Marekani: Muda wa mazungumzo kuhusu Korea Kaskazini umekwisha
Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe anasema yeye pamoja na rais wa Marekani Donald Trump wamekubaliana kuwa upo umuhimu wa kupambana na Korea ya Kaskazini katika mipango yake ya majaribio ya makombora.
Abe amewaambia waandishi wa habari kuwa anashukuru kujitolea kwa Rais Trump katika suala la Korea ya Kaskazini.
Mapema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema muda wa mazungumzo umemalizika.
Haley amesema hakuna sababu ya kuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo hakutakuwa na matokeo, yatakayoipa mbinyo Korea Kaskazini na China ni lazima iamue kama itaamua kuchukua hatua hii muhimu.
Hatua hiyo imekuja baada ya Korea kaskazini kufanya jaribio lingine la makombora yake siku ya Ijumaa.