Monday 27 March 2017

Uholanzi yamtimua kocha wa timu ya taifa

Danny Blind ni baba wa mlinzi wa Man United Daley Blind

Danny Blind ni baba wa mlinzi wa Man United Daley Blind
img-20161130-wa0008

Uholanzi imemtimua kocha wa timu yake ya taifa Danny Blind baada ya kudumu kwa takriban miaka miwili.

Hii inafuatia kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Bulgaria siku ya Jumamosi na kuwaacha Uholanzi katika nafasi ya nne kwenye mbio za kufuzu kushiriki kombe la dunia.

Blind mwenye miaka 55 alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Guus Hiddink mwaka 2015 huku ikishuhudiwa kikosi chake kikishindwa kufuzu fainali za michuano ya Ulaya mwaka jana.

Chama cha soka nchini Uholanzi kimesema kuwa ameicha timu hiyo katika wakati mgumu kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi.

Fred Grim ameteuliwa kuwa kocha wa mpito na atakiongoza kikosi hicho siku ya Jumanne dhidi ya Ufaransa.

Wasichana waliovalia suruali za kubana wazuiwa kuabiri ndege ya United Airlines Marekani

Ndege za United Airlines

Shirika hilo la ndege limeshutumiwa sana kwenye Twitter
img-20161130-wa0008

Shirika la ndege la United Airlines nchini Marekani limeshutumiwa sana baada ya kudaiwa kuwazuiwa wasichana wawili waliokuwa wamevalia suruali ndefu za kubana kuabiri ndege hiyo.

Kisa hicho kilitokea kwenye safari ya ndege iliyokuwa ikitokea Denver kuelekea Minneapolis Jumapili asubuhi, mwanaharakati Shannon Watts amesema.

Shirika la United limesema wasichana hao walikuwa wanasafiria hati maalum, ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa shirika la ndege na wageni wao.

United wamesema huwa kuna kanuni za mavazi kwa wanaotumia hati hiyo kusafiria.

Shirika hilo limefafanua kwamba abiria wa kawaida, ambao wanalipia tiketi zao, wako huru kuvalia mavazi yao ya kubana.

Hati hiyo maalum ya kusafiria ya United huwawezesha walio na hati hiyo kusafiri kwa ndege bila malipo au kwa tiketi za bei nafuu sana.

Kanuni za mavazi kwa wanaotumia hati hiyo huel

UN yalaani mauaji ya watoa misaada Sudan Kusini

Wafanyakazi 12 wa mashirika ya kutoa misaada wameuawa mwaka huu pekee

Wafanyakazi 12 wa mashirika ya kutoa misaada wameuawa mwaka huu pekee
img-20161130-wa0008

Umoja wa mataifa umelaani vikali mauaji ya wafanyakazi sita wa kutoa misaada nchini Sudan Kusini.

Miongoni mwa waliouawa ni raia watatu kutoka Kenya, na watatu kutoka Sudan Kusini ambao walitekwa siku ya Jumamosi walipokuwa wakisafiri kutoka mji mkuu Juba kwenda mji wa Pibor.

Hili ni tukio la tatu la aina hiyo ndani ya mwezi mmoja likiwa limepoteza maisha ya watu wengi tokea kuanza kwa mgogoro huo mwaka 2013.

Mkuu wa mashirika ya kibinaadam nchini Sudan Kusini Eugene Owusu ameelezea mauaji hayo kama uhalifu wa kutisha.

Wafanyakazi 12 wa mashirika ya kutoa misaada waneuawa mwaka huu, wakati huu ambapo wanajaribu kuelekea sehemu ambazo umaskini ni mkubwa kutokana na vita.

Urusi: waandamana kupinga matumizi mabaya ya madaraka

Polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji

Polisi wanatuhumiwa kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji
img-20161130-wa0008

Maelfu ya raia wamekusanyika katika maeneo tofauti nchini Urusi wakiandamana kupinga kile wanachodai matumizi mabaya ya fedha za umma.

