Marekani na K. Kusini zaonya kuishambulia Korea Kaskazini
Marekani na Korea kusini zimeionya kwa pamoja Korea Kaskazini kwamba huenda kukazuka vita kufuatia hatua ya taifa hilo kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu siku ya Jumanne.
Maafisa wawili wakuu wa mataifa hayo mawili walio na makao yao Korea Kusini wamesema kuwa kujizuia ni chaguo lao na kwamba hatua hiyo inaweza kubadilika wakati wowote.
Wamesema kuwa itakuwa ''makosa makubwa'' kutofikiria kuchukua hatua kali.
Onyo hilo linajiri wakati ambapo mataifa hayo mawili yamefanya zoezi la pamoja la kijeshi la makombora ya masafa marefu.
Kituo cha habari cha Korea Kaskazini kilimnukuu kiongozi wa taifa hilo Kim Jong-un akisema kuwa jaribio hilo la kombora la masafa marefu ni zawadi kwa Wamarekani wakati was siku yao ya uhuru .
Mapema, waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson aliionya Pyongyang kwamba inaendeleza vitisho dhidi ya Marekani na dunia nzima kwa jumla.