Tuesday 27 June 2017

MWINYI ATAMANI RAIS MAGUFULI AONGOZE MILELE


Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Alli Mwinyi(kulia).
Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Rais Mstaafu Alli Mwinyi(kulia).IMG-20170426-WA0006

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi amesema isingekua Katiba anatamani Rais Dkt.John Pombe Magufuli aongoze Milele

Meya Jacob: Kutoa Bango La Mtaa Wa Victor Wanyama Ni Siasa Chafu

Meya Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob.
Meya Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob.
IMG-20170426-WA0006

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema kuwa mpango wa kuondolewa kwa bango la Mtaa wa Mchezaji wa Soka wa Ligi Kuu Nchini Uingereza, Victor Wanyama ni mpango ulioratibiwa kwa chuki za kisiasa dhidi yake.

Amesema kuwa aliyeratibu mpango huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa anahakiki kama taratibu za kuupa jina Mtaa Wanyama zilifuatwa ama hapana.

Amedai kuwa kitendo hicho kimedhihirisha chuki kutokana na dalili za uwepo wa Meya huyo wa Chadema katika mchakato wa kuupa mtaa huo jina la Mchezaji Wanyama ambaye yupo nchini kwa Matembezi.

Meya Jacob amesema kuwa mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ aliyekubali kushiriki kuangalia ligi ya Ndondo Cup alionesha nia ya kuwasaidia vijana wa kitanzania wenye hamasa ya kucheza soka lenye tija.

“Kitendo hicho ambacho si cha kiuungwana kinaweza kumkatisha tamaa mchezaji huyo ambaye angeweza kuwa rafiki mzuri wa Tanzania na kupata mafanikio kupitia mlango wa soka,” amesema.

Jacob amefafanua kuwa taratibu zote za kuupa mtaa huo jina zilipitiwa.Victor Wanyama akizindua mtaa uliopewa jina lake katika Manispaa ya Ubungo.

Victor Wanyama akizindua mtaa uliopewa jina lake katika Manispaa ya Ubungo.

19510085_1500322923344454_861370004019848212_n
19399009_1500322866677793_8835901741559392841_n

Ujumbe Wa Makamu Wa Rais Sikukuu Ya Eid El Fitri


6ae1764a-418e-46f4-9453-af9c8257653e
IMG-20170426-WA0006

Wednesday 21 June 2017

Mghwira Abariki Shamba La Mbowe Kuharibiwa

Anna Mghwira Kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Anna Mghwira  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
IMG-20170426-WA0006

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gellasius Byakanwa dhidi ya shamba la Kilimanjaro Veggie linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, sio za kisiasa bali ni utaratibu wa kisheria wa kulinda vyanzo vya maji.

Mgwhira ametoa kauli hiyo alipotembelea shamba hilo lililopo Kijiji cha Nshara ili kujionea hali halisi ya uharibifu wa mazingira uliofanywa katika shamba hilo linalomikiwa na Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai.

Amesema hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ni sahihi katika kulinda vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, kifungu 81.

“Mmiliki wa shamba alikubali jambo hili na kukiri kuwa ni kosa kisheria na kukubali kuondoa mazao yake ifikapo Mei 23 baada ya kukubaliana na Mkuu wa Wilaya ya Hai ya kwamba atatumia miezi minne kuondoa mazao hayo lakini hakufanya hivyo,” amesema Mwenyekiti huyo wa zamani wa ACT­Wazalendo.

Awali akizungumzia hatua hiyo, Mbowe ameelezea kusikitishwa na kitendo hicho cha kuharibu miundombinu ya umwagiliaji katika shamba hilo la kisasa na kudai kitendo hicho kimemsababishia hasara ya mamilioni ya fedha na kukosesha ajira zaidi ya vijana 100.

Hatahivyo, amesema suala hilo linashughulikiwa na wanasheria wake na pindi litakapokamilika watachukua hatua.