Mkusanyiko mkubwa upo katika mji wa Moscow ambapo shinikizo ni kumtaka waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev kujiuzulu.

Wanaharakati wanasema kuwa hadi sasa watu 800 wanashikiliwa na Polisi.

Maandamano haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi ya yale yaliyowahi kutokea nchini Urusi kwa miaka mingi, ambapo wanadai kuwa waziri mkuu wao Dmitry Medvedev amekuwa akutumia fedha za umma

katika mambo yake binafsi kwa kujenga majumba kifahari, kununua boti za kifahari, mashamba ya mvinyo na jumba la kufugia bata.

Maandamano makubwa yalikuwa katika mji wa Moscow
Maandamano makubwa yalikuwa katika mji wa Moscow

Katika viunga vya Pushkin mjini Moscow, kuna kundi kubwa la waandamanaji waliokusanyika, mmoja wao amesema kuwa fedha za serikali zinaibiwa.

Marekani imeilaumu Urusi kwa hatua yake ya kuwashikilia mamia ya waandamaji kwa madai kuwa wanavuja haki dhidi ya maandamano ya amani kwa mujibu wa haki za binadamu.

Friday 24 March 2017

Nchemba Amtwisha Zigo IGP Nape Kutishwa Na Bastola

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba.
img-20161130-wa0008

 Waziri wa mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amemtaka IGP Ernest Mangu kumchukulia hatua Askari aliyemtisha Nape Nnauye kwa Bastola jana wakati anazungumza na Waandishi wa habari jijini hapa.

Kupitia taarifa yake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Nchemba amesema tukio lile halikuwa sahihi na kuagiza hatua zichukuliwe kwa kuwa Nape Nnauye si jambazi, hakuwahi kuwa na taarifa za uhalifu, sasa kwanini mtu amtishe kwa bastola tena mbele ya umati mkubwa uliojaa waandishi wa habari.

“Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni Mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha ki asikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.”

Aidha, Waziri Nchemba amesema kuwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kumbaini mtu huyo aliyefanya kitendo hicho na kumchukulia hatua stahiki.

Magufuli Aibua Madudu Akishitukiza Bandarini

Rais Dkt.John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushitukiza Bandarini jana.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushitukiza Bandarini jana.

img-20161130-wa0008Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu imebanisha kuwa Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 02 Machi, 2017.

Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Akiwa bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.

Maafisa wa bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana mitumba ya nguo na viatu.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.

Leo mmenifurahisha sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa, tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha, ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini, kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.Baadhi ya kontena lenye gari la kifahari likidaiwa kuwa na mitumba.

Nape Azungumza Chini Ya Ulinzi Wa Polisi

nape
img-20161130-wa0008

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewashukuru wanahabari kwa ushirikiano wao katika kipindi chote cha mwaka mmoja alichokuwa Waziri mwenye dhamana ya Habari.

Nape ametoa shukrani hizo leo nje ya Hoteli ya Protea, Jijini Dar es Salaam alipokuwa amepanga kukutana na wanahabari kabla ya Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzana Kaganda kumpigia simu mmiliki wa hoteli hiyo na kuzuia mkutano huo na kusema kuwa ameshangazwa na kitendo cha polisi kumuonyeshea bunduki alipokuwa akitaka kuzungumza na wanahabari.

Nape amemshukuru pia Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo na sasa muda umefika ameona aondoke katika wizara hiyo na kwamba hana kinyongo na uamuzi huo.

Amewataka wanahabari kuendelea kushirikiana vyema na Waziri anayekuja katika Wizara ya Habari, Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli ili kuzidi kuijenga Tanzania.

Awali Meneja wa Protea Hotel alidai kuwa amepigiwa simu na Kamanda wa polisi Kinondoni kusitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao uliitishwa na aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nauye na hivyo kumlazimu kuongea akiwa juu ya gari.

