Wednesday, 20 July 2016

Wanafunzi 382 Warejeshwa UDOM


Tarehe July 20, 2016udom
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema wanafunzi 382 pekee kati ya 7,805 waliokuwa wanasoma Stashahada Maalum katika Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) ndio wenye sifa za kurejea chuoni hapo ili kuweza kuendelea na masomo.
Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi  ilikiagiza Chuo cha Dodoma kuwarudisha nyumbani wanafunzi wa  Stashahada za Elimu (Sayansi, Hisabati na Teknolojia) kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na Tatizo la ufundishaji wa Stashahada hizo chuoni hapo.
Hatahivyo sakata hilo la wanafunzi hao kurudishwa liliibua mijadala ya kitaifa na bungeni huku baadhi ya wabunge wakiomba miongozo kutaka suala hilo lijadiliwe kama jambo la dharura baada ya wanafunzi hao kupewa masaa machache kupotea katika chuo hicho.
Akizungumza bungeni kutoa taarifa ya Serikali, Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako alisema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya walimu waliokuwa wanawafundisha wanafunzi hao kugoma kufundisha kwa muda wa mwezi mmoja.
Hatahivyo Rais Magufuli alisema baadhi ya wanafunzi hao hawakuwa na sifa stahiki na wale wasiokuwa na sifa kuwaita ‘vilaza’ huku akiahidi kuwa wanafunzi hao wataangaliwa upya na wale wenye sifa watarejea kuendelea na masomo yao.

clouds stream