Rais Uhuru Kenyatta aionya mahakama
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya mahakama nchini humo akiitaka kutousaidia upinzani na kuhujumu uchaguzi unaokuja.
Uchaguzi wa urais utafanyika mwezi ujao ambapo uhuru Kenyatta anataka kuchaguliwa tena.
Siku ya Ijumaa, kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani na upinzani, mahakama kuu iliamrisha tume ya uchaguzi isichapishe makaratasi ya kupigia kura.
Bwana Kenyatta alisisitiza kuwa uchaguzi huo utafanyika jinsi ulivyopangwa,.
Amesema kuwa mahakama hauwezi kudai kuwa huru na kutumia uhuru huo kuingilia idara zingine za serikali.
Muungano wa upinzani wa Nasa ulidai kuwa rais alikuwa na uhusiano na kampuni ya Dubai la Al Ghurair ambayo ilishinda zabuni ya dola milioni 24 kuchapisha makatasi hayo.
Hata hivyo Jaji mkuu wa Kenya David Maraga, ametoa onyo kwa Rais Uhuru Kenyatta kutohujumu imani ya umma juu ya mfumo wa kisheria.
Nayo tume ya Uchaguzi nchini Kenya IEBC leo inatarajiwa kukutana na wagombea wote wanane wa kiti cha uraisi akiwemo Rais Uhuru Kenyata.
Mawakili wa Tume hiyo pia watafika mbele ya mahakama ya rufaa kupata ufafanuzi zaidi juu ya uamuzi huo