Hatahivyo, Kamanda Kaganda alifika eneo hilo na mara baada ya Nape kuagana na waandishi waliokuwa wakitaka aendelee kuzungumza aliitwa katika gari alimokuwa Kamanda Kaganda na kuzungumza kwa dakika chache kasha kurejea katika gari lake na kusema kila kitu kipo sawa.

“Naomba muendelee na shughuli zenu hakuna kitu chochote cha ajabu, huyu alikuwa anapita tukakutana hapa hivyo msiwe na wasiwasi. Mtanisaidia kama mtaondoka eneo hili,” Nape aliwaeleza waandishi wa habari waliokuwa wakipiga kelele kutaka kujua yaliyozungumzwa kati yake na Kamanda Kaganda.

Awali leo asubuhi Rais Magufuli amefanya mabasiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kwa kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria huku Dkt. Harrison Mwakyembe akiteuliwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Alichosema Nape Baada Ya ‘Kutumbuliwa’, Zitto Akimuita Shujaa


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye.n
img-20161130-wa0008

C7lXY4tVYAAvddw
zit

Rais Magufuli ‘Amtumbua’ Nape Nnauye, Mwakyembe Apewa Wizara Yake

Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

img-20161130-wa0008
17425962_1406704009373013_1475029251588069772_n

Sunday 19 March 2017

Arsenal yatwangwa na West Brom Albion

Arsenal ilishindwa kwa mabao 3-1

Arsenal ilishindwa kwa mabao 3-1
img-20161130-wa0008

Arsenal ilipata pigo la nne katika mechi tano za ligi baada ya mabao mawili ya Craig Dawson kuisaidia West Bromwhich Albion kuilaza timu hiyo ya Arsene Wenger kwa mabao 3-1.

Dawson alitumia fursa ya makosa yaliofanywa na walinda lango la Arsenal kufunga mabao yake yote mawili kwa kichwa kupitia kona zilizopigwa na hivyobasi kuathiri uwezo wa Arsenal wa kumaliza katika timu nne bora.

Awali Arsenal ilikuwa imejikakamua baada ya kuwa bao moja chini ,na kusawazisha kupitia Alexi Sanchez likiwa bao la 18 la mchezaji huyo wa Chile msimu huu.

Hatahivyo walisalia nyuma kwa mara ya pili dakika kumi za kipindi cha pili baada ya mchezaji wa ziada Hal Robson Kanu kufunga bao, dakika mbili tu baada ya kuingia.

Arsenal ambayo ilimpoteza kipa Petr Cech kupitia jeraha walikabiliwa na kutawaliwa na kushindwa kupata bao la pili.

Na mwisho wamechi hiyo mashabiki wa timu ya Arsenal waliendelea jitihada za za kumtaka kocha wa klabu hiyo kufutwa kazi kwa matokeo mabaya.

Walibeba mabongo yaliomtaka kocha huyo kuondoka

Korea Kaskazini 'yafanyia majaribio injini mpya ya kurusha roketi'

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anasemekana ametaja uzinduzi huo kama wa

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, anasemekana ametaja uzinduzi huo kama wa "kihistoria"
img-20161130-wa0008

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, vinasema kuwa taifa hilo limefanyia majaribio injini moja kubwa maalum yenye uwezo wa kurusha angani mtambo wa Satellite.

Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, amenukuliwa akisema kuwa, injini hiyo mpya itaisaidia Korea Kaskazini, kufikia uwezo wa kimataifa wa kufyatuaji Satellite angani.

Wachanganuzi wanasema majaribio ya mtambo huo wa kurusha angani roketi--ambayo bado haijathibitishwa-- pia itakuwa jambo la kuangaliwa kwa undani katika nia ya Pyongyang kuunda zana za kinuklia zenye masafa marefu.

Tangazo hilo linatokea wakati wa waziri wa maswala ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, anapofanya mazungumzo na viongozi wa China huko, Beijing.

Awali, Bwana Tillerson, aliionya Marekani kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, kwamba inaweza kuharibu mambo hata zaidi.

