Wednesday, 5 July 2017

Sare Za JWTZ Zamponza Manji

Mfanyabiashara Yusuph Manji.
Mfanyabiashara Yusuph Manji.
IMG-20170426-WA0006

Mfanyabiashara Yusuph Manji na wenzake wamekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi katika ghala la Quality Motors Group.

Mara baada ya kukamatwa waliombewa dhamana lakini ilikataliwa kwa sababu zisizojulikana. Kupitia hati ya kiapo, Wakili Gudson Ndusyepo amebainisha kuwa kukamatwa kwa walalamikaji sio halali kwa sababu kosa linalodaiwa dhidi yao linahusiana na masuala ya Kampuni ya Quality Motors ambayo inaongozwa na Wakurugenzi wake na Manji.

”Kama Wakili wa waombaji nimefuatilia suala la dhamana hadi sasa saa 48 zimeshapita tangu walipokamatwa, lakini hawajafikishwa Mahakamani. Jambo hilo ni kinyume na sheria.” alisema Wakili Ndusyebo.

clouds stream