Wednesday 30 November 2016

Sababu za kuanguka ndege ya Brazil zatajwa

  • Colombia
Visanduku vya mawasiliano ajali ya ndege ya Brazil vyapatikana


Ndege iliyokuwa imewabeba wachezaji wa timu ya mpira kutoka nchini Brazil ambayo ilipata ajali nchini Colombia inasemekana kwa muujibu wa taarifa zilizovuja ndege hiyo iliishiwa mafuta kutoka katika kifaa cha kurekodia mawasiliano.

Katika mnara wa mawasiliano ya ndege , rubani alisikika akirudia mara kadhaa akiomba ruhusa ya kutua kwa dharura kutokana na hitilafu ya umeme iliyokuwamo ndegeni pamoja na kuishiwa mafuta ya ndege.

Kabla hata mawasiliano hayo yaliyorekodiwa kufikia mwisho ,rubani alisikika akisema yuko angani umbali wa futi elfu tisa sawa na mita elfu mbili mia saba na arobaini na tatu.Taarifa za mawasiliano hayo zimekuwa gumzo katika mitandao kadhaa nchini Colombia na hata katika vyombo vya habari nchini humo, na hivyo kumekuwepo fununu za taarifa hizo kuwa huenda zikawa na chembe ya ukweli kwamba kuishiwa kwa mafuta ndiyo chanzo zha ajali ya ndege hiyo.

Wanajeshi wa Colombia waliliambia shirika la habari la AFP, kwamba pamoja na ndege hiyo kuanguka kuna shaka juu ya ajali hiyo kwani pamoja na ndege hiyo kuanguka hakukuwa na mlipuko wowote na kwamba huenda kulitumika nguvu ingine tofauti na nadharia ya kwisha kwa mafuta ndegeni.

Wadadisi wa mambo na wachunguzi bado hawako tayari kufungua mdomo na kuzungumzia juu ya chanzo chochote cha ajali hiyo na kwamba taarifa kamili ya uchunguzi itatolewa baada ya miezi kadhaa.

Wachezaji wa timu ya Chapecoense walikuwa safarini kuelekea nchini Colombian kwenye mji wa Medellin mahali kulikotarajiwa mechi kubwa ya mpira wa miguu ya kihistoria na badala yake wachezaji hao wameacha historia .Kufuatia vifo vya wachezaji wa timu hiyo, ulimwengu mzima umeungana kuomboleza vifo vyao.

Kwa muujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika shirika la ndege la Lamia watu wanne waliokuwa wasafiri na ndege hiyo wameponea chupuchupu kuwa miongoni mwa waliokufa baada ya kukosa tiketi.

Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye ni fundi wa ndege Erwin Tumiri, ameeleza namna alivyokwepa kifo, kwamba yeye alifuata maelekezo yote ya namna ya kujiokoa ,anasema abiria wenzie , walio wengi walisimama na kuanza kupiga kelele nay eye aliamua kuweka sanduku lake la kusafiria kati kati ya miguu yake na kuamua kubaki hivyo.

Visanduku viwili vya mawasiliano vya ndege hiyo vyote vilipatikana na tayari vimeanza kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa masuala ya anga.

Wachunguzi wataalamu kutoka nchini Uingereza wanasaidiana na mamlaka za Amerika Kusini kwasababu ndege iliyopata ajali ilitengenezwa na wana anga wa Uingereza BAE nchini Uingereza.Brazil imeanza siku tatu za maombolezo wakati maelfu ya watu na washabiki wa timu ya Chapecoense wako katika mji yaliko makao makuu ya timu hiyo Chapeco wanaendelea mkesha wa maombolezo wakati maandalizi ya kuchukua mabaki ya wachezaji hao inafanywa na jeshi kurejeshwa Brazil ili kuzikwa kwa pamoja katika uwanja wa Chapeco.

Nchi ya Bolivia tayari imekwisha tuma ndege ya kuchukua mabaki ya raia wake waliokufa katika ajali hiyo nchini Colombia.

Timu hiyo iliandika historia ya mafanikio katika soka kwa kuwa kileleni mwa ligi ya Brazil kwamara ya kwanza mwaka 2014.Kati ya watu 77 waliokuwa wameabiri ndege hiyo miongoni mwao ni watu sita tu ndiyo walionusurika .Abiria walio wengi walikuwa ni wachezaji wa timu ya Chapecoense na waandishi habari wapatao ishirini walikuwa miongoni mwa walipoteza maisha .

