Monday 28 December 2015

CCM Wajipanga Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

CCM Wajipanga Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

Tarehe December 28, 2015
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduz Dk Alli Mohamed Shein.(aliyekaa) pembeni ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduz Dk Alli Mohamed Shein.(aliyekaa) pembeni ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar   chini ya Mwenyekiti wake Dk Ali Mohamed Shein kimewataka wananchi na wanachama kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa marudio visiwani humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, amesema wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la kupotosha ukweli..
Amesema  matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru wa kidemokrasia.
Aidha, chama hicho  kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu. Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu.
Kamati hiyo  inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Kwa upande wake  Rais wa Zanzibar, Dk Shein baada ya kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili itatolewa  yatakapofikia tamati.
Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu utaorudiwa, Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.
Licha ya chama cha Mapinduzi kujiandaa na uchaguzi mkuu Zanzibar, chama cha Upinzani cha CUF bado hakijatoa tamko lolote hadi sasa kufuatia kupinga vikali kurudiwa uchaguzi mkuu  visiwani humo.

Van Gaal Akubali Kuondoka Mwenyewe


Van Gaal Akubali Kuondoka Mwenyewe


Tarehe December 27, 2015


Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amesema kuwa anaweza “kujiuzulu mwenyewe” baada ya Stoke City kuwapiga magoli 2-0 katika kichapo chao cha nne mfululizo katika michuano yote.
Mholanzi huyo, ambaye anakabiliwa na shinikizo baada ya kusajili mechi saba sasa bila ushindi, aliulizwa katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya mechi iwapo ”anahofia kibarua chake kitaota nyasi ?”
Van Gaal, 64, alijibu kuwa hjilo lilikuwa jambo analostahili kujibu katika mazungumzo na mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward na si vyombo vya habari.
“Si siku zote ambapo ni klabu ndiyo inauwezo wa kufurusha kocha la ”
“Wakati mwingine mimi mwenyewe naweza kuchukua jukumu hilo mwenywe na kuhusiana na hilo sharti niende nifanye mkutano na mamlaka inayosimamia Manchester United safu yangu ya ukufunzi na kisha wachezaji wangu wala sio waandishi wa habari” alifoka van Gaal.
United imekuwa na msururu wa matokeo duni uliosababisha Red Deivls wakatupwa nje ya Ligi ya Mabingwa katika hatua ya makundi mbali na kuporomoka kutoka kwenye orodha ya nne bora katika jedwali la ligi kuu ya Uingereza.
Van Gaal, aliyechukua nafasi ya David Moyes katika msimu wa 2014, alisema klabu hiyo alimuunga mkono siku zote ila aliongeza: “Tumepoteza hivyo kuna hali mpya.
“Nahisi msaada wa wachezaji wangu na bodi yangu,Hata hivyo mashabiki wataudhika lakini hiyo inatarajiwa baada ya kushindwa mara nne ,” Van Gaal hafikiri ni muhimu kwamba Woodward haja muunga mkono hadharani .
“Kwangu mimi ni muhimu zaidi kwamba watu wanasema nini kuhusu utendaji kazi wangu ” alisema. “Mimi sina haja sana na matamshi ya umma.”

Lowassa Sasa Ni Mchungaji Ng’ombe?

Lowassa Sasa Ni Mchungaji Ng’ombe?

Tarehe December 26, 2015
Aliyekuwa Mgombea urais Edward Lowassa akichunga ng'ombe zake.
Aliyekuwa Mgombea urais Edward Lowassa akichunga ng’ombe zake.
Aliyekuwa Mgombea urais wa tiketi ya Ukawa Edward Lowassa ameanza rasmi uchungaji ng’ombe ikiwa ni ahadi yake kwa wananchi kuwa endapo akishindwa urais atakwenda kuchunga ng’ombe.
Aidha, hizi ni baadhi ya picha zikimuonesha Lowassa akiswaga  mifugo yake porini ambapo baadhi ya wananchi wameoneshwa kufurahishwa na utekelezaji wa ahadi zake mwenyewe.
Katika hizo Picha Lowassa alikuwa   akichunga ng’ombe zake huko Handeni mkoani Tanga.
Mwanasiasa Edward Lowassa akiswaga ng'ombe zake.
Mwanasiasa Edward Lowassa akiswaga ng’ombe zake.

