Tarehe July 29, 2016
Chama cha ACTWazalendo kimetoa neno kuhusiana na operesheni ‘Ukuta’ iliyotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kudai kuwa hawakubaliani na jambo hilo kufanywa na CHADEMA.
ACTWazalendo wametoa lao hilo la moyoni kupitia akaunti yao ya Twitter na kutaka wanasiasa wa upinzani kuungana na kupigana vita moja.
Juzi CHADEMA walitangaza operesheni Ukuta ambapo wamepanga kufanya mikutano na maandamano nchi nzima Septemba 1, mwaka huu kama njia ya kupinga baadhi ya mambo wanayoyaona kuwa wananyanyasika kwa kile wanachokiita udikteta.
Tayari tamko hilo la CHADEMA limepingwa vikali na Msajili wa Vyama vya Siasa na kudai kuwa ni uchochezi utakaovuruga amani ya nchi huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikidai kuwa madai ya Chadema ni uongo mtupu uliojaa ubabaishaj