KAMPENI MBIO ZA URAIS NCHINI RWANDA ZAANZA RASMI
Wakati nchi ya Kenya ikijiandaa kufanya Uchaguzi Mkuu Agosti 8, mwaka huu, shughuli za kampeni za uchaguzi wa Rais nchini Rwanda zimeanza rasmi ambapo wagombea wa kiti cha urais ni watatu, Rais Paul Kagame anayewania muhula wa tatu baada ya Katiba ya nchi hiyo kubadilishwa.
Kagame anapambana na Frank Habineza wa Chama cha Green na Philippe Mpayimana ambaye ni Mgombea wa Kujitegemea.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Tawala RPF, Rais Paul Kagame alianzia kampeni kusini mwa Rwanda, Mjini Ruhango na mgombea wa kujitegemea Philippe Mpayimana alianzia kampeni kusini mashariki mwa nchi hiyo.