Ridhiwani Aukana Utajiri, Atoa Tamko Utoroshwaji Makontena

Ridhiwani Aukana Utajiri, Atoa Tamko Utoroshwaji Makontena

Tarehe December 26, 2015
Ridhiwani Kikwete
Ridhiwani Kikwete
Familia ya aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete kupitia Mbunge wa Chalinze,  Ridhiwani Kikwete,  ambaye ni mtoto wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiiwakilisha familia ametoa kauli kuhusiana na kuhusishwa na  tuhuma za upitishaji makontena bila kulipiwa kodi bandarini.
Akizungumzia sakata hilo Ridhiwani alisema baada ya Rais Kikwete kumaliza muda wa miaka 10  madarakani, baadhi ya watu wamekuwa wakiiandama familia yao kwa tuhuma mbalimbali.
Alizitaja tuhuma hizo kuwa ni utoroshaji wa makontena kwenye bandari ya Dar es Salaam na kusisitiza kwamba tuhuma zote zinazotolewa hazina ukweli wowote bali zimelenga kumchafua yeye na familia yake.
Ridhiwani alisema tangu serikali ya awamu ya tano ianze kuwabana  watu wanaokwepa kulipa kodi za serikali,baadhi ya watu wanafanya jitihada za kumhusisha  na  watuhumiwa  hao.
Alisema hajawahi kuagiza bidhaa yoyote kutoka nje,kuwa na kontena la kulipiwa ushuru,kukwepa au kumuombea msamaha wa kupunguziwa kodi mfanyabiashara yeyote aliyeagiza kontena kutoka nje, hivyo mwenye ushahidi juu ya hilo autoe.
“Kama kuna mtu mwenye ushahidi autoe hadharani mimi niuone,dunia iuone, nawahakikishia ushahidi huo haupo na hautokuwepo labda uwe wa kughushi na wakifanya hivyo wataumbuka.
Kuhusu madai ya kumiliki Malori, mabasi na vituo vya mafuta Ridhiwani amesema ,
“Sina na sijawahi kumiliki lori au basi katika maisha yangu.Sina hisa wala ubia na mtu yeyote  au kampuni ya malori au mabasi.” Alisema Ridhiwani
“Naambiwa hapa nchini siku hizi kila jengo jipya linalojengwa inasemekana ni langu na vituo vipya vya mafuta naambiwa ni vyangu.Huo ni uongo mtupu”.Amesema Ridhiwani
Amesisitiza kuwa wanaosema, kuandika na kueneza maneno hayo wanajua wanasema uongo isipokuwa wanafanya hivyo kwa nia mbaya dhidi yake  na familia yake.

Tuesday 22 December 2015

Sanchez Kukosa Mechi Nne Tena

Sanchez Kukosa Mechi Nne Tena

Tarehe December 22, 2015
Alexis Sanchez
Alexis Sanchez
kocha wa Arsenal,Arsene Wenger amethibitisha kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Alexis Sanchez atalazimika kukaa nje kwa michezo minne ijayo kutokana na jeraha lake la awali kutokupona kwa wakati.
Sanchez aliumia sehemu ya kifundu cha mguu baada ya kugongana na mpiga picha wakati timu hiyo ikikutana na Norwich
“Sanchez atakaa nje hadi Januari 10 mwakani pia tulipanga awe katika benchi wakati tulipokutana na Man City ila imeshindikana na hayo ni masuala ya kitabibu,”amesema Wenger.
Sanchez  atalazimiaka kukosa mchezo dhidi ya  Southampton, Bournemouth, Newcastle pamoja na mchezo wa  FA Cup wakicheza na Sunderland on Januari 9 2016.

