Thursday, 6 July 2017

Zambia kucheza fainali ya Cosafa na Zimbabwe

COSAFA

Wachezaji wa Tanzania wenye jezi nyeupe Himid Mao na Mzamiru Yassin wakikabwa na mchezaji wa Zambia
IMG-20170426-WA0006

Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars imeshindwa kusonga mbele kwenye hatua ya fainali baada ya kuchapwa kwa mabao 4-2 na Zambia Chipolopolo katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Cosafa.

Beki Erasto Nyoni alianza kuipatia Taifa Stars bao la kuongoza katika dakika ya 14, lakini katika dakika ya 44 Brian Mwila, akasawazisha goli hilo, dakika moja baadae Justin Shonga akaifungia Zambia goli la pili.

Kipindi cha Pili, dakika ya 56 Chipolopolo wakaongeza goli la tatu kupita kwa Chirwa aliyefunga kwa mkwaju wa penati, Justin Shonga akahitimisha kazi kwa goli la nne katika dakika ya 68.

Winga Simon Msuva aliipatia Stars goli la pili katika dakika ya 84, mchezo wa mshindi wa tatu utazikutanisha Tanzania na Lesotho ambao walifungwa na Zimbabwe kwa mabao 4-3.

Mchezo wa fainali utachezwa Jumapili ya Julai 9 kwa Zambia kukipiga na Zimbabwe

clouds stream