Bunge La Senate Lamtega Trump Kwa Urusi
Waandishi wa masuala ya siasa wanasema kuwa ikiwa Trump atajaribu kuukataa mswaada huo basi itakuwa ishara tosha kuwa anaiunga mkono sana Urusi.

Bunge la Senate nchini Marekani limepiga kura ya kuziwekea vikwazo vipya Urusi, Iran na Korea Kaskazini licha ya pingamizi kutoka Ikulu ya White House.
Bunge la wawakilishi liliidhinisha mswaada huo mapema wiki hii kwa kura nyingi baada ya mswaada huo kupita katika mabunge yote na sasa utapelekwa kwa Rais Donald Trump kuwekwa sahihi.
Lakini bwana Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi na anaweza kuukataa mswada huo licha ya uungwaji mkono uliopata.
Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.
Lakini mjadala kuhusu vikwazo hivyo vipya unafanyika huku uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.
Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake.