Tuesday 21 April 2015

Bayern Munich yasonga mbele, yaichinja Porto nyumbani

Bayern Munich yasonga mbele, yaichinja Porto nyumbani


Thiago Alcantara akiifungia Bayern Munich goli la kwanza kwenye mchezo wa jana
Thiago Alcantara akiifungia Bayern Munich goli la kwanza kwenye mchezo wa jana
Bayern Munich imeichapa FC Porto ya Ureno kwa bao 6-1 katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa Ulaya iliyopigwa jana usiku kwenye dimba la Allianz Arena, mjini Munich, Ujerumani.
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia moja kati ya magoli yao waliyofunga kwenye mechi dhidi ya FC Porto
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia moja kati ya magoli yao waliyofunga kwenye mechi dhidi ya FC Porto
Watu wengi walifikiri Bayern itaaga michuano hiyo kutokana na kipigo cha 3-1 ilichoambulia kutoka kwa FC Porto kwenye mchezo wa awali uliopigwa Ureno.
Katika mechi hiyo ya marudiano ya robo fainali wenyeji walipata mabao yao kupitia kwa Thiago Alcantara, Robert Lewandowski aliyefunga mawili, Thomas Muller, Jerome Boateng na Xabi Alonso wakati wageni walipata bao pekee kutoka kwa Martnez.
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake
Kwa maana hiyo, Bayern Munich wamefuzu kucheza hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mabao 7-4 dhidi ya FC Porto.
Tarehe April 22, 2015
Thiago Alcantara akiifungia Bayern Munich goli la kwanza kwenye mchezo wa jana
Bayern Munich imeichapa FC Porto ya Ureno kwa bao 6-1 katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa Ulaya iliyopigwa jana usiku kwenye dimba la Allianz Arena, mjini Munich, Ujerumani.
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia moja kati ya magoli yao waliyofunga kwenye mechi dhidi ya FC Porto
Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia moja kati ya magoli yao waliyofunga kwenye mechi dhidi ya FC Porto
Watu wengi walifikiri Bayern itaaga michuano hiyo kutokana na kipigo cha 3-1 ilichoambulia kutoka kwa FC Porto kwenye mchezo wa awali uliopigwa Ureno.
Katika mechi hiyo ya marudiano ya robo fainali wenyeji walipata mabao yao kupitia kwa Thiago Alcantara, Robert Lewandowski aliyefunga mawili, Thomas Muller, Jerome Boateng na Xabi Alonso wakati wageni walipata bao pekee kutoka kwa Martnez.
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski akishangilia baada ya kuifungia goli timu yake
Kwa maana hiyo, Bayern Munich wamefuzu kucheza hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mabao 7-4 dhidi ya FC Porto.

Barcelona yafuzu kucheza nusu fainali ligi ya mabingwa Ulaya

Barcelona yafuzu kucheza nusu fainali ligi ya mabingwa Ulaya


Neymar Jr akiifungia Barcelona goli la pili kwenye mchezo wa jana
Neymar Jr akiifungia Barcelona goli la pili kwenye mchezo wa jana
Barcelona imeshinda magoli 2-0 katika mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyopigwa jana usiku kwenye uwanja wa Camp Nou dhidi ya PSG.
Neymar Jr akiifungia Barcelona bao la pili kwenye mechi ya jana dhidi ya PSG
Neymar Jr akiifungia Barcelona bao la pili kwenye mechi ya jana dhidi ya PSG
Magoli yote mawili ya Barcelona yamefungwa na mshambuliaji raia wa Brazil Neymar Jr.
Mlinda mlango wa Barcelona akimiliki mpira mbele ya mshambuliajiwA PSG Cavani
Mlinda mlango wa Barcelona akimiliki mpira mbele ya mshambuliajiwA PSG Cavani
Kwa ushindi huo Barca wanafuzu kucheza hatua ya nusu fainali kwa jumla ya goli 5-1 kutokana na ushindi wa goli 3-1 walioupata kwenye mechi ya awali wakiwa ugenini mijini Paris, Ufaransa.

