Vitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi baharini

Vietnam imesitisha shughuli ya uchimbaji gesi katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya China, kufuatia vitisho vikali kutoka China.
Taarifa zinaiambia BBC kuwa kampuni iliyokuwa ikiendesha uchimbaji huo iliamrishwa kuondoka eneo hilo.
Inajiri siku chache baada ya kampuni ya Respol kusema kuwa imegundua gesi nyingi.
Ripoti zinasema kuwa wakurugenzi wa Respol waliambiwa wiki iliyopita na serikali wa Viertman kuwa China ilikuwa imetisha kushambulia vituo vyake katika visiwa vya Spratly ikiwa uchimbaji huo haungesitishwa.
China inadai kuwa karibu eneo lote la kusini mwa bahari ya China ni lake, visiwa ambavyo pia vinavyodaiwa na mataifa mengine.
Vietnam inaliita eneo hilo Block 136-03 na imeipa zabuni kampuni inayoitwa Talisman-Vietnam.
China nayo inaliita eneo hilo Wanan Bei-21 ikiwa imetoa kandarasi kwa kampuni tofauti.
Vitisho vya China vyasababisha Vietnam kusitisha uchimbaji wa gesi