Zitto Apata Pigo Lingine,Kada ACT-Wazalendo Atimkia CCM

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Kiongozi wa Chama cha ACT­Wazalendo.
IMG-20170426-WA0006

Kada wa chama cha ACT­ Wazalendo mkoani Pwani wilayani Kibaha amehamia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa Rais Magufuli katika uwanja wa Bwawani wilayani Kibaha leo.

Akizungumza mara baada ya kupewa na nafasi na Msemaji wa Chama Humprey Polepole Kada huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja amesema katika kampeni za urais mwaka 2015 alimpigia kura Rais Dkt.John Magufuli kutokana kile alichosema ni sauti ya Mungu ikimtaka afanye hivyo.

Chama cha ACT­Wazalendo kime endelea kupata pigo kufuatia Vigogo wake kupata shavu katika Serikali ya Rais Magufuli akiwemo Mwenyekiti wa ACT­Wazalendo Anna Mghwira kuteuliwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na Prof. Kitila Mkumbo kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Majina Umwagiliaji,

JPM: Waombeeni Wauaji Wa Pwani Waokoke


Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
IMG-20170426-WA0006

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania wote kuwaombea wahalifu wanaofanya mauaji huko Mkoani Pwani, ili waweze kuokoka na kujua thamani ya damu ya mtu.

Rais Magufuli amesema hayo mapema jana wakati akihutubia mkutano wake wa kwanza katika ziara ya siku tatu Mkoani humo.

“Niwaombe wananchi wa Pwani, msishirikiane na watu waovu kwakuwa wanachelewesha sana maendeleo na ndio maana huko Kibiti hakuna hata kiwanda na hakuna imani ya dini yoyote ile inayosema watu wauane,” amesema.

Hatahivyo, amesema kuwa wauaji hao wameshaanza kuuona moto na kuonya kuwa Serikali ya Awamu ya Tano sio ya kuchezea.

“Watanyooka tu, wameshaanza kunyooka, kama wapo hapa wanaotusikiliza basi wakapeleke salamu.Niwaombe sana, tuwaombee hawa watu waokoke, ili wajue damu ya mtu ina thamani kubwa sana,” ameongeza.

Friday 16 June 2017

BAADA YA KUFUNGIWA , MAWIO KUKIMBILIA MAHAKAMANI


19095661_1492340464142700_72509215397706043_o
IMG-20170426-WA0006

Uongozi wa gazeti la MAWIO umeapa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa kipindi cha miezi 24.

Uamuzi wa kulifungia gazeti hilo ulitangazwa jana na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo sababu iliyotajwa ni gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali ya kutowahusisha marais wastaaf,u Mzee Mkapa na Dkt. Kikwete.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Victoria Media Services Ltd ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la MAWIO, Simon Martha Mkina, amesema kuwa uamuzi huo si wa haki na utapingwa mahakamani.

“Bodi itakutakana kujadili uamuzi huo kama jambo la dharura, lakini tunachoweza kukwambia kwa sasa, tutakwenda mahakamani,” amesema Mkina.

“Sina budi kulifungia gazeti lako, na kukutaka usitishe kuchapisha nakala ngumu au ya mtandaoni katika kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne (24) tangu tarehe ya barua hii, kwa mamlaka niliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 kifungu cha 59,” ilisema sehemu ya taarifa ya Waziri Dkt. Mwakyembe iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo.

Gazeti hilo liliandika habari iliyokuwa na ujumbe wa jumla kuwa, marais hao wamelisababishia taifa hasara kubwa sana kutokana na usafirishaji wa mchanga nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 19.

Thursday 15 June 2017

CCM ‘Yawacharukia’ Waliotajwa Ripoti Makinikia

POLEPOLEE CCM
IMG-20170426-WA0006

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wote waliotajwa katika ripoti ya kamati ya pili iliyochunguza makontena 277 ya mchanga wa madini, kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola vitakavyowahoji.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema hayo leo katika ofisi za Chama, Lumumba na kudai kuwa waliotajwa wote wanapaswa kutoa ushirikiano ili vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa haraka na ufanisi.

