Wednesday, 5 July 2017

KENYATTA , ODINGA ‘WAKACHA’ MDAHALO WA WAGOMBEA KENYA


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amwashikanisha mikono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Raila Odinga ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya chakula mara baada ya kula kiapo cha kuwa Rais wa Tanzania.Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amwashikanisha mikono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Raila Odinga Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya chakula mara baada ya kula kiapo cha kuwa Rais wa Tanzania.
IMG-20170426-WA0006

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga wamejiondoa kutoka kwenye mdahalo wa moja kwa moja kupitia luninga wa wagombea urais nchini humo.

Mdahalo huo ulikuwa umepangiwa kufanyika Julai 10 na marudio Julai 24.

Wagombea hao wamesema hawatahudhuria mdahalo huo kwa sababu hawakushirikishwa wakati wa maandalizi ya mdahalo huo.

Rais Kenyatta, wa chama cha Jubilee, alikuwa wa kwanza kutangaza kujiondoa.

Katibu Mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amesema waandalizi wa mdahalo huo hawakuwasiliana rasmi na maafisa wa Ikulu au chama cha Jubilee rasmi kuhusu mdahalo huo.

Tuju amesema mdahalo huo unaadaliwa kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari na watu ambao hawawafahamu.

Saa chache baada ya hatua ya chama hicho tawala, muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA) ulitangaza kuwa Odinga pia hatahudhuria.

“Mgombea urais wa NASA Raila Odinga hatashiriki katika mdahalo wa urais wa 2017 chini ya mpangilio wa sasa uliopendekezwa,” taarifa kutoka afisa wa mawasiliano wa Bw Odinga Salim Lone ilisema.

Mdahalo huo umekuwa ukiandaliwa na kampuni kwa jina Debates Media Limited.

clouds stream