Marekani na Qatar waafikiana kuukabili ugaidi duniani
Marekani na Qatar wamefikia makubaliano ya jitihada za kukabiliana na kudhamini ugaidi.
Makubaliano hayo yametiwa saini mjini Doha na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ambaye yuko ziarani nchini humo.
Makubaliano hayo yanafanyika wakati ambapo Qatar ipo katika mgogoro mkali na majirani zake, ikiwemo Saudi Arabia.
Wote wamekata uhusiano na Qatar baada ya kuituhumu kuunga mkono makundi ya wapiganaji wa kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, makubaliano hayo na Marekani, ambayo inasaidia kusuluhisha mgogoro huo, imeashiria kwamba inaiona Qatar kama mshirika mwaminifu katika mapambano dhidi ya ugaidi.