Wanajeshi kudhibiti ghasia dhidi ya wageni Afrika Kusini

Wanajeshi kudhibiti ghasia dhidi ya wageni Afrika Kusini

Baadhi ya raia wa kigeni wakitafuta msaada Afrik kusini.
Baadhi ya raia wa kigeni wakitafuta msaada Afrik kusini.
Jeshi nchini Afrika kusini limeanza kuelekea kwenye maeneo ambayo yameathiriwa na wimbi la machafuko dhidi ya wahamiaji kutoka nchi nyingine za Afrika.
Wanajeshi wanafanya doria katika baadhi ya majimbo ya Kwa-Zulu Natal na Gauteng, pia mjini Alexandra uliopo jiji la Johannesburg ambako Raia wa Msumbiji aliuawa na wengine raia wengine kadhaa kutoka Zimbabwe walinusurika na shambulio.
Watu wameonekana katika makundi wakiwa wamebeba mishumaa karibu na jengo la Mahakama kuu mjinin Johannesburg wakitoa wito wa kukomesha machafuko,ambayo yamegharimu maisha ya watu saba.
Historia ya nchi hiyo inaonyesha kuwa nnamo mwaka 2008, Jeshi la Afrika kusini lilisambazwa nchini humo baada ya Watu 63 kuuawa kutokana na mashambulizi ya wenyeji dhidi ya wageni.

Mfalme aingilia kati ghasia za wageni kutimuliwa Afrika Kusini

Mfalme aingilia kati ghasia za wageni kutimuliwa Afrika Kusini


Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini (katikati).
Mfalme wa Jamii ya Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini (katikati).
Vurugu za kuwatimua wageni nchini Afrika Kusini.
Vurugu za kuwatimua wageni nchini Afrika Kusini.
Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini, anatarajiwa kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujiepusha na ghasia, kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya kibaguzi nchini humo.
Mfalme huyo ameshutumiwa kwa kuchochea mashambulio hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu saba, alinukuliwa akisema kuwa raia wote wa kigeni wanapaswa kurejea katika mataifa yao.
Maelfu ya watu wanatarajiwa kufurika uwanja mmoja ulioko mji wa Mashariki wa Durban kusikiliza hotuba hiyo ya Mfalme Zwelithini.
Kwa upande wake  Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, amesema mashambulio hayo yanakwenda kinyume na maadili yote wanayoamini.
Makundi kadhaa yaliyojihami yameshambulia na kupora maduka kadhaa yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.

Zitto ajibu mapigo, awataja maadui wa ACT

Zitto ajibu mapigo, awataja maadui wa ACT


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe .
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe .
Wananchiwalio hudhuria mkoani Mwanza katika mkutano wa chama cha ACT.
Wananchi walio hudhuria mkoani Mwanza katika mkutano wa chama cha ACT.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amewataja maadui zake pamoja na watu wasiokitakia mema chama cha  kipya katika medani za siasa  ACT-Wazalendo.
Akiuhutuba mamia ya wananchi jana katika viwanja vya Furahisha mkoani Mwanza Zitto  amesema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha. Pamoja na hali hiyo ACT-Wazalendo haiko tayari kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya njema kwa siasa za upinzani.
Amesema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele,  wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.
“Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki,” amesema Zitto.
Amesisitiza kuwa  hakufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani, kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana.
Akizungumzia ujamaa amesema ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Chama cha ACT-wazalendo leo kinatarajia kuendelea na ziara yake  Musoma baada ya kufanya mikutano katika mikoa ya Ruvuma,Singida na Tabora.

Ghasia Afrika kusini: Watanzania 21 kurejeshwa, 3 wafariki dunia

Ghasia Afrika kusini: Watanzania 21 kurejeshwa, 3 wafariki dunia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe Membe.
kusini zinazohusisha wazawa kuwatimua wageni nchini humo.
Akizungumzia uamuzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amesema watanzania 21 watarejeshwa nchini kutokana na vurugu zinazoendelea za wenyeji kuwashambulia wageni huko Afrika Kusini.
Ameongeza kuwa   watanzania watatu wamefariki kwa maradhi lakini si kuuawa katika vurugu hizo, na kusisitiza kuwa  hakuna mtanzania aliyeuawa kutokana na machafuko hayo.
Amesema habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba kuna watanzania waliokufa ni kweli il watanzania hao wamekufa katika matukio tofauti na vurugu hizo. Watanzania hao ni Athman China aliyefariki kwa kupigwa kisu gerezani, Rashidi  mohamed  aliyeuawa kilomita  90 toka tukio la uporaji pamoja na Ali Heshi Mohamed aliyekufa kwa ugonjwa wa TB kutokana na maelezo ya polisi nchini humo.
Katika hatua nyingine Waziri Membe amewataka watanzania kujiandikisha  katika ubalozi  Tanzania nchini humo ili serikali iweze kuwarejesha nchini wakati  serikali ya Afrika kusini ikilishughulikia suala hilo.

