Friday 29 September 2017

WAZIRI,WABUNGE 25 AKIWEMO BOBI WINE WAPIGWA ‘STOP’ UGANDA





Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga amewasimamisha Waziri mmoja na wabunge 25 kuhudhuria vikao vya bunge kwa
madai ya kushiriki katika vurugu ambayo ilimlazimisha kuahirisha kikao siku ya Jumatano.
Mmoja wa waliozuiliwa kuhudhuria vikao ni Waziri wa Maji, Ronald Kibuule kwa madai ya kwenda katika ukumbi wa bunge akiwa
na silaha.
Wabunge wengine waliosimamishwa kuhudhuria vikao wengi wao ni wa upinzani wanaopinga kufutwa kwa kifungu 102(b) kutoka
katika katiba ambayo inakataza watu ambao wana umri zaidi ya miaka 75 kugombea nafasi ya urais, ambao siku ya jana
walikataa kutoka katika ukumbi wa bunge na kumlazimisha spika kuahirisha kikao.
Miongoni mwa waliozuiwa kuhudhuria vikao vya bunge ni pamoja Robert Kyagulanyi a.k.a Bobi Wine (Kyaddondo Mashariki), MP
Allan Ssewanyana (Makindye Magharibi), Monica Amoding (Wilaya ya Kumi ), Dkt. Sam Lyomoki (Wafanyakazi) Betty Nambooze
(Manispaa ya Mukono) Ibrahim Kasozi (Makindye Mashariki) na Moses Kasibante (Rubaga Magharibi).
Baada ya mgogoro huo, maafisa wa ulinzi wakiwa katika vazi la suti walivamia Ukumbi huo na kuwalazimisha Kyagulanya na
Ssewanyana kutoka nje.
Serikali ya Uganda inataka kuondoa ukomo wa umri kwa wagombea urais kitu kilicholeta vurugu Jumatano katika Bunge la
Uganda baada ya Spika kuanza kuzungumzia suala hilo.
Hatua hiyo ya Serikali itamwezesha Rais, Yoweri Museveni kuendelea na nafasi yake ya urais na kugombea katika uchaguzi ujao.
Sheria hizo zilikuwa tayari zimebadilishwa mwaka 2005 zikiondoa ukomo wa awamu mbili ambapo ilimwezesha Museveni ambaye
sasa ana umri wa miaka 72 kuendelea kuwepo madarakani akiwa anahudumu awamu yake ya tano sasa.
Chini ya katiba iliyokuwepo Rais Museveni atakuwa amepitiliza umri unaoruhusiwa na katiba kugombea katika uchaguzi wa
mwaka 2021.

Upinzani Kenya waitisha maandamano makubwa wiki ijayo

Raila Odinga

Raila Odinga


Muungano wa upinzani nchini Kenya umeitisha maandamano ya umma kupinga mapendekezo ya kuifanyia mabadiliko sheria ya uchaguzi.

Wabunge wanaoegemea upande wa serikali wanafanya hima kupitisha mswada ambao utamwezesha Uhuru Kenyatta kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa upinzani utasusia marudio ya uchaguzi tarehe 26 mwezi Oktoba.

Wanachama wa upinzani walitoka nje wakati upande wa serikali ukitumia wingi wake bungeni kuharakisha mabadiko ambayo yatasababisha mswada huo kuwa sheria kabla ya marudio ya uchaguzi.

Kati ya yale yaliyo kwenye mswada huo ni kuruhusu mgombea kutangazwa rais bila ya kufanyika uchaguzi ikiwa mgombea mwingine atasusia uchaguzi.

Marudio hayo ya uchaguzi yana wagombea wawili, Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Mswada huo pia unasema kuwa mahakama ya juu haiwezi kufuta matokeo ikiwa mfumo wa eletroniki utafeli

Kufeli kwa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya eletroniki ndio ilikuwa sababu kuu ya kufutwa kwa matokeo ya urais.

Mgombea wa Upinzani Raia Odinga amekashifu hatua hizo kama jaribio la kuiba kura na kumpendela rais Uhuru Kenyatta.

Ametisha maandamano ya kote nchini kila Jumatatu na Ijumaa kuanzia wiki ijayo.

BUNGE LATOA NENO MBOWE KUNYANG’ANYWA GARI NAIROBI



Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.



Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema Mbunge wa Hai (Chadema)
naKiongozi wa Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni (KUB), Mhe. Freeman Mbowe hajanyang’anywa gari kama ilivyotaarifiwa mapema jana jioni ila limerudishwa nchini ili dereva wake aweze kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi.

