Monday 18 July 2016

Makonda Afafanua Kauli Yake Ya Kutaka Vijana Wasiokuwa Na Kazi Wakamatwe


Tarehe July 18, 2016Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amefafanua zaidi kauli yake ya kutaka vijana wasiokuwa na kazi wakamatwe na kudai kuwa imechukuliwa vibaya katika namna ambayo siyo aliyoilenga huku akisisitiza kuwa lengo lilikuwa ni katika kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkoa huu wenye pilika pilika nyingi sana.
Mhe. Makinda amesema alipoteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alifanya mkutano na wenyeviti wa mitaa ambao wana mamlaka makubwa katika mitaa yao na kuzungumzia suala la ulinzi na usalama.
Amesema katika mkutano wake na viongozi hao wa mitaa alizungumzia mambo mawili makubwa ya kuwataka kuwafahamu vizuri wakazi wao katika serikali za mitaa na pia kujua shughuli zinazofanywa na wakazi hao katika dhana nzima ya kujenga misingi ya ulinzi na usalama na kujihakikishia amani katika jamii yetu.
Kwa mujibu wa Makonda, kwa kuwafahamu wananchi wako na shughuli wanazofanya kunatoa picha kamili ya hali ya usalama katika mitaa husika na mkoa kwa ujumla na kwamba hilo ndilo lilikuwa lengo la kauli yake ya kuwakamata Vijana wasiokuwa na kazi.
Hivi karibuni kumekuwa na majadilianao yanayoendelea mitaani na katika mitandao ya kijami juu ya kauli ya Mhe. Makonda ya kutaka kuwepo na msako wa nyumba kwa nyumba katika kuwasaka Vijana wasiokuwa na kazi huku wengi wakilalamikia agizo hilo na kudai kuwa halitekelezeki.

clouds stream