Monday, 4 July 2016

Taarifa : Yanga Vs Medeama Kitapigwa Taifa, Julai 16 Saa Kumi Alasiri


Tarehe July 5, 2016Wachezaji wa Yanga
Wachezaji wa Yanga
Wachezaji wa Yanga kutoka kulia Vicent Bosou,Donald Ngoma na Deoratius Munish
Mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya Medeama utachezwa tarehe 16/7/2016 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mchezo utaanza saa 10 : 00 jioni kwa masaa ya hapa nyumbani.
Mipango ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga kujinasua mkiani mwa msimamo wa Kundi A la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imepata nguvu zaidi baada ya ombi lao la kubadilisha siku ya mchezo wao na Medeama kukubaliwa.
Shirikisho la Soka Barani Afrika limebadili tarehe ya mchezo wa Yanga dhidi ya Medeama kutoka siku ya Ijumaa ya tarehe 15 Julai na sasa kuchezwa Jumamosi ya tarehe 16 Julai.
Awali ikumbukwe CAF waliwakatalia Yanga kubadili siku ya mchezo wa pambano lao dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa walichelewa kuwasilisha ombi lao. Kwa kulitambua hilo, Yanga walituma ombi lao mapema kuomba kubadilishwa kwa mchezo wao dhidi ya Medeama na CAF kuwakubalia hii leo.
Pambano kuchezwa Jumamosi kutatoa fursa kwa Yanga kupata nguvu ya mashabiki zaidi kulinganisha na tarehe ya awali ya Ijumaa.
Yanga iliyofungwa na TP Mazembe bao 1-0 katika mchezo uliopita na kujikuta wakiburuza mkia katika kundi A baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo.

clouds stream