Friday 10 April 2015

Breaking News: Mgomo wa Madereva Waanza Asubuhi ya Leo Sehemu Mbalimbali Nchini

Breaking News: Mgomo wa Madereva Waanza Asubuhi ya Leo Sehemu Mbalimbali Nchini.


Mgomo  wa  Madereva  umeanza  rasmi  leo  katika  maeneo  mbalimbali   nchini kama ambavyo muungano wa madereva wa vyombo vya usafiri waliahidi wakidai kutotatuliwa kero zao na serikali.
Sababu  kubwa  ya  madereva  hao  kugoma  ni  kuishinikiza  serikali  kuweka  mfumo  mzuri  wa  ajira  na  kupinga  kanuni  inayowataka  kurudia  kusoma  katika  chuo  cha  taifa  cha  usafirishaji,NIT  kila  leseni  zao  zinapokwisha  muda. 
Madereva  hao  wanadai  malalamiko  yao  makubwa  ni  kitendo  cha  Serikali  kuongeza  kifungu  kidogo  katika  sheria  mpya  ya  mwaka  2015  namba 31  inayowataka  madereva  wote  wenye  leseni  za  madaraja  E,C1,C2,C3  na  C kurudi  darasani  kila  baada  ya  miaka  mitatu  kuongeza  utaalamu  katika  fani  hiyo  ya  udereva  ili  kupunguza  ajali  za  mara  kwa  mara  zinazotokea. 
 
Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungu huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
 
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.

Sakata la Gwajima: Polisi Wamhoji Kwa Masaa Matano..... Atakiwa Kurudi Polisi Wiki Ijayo na Hati ya Usajili wa Kanisa Lake,Helkopta na Viwanja Anavyomiliki

Sakata la Gwajima: Polisi Wamhoji Kwa Masaa Matano..... Atakiwa Kurudi Polisi Wiki Ijayo na Hati ya Usajili wa Kanisa Lake,Helkopta na Viwanja Anavyomiliki


Askofu wa  Kanisa la Ufufua na Uzima Josephat Gwajima amelitikisa  tena  Jiji la Dar es Salaam jana  mara   baada  kuwasili makao  makuu  ya  Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ili  kuendela  na  mahojiano kuhusu tuhuma za kumkashfu  Askofu Pengo.
 
Gwajima aliwasili  Makao Makuu ya Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Majira ya saa mbili kamili asubuhi huku akisindikizwa na viongozi mbali mbali wa Kanisa la Ufufuo na Uzama pamoja na Mwanasheria wake .
 
Eneo  lote  la  kituo  hicho  cha  polisi  lilikuwa  chini  ya  ulinzi  mkali wa maofisa mbalimbali wa Usalama wa Taifa wakisaidiwa na Jeshi la Polisi.
 
Baada  ya  kuwasili  kituoni  hapo, umati mkubwa  wa Waumini wake ulizunguka  maeneo yote ya  Kituo hicho   huku  wengine  wakiwa maeneo ya stendi ya Treni ya Reli ya kati.
 
Kama  kawaida, Waumini  hao walikuwa  wakiimba nyimbo mbalimbali ambazo wanadai zilikuwa  mahususi  kumpa nguvu Askofu huyo ajibu kesi hiyo kwa ufasaha.
 
Baada  ya  Mahojiano  ya  takribani  masaa  Matano, hatimaye   Askofu Gwajima  alitoka  ndani  ya kituo  hicho,lakini  katika  hali  isiyo  ya  kawaida,Askofu  huyo  aligoma kuongea na vyombo vya habari.
 
Baada  ya  Gwajima  kugoma  kuongea,mwandishi wetu  alimfuata Mwanasheria  wake  aliyekuwa  ameambatana  naye,John Mallya  ambaye alisema kuwa  mteja  wake  alikuwa  amechoka, hivyo  asingeweza  kuongea.