Amesema chama hicho chenye Serikali kinaviagiza vyombo vya dola kuwahoji waliohusika kwa haraka ili Watanzania wajue ukweli wa yaliyotokea.

Waliotajwa katika ripoti ya pili ni aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Profesa Sospeter Muhongo na na Nazir Karamagi.

Aidha, amempongeza Rais John Magufuli kwa kuthubutu kudai rasilimali ambazo zimekuwa zikiibiwa na kuwataka wananchi kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anayoifanya badala ya kugawanyika.

Lema Afunguka Magufuli Kukutana Na Bosi ACACIA

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
IMG-20170426-WA0006

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema. Mbunge wa Arusha Mjini Bw.Godbless Lema amefunguka kuhusiana na Rais Magufuli kukutana na Bosi kampuni ya madini ya ACACIA ambaye amekubali kulipa fedha zote kampuni hiyo inazodaiwa toka ianze kuchimba madini hapa nchini.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema jana kuwa amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton Ikulu jijini Dares salaam.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Lema amesema amependa Rais alivyokutana na Bosi wa Acacia na kufanya nae mazungumzo kwa upole na kufikia muafaka wa kuilipa serikali madeni yote.

Screenshot_20170614-235506-768x341 (1)

MBUNGE AHOJI UJENZI UWANJA WA NDEGE CHATO


chatoairpotIMG-20170426-WA0006

Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe. Salome Makamba amehoji sababu zilizoifanya serikali kujenga uwanja wa ndege wilayani Chato, ambako ni nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kuacha kufanya hivyo kwenye maeneo mengine mengi yenye fursa za kiuchumi.

Mhe. Salome ameyasema hayo bungeni wakati akichangia kwenye bajeti ya mwaka huu ambapo amesema sababu kubwa ya kushindwa kutekeleza kwa bajeti iliyopita, ni kwa sababu ya serikali kushindwa kusimamia mambo ya msingi.

Bi. Salome ameenda mbele na kutaka kujua ni utaratibu gani umetumika kusimamia gharama za ujenzi wa uwanja huo, sambamba na kutaka kujua kuhusu ununuzi wa ndege uliofanywa na serikali. Akataka ufafanuzi pia utolewe kwenye ujenzi wa barabara ya Mwenge­Morocco Jijini Dar es Salaam.

Sunday 11 June 2017

Marekani yazitaka nchi za kiarabu kulegeza kamba kwa Qatar

Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar

IMG-20170426-WA0006Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasema kuwa nchi za Ghuba ni lazima zilegeze hatua yao dhidi ya Qatar ambayo inalaumiwa na majirani zake kwa kuunga mkono Ugaidi.

Saudi Arabia, Muungano wa nchi za kiarabu, Misri na Bahrain walikata uhusiano wa usafiri na wa kidiplomasia na Qatar siku ya Jumatatu.

Bwana Tillerson anasema kuwa hatua hiyo inasabisha kuwepo madhara ya kibinadamu.

Licha la kumsifu Emir wa Qatar kwa kupuza uungwaji mkono makundi ya kigaidi, Bwana Tillerson anasema mengi yanahitaji kufanywa.

Naye Rais Trump ameishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na kuitaka ikome

Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar, na hata kudai kuwa alishiriki katika uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia pamoja na nchi zingine.

Ndege za Qatar zilipigwa marufuku ya kutumia anga za baadhi ya majirani zake.

Hatua hiyo ya ghafla ilichukuliwa baada ya msukosuko ambao umedumu miaka kadha kati ya Qatar na majirani zake wa Ghuba.

Saudi ArabiaNchi za Ghuba

Wafungwa watoroka kutoka kituo cha polisi DRC

Wafungwa watoroka kutoka kituo cha polisi DRC

Wafungwa watoroka kutoka kituo cha polisi DRC
IMG-20170426-WA0006

Watu wenye silaha wameshambulia ofisi ya mkuu wa mashtaka na kituo cha polisi kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Kinshasa na kusababisha wafungwa kadha kutoroka.