Arsenal Noma, Yaitandika Man City 2-1

Arsenal Noma, Yaitandika Man City 2-1

Tarehe December 22, 2015
Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Theo Walcot ambaye alifunga goli la kwanza wakati timu hiyo ilipokutana na Man City
Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Theo Walcot ambaye alifunga goli la kwanza wakati timu hiyo ilipokutana na Man City
vijana wa Arsen Wenger leo wamezuia pointi tatu muhimu kwa kuitandika Manchester City kwa
moja katika mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza uliomalizika hivi punde.
Arsenal walianza kuzitingisha nyavu za Man City dakika ya 33 ambapo mshambuliaji machachari
wa timu hiyo Theo Walcot alikwamisha mpira wavuni baada ya mabeki wa Man City
kujichanganya.
Oliver Girioud aliipatia Arsenal goli la pili dakika ya 45 na kufanya timu hiyo iende
mapumziko ikiwa mbele kwa magoli mawili kwa bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Man City walifanikiwa kupata bao la kufutia machozi
kupitia Yaya Toure dakika ya 82,hivyo basi mpaka mpira unamalizika Arsenal walichukua pointi
tatu katika mchezo huo

Blatter,Platini Wafungiwa Miaka Nane

Blatter,Platini Wafungiwa Miaka Nane

Tarehe December 21, 2015
Rais wa FIFA, Joseph Sepp Blatter na Michel Platini
Rais wa Fifa ,Sepp Blatter na yule wa Uefa Michel Platini wamefungiwa kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka nane na kamati ya madili ya FIFA.
Blatter na  Platini wote wamekuwa kizuini kwa muda ambapo kamati ya maadili ya FIFA ilikuwa ikiwachunguza ambapo wote walisimamishwa mwezi oktoba kutokana na kashfa ya ufisadi wa kuhamisha Pauni Milioni 1.34 kutoka kwa Blatter kwenda kwa Platini ambaye Rais wa FIFA,Blatter alithibitisha mualamala huo.
Kamati ya maadili imewapata na hatia na hivyo wameonywa kutokujiingiza katika masuala ya soka kwa kipindi hicho pamoja na kungoja taratibu nyingine za kisheria kufuata

Rais Magufuli Amng’oa Mkurugenzi Mwingine

Rais Magufuli Amng’oa Mkurugenzi Mwingine

Tarehe December 22, 2015
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli leo  ametangaza kumsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni ya RAHCO Mhandisi Benhadad Tito na kuvunja Bodi hiyo.
Aidha, RAHCO ni Kampuni Miliki ya Rasilimali za Watu iliyo chini shirika la Reli Tanzania TRL.
Katika hatua nyingine Bodi hiyo iliiyovunjwa leo ilizinduliwa  na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta tarehe 29 Oktoba, 2015 chini ya Mwenyekiti Prof. Mwanuzi Fredrick.
Taarifa kamili itakujia katika mtandao huu hivi punde.

Rais Magufuli, Maalim Seif Wapata Suluhu Mgogoro Zanzibar ?

Rais Magufuli, Maalim Seif Wapata Suluhu Mgogoro Zanzibar ?

Tarehe December 22, 2015
Picha ya pamoja ya Maalim Seif,Rais Dkt John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu.
Picha ya pamoja ya Maalim Seif,Rais Dkt John Magufuli pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana  amekutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad,  Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea mara baada ya kutokea mgogoro huo wa kisiasa visiwani humo.
Katika mkutano huo  Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.
Rais Magufuli pia  amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.
Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif  Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane
Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi hao  wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema huku wakieleza  matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.
Kwa upande mwingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar.