Zanzibar yamwaga bidhaa zisizofaa

  • Zanzibar

Wafanyakazi wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) wakiwa katika maandalizi ya kuharibu chakula na dawa zilizoharibika na kupitwa na wakati katika dampo la Kibele.




img-20161130-wa0008

Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDB) imeangamiza zaidi ya tani 62 za vyakula vibovu na vilivyopitwa na wakati katika zoezi lililofanyika Kibele Mkoa Kusini Unguja.Mkuu wa Idara ya Biashara na Uendeshaji wa ZFDB Ndugu Abdulaziz Shaib Mohd amesema bidhaa hizo mbovu zinatokana na tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kujenga matumaini ya kuingiza faida kwa bidhaa wanazouza bila kuangalia usalama wa bidhaa hizo kwa afya za watumiaji.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuangamiza bidhaa hizo, Ndugu Abdulaziz ambae pia ni Mkuu wa operesheni wa uangamizaji amesema bidhaa hizo zimegundulika kufuatia operesheni iliyofanywa na Bodi katika maghala na maduka mbali mbali ya Unguja.Amesema ZFDB ambayo moja ya jukumu lake ni kusimamia ubora na usalama wa chakula, dawa na vipodozi kwa matumizi ya wananchi, itaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika maghala yanayowekwa bidhaa na kwenye maduka ili kuhakikisha jukumu hilo linafanikiwa.

Amewataka wafanyabiashara kuwa wazalendo kwa wananchi wenzao na kujuwa kwamba biashara mbovu ama zilizopitwa na wakati ni sumu na zinaweza kudhofisha afya zao.Mkuu wa Idara ya Chakula bibi Aisha Suleiman amesema mchango mkubwa wa raia wema ndio uliofanikisha kugundulika bidhaa mbovu na zilizopitwa na wakati katika maduka na maghala mbali mbali.

Hata hivyo amewataka wananchi kujenga tabia ya kuchunguza tarehe ya kumaliza muda bidhaa wanazonunua na wanapogundua bidhaa imepitwa na wakati watoe taarifa katika Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

Wakati huo huo;

Afisa Mkuu wa Idara ya Dawa na Vipodozi Ndugu Mwadini Ahmada Mwadini ,amesema vipodozi haramu vilivyokamatwa baadhi yake vina kemikali zenye sumu na hazifai kwa afya ya binadamu.Amewashauri wafanyabiashara wanaotaka kuanzisha biashara ya dawa na vipodozi kushirikiana na Bodi hiyo kwa lengo la kulinda afya za wananchi.

Dawa zilizoangamizwa katika operesheni hiyo ni mafuta ya kula lita 10,105, sukari tani 2.15, mchele tani 26, tende tani 10, bidhaa mchanganyiko za mboga mboga tani 13, dawa na vipodozi tani tatu.

Tuesday 29 November 2016

Chanjo ya ukimwi kujaribiwa Afrika Kusini

Afrika Kusini

Chanjo ya ugonjwa na virusi vya ukimwi

Chanjo mpya dhidi ya virusi vya ukimwi na ukimwi inatarajiwa kufanyiwa majaribio hii leo nchini Afrika Kusini.wanasayansi wanaeleza kwamba itakuwa kliniki kubwa na ya aina yake katika nchi ambayo ugonjwa wa ukimwi umeota miziz.

Taasisi ya kitaifa ya Afya nchini Marekani, ambayo inafadhili jaribio hilo, imeeleza kwamba zaidi ya watu elfu moja hupata maambukizi mapya kila siku nchini humo.

Utafiti huo umepewa jina HVTN 702 una lengo la kuwafikia zaidi ya watu 5000 wanaojishirikisha na ngono wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi na ukimwi kwa wanaume na wanawake nchini Afrika Kusini.

Idadi hiyo imeahidiwa kupata sindano tano kwa mwaka. Chanjo hiyo ilikwisha fanyiwa majaribio mwaka 2009 nchini Taniland na kuonekana inaouwezo wa kuzuia maambukizi kwa asilimia thelathini na moja katika kipindi cha miaka mitatu.

Wanasayansi bado wanalo tumaini kwamba kwa asilimia hamsini na zaidi chanjo hiyo inao uwezo wa kuonesha mafanikio nchini Afrika Kusini kwa watu wanaokadiriwa kufikia milioni saba ambao wanaishi na virusi vya ukimwi na ukimwi.