Kuna ripoti tofauti kuhusu ni wafungwa wangapi walifanikiwa kutoroka.

Redio inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ya Radio Okapi, inasema kuwa wafungwa 17 walitoroka, wengi kutoka kwa kituo cha polisi.

Mtandao mmoja wa habari nchini Congo wa Politico, unasema kuwa washambuliajia walikuwa ni wanachama wa Bunda dia Kongo ambalo ni kundi la dini lililo na mtazamo wa siasa.

Serikali inalilaumu kundi hilo kufuatia shambulizi lililotokea katika gereza kuu la Kinshasa mwezi uliopita ambapo mamia au hata maelfu ya wafungwa walitoroka.

Saturday 10 June 2017

Mwana wa Gaddafi Saif al-Islam aachiliwa huru Libya

Saif al-Islam Gaddafi 2011

Saif al-Islam Gaddafi (katika picha hii iliyopigwa 2011 baada yake kukamatwa) alihukumiwa kifo nakama mjini Tripoli mwaka 2015
IMG-20170426-WA0006

Saif al-Islam Gaddafi, mwana wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi anadaiwa kuwa huru baada ya kuzuiliwa kwa kipindi cha miaka sita.

Kuna wasiwasi huenda hatua hiyo ikatikisa zaidi hali ya kisiasa na kiusalama nchini Libya.

Saif al-Islam anadaiwa kuachiliwa huru baada ya kupewa msamaha.

Ndiye aliyependelewa na babake kuwa mrithi wake na amekuwa akizuiliwa na kundi la wanamgambo katika mji wa Zintan kwa miaka sita.

Wanamgambo hao wa Abu Bakr al-Siddiq Battalion walisema aliachiliwa huru Ijumaa lakini bado hajaoneshwa hadharani.

Taarifa nchini Libya zinasema kwa sasa amo katika mji wa Bayda, mashariki mwa Libya, kwa jamaa zake.

Wanamgambo hao wanadaiwa kumuachilia huru baada ya ombi kutoka kwa "serikali ya muda".

Serikali hiyo - yenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo - ilikuwa tayari imetoa msamaha kwa Saif al-Islam.

Hata hivyo, alikuwa amehukumiwa kifo na mahakama mjini Tripoli, magharibi mwa nchi hiyo bila yeye kuwepo mahakamani.

Maeneo ya magharibi yanatawaliwa na serikali inayopingana na serikali ya mashariki mwa Libya, lakini serikali hiyo ya magharibi yenye makao yake makuu Tripoli ndiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Kwa kirefu, inafahamika kama Serikali ya Mwafaka wa Kitaifa.

Taarifa zilizowahi kutolewa awali kuhusu kuachiliwa kwa Saif al-Islam Gaddafi baadaye zilibainika kuwa na uongo.

Ikithibitishwa kwamba Saif al-Islam Gaddafi ameachiliwa huru, hilo huenda likaongeza wasiwasi na kutotabirika katika siasa Libya.

Alikamatwa jangwani Novemba 2011 akijaribu kutorokea Niger, na baadaye akaoneshwa kwenye runinga akiwa bila vidole kadha.

Alionekana na mataifa ya Magharibi kama sura ya hadharani ya utawala wa Gaddafi na ndiye aliyeonekana kupendelewa na babake kuwa mrithi wake.

Ingawa anachukiwa sana na wengi - nyumbani na nje ya nchi - bado ana uungwaji mkono fulani Libya na huenda akajiingiza katika siasa humo.

Anatafutwa pia na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yenye makao yake mjini The Hague, Uholanzi kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu, makosa anayodaiwa kuyatekeleza wakati wa juhudi zilizofeli za kujaribu kuzima maasi kabla ya babake kuondolewa madarakani na kuuawa.

