Tarehe July 28, 2016.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, ambao pamoja na mambo mengine utalenga kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu amesema Rais Magufuli atawasili Mjini Kahama siku ya Jumamosi jioni na kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili, Julai 31, mwaka huu.
Amewataka wananchi wa Kahama kujitokeza kwa wingi ili kumlaki kiongozi huyo katika ziara hiyo muhimu ya Rais Magufuli.
“Lengo lake ni kuwapongeza wananchi wa Kahama kwa kumpa kura nyingi katika Uchaguzi uliomalizika mwaka jana,” amesema Nkulu.