Kasi Ya Rais Magufuli Yatua Rwanda, Kagame Afunguka

Kasi Ya Rais Magufuli Yatua Rwanda, Kagame Afunguka

Tarehe December 22, 2015
Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais wa Rwanda Paul Kagame   amefunguka kwa mara ya kwanza mara baada ya rais John Magufuli kuingia Ikulu Novemba 5 mwaka 2015.
Kwa mujibu wa Balozi wake nchini, Uegene Kayihura amesema kwamba Rais Kagame amefurahishwa na hatua ambazo Rais John Magufuli anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa bandari.
Kayira amesema hayo alipofika Ikulu ya Rais Magufuli  ambapo  amemhakikishia kuwa Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania, hasa katika kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kwa  kuwa Rwanda inapitisha asilimia 70 ya mizigo yake katiba Bandari ya Dar es salaam.
Ameongeza kuwa  Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa hatua alizochukua kusafisha uozo katika bandari, kufichua ufisadi wa mabilioni ya shilingi kutokana na upotevu wa makontena, ambayo hayakulipiwa kodi stahili kwa serikali, kuvunjwa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Awadhi Massawe na kusimamisha maofisa kadhaa wa bandari hiyo na wengine wanaohusika na usimamizi wa bandari kavu.
Katika kuimarisha utendaji Bandarini  na Mamlaka ya Mapato Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na maofisa wengine wa mamlaka hiyo, ambao miongoni mwao tayari wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutokana na ubadhirifu huo.

Monday 7 December 2015

Mgombea urais Uganda amtumia Magufuli kuingia Ikulu

Mgombea urais Uganda amtumia Magufuli kuingia Ikulu

Tarehe December 7, 2015
MgombeaUrais Bw. Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC).
MgombeaUrais Bw. Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC).
Kampeni za uchaguzi mkuu zimepamba moto nchini Uganda ambapo Mgombea Urais  wa upinzani anayemtikisa Rais Yoweri Museveni katika kinyang’anyiro hicho, Dk. Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change (FDC) amemtumia Rais Magufuli kuomba kura kwa wananchi.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni  wiki iliyopita Kiiza alisema  kuwa atafuata nyayo za Rais John Magufuli katika kuhakikisha kuwa serikali inaendesha mambo yake kwa nia ya kubana matumizi yasiyo ya lazima, kukomesha ufisadi na mwishowe kuwanufaisha watu wa tabaka la chini kupitia uboreshaji wa huduma za jamii
Aliongeza kuwa  ili kubana matumizi ataiuza  ndege  inayotumiwa na Museveni kwa maelezo kuwa inalibebesha taifa lao gharama kubwa ambazo zinaweza kutumiwa katika kuboresha huduma za jamii.
Besigye alisema yeye anaunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais mpya wa Tanzania, Magufuli kutokana na kuchukua hatua kadhaa dhidi ya ufisadi na  kuongeza ufanisi wa kazi katika ofisi za umma na pia kuongeza nidhamu ya matumizi kwa manufaa ya taifa na siyo watu wachache Uchaguzi Mkuu nchini Uganda unatarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Februari, 2016.

Rais Magufuli amfukuza Kazi katibu mkuu wizara ya uchukuzi

Rais Magufuli amfukuza Kazi katibu mkuu wizara ya uchukuzi

Tarehe December 7, 2015
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Rais John Pombe  Magufuli  leo amemsimamisha  kazi katibu mkuu wizara ya uchukuzi Bw.Shabani Mwinjaka.
Licha ya kumfukuza kazi Katibu Mkuu amevunja bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa bandari Bw. Awadhi Massawe, Mwenyekiti wa bodi ya bandari pamoja maofisa 8 wa bandari na kuagiza wawekwe chini ya Ulinzi.
Habari kamili itafuata hivi punde.

CCM wajitokeza Kuzungumzia Kasi ya Rais Magufuli

CCM wajitokeza Kuzungumzia Kasi ya Rais Magufuli

Tarehe December 7, 2015
Rais John Pombe Magufuli.
Rais John Pombe Magufuli.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimejitokeza kwa mara ya kwanza na Kumpongeza Rais John  Magufuli katika utendaji wake tangu aingie madarakani mapema novemba,2015.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida amesema kuwa CCM inamuunga mkono hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Rais John Magufuli za kutumbua majipu.
Wamempongeza kwa  kubana matumizi ya umma, kuziba mianya ya rushwa, kupiga vita ubadhirifu wa mali ya umma na kurejesha nidhamu na uwajibikaji kwenye taasisi za umma na nchi kwa ujumla.
Wenyeviiti hao  wamemuomba Rais Magufuli aendeleze kasi yake ya kutekeleza majukumu yake na asisite kuwawajibisha watendaji wote wazembe wanaozalisha kero ya utoaji huduma duni kwa wananchi.
Madabida alisema katika kampeni zilizoendeshwa kote nchini, Dk Magufuli aliahidi Watanzania watakapomchagua kuwa Rais atatekeleza kwa juhudi na maarifa masuala ya kuondoa umasikini; kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana; kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama kwa maisha ya wananchi na mali zao. Kwa upande mwingine  wenyeviti hao wamefadhaishwa na vitendo vya vilivyofanywa na wabunge wa kambi ya Upinzani vya kupiga kelele na kusababisha kutolewa nje kabla ya Dk Magufuli kutoa hotuba yake Bungeni  hivi karibuni.