Saif al-Islam pictured before his capture in 2011

Saif al-Islam, katika picha iliyopigwa kabla ya kukamatwa kwake

Saif al-Islam, alitunukiwa shahada ya uzamifu (PhD) kwa njia yenye utata na chuo kikuu cha uchumi, London School of Economics mwaka 2008.

Alikamatwa Novemba 2011 baada ya kuwa mafichoni kwa miezi mitatu kufuatia kuondolewa madarakani kwa babake, Kanali Gaddafi.

Awali, alikuwa ametekeleza mchango muhimu katika kufufua na kujenga upya uhusiano kati ya serikali ya babake na nchi za Magharibi baada ya 2000.

Alitazamwa na mataifa hayo kama mwanamageuzi na mpenda mabadiliko katika serikali ya babake.

Lakini baada ya maasi ya mwaka 2011, alijipata akituhumiwa kuchochea ghasia na mauaji ya waandamanaji.

Miaka minne baadaye, alihukumiwa kuuawa kwa kupigwa risasi baada ya kukamilishwa kwa kesi iliyomhusisha yeye na washirika 30 wa karibu sana wa Gaddafi.

A map showing Libya

Saif al-Islam: Mrithi aliyegeuka mfungwa

  • Juni 1972: Azaliwa Tripoli, Libya, mwana wa pili wa kiume wa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi

  • Februari 2011: Maasi dhdii ya utawala wa Gaddafi ryaanza

  • Juni 2011: Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yatoa kibali cha kukamatwa kwa Saif al-Islam kwa tuhuma za kutenda makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu

  • Agosti 2011: Aukimbia mji mkuu baada ya Tripoli kutekwa an wapiganaji waliokuwa wanaipinga serikali; atorokea Bani Walid

  • Oktoba 2011: Babake na kakake mdogo wauawa

  • 19 Novemba 2011: Akamatwa na wanamgambo akitorokea Niger, kusini mwa Libya. Azuiliwa Zintan

  • Julai 2015: Ahukumiwa kifo na mahakama Tripoli bila yeye kuwepo mahakamani

  • Juni 2017: Aachiliwa huru baada ya msamaha uliotolewa na moja ya serikali mbili zinazoshindania kuongoza Libya

Thursday 8 June 2017

Korea Kaskazini yarusha kombora la kushambulia meli

Korea Kaskazini ikionyesha makombora ya Styx 2012

Korea Kaskazini ikionyesha makombora ya Styx 2012.

Korea kaskazini imerusha makombora kadha ya kushambulia meli mashaiki mwa pwani yake, kwa mujibu wa Korea Kusini

Mamlaka zilisema kwa makombora hayo yaliyorushwa Alhamisi asubuhi karibu na mji wa Wonsan yalikuwa ni ya masafa mafupi.

Makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 20o kabla ya kuanguka baharini.

Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini mwaka huu yamekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Wataalamu wana hofu kuwa majaribio hayo na hatua za Korea kutundika silaha za nuklia katika vichwa vya makombora.

Map of North Korea showing Wonsan in east
Ramani ya Korea Kaskazini.

Msemaji wa Jeshi la Korea Kusini amesema kuw majiribio ya hivi punde yalionyesha kuwa Korea Kaskazini ilitaka kuonyesha kuwa ina uwezo wa kulenga meli kubwa baada ya mazoezi ya hivi majuzi kati ya Marekani na vikosi vya Korea Kusini

Makomboa ya kushambulia meli ni makombora ambayo huelekezwa. Mwaka 2012 Korea Kaskazini ilionyesha makomboa kadha kama hayo yanayojulikana kama Styx.

Lakini hapo awali Korea ilijaribu bila mafanikio kufanyia majaribio makombora ya kushambulia meli.

Marekani inaweka mitambo ya kujikinga nchini Korea Kusini
Marekani inaweka mitambo ya kujikinga nchini Korea Kusini.

