Thursday, 7 July 2016

BAVICHA Bado ‘Kichwangumu’ Kuzuia Mkutano Wa CCM Licha Ya Kuhojiwa Polisi


Tarehe July 7, 2016Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick ole Sosopi.
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick ole Sosopi.
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick ole Sosopi.
Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limeendeleza msimamo wake wa kuzuia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, uliopangwa kufanyika Julai 23, mwaka huu mjini Dodoma licha ya viongozi wake kuhojiwa na Jeshi la Polisi.
Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Patrick ole Sosopi, amesema kuna vijana watakaotoka sehemu mbalimbali nchini ili kuzuia mkutano wa CCM.
Amesema katika kuhakikisha linatimiza azma yake hiyo, zaidi ya wanachama wake wapatao 4,000 wamejiandaa kushiriki kwenye shughuli hiyo.
Sosopi amesema Bavicha watakwenda Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kwa kile walichodai kusaidia Jeshi la Polisi kutekeleza amri yake ya kuzuia mikutano ya kisiasa hadi 2020.
“Kuna watu wamejitolea kutoa magari kwa ajili ya kuwabeba vijana hao ili kuwafikisha Dodoma kuunga mkono agizo la polisi,” amesema.
Wakati huohuo, Sosopi ameliomba Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kutokana na kauli zao za vitisho walizozitoa dhidi ya Bavicha hivi karibuni.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamad Shaka, aliionya Bavicha wasiende Dodoma kuzuia Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kwa kuwa watatumia kila mbinu kuwazuia ili kulinda heshima ya chama chao.

clouds stream