Monday, 31 July 2017

TEGETA ESCROW YAMPAISHA KAFULILA , APATA SHAVU MAREKANI

Image result for kafulila bungeni
IMG-20170426-WA0006
Hatimaye,baada ya kutetea maslahi ya umma katika Sakata la Tegeta Escrow aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amepata nafasi ya kufanya ziara nchini Marekani.
Akizungumzia ziara hiyo Kafulila alisema amechaguliwa na nchi ya Marekani kufanya ziara ya mafunzo ya masuala ya uwazi na uwajibikaji kwa muda wa wiki tatu.
Hivi karibuni Kafulila alipata pongezi kutoka kwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutokana na kuliibua sakata la Tegeta Escrow ambalo baadaye lilikuwa gumzo kubwa na kupelekea kufanywa uchunguzi na wahusika kufikishwa Mahakamani.

clouds stream