Tarehe July 16, 2016
Serikali imemtaka Dkt. Juma Mwaka ‘Dkt. JJ Mwaka’ aliyefutiwa usajili wa tiba asilia hivi karibuni kwutumia vyombo vya sheria kuelezea hisia zake kama anahisi ameonewa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akiongea na wadau wa afya katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera.
Amesema uamuzi wa Serikali kukifutia usajili kituo hicho ni sahihi kwani matangazo na huduma alizokuwa akitoa zilikuwa haziendani na maadili na taratibu za udaktari wa tiba asilia.
“Hapaswi kuichonganisha Serikali na wananchi wake kwa kudai kuwa ameonewa na kwamba wananchi wamenyimwa fursa ya kupata huduma katika kituo hicho bali uamuzi huo ni sahihi na hajaonewa,” ameongeza.
Waziri Ummy ameongeza kuwa kama anaona kweli ameonewa basi aende mahakamani ili tukutane huko na chombo hicho cha haki kiamue ukweli ni upi na uongo uko wapi.