Mapema jana jioni Chadema ilisema kuwa kiongozi huyo alinyang’anywa gari hilo akiwa analitumia Jijini Nairobi, Kenya kwa ajili yakumsaidia katika kumuuguza Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa nchini Kenya kufuatiakushambuliwa kwa kupigwa risasi Septemba 7, mwaka huu, Mkoani Dodoma.

Tuesday 26 September 2017

Abiria Wanusurika Kufa Baada Ya Basi Kuteketea Moto Barabarani



Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam wamenusurika kufa baada ya basi walilokuwa wamepanda
la Kampuni ya Tashriff kuteketea kwa moto.
Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa waliona moshi ukitoka chini ya basi hilo ndipo wakapiga kelele na kusababisha dereva
kusimama dakika chache baada ya hapo likaanza kuwaka moto.
“Tulisikia kelele kutoka kwa watu waliokuwa nje tukaona dereva kasimamisha basi muda si mrefu moshi ulianza kutoka mara
moto ukalipuka,” abiria mmoja aliyesafiri na basi hilo amenukuliwa akisema.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali majira ya saa nane mchana katikaeneo la Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga.
Kamanda Wakulyamba amesema basi hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa na Hemed Ali (35) lilikuwa na abiria 29 ambapo hakuna
aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha.
“Hakuna aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha, abiria wote walitoka salama isipokuwa mizigo na mali zao zote zimeteketea moto,”ameongeza.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha moto huo katika ajali hiyo.

Jeshi La Polisi Lasema Haya Kuhusu Maiti 3 Zilizokutwa Coco Beach


Jeshi la Polisi limesema kuwa bado halijapelekewa uthibitisho kuhusiana na maiti za wanaume watatu waliokutwa pembezoni
mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach ili liweze kutolea ufafanuzi.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema iwapo atapelekewa udhibitisho huo ni lazima
atatolea ufafanuzi suala hilo kiundani zaidi.
“Sijaletewa ‘fact’ nikiletewa nitalitolea ufafanuzi,” amesema Kamanda Mambosasa.
Maiti za watu hao zilikutwa juzi Septemba 24 huku mbili zikiwa zimefungwa kwenye viroba na nyingine ikiwa imekutwa na jiwe
kubwa lililofungwa na kamba.
Maiti hizo ziligunduliwa na wafanyabiashara wa mihogo wa eneo hilo waliokuwa katika biashara zao asubuhi na ghafla waliona
maiti moja ikielea karibu na miti aina ya mikoko ikiwa na jiwe lililofungwa kifuani huku mikono yake ikiwa imefungwa na kamba.
Mmoja wa wafanyabiashara, Aziza Ally amesema baada ya kuona maiti hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika saa 4 asubuhi
na kuichukua kwenye gari lao.
Amesema ilipofika saa 8 mchana waliona maiti mbili kila moja ikiwa kwenye kiroba zikielea ndipo mmoja wao alipoamua kutoa
taarifa polisi baadaye zikachukuliwa.
“Polisi walipokuja kuchukua hizi maiti hakuna hata mtu mmoja aliyeruhusiwa kusogelea na kupiga picha tulishangaa sana kuona
ulinzi mkali tofauti na siku zote na aliyebainika amepiga alipokonywa simu yake,” amesema Ally.

WAFUASI WA ODINGA WAINGIA BARABARANI




Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Kenya ‘IEBC’, Ezra Chiloba amedaiwa kutangaza kuachia ngazi leo huku
wafuasi wa Muungano wa Upinzani (NASA) wakifanya maandamano katika baadhi ya maeneo nchini humo kushinikiza
kuondolewa kwa maafisa 12 wa tume hiyo akiwemo Ofisa Mtendaji Mkuu wa IEBC kwa shutuma za kuvuruga uchaguzi wa Agosti8, mwaka huu.
Maandamano hayo yaliyotawaliwa na ghasia katika baadhi ya maeneo ni mwitikio wa wito uliotolewa jana na Kiongozi wa
Upinzani, Raila Odinga aliyewataka wafuasi wake kujitokza kwa wingi kuandamana hadi Makao Makuu ya IEBC, ikiwa ni siku
chache tu zimepita tangu Mahakama ya Juu Kenya kufutilia mbali matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.
Wafuasi wa NASA walikuwa wakimshutumu Chiloba na watendaji wengine kufanya njama za kuingilia mchakato wa uchaguzi huo
na kumsaidia Rais Kenyatta kuibuka kidedea.
Waandamanaji hao wamebeba matawi ya miti, mabango, huku wakipiga mayowe na honi za pikipiki kuanzia barabara ya Obote,
kasha mtaa wa Oginga Odinga kabla ya kuchukua barabara kuu ya Kenyatta hadi Mtaa wa Ang’awa katikati ya Jiji la Nairobi huku
watu wachache wakiwa wametiwa nguvuni na Jeshi la Polisi.
Haya yanajiri ikiwa ni siku 30 tu zimesalia hadi kufanyika uchaguzi wa marudio, Oktoba 26, mwaka huu.