Nyota wa Rock and roll Chuck Berry amefariki

Charles

Charles "Chuck" Berry alizaliwa huko St Louis, Missouri mnamo Tarehe 18 Octoba 1926
img-20161130-wa0008

Mmoja wa waanzilishi wa muziki aina ya rock and roll, Chuck Berry, amefariki akiwa na umri wa miaka 90 nyumbani kwake katika jimbo la Missouri, huko Marekani.

Muimbaji na mchezaji gitaa huyo alifahamika kote duniani kwa vibao vikali alivyovizindua miaka ya 50s, ukiwemo kibao "Roll Over Beethoven", ''Sweet Little Sixteen'' na "Johnny B. Goode".

Alianzisha utumiaji wa gitaa wa mchezaji mmoja maarufu kama solos na showmanship kwa wapenzi wa mziki na kuhamasisha mabendi kama vile The Beatles na the Rolling Stones.

Risala za rambi rambi zimekuwa zikimiminika kutoka kwa wanamziki wenzake.

Berry, pichani mwaka 1965, alizindua kibao chake cha kwanza miaka ya 50s
Berry, pichani mwaka 1965, alizindua kibao chake cha kwanza miaka ya 50s

Bruce Springsteen anasema kuwa, Berry alikuwa mtunzi hodari mno wa magoma aina ya rock `n' roll kuwahi kuishi duniani.

Mick Jagger wa Rolling Stones naye anasema kwamba, 'aliasha moto wa miaka ya ujanani na kuingiza uhai kwenye ndoto yetu".

Miezi kadhaa iliyopita, wakati wa maadhimish

Thursday 16 March 2017

UN yaitaja Israel kama nchi ya kibaguzi

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
img-20161130-wa0008

Umoja wa mataifa umetoa ripoti inayoituhumu Israel kuwa ni nchi ya kibaguzi, madai ambayo nchi hiyo pamoja na washirika wake wameyakana kwa nguvu.

Ripoti hiyo inasema kuwa Israel imeanzisha mfumo unaowatenga raia wa kutoka Palestina.

Imetolewa na kamisheni ya uchumi na masuala ya kijamii kwa nchi za Magharibi mwa bara la Asia ambapo mkuu wake Rima Khalaf amesema kuwa hii ni kwa mara ya kwanza UN kukiri kuwa Israel ni nchi ya kibaguzi.

Lakini umoja wa mataifa umesema kuwa ripoti hiyo inawakilisha tu mawazo ya waandishi walioiandika ambao ni kutoka Marekani.

Israel katika taarifa yake imesema ni nchi yenye demokrasi zaidi katika nchi za Mashariki ya kati.

Mahakama yazuia marufuku mpya ya Trump Marekani

Waandamanaji karibu na White House Machi 11

Maandamano yamefanyika Marekani kupinga marufuku hiyo
img-20161130-wa0008

Mahakama moja katika jimbo la Hawaii imezuia utekelezaji wa marufuku mpya ya usafiri iliyokuwa imetangazwa na Rais Donald Trump.

Marufuku hiyo ilizuiwa saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa saa sita usiku Alhamisi.

Jaji Derrick Watson alisema ushahidi uliotolewa na serikali katika kutetea marufuku hiyo ni wa kutiliwa shaka.

Serikali ilikuwa imejitetea mahakamani ikisema marufuku hiyo inalenga kuimarisha usalama wa taifa.

Rais Trump ameeleza uamuzi huo wa jaji kuwa wa kushangaza na akasema mahakama imevuka mpaka.

Agizo lililokuwa limetolewa na Trump, ambalo lilifaa kuanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, ungepiga marufuku kwa miezi mitatu raia kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi kuzuru Marekani.

Mataifa hayo ni Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen.

Aidha, ingezuia wakimbizi kuingia Marekani kwa kipindi cha siku 120.

Bw Trump amesisitiza kwamba hatua hiyo inalenga kuzuia magaidi wasiingie Marekani lakini wanaoipinga wamesema inabagua makundi ya watu.