Mallya  alimweleza  mwandishi kuwa  mambo aliyohojiwa  Gwajima   ni kuhusu mali zake na sio matamshi ya kumtukana Askofu  Pengo.
 
“Mahojiano yamekwenda vizuri lakini nasikitika sana kutokana na mambo waliyokuwa wanamhoji. Wamemuuliza mambo ambayo hayahusiani kabisa na kile tulichotarajia na ndicho kilichotuleta hapa, nilidhani mteja wangu ataulizwa kuhusiana na matumizi ya lugha chafu iliyodaiwa kutumika kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini,” alihoji wakili wa Gwajima.
 
Aliendelea kusema kuwa, mambo aliyoulizwa ni kuhusiana na ukoo wake, wazazi wake hata ndugu zake na watu wengine wa kwao waliokufa.
 
Alisema walihoji pia juu ya mambo mengine kama umiliki wa helikopta, utajiri wake, nyumba anayoishi, uhusiano wake na watu mbalimbali.
 
“Nimeshangaa sana kuona mteja wangu ameulizwa vitu kama hivyo ambavyo havihusiani na madai ya hapo awali ya matumizi ya lugha ya matusi. Tumeagizwa tulete nyaraka kumi siku ya mahojiano yetu tena yatakayofanyika tarehe 16 mwezi huu na sisi tutafanya hivyo,” alisema Mallya.
 
Alizitaja nyaraka na vitu vingine wanavyotakiwa kuvipeleka Aprili 16 ni hati ya usajili wa kanisa, bodi ya udhamini wa kanisa na majina yao, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake, na muundo wa uongozi wa kanisa lake.
 
Vingine ni namba ya usajili wa kanisa, ritani za kanisa lake (mapato na matumizi ya fedha za kanisa lake), mtu anayechukua na kurekodi mkanda wa video kanisani kwake, pamoja na waraka wa Baraza la Maaskofu uliosomwa makanisani.

Ngorika, Ratco za ua 10 Tanga.



Ngorika, Ratco za ua 10  Tanga.




Basi la Ngorika mara baada ya kupata ajali.
Watu 10 wamefariki dunia katika  ajali iliyohusisha magari 3 katika eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani  Handeni  Mkoani  Tanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga,  Juma ndaki  amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaam kwenda Tanga na Arusha.
Ameongeza kuwa baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha. Katika ajali hiyo kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano na wanawake watano.

Thursday 9 April 2015

Tishio la Ugaidi: Jeshi la Polisi laimarisha Ulinzi Dar es salaam


Tishio la Ugaidi: Jeshi la Polisi laimarisha Ulinzi Dar es salaam



Askari wa kikosi cha mbwa .
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jijini  la Dar es salaam kufuatia kuwepo kwa taishio la kutokea ugaidi katika mikoa ya Dar es salaam na Mwanza.
Akizungumza na Mtandao wa Hivisasa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam  Suleiman Kova amesema kwamba  hali  ya  usalama ni shwari na kuahidi kuongeza   opereshini ya kukamata wauza dawa za kulevya, wahalifu  na  pamoja na kulinda maeneo ya fukwe ambayo ni vichochoro vya matukio ya kihalifu.
Ameongeza kuwa Jeshi hilo   limejipanga  kukabiliana  na  vitendo  vya  kigaidi  ambapo  wanafanya  uchunguzi  kila  mahali  kwa  kutumia  vikosi  vya  mbwa, farasi, helkopta, magari, pikipiki  na  kutembea  kwa  miguu  katika  maeneo  yote  ya  jiji.
Tishio la kigaidi nchini Tanzania linafuatia tukio la kukamatwa mtanzania nchini Kenya anayedaiwa kuwa ni mmoja wa magaidi walio wauwa takribani wanafunzi  148 katika chuo kikuu cha Garissa.

