Tarehe July 27, 2016
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi na wafuasi wa Chama cha Mapiduzi katika hafla ya kumpongeza na kumkaribisha nyumbani Bagamoyo baada ya kustaafu Uenyekiti CCM.
Rais Mstaaafu wa Awamu ya Nne na Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa
anataka kupumzika na hayuko tayari kufanya shuguli za kichama wala kiserikali isipokuwa kutoa ushauri katika shughuli za
kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kilimo na mifugo.
Kikwete ameyasema hayo Mjini Bagamoyo katika sherehe za kumkaribisha nyumbani na kumpongeza ikiwa ni siku chache tu
tangu kukabidhi uenyekiti wa CCM kwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Amesema anamshukuru Mungu kwa kuwa katika kipindi chake ameweza kuongoza na kuiacha nchi ikiwa salama na tulivu licha
ya kupitia katika vipindi vigumu tofauti.
“Namshukuru Mungu kwani nchi iko salama na chama pia kipo imara hivyo nataka nipumzike nisijihusishe tena na masuala ya
kisiasa au kiserikali kwani kwa sasa kuna viongozi wenye uwezo isipokuwa kama mkija kwa masuala ya kimaendeleo nipo tayari
kufanya hivyo,” amesema Kikwete.
Awali mbunge wa Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alisema kuwa watamuenzi Dkt. Kikwete kwa kujenga mnara wa
kumbukumbu katika ofisi ya CCM Mkoa wa Pwani takika mti wa Mkungu Maarifa mahali ambapo kwa mara ya kwanza alitangaza
nia ya kuwania Urais.