Tuesday, 11 July 2017

KADA MWINGINE CHADEMA ATIMKIA CCM KUMUUNGA MKONO JPM

magufuli-5

IMG-20170426-WA0006

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa FFU uliopo Kata ya Muriet, Mkoani Arusha, Anacletus Edward anadaiwa kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Huu ni muendelezo wa viongozi wa CHADEMA kujivua nafasi zao na kutangaza kumuunga mkono Rais Magufuli, ambapo kwa siku ya jana, Diwani wa Ngabobo (Chadema), Solomon Laizer ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na CCM kwa maelezo kuwa anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Laizer sasa anakuwa diwani wa tano katika Halmashauri ya Meru kujiuzulu kwa kutoa sababu kuwa anamuunga mkono Rais Magufuli. Hadi sasa madiwani watano wa Chadema waliojiuzulu ni Credo Kifukwe wa Kata ya Murieti Jijini Arusha.

Wengine waliojiuzulu katika Jimbo la Arumeru Mashariki na kata zao kwenye mabano ni Anderson Sikawa (Leguruki), Emmanuel Mollel (Makiba), Greyson Isangya (Maroroni) na Josephine Mshiu (Viti Maalumu).

clouds stream