Monday 25 September 2017

Alexander Lacazette Shujaa wa Arsenal

Alexandre LacazetteMshambuliaji mpya wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette jana jumatatu usiku alifanikiwa kuifungia mabao 2 - 0 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi kuu ya England , kwa bao la dakika ya 20 kipindi cha kwanza na bao lingine la dakika ya 67 kipindi cha alilofunga kwa njia ya penati.

Alexandre Lacazzete mpaka sasa amevunja rekodi ya Brian Marwood iliyowekwa mwaka 1988 ya kufunga katika michezo mitatu ya mwanzo ya ligi ya Epl. Kwa matokeo hayo yanawafanya Arsenal kubaki katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama zao 10 huku Manchester City wakiwa kileleni.

Upinzani kuandamana Kenya


Viongozi wa upinzani nchini Kenya Kalonzo Musyoka, Raila Odinga na Musalia MudavadiVinara wa upinzani Kenya Kalonzo Musyoka, Raila Odinga na Musalia Mudavadi

Chama cha upinzani nchini Kenya NASA kimeitisha maandamano Jumanne nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.

Hatua hii ni ya kushinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya maafisa wa juu wa tume hiyo walioshiriki kuandaa uchaguzi mkuu wa August 8 mwaka huu uliobatilishwa na mahakama ya juu nchini.

NASA umeeleza kwamba hautovamia makao ya tume ya IEBC kama ilivyotajwa awali kuwatimua kwa lazima maafisa hao, badala yake unasema maandamano yatakuwa ya amani katika barabara za mji mkuu Nairobi kushinikiza kujiuzulu kwao.

Hilo ni mojawapo ya masharti iliyotoa NASA kushiriki uchaguzi wa marudio uliotangazwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.

Rais Uhuru Kenyatta ametoa onyo kwa wapinzani ambao amesema watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yao yataingilia shughuli za kiuchumi za raia wa nchi hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta ameuonya upinzani kuwa watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yatakumbwa na ghasiaUhuru Kenyatta ameuonya upinzani kuwa watakumbana na mkono wa sheria iwapo maandamano yatakumbwa na ghasia

Amesema, 'Endeleeni na maandamano yenu, mukigusa mboga za mama wanaouza barabarani, tuko na nyinyi. Mukigusa maduka ya watu tuko na nyinyi. Lakini kama hamuna lingine lolote la kufanya isipokuwa kutembea - tembeeni. Mimi nawaambia hata mukinitukana mpaka asubuhi, haitabadilisha dunia'.

Upinzani unasisitiza kuwa una haki ya kuandamana kwani hata upande wa serikali - Muungano wa Jubilee - umeshafanya maandamano kama hayo hivi juzi walipoelekea katika mahakama ya juu zaidi wakitaka majaji wa mahakama hiyo waondolewe.

Mmoja ya vinara waandamizi wa kambi ya upinzani, Musalia Mudavadi ameiambia BBC, kuwa mahakama ya juu zaidi ilisema IEBC ilishindwa kuandaa uchaguzi mkuu kulingana na sheria.

Ameeleza, 'Tume ya IEBC sio vyombo tu, bali ina watu ndani ambao ni maafisa wanaohudumu katika kitengo cha usajili wa watu, masuala ya teknolojia ya mawasiliano na kadhalika, walishindwa kutekeleza wajibu wao na ndio wanaoweza kuondolewa.

Muungano wa NASA unataka jumla ya maafisa 12 wa tume hiyo washtakiwe kwa kutowajibika katika uchaguzi uliobatilishwa wa Agosti 8.

Unataka pia mfumo wa teknolojia uliotumiwa wakati wa uchaguzi huo ubadilishwe.

