Tuesday 26 July 2016

Alichosema Zitto Kuhusu Serikali Kuhamia Dodoma


Tarehe July 26, 2016Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.


Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.
Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zito Kabwe.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameunga mkono harakati za Serikali kutaka kuhamia Mkoani Dodoma mara baada ya Rais, Dkt. John Magufuli kutangaza azma hiyo mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, ameandika yafuatayo;
Katika kutekeleza dhana ya kuirudisha nchi katika misingi ya kuasisiwa kwake, katika kampeni zetu za uchaguzi wa mwaka 2015, tuliahidi kwamba, kama tungeshinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, serikali ingehamia Dodoma mara moja. Aidha mgombea wetu wa urais aliahidi kwamba angekula kiapo cha urais mjini Dodoma.
“Tulienda mbali zaidi tukasema kwamba kulikuwa na haja ya kuzitawanya wizara katika mikoa mbalimbali ili kuiweka serikali karibu na wananchi na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika pande zote za nchi. Katika kutekeleza hili, kwa kuanzia, tukaweka nia ya kuihamishia wizara ya kilimo mkoani Mbeya, Wizara ya Nishati na Madini mkoani Mwanza na Wizara ya Utalii na Mali Asili mkoani Arusha,”  ameandika Zittto.
Ni katika msingi huu wa kisera tunachukua nafasi hii kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake sahihi na wa kijasiri wa kuhamishia serikali Makao Makuu ya nchi Mjini Dodoma. Uamuzi wa kuhamishia serikali Dodoma ulifanywa miongo mine iliyopita lakini serikali ya CCM ilishindwa kuutekeleza kwa visingizio mbalimbali. Nchi kadhaa zilizokuja kujifunza kwetu namna ya kuhamisha makao makuu zilikwishatekeleza uamuzi huu wa kisera bila kigugumizi. Nchi mojawapo ni Nigeria iliyohamisha makao makuu yake kutoka Lagos kwenda Abuja.
“Tutaendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kila mara atakapochukua maamuzi ya kisera tunayoamini kwamba yana maslahi mapana kwa Taifa. Hatahivyo, tutaendelea kutekeleza kwa bidii wajibu wetu wa kumkanya na kumkosoa pale tunapoamini kwamba maamuzi ya serikali yake hayana maslahi mapana kwa Taifa, ikiwemo kumnya na kukandamiza misingi ya Demokrasia na kufifisha utawala wa sheria,” amemaliza kuandika Zitto.

clouds stream