Marufuku nyingine ya awali aliyokuwa ameitoa Januari ilisababisha mtafaruku na maandamano kabla ya kuzuiwa na jaji mjini Seattle.

Akihutubu katika mkutano wa hadhara mjini Nashville, Tennessee Jumatano jioni, Bw Trump alisema uamuzi huo wa jaji mjini Hawaiii uliifanya Marekani "kuonekana dhaifu".

Alisema ataendelea na kesi hiyo "hadi itakapofikia", ikiwemo kwenda Mahakama ya Juu.

ALiongeza: "Tutashinda."

President Donald Trump holds a rally at the Municipal Auditorium in Nashville, Tennessee, March 15, 2017Hawaii ni mojawapo ya majimbo kadha ya Marekani yanayopinga marufuku hiyo.

Mawakili wa jimbo hilo waliambia mahakama kwamba marufuku hiyo inakiuka katiba ya Marekani kwamba watu hawafai kubaguliwa kwa misingi ya asili yao.

Jimbo hilo pia limesema marufuku hiyo itaathiri utalii na uwezo wa serikali ya jimbo hilo kupokea wanafunzi na wafanyakazi kutoka mataifa ya nje.

Tuesday 14 March 2017

Maharamia wanadai fedha kuachia Meli, Somalia

Meli katika pwani ya Somalia

Meli katika pwani ya Somalia
img-20161130-wa0008

Kikosi cha Jeshi la majini la kupambana na Uharamia la Umoja wa Ulaya, kimethibitisha kuwa watu wenye silaha wanataka kupewa fedha, kuiachia meli ya mafuta iliyokamatwa nje kidogo ya pwani ya Somalia siku ya Jumatatu.

Kikosi hicho kimesema kimefanya mawasiliano kwa njia ya simu na mmiliki wa meli hiyo, ambaye amesema meli na wafanyakazi wake walikamatiwa Kaskazini mwa pwani ya Puntland.

ARIS-13 ilikuwa ikisafiri kutoka Djibouti kwenda katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu wakati ilipotuma alama ya hatari ikisema kuwa inafuatwa na boti inayokwenda kasi.

Hii ni mara ya kwanza kwa meli ya kibiashara kutekwa nyara baharini katika eneo la pwani ya Somalia tangu mwaka 2012.

Maharamia walikuwa wamepiga kambi katika maeneo hayo mpaka pale vikosi vya jeshi la majini vya Umoja wa Ulaya vilipoanza kufanya doria na kudhibiti hali hiyo.

Bunge La Uiingereza Latoa Idhini Kujitoa EU

_95138953_f9eec283-e008-43a8-a9a4-4075473fa441
img-20161130-wa0008

Bunge la Uingereza limetoa idhini ya mwisho ya sheria muhimu katika hatua ya mchakato wa kuelekea kutaka kujitoa katika Jumuiya ya Ulaya (EU).

Serikali ya Uingereza inapanga kuanza hatua rasmi za kujiondoa ndani ya jumuiya ya Ulaya ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Hatua hii inatarajiwa kuwa na utata kufuatia tangazo la Scotland linalodai kuwa wana mpango pia wa kuwa na kura ya maoni kuhusiana na kujitenga kwao na Uingereza na kisha kuwa taifa huru.

Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya bunge la Uingereza zinasema kuwa hakuna uwezekano wa mchakato huo kuanza wiki hii na kwamba Waziri Mkuu atatakiwa kusubiri hadi mwisho wa mwezi huu muda ambao ni rasmi.

Chama Upinzani cha Liberal kimesema kuwa serikali imeshindwa kuonyesha msimamo juu ya haki za raia wa EU wanaoishi nchini Uingereza na kutoa wito kwa makundi mbali mbali kusisitiza juu ya mabadiliko.

Ridhiwani Ahojiwa Madawa Ya Kulevya, Afunguka Haya

17310306_1412991418764848_4756928326927975667_o
img-20161130-wa0008

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete jana amehojiwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya na kudai kufurahishwa kwake na hatua hiyo ya kuitwa na kuhojiwa.