Msigwa ‘Akabana Koo’ Na Polisi

Related image
Mchungaji Msigwa Mbunge wa Iringa mjini.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema atalishitaki Jeshi la Polisi, kwa tuhuma za kuingilia
majukumu yake ya kikazi pale anapokuwa akitimiza wajibu wake wa kibunge ikiwemo kuongea na wananchi.
Mchungaji Msigwa amesema hayo kufuatia zuio kutoka Jeshi la Polisi linalomtaka kutoendelea na mikutano yake ya hadhara katika
kata za Mkoani humo hado pale Jeshi hilo litakaposema vinginevyo saa chache baada ya kumkamata akiwa jukwaani kwa tuhuma
za uchochezi kwa madai ya kukiuka masharti alipohutubia katika Kata ya Mlandege.
Amesema hatahivyo atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo kwani alitarajia kufanya mikutano katika kata za Kihesa na Kitwiru
Mchungaji Msigwa amesema chombo pekee kinachoweza kumtia hatiani kwa kufanya uchochezi ni Mahakama na sio polisi.
“Walinikamata tangu saa 11:30 na kuanza kunihoji mpaka saa 3:15 usiku kwa tuhuma za kufanya uchochezi lakini mimi nakataa
sijafanya uchochezi kwa sababau hakuna mtu anaweza kunizuia kuongea na wananchi wangu, wanadai nimeleta hofu na
kuvichonganisha vyombo vya dola na wananchi,” amesema Mchungaji Msigwa .
Amesema kwasasa yupo nje kwa dhamana na tayari ameripoti polisi asubuhi jana Jumatatu, amehojiwa lakini ameambiwa ataitwatena kwa mahojiano zaidi.
“Mimi niko tayari hata kama wangeniweka ndani wiki mbili siogopi kwa sababu sitanyamaza nitaendelea kuongea na sitaacha
kusema kilichomtokea Tundu Lissu na ili kuninyamazisha ni lazima waniue kwa sababu nishajiandaa kisaikolojia,” amesema
Mchungaji Msingwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema walimkamata Msigwa kwa kuwa alikuwa anatoa maneno ya uchochezi
kwa wananchi aliokuwa anawahutubia mkutano wa hadhara Kata ya Mlandege.
Kamanda Mjengi amesema bado jeshi hilo linaendela na upelelezi juu ya tuhuma hizo na mara utakapokamilika watamfikisha
mahakamani Mbunge Msigwa.

Friday 8 September 2017

VIGOGO WALIOTAJWA SAKATA LA MADINI WATAKIWA KUJIUZULU

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Rais Dkt.John Pombe Magufuli amewataka Vigogo wote wakiwemo Mawaziri aliowateua kujitathimini kufuatia kutajwa na Kamati mbili za Bunge zilizochunguza biashara ya madini ya Almasi na Tanzanite.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea ripoti mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuchunguza biashara ya madini ya Almasi na Tanzanite ambazo zimeibua uozo zikiwahusisha baadhi ya watendaji wa Serikali.

Vigogo hao ni waziri George Simbachawene ambaye kwa sasa ndiye Waziri katika Ofisi ya Rais Tamisemi ambaye alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, anatajwa kuhusiana na biashara ya Tanzanite ambapo aliridhia mabadiliko katika mauzo ya kampuni uchimbaji Tanzanite na utoaji wa leseni kinyume na utaratibu.

Naibu Waziri Edwin Ngonyani naye ametajwa kuhusiana na kadhia ya kuzuia Serikali kununua mgodi wa almasi kwa dola milioni 10 na kuikosesha Serikali zaidi ya dola milioni 300, fedha ambazo zilienda kwa kampuni iliyonunua hisa.

Aidha kamati hiyo ilihoji namna ambavyo walioshiriki kukataa Serikali kununua mgodi huo wa almasi walivyopata bahati ya kuchaguliwa katika bodi ya waliouziwa hisa.

Kitendo cha Eliakim Maswi kusema kwamba alipatwa na hasira baada ya kutoka katika mgodi huo wa almasi na kujionea madudu na kuapa kutokanyaga tena kulielezwa na kamati hizo kuwa moja ya sababu ya watendaji kuacha mambo yakiharibika.

Aidha aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo ametajwa kupindisha mambo kadhaa na kufanya maamuzi bila kushirikisha bodi zinazotakiwa na hivyo kusababisha hasara kubwa.

Watu wengine waliotajwa katika taarifa zote mbili ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngereja, mwanasheria wa zamani George Werema Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) nalo limetajwa kuwa limeshindwa kusimamia Mikataba na Biashara ya Madini hivyo kupelekea Taifa kupata Hasara kubwa.

Mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hizo Rais Magufuli naye amekabidhi kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili ziwakamate na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria vigogo hao.

Kwa mujibu Ushauri wa kamati Kwa upande wa kamati ya Dk Bitego iliyochunguza tanzanite imesema kuna haja ya kuwawajibisha wote waliohusika kuliingiza taifa hili katika mikataba mibovu isiyokuwa na tija na kuleta hasara.

