameibuka na kudai kuwa hawezi kukubali uteuzi wowote ule kutoka kwa Rais Magufuli kushika nafasi yoyote ile.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini amedai kuwa kukubali uteuzi kutoka kwa Rais Magufuli kutamnyima nafasi ya kujenga chama chake cha ACT.

Hivi karibuni Rais Magufuli alishangaza wengi pale alipoamua kuteua watendaji wawili katika Serikali yake kutoka chama cha ACTWazalendo, ambao ni wapinzani baada ya kumteua aliyekuwa Muasisi na Mshauri wa ACT Wazalendo, Profesa Kitila Alexander Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Siku chache baadaye Rais Magufuli alimteua aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo na aliyegombea Urais kupitia chama hicho, Mama Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

clouds stream