Amesema baada ya kupata fursa ya kueleza ukweli imebainika kuwa hauzi wala kusafirisha dawa za kulevya.

Naye Kamishna wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, William Siang’a amesema wanamhoji kila mtu aliyetuhumiwa na ikibainika ana kosa anachukuliwa hatua.

Msukuma Aibua Mapya Kukamatwa Kwake, Atishia Kuzungumza Na Gwajima

msukuma
img-20161130-wa0008

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku “Msukuma” ametoa siku tano za kuombwa na radhi na wanaodaiwa kuwa ni Maofisa Usalama wa Taifa waliotoa taarifa za uongo dhidi yake na kusababisha akamatwe Mjini Dodoma.

Juzi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, liliwatia nguvuni Msukuma, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe, Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, na Adam Malima, kwa madai ya kupanga kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika hivi karibuni.

Mwanasiasa hao walikamatwa na kuhojiwa, kabla ya kuachiwa kwa dhamana lakini Msukuma amesema hawezi kukaa kimya juu ya suala hilo na kwamba wapo maofisa usalama waliosambaza taarifa juu yake na kusababisha hofu lazima wamuombe radhi.

“Hawa ni wapiga dili, Rais lazima aiangalie upya Idara ya Usalama wa Taifa. Wameniundia mimi zengwe, mpaka nikakamatwa, na nchi ikawa kwenye presha, kama chama kisipozungumza mimi nitaenda kuzungumza na watoto wangu kama Askofu Gwajima (Josephat),” amesema.

Mbunge huyo anayesifika kwa vituko visivyoisha, amesema atapigania heshima yake kwani hajawahi kupata kashfa na lazima atashinda.

“Sitazungumza kitaifa, nitaenda kuzungumza na wapiga kura jimboni kwangu, nieleze kwanini watu wametengeneza kinyago wakakiweka sebuleni halafu kinawatisha wenyewe. Kama kuna usalama wa taifa aliyeshiriki natoa siku tano awe ameniomba msamaha,” amesema Msukuma.

Hofu ya kuibuka kwa vurugu katika mkutano mkuu wa CCM uliofanyika jana iliibuka baada ya juzi Halmashauri Kuu – NEC ya chama hicho kuchukua uamuzi wa kuwafukuza viongozi mbalimbali wanaodaiwa kuwa walikisaliti chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Waliofukuzwa uanachama ni pamoja na wenyeviti wa CCM katika mikoa minne wakiwemo Ramadhani Madabida (Dar es Salaam) na Jesca Msambatavangu (Iringa). Sophia Simba, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum alikutana na kadhia hiyo.

Saturday 11 March 2017

Donald Trump amwalika rais wa Palestina Mohamud Abbas

Rais wa Palestina Mohamud Abbas

Rais wa Palestina Mohamud Abbas
img-20161130-wa0008

Ikulu ya white house inasema kwamba rais Donald Trump amemwalika kiongozi wa Palestina, Mohamud Abbas, nchini Marekani hivi karibuni.

Bwana Trump amemwalika Abbas baada ya mazungumzo ya kwanza ya simu na kiongozi huyo tangu aingie maamlakani.

Trump amependekeza kuhusika katika juhudi za amani mashariki ya kati, japo viongozi wa Palestina wanalalamika kwamba sera ya kigeni ya rais Trump inaonekana kupendelea Israeli.

Hakujakuwa na mazungumzo ya amani ya haja kati ya Israel na Palestina tangu mazungumzo ya amani yalioanzishwa na Marekani kugonga mwamba mnamo mwezi Aprili 2014.

Msemaji wa Trump Sean Spicer alithibitisha siku ya Ijumaa kwamba rais wa Marekani alimualika Abbas katika ikulu ya Whitehouse hivi karibuni.

Rais Donald Trump wa Marekani na waziri mkuu Benjamin Netayahu wa Israel
Rais Donald Trump wa Marekani na waziri mkuu Benjamin Netayahu wa Israel

Rais huyo alimwambia kiongozi huyo wa Palestina kwamba watajadiliana vile watakavyoanzisha tena mazungumzo ya amani kulingana na msemaji wa Abbas aliyenukuliwa na Reuters akisema.