Mabaki ya ndege ya Myanmar na maiti za abiria zapatikana baharini

Picha ya maktaba ya ndege ya jeshi la angani la Myanmar muundo wa Y-8

Picha ya maktaba ya ndege ya jeshi la angani la Myanmar muundo wa Y-8

IMG-20170426-WA0006

Jeshi la Burma limesema kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka Jumatano katika anga ya bahari ya Andaman ikiwa abiria 122 wengi wao wanajeshi na familia zao, yamepatikana.

Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa iliyotolewa na idara ya jeshi.

Ndege hiyo aina ya Y8, iliyotengezwa nchini China, ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.

Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa, wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano.

A map showing Myeik, Dawei, and Yangon in Myanmar
Myeik, Dawei, na Yangon nchini Myanmar

Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.

Mynmar imekumbwa na ajali kadha za ndege miaka ya hivi karibuni. Lakini ajali hii ya sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi, walifariki wakati ndege yao kuanguka kwenye mji mkuu wa Nay Pyi Taw.

Miezi mitatu baadaye maafisa watatu, waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilipoanguka kati kati mwa Mynmar.

WANAUME WENYE VIPARA WAGEUZWA ‘DILI’ MSUMBIJI


bald_black_guy

IMG-20170426-WA0006

Polisi nchini Msumbiji wameonya kuwa wanaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi yanayohusiana na uchawi, pamoja na matambiko fulani, baada ya kuuliwa kwa wanaume wawili kama hao mwezi uliopita.

Wanaume hao wawili wenye upara na ambapo mmoja wao alipatikana akiwa amekatwa kichwa na viungo vya mwili vikiwa vimetolewa, waliuliwa katika Mkoa wa Zambezi.

“Mwezi uliopita, mauaji ya watu wawili wenye vipara yalisababisha kukamatwa kwa washukiwa wawili,” msemaji wa polisi Inacio Dina alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Maputo.

Kwa mujibu wa BBC Mjini Maputo, baadhi ya watu wana imani potofu kuwa watu wenye vipara wako na dhahabu kwenye vichwa vyao.

Visa vya kuuliwa watu wenye upara kwa maswala ya uchawi havijaripotiwa siku za nyuma. Washukiwa ni vijana wa Msumbiji, waliowaambia polisi kuwa viungo hivyo vingetumiwa kwa uchawi na matambiko nchini Tanzania na Malawi.

Tanzania inafahamika duniani kwa watu wenye matatizo ya ngozi kuuwawa na viungo vyao kutumika kwenye matambiko ya kichawi.

ZITTO AFUNGUKA UTEUZI WA MGHWIRA , ATAKA WANACHAMA ACT WASILUMBANE NA ‘NYUMBU’

Image result for zitto kabwe
IMG-20170426-WA0006

Kiongozi wa Act­Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe hatimaye amefunguka na kuzungumzia kitendo cha Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Bi. Anna Elisha Mghwira kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Tayari chama hicho kimemuondoa mteule huyo mpya katika nafasi yake ya Uenyekiti na kupitia ukurasa wake wa facebook, Zitto Kabwe amefunguka yafuatayo;

Chama chetu cha Act Wazalendo ni kichanga Kwa umri lakini ni kibobevu kwenye Uongozi. Unajua uimara wa Vyama kwenye mitihani Kama Hii inayotukuta sisi. Tunavuka na Mola anatusaidia kuishinda mitihani.

Kuna ambao toka tuanzishe Chama wameshindwa kukubali hali halisi na ku move on. Kila siku wanatushambulia Kwa kejeli na maneno. Sisi hatuwajibu. Tunafanya yetu. Hatuwashangai maana tunawaongoza kwenye hoja. Tutaendelea kuwaongozakwenye hoja. Hatubabaishwi na kelele zao.

Hakuna Chama Cha Siasa nchi Hii kinaweza kuthubutu kubeza uwezo wetu wa hoja na kuchambua hoja. Kelele hatuna. Matusi hatuna. Kebehi hatuna. Hoja hapa ni mtakuja.

