Wednesday, 2 August 2017

MSEMAJI WA JESHI LA KENYA ATOWEKA

kenya logo
IMG-20170426-WA0006

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Kanali, Joseph Owuoth ameripotiwa kutoweka na haijulikani mahali alipo, familia yake imekaririwa ikisema.

Kanali huyo anadaiwa kuwa alikuwa akiwasiliana na dada yake aliyetambuliwa kwa jina la Elizabeth kabla ya kukatika kwa mawasiliano akiwa katika eneo linalodhaniwa kuwa ni Nakuru.

Kiongozi huyo wa Jeshi amewahi kukiri kuwa Jeshi hilo linaendesha mafunzo maalum kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, huku zikiwa zimepita wiki mbili tu tangu Muungano wa Upinzani (NASA) kuibua tuhuma nzito zinazolihusisha jeshi hilo na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 8, mwaka huu.

Inadaiwa kuwa Kanali Owuoth aliamriwa kwenda katika likizo ya lazima mara tu baada ya kutoa kauli iliyothibitisha madai ya NASA na kuamriwa kutoongea na chombo chochote cha habari na kwenda nyumbani kwake huko Koru. Alikuwa katika mawasiliano ya karibu na dada yake Elizabeth, ambaye anadaiwa kumueleza kila kitu alichokuwa akiamrishwa kufanya na waajiri wake.

Akiwa anawasiliana na dada yake, Owuoth anadaiwa kupanda usafiri wa jumuiya ‘Public Transport’ Jijini Nairobi lakini ghafla akaenda kimya alipofika Nakuru, na tangu hapo hakusikika tena.

Kanali Owuoth anaripotiwa kutoweka ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Mtaalam wa Teknolojia wa (IECB), Chris Muhando kuripotiwa kutoweka na baadae mwili wake kukutwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ilhali ukiwa umekatwa mkono mmoja.

clouds stream