Tuesday, 22 August 2017

Hali Ya Bulaya Yazidi Kuzorota, Akimbizwa Muhimbili

Mbunge wa jimbo la Bunda-mjini, Esther Amos Bulaya.
Mbunge wa jimbo la Bunda-mjini, Esther Amos Bulaya.
IMG-20170426-WA0006

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Mh. Joyce Sokombi amesema hali ya Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mh. Ester Amos Bulaya imezidi kuwa mbaya.

Mh. Sokombi amesema pamoja na kwamba amepelekwa katika hospitali ya mkoa Mara Mbunge huyo hajapata nafuu, hivyo amepewa rufaa ya kuja hospitali kuu ya Taifa Muhimbili.Ester Bulaya alipata matatizo ya presha na kukimbizwa hospitali hapo jana huku akiwa kizuizini, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana.

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Esther Bulaya amekamatwa na jeshi la Polisi akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kujiandaa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe alisema wabunge Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Tarime.

clouds stream