Wanachama 400,032 wa ACT Wazalendo mliotapakaa nchini nzima msiingie kwenye malumbano na nyumbu. Nyumbu hawawazi. Wanafuata tu. Wajibu wetu ni kuwaongoza nyumbu wavuke salama mto mara. Asili ya kuanzishwa kwetu ni kuukataa unyumbu. Tuendelee kuukataa unyumbu Kwa kumrejea Nkrumah ” Forward Ever, Backward Never “.

      Sisi ni Gogo la Udi. Unavyolichoma ndio linavyonukia.

                        Utu. Uzalendo. Uwajibikaji.

UTAFITI: BODABODA , BAISKELI JANGA JIPYA KWA NGUVU ZA KIUME

Madereva bodaboda wakerwa mwenzao kutelekezwa baada ya kupigwa risasi.

IMG-20170426-WA0006

Kazi ya kuendesha baiskeli za kubeba abiria pamoja na baiskeli zinazopatikana kwenye vituo vya mazoezi (gym) vimebainika kuwa chanzo cha kupunguza uwezo wa wanaume wanaposhiriki tendo la ndoa.

Hayo yamebainika kupitia utafiti uliofanywa hivi karibuni na jopo la wataalam wa afya ya uzazi likiongozwa na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, Wamalwa nchini Kenya.

Matokeo ya utafiti huo uliowahusisha waendesha baiskeli (bodaboda) 115 wenye umri kati ya miaka 18 na 40, katika eneo la Bungoma, Mashariki mwa Kenya, ulibaini kuwa asilimia 35.9 walikuwa na matatizo ya uwezo mdogo wa kushiriki tendo la ndoa ipasavyo, kwakuwa wameathiriwa misuli ya uume.

Vijana hao walipimwa na wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Taifa ya Kenyatta wakishirikiana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta, ambapo majibu yalionesha kuwa asilimia 39.5 walikuwa na tatizo la kusisimua misuli ya uume.

Utafiti huo ulionesha kuwa vijana hao waliathirika kutokana na kutumia nguvu nyingi katika kuendesha baiskeli na kwamba walioendesha baiskeli kwa muda wa saa 60 au zaidi kwa wiki ndio waliathirika zaidi.

Wamalwa alitahadharisha pia kuwa vijana wengi walio kwenye vituo vya kufanyia mazoezi (gym) wakiendesha baiskeli zisizokuwa na vizuizi maalum dhidi ya sehemu za uume, wako kwenye hatari ya kukutwa na tatizo la kutokuwa na uwezo wa kushiriki ipasavyo tendo la ndoa.

Aidha, matokeo ya utafiti huo pia yanaendana na matoekeo ya tafiti zilizofanywa na watafiti wengine sita wa Chuo Kikuu cha Moi zilizowahusisha vijana 131 wa mjini Eldoret, wenye umri kati ya miaka 18 na 56. Kati ya waliopimwa, asilimia 76 walibainika kuwa na matatizo ya kutosisimua ipasavyo misuli ya uume.

“Ujumbe wetu ni muhimu kwao pia, kwamba wanafaa kuwa wanapumzika kwa muda kutoka kwa kazi yao. Wanapojikakamua kutafuta posho, wanafaa pia kujali uwezo wao kitandani,” Mhadhiri Wamalwa ameviambia vyombo vya habari.

Tuesday 6 June 2017

PICHA: RC Kilimanjaro, Anna Mghwira Akitoka Ikulu Kula Kiapo


kili
IMG-20170426-WA0006
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Elisha Mghwira akiondoka katika viunga vya Ikulu mapema leo mara baada ya kula kiapo mbele ya Rais.
Kabla ya uteuzi alikuwa Mwenyekiti wa chama cha ACT – Wazalendo na mgombea wa kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.
1-34-48.7-28-1

clouds stream