Thursday 2 April 2015

Simba yaingia mkataba ‘mnono’ na EAG Group Limited

Simba yaingia mkataba ‘mnono’ na EAG Group Limited


Makamu wa Rais wa klabu ya Simba SC Godfrey Nyange ‘Kaburu’ akifafanua jambo
Klabu ya ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba, leo imeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya EAG Group Limited ambao utahusika na masuala ya kuitafutia dili za kuiingiza pesa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi wa EAG Imani Kajula amesema kuwa, mipango yote ya kuendesha dili hilo anaipata kutoka katika Klabu ya Arsenal ya England ambayo anafanya nayo kazi.
Kajula amesema katika mkataba huo anataka kuiona Simba inakuwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa kuitafutia vyanzo vingi vya mapato ili iache kutegemea mapato ya mlangoni na ada ya wanachama pekee.
Naye rais wa klabu hiyo Evans Aveva amesema, anaamini mpango huo utawawezesha kuendeleza jengo lao la makao makuu liliopo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar.
Aidha katika hatua nyingine, klabu hiyo imetangaza kuwa kila mwisho wa msimu itakuwa inamtangaza mchezaji wao bora wa klabu kwa mwaka ambapo atazawadiwa zawadi ya gari la kisasa huku mchezaji bora kijana akipewa pesa shilingi milioni tano na mchezaji mwenye nidhamu atapokea milioni mbili.
Amesisitiza kuwa washindi hao wote kila mmoja pia atazawadiwa simu ya kisasa aina ya Huawei Ascend Mate 7 yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kutoka kampuni ya Huawei ambayo wameingia udhamini na klabu hiyo.

Mjomba afukua kaburi la Ndugu yake mwenye ualbino na Kuiba mifupa

Mjomba afukua kaburi la Ndugu yake mwenye ualbino na Kuiba mifupa


Watu wawili  akiwemo mjomba wa marehemu ajulikanaye kama  January Korongo wamekatwa na Jeshi la Mkoani Kagera kwa tuhumza za kufukua kaburi la mtu mwenye ulemavu wa ngozi albino aliyefariki dunia mwaka 1991 na kuchukua mifupa yote iliyokuwemo katika jeneza kwa lengo la kuiuza.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Laston Faustine (41), ambaye ni mkazi wa Lukulaijo aliyekutwa na mfuko uliokuwa umehifadhi mifupa mitatu ya binadamu na mwingine ni January Korongo (43), mkazi wa Kadengesho, wiyani Karagwe.
Watu hao walikamatwa Machi 27, mwaka huu, katika nyumba moja ya kulala wageni, iliyoko eneo la Kyaka, Wilaya ya Missenyi baada ya kukutwa wakiwa na baadhi ya viungo hivyo, ambavyo walikuwa wanakwenda kuviuza walivovitoa katika jeneza mwaka 2009.
Mwaibambe alisema baada ya kumhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi nyumbani kwake, ambako alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali, ambayo ilikuwa imefungwa kwenye mfuko nje ya nyumba yake.
Hata hivyo jeshi la polisi lilifanikiwa kufukua kaburi hilo na kukuta viungo vyote vimetolewa.
Watuhumiwa hao wote wanatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma hizo hivi karibuni.

Mambo 10 usiyojua kutoka kwa Rais mpya wa Nigeria

Mambo 10 usiyojua kutoka kwa Rais mpya wa Nigeria


Taifa kubwa barani Afrika Nigeria limemaliza mchakato wa urais huku ushindi wa kishindo wa Muhammadu Buhari akimuangusha Goodluck Jonathan kwa kura milioni 15.4 kwa kura za mpinzani wake Goodluck Jonathan ambaye alipata kura milioni 12.9. Hapa inaonekana wananchi wa Nigeria wameona wachagua rais mwingine ambaye ataweza kubadilisha hali ya machafuko nchini humo yanayofanywa na Boko Haram ambaye Rais aliyekuwepo Goodluck Jonathan alishindwa.

Akihojiwa mara baada ya kutangazwa mshindi wa Urais nchini Nigeria Rais Muhammadu Buhari alisema maeneno machache ambayo ni ushindi wake huo ni wa wananchi wote wa Nigeria.
Mambo 10 usiyoyajua kutoka kwa Rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari;
-Ana miaka 72
-Rais wa kwanza wa Nigeria kutoka chama cha upinzani
-Muislamu kutoka kaskazini mwa Nigeria
-Alikuwa kiongozi wa Jeshi kuanzia 1984-1985
-Ana rekodi mbaya ya haki za binadamu
-Mtu anaependa sana nidhamu kazini
-Alitoroka kwenye mauaji ya Boko Haram
– Sio mpenda Rushwa
-Ameshinda uchaguzi kwa tofauti ya kura milioni 2.1
Rais wa kwanza wa Nigeria kutoka chama cha Upinzani

clouds stream