Matokeo ya utafiti wa chanjo hiyo yanatarajiwa kutolewa hadharani katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Frederick Sumaye anyang'anywa ardhi

Tanzania

Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania katika awamu ya tatu Fredrick Sumaye

Rais wa Jamhuri ya Tanzania amefuta hati ya umili ardhi ya shamba kubwa lililokuwa likimilikiwa na waziri mkuu mstaafu Frederick Sumaye kwasababu zilizoelezwa na serikali wa mtaa kuwa liliachwa bila kuendelezwa .

Hatua hiyo imekuja baada ya Tanzania kuzindua kampeni kubwa ya kurejesha ardhi mikononi mwa watanzania ambayo haijaendelezwa na wawekezaji waliomilikishwa awali na kuwapa wakulima masikini .

Hata hivyo, Frederick Sumaye ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu kwa muda wa miaka kumi kuanzia mwaka 1995 na kuamua kuhamia kambi ya upinzani baada ya uchaguzi wa Tanzania mwaka wa jana uamuzi ulioelezwa kuwa na msukumo wa kisiasa.

Sumaye alisema kama lengo la kumnyang'anya ardhi yake ni jaribio la kumlazimisha kurejea katika chama tawala, "wasahau ''.

Rais Magufuli azuru gereza la Ukonga ghafla

Tanzania

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,akiwa katika gereza la Ukonga.

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar -Es - Salaam na kupiga marufuku uuzwaji wa sare za majeshi nchini humo na watu binafsi na kutaka wale wote wanaouza sare hizo wazikabidhi kwa majeshi husika mara moja.

Rais Magufuli amepiga marufuku hiyo kufuatia maelezo kutoka kwa baadhi ya askari wa Jeshi la Magereza kuwa wamekuwa wakinunua sare za jeshi hilo kutoka kwa watu binafsi kinyume na taratibu za majeshi na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua mara moja wale wote watakaobainika kuuza sare za majeshi.

Hali kadhalika Rais magufuli amepiga marufuku kwa majeshi yote nchini mwake kuingia ubia na watu binafsi kupangisha ama kuuza maeneo yao kwa ajili ya kufanya biashara na kutaka maeneo yote ya majeshi yabaki katika jeshi husika.''Haiwezekani sare za majeshi yetu hapa nchini kuuzwa na watu binafsi hilo haliwezekani kamwe labda baada ya kumaliza muda wangu , amesema Rais magufuli''

Aidha Rais Magufuli ametoa shilingi Bilioni Kumi kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kujenga nyumba mpya zitakazotumika kwa ajili ya makazi ya askari wa Jeshi la Magereza katika Gereza la Ukonga jijini DSM.

Hatua hiyo inafuatia kilio cha askari Magereza kuwa wengi wao wamekuwa wakiishi uaraiani kitu ambacho ni tofauti na taratibu za majeshi na hata kuzorotesha utendaji kazi wa askari wa Jeshi hilo.

Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia ameagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanatumika katika uzalishaji mali badala ya mfumo wa sasa ambapo baadhi ya wafungwa wamekuwa wakitumia rasilimali za serikali bila kuzifanyia kazi.

Rais Magufuli amewahakikishia Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza kuwa serikali itaendelea kuboresha maslahi yao na vitendea kazi kama inavyofanya kwa majeshi mengine nchini Tanzania.

Sunday 27 November 2016

Maalim Seif: Sijahusika Kumfukuza Lipumba

Mwenyekiti wa chama cha CUF Prof Ibarahim Lipumba na makamu mwenyekiti wake Maalim Seif.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif amesema kuwa yeye sio sababu ya mgogoro uliopo sasa katika chama hicho na wala hajahusika kumfukuza uanachama Lipumba. Amesema CUF kupitia Baraza lake la Uongozi la Taifa liliamua kumfuta uanachama kwa sababu ya kukiuka katiba ya chama hicho.

“Sina ugomvi na Lipumba, sijamfukuza, na niko radhi kufanya nae mdahalo ili aeleze siri ya kujiuzulu na kung’ang’ania uenyekiti wa CUF. Na hata tukipatanishwa haitasaidia kitu sababu, siwezi badilisha, chama ndicho kilichomfukuza kwa kura za wajumbe zaidi ya asilimia 70,” amesema.

Maalim amedai kuwa, Lipumba anatumiwa na baadhi ya watu kuuzima mgogoro wa uchaguzi uliotokea visiwani Zