Tarehe July 21, 2016
Vigogo 3 kati ya 4 waliotumbuliwa mnamo tarehe 15/2/206 na Waziri wa Afya, Manedeleo ya Jamii Jinsi na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(Mb) wameponea chupuchupu kung’olewa katika taasisi hiyo ya MSD.
Vigogo hao ambao ni wakurugenzi walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinawakabili.
Wakurugenzi hao ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa wateja Bw.Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Bw. Joseph Tesha, Mkurugenzi Ugavi Bw. Misanga Muja na Mkurugenzi wa Ununuzi Bw.Heri Mchunga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Wadhamini imebanisha kuwa baada ya kufanya uchunguzi Bw. Heri Mchunga ameonekana hana kosa hivyo amerudishwa kazini pamoja na kuhamishiwa kurugenzi ya ugavi kuwa Mkurugenzi.
Bw. Joseph Tesha naye amerudishwa kazini huku akitenguliwa ukurugenzi na atasubiri kupangiwa kazi nyingine.
Mwingine ni Misanga Muja aliyekuwa mkuurugenzi Ugavi amerejeshwa kazini huku akitenguliwa nafasi yake hivyo atakaa benchi kusubiri kazi nyingine.
Aliyetumbuliwa ni Cosmas Mwaifwani kufuatia Bodi hiyo kubaini kuwa ana makosa katika utendaji wake hivyo utendaji wake umesimamishwa kuanzia tarehe 8/7/2016.