Alisema kwamba bwana Trump alisisitiza kuhusu juhudi zake za mpango wa amani ambao utaleta amani ya kweli kati ya Palestina na Israel.

Maafisa wa Palestina walikuwa wamesema kwamba kabla ya simu hiyo ya siku ya Ijumaa. bwana Abbas atamsisitizia rais huyo wa Marekani kuhusu ujenzi wa majumba ya walowezi katika ardhi ya Palestina na umuhimu wa mataifa mawili yalio huru.

Dkt Mohamed Shein achukizwa na vitisho vya Tanesco

Rais wa kisiwa cha Zanzibar Ali Mohamed Shein asema hatishwi na vitisho vya Tanesco

Rais wa kisiwa cha Zanzibar Ali Mohamed Shein asema hatishwi na vitisho vya Tanesco
img-20161130-wa0008

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema serikali yake haitishiki na tishio la kukatiwa umeme na iko tayari kutumia vibatari na deni linalodaiwa sio la leo wala jana.

Matamshi yake yanajiri siku moja tu baada ya shirika la umeme nchini Tanzania Tanesco kutoa ilani ya siku 14 kwa wadeni wake kwamba litawakatia moto.

Hatua hiyo ya Tanesco inajiri baada ya rais Magufuli kuiagiza Tanesco kuwakatia umeme wadeni wake wote kikiwemo kisiwa cha Zanzibar.

Makamu wa rais wa kwanza nchini Tanzania Dkt. Shein ametoa msimamo huo katika mkutano wake na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Zanzibar mara aliporejea kutoka Indonesia.

Ziara hiyo ya Indonesia ilikuwa ya kuhudhuria mkutano wa nchi zilizopakana na bahari ya hindi ambapo alimwakilisha Rais John Magufuli.

Amesema deni linalodaiwa serikali italipa na yeye kama rais hana taarifa yoyote ya Zanzibar kukatiwa umeme ingawa hatarajii kitendo hicho kufanyika.

Dkt. Shein ameelezea mkutano huo na makubaliano yaliyofikiwa ambapo amesema utaleta tija na faida kubwa kwa Wazanzibari na Watanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo utalii, uvuvi, ulinzi ,vita dhidi ya uharamia na uchumi wa bahari.

Dkt. Shein ambaye aliongoza ujumbe wa mawaziri katika mkutano ambao ulikuwa wa kutimiza miaka 20 ya jumuiya ulihudhuriwa na marais wa nchi hizo za bahari ya hindi huku mkutano ujao unatarajiwa kufanyika Afrika Kusini.

Rais Tump ‘Amfagilia’ Magufuli, Asema Haya Kuhusu Tanzania

Rais wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Donald Trump.
img-20161130-wa0008

Rais wa Marekani Donald Trump amempongeza Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa mfano mzuri wa viongozi wa Afrika.

Wakati akisaini sheria ambayo itakuwa ikizuia waafrika kutoka nchi ambazo marais wake hawafanyi lolote na wale ambao wamegoma kuondoka madarakani, Trump amesema Rais Magufuli ni mfano wa viongozi bora wa Afrika na nchi yake inastahili kutendewa kipekee.

Amesema kuwa sheria hiyo itaziathiri nchi kama Zimbabwe, Uganda na nyingine za Afrika ambazo marais wake wamekataa kuondoka madarakani wakiwa hawafanyi lolote na kusema kuwa Tanzania si miongoni mwa nchi hizo kwa kuwa rais wake, John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri.

Kwa mujibu wa Rais Trump , Watanzania hawatazuiwa kwenda Marekani na watapewa upendeleo maalum kwa hisani ya Rais Magufuli.

Trump amehitimisha kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake akisema “Hongera wajina wangu John Magufuli, wewe ni shujaa wa Afrika”.

clouds stream