Thursday 7 September 2017

CHAMA CHA KENYATTA CHAPINGA KUFUMULIWA TUME YA UCHAGUZI

Uhuru Kenyatta.
Uhuru Kenyatta.
IMG-20170426-WA0006

Chama cha Jubilee, cha rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kimepinga kundi la Vigogo tisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya mwezi ujao.

Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maafisa hao ambao kinasema wanajulikana kwamba “wanapendelea upande fulani”.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC alitangaza kundi la maafisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 17 Oktoba siku ya Jumanne.

Maafisa hao ambao wanajumuisha mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na msimamizi wa kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo watafanya kazi kwa miezi mitatu.

Chama cha Jubilee kimesema: “Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maafisa hao (watakaosimamia uchaguzi) kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande Fulani.”

Mahakama ya Juu imefuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti ambapo Rais Kenyatta alitangazwa mshindi kwa madai kuwa Tume ya Uchaguzi IEBC haikuandaa uchaguzi huo kwa njia na kwa kiwango kinachokubalika kikatiba.

CHAMA CHA KENYATTA CHAPINGA KUFUMULIWA TUME YA UCHAGUZI

Uhuru Kenyatta.
Uhuru Kenyatta.
IMG-20170426-WA0006

Chama cha Jubilee, cha rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kimepinga kundi la Vigogo tisa wakuu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo ambao wanatarajiwa kusimamia uchaguzi mpya mwezi ujao.

Chama hicho kimetoa orodha ya majina ya maafisa hao ambao kinasema wanajulikana kwamba “wanapendelea upande fulani”.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC alitangaza kundi la maafisa saba watakaoongoza maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika tarehe 17 Oktoba siku ya Jumanne.

Maafisa hao ambao wanajumuisha mkuu wa kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na msimamizi wa kituo cha taifa cha kujumlishia matokeo watafanya kazi kwa miezi mitatu.

Chama cha Jubilee kimesema: “Tuna habari za kuaminika kwamba kwenye orodha ya maafisa hao (watakaosimamia uchaguzi) kuna watu wanaofahamika wazi kuegemea upande Fulani.”

Mahakama ya Juu imefuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 8 Agosti ambapo Rais Kenyatta alitangazwa mshindi kwa madai kuwa Tume ya Uchaguzi IEBC haikuandaa uchaguzi huo kwa njia na kwa kiwango kinachokubalika kikatiba.

Taarifa Uchunguzi Almasi, Tanzanite Kutua Kwa JPM ‘Live’ Leo

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli leo anatarajiwa kupokea taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite na Almasi uliofanywa na Kamati Maalum mbili zilizoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai.

21317572_994121220729369_7894129644206341507_n

Tuesday 5 September 2017

Wabunge UKAWA Wasusia Kuapishwa Kwa Wabunge Wa CUF

Related image

Wabunge kutoka Upinzani katika Umoja wa Ukawa leo asubuhi wametoka nje ya Bunge na kususia shughuli ya kuapishwa kwa wabunge 7 wa Viti Maalum CUF.

Shughuli ya kuapishwa kwa wabunge hao imefanyika leo na Spika Job Ndugai kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu katika Mkutano wa 8 Bunge la 11.

Wabunge hao waliteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuziba nafasi ya wabunge nane wa Viti Maalum CUF waliotimuliwa uanachama na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.

Mmoja wa wateule hao, Bi. Hindu alifariki dunia siku chache kabla ya kuapishwa na hivyo kufanya idadi ya wabunge waliokula kiapo leo kuwa saba badala ya nane kama walivyoteuliwa.

Meya Chadema,Waziri Ummy Wazindua Bima Ya Afya Bure Kwa Wazee

Wazee mara baada ya kupata Bima ya  Afya.
Wazee mara baada ya kupata Bima ya Afya.
IMG-20170426-WA0006

Meya wa Ubungo Boniface Jacob pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu wamezindua huduma ya Bima ya Afya Bure kwa wazee wilaya ya Ubungo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa vitambulisho vya wazee Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema utekelezaji wa matibabu bure kwa wazee ni wa lazima na siyo hiari kwakuwa serikali ya awamu ya tano imeweka sera zinazotekelezeka kwa kila hospitali za umma.

Mwalimu amezitaka Hospitali kubwa za rufaa kuweka taratibu maalumu za kuwasaidia wazee wenye kadi za bima ya afya ili kuhakikisha wanaokoa maisha yao.

Naye Mstahiki Meya wa Ubungo Boniface Jacob amesema gharama zilizotumika ni za mapato ya wilaya hiyo na sio mkopo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori amesema utekelezaji wa kutoa huduma kwa wazee kwa Manispaa hiyo kwa kufuata kadi hizo utazingatia weledi na haki ili kuondoa kero kwa wazee hao.

clouds stream