Kasi ya Rais Magufuli yawakumba Omba Omba Dar es salaam

Kasi ya Rais Magufuli yawakumba Omba Omba Dar es salaam

Tarehe December 6, 2015
Omba omba katika moja ya eneo jijini Da res salaam.
Omba omba katika moja ya eneo jijini Da res salaam.
Kasi ya Rais John  Magufuli ime endelea kutikisa katika maeneo mbalimbali ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Sadiki  amesema kwamba utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.
“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” alisema.

Amesisitizia  Wakurugenzi hao kuhakikisha kuwa ombaomba hao hawarudi mjini kutokana na kuwa na mazoea wakiondolewa kurudi tena katika maeneo hayo.
Licha ya timua timua hiyo kuwakumba  Omba omba wapiga debe  nao wameunganishwa katika kundi la watakao ondolewa  kufuatia kuwa kero kwa abiria.

Kasi ya Rais Magufuli yawatimua Vigogo 7 Tanecso

Kasi ya Rais Magufuli yawatimua Vigogo 7 Tanecso

Tarehe December 6, 2015
Makao makuu ya Shirika la Umeme Tanzania.
Makao makuu ya Shirika la Umeme Tanzania.
Kasi ya Rais John Pombe Magufuli ime endelea kushika kasi katika kuwashughulikia watendaji wazembe ambapo Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewatimua kazi  wafanyakazi 7 kutokana na makosa mbalimbali.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Tanesco imebainisha kuwa imewachukulia hatua wafanyakazi ambao wamekuwa wakitoa huduma  mbaya na kuwa Kero kwa wateja zikiwemo lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma, kucheleweshewa huduma na ubadhirifu.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.
Aidha, Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na vyombo vya habari jana. Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, Wahandisi na Wahasibu.


Taarifa hiyo imesisitiza kuwa  Shirika linaendelea na uchunguzi na mfanyakazi ye yote atakayebainika analaghai wateja, anadai rushwa, anatoa lugha chafu au huduma mbovu atawajibishwa mara moja na pale atakabobainika    ataachishwa kazi.
Kwa upande mwingine shirika hilo limesema kwamba ili kuendana na agizo la Rais Magufuli la kufanya usafi Desemba 9 nchini Wafanyakazi wote wa TANESCO watashiriki katika shughuli mbali mbali za usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayozunguka ofisi, mitambo na vituo nchi nchi nzima.

Makampuni 41 yatajwa ukwepa kodi Sakata la makontena 329

Makampuni 41 yatajwa ukwepa kodi Sakata la makontena 329

Tarehe December 6, 2015
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA,Phillip Mpango.
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA,Phillip Mpango.(katikati) akizungumza na wanahabari.
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA)  imeyataja majina ya kampuni 41 na wamiliki wa makontena 329 ambayo yalipitishwa bandarini bila kulipiwa ushuru.
Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango alisema Mamlaka hiyo iliagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa kuchukua hatua mara moja kwa kufuatilia na kubaini wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) zilizohusika katika kashfa hiyo.
Bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo ni pamoja na matairi ya magari, samani mbalimbali, betri za magari, vifaa vya ujenzi, nguo na bidhaa zingine mchanganyiko.
Dk. Mpango aliyataja majina ya makampuni na watu binafsi na idadi ya makontena waliyopitisha bila kulipia ushuru ambayo ni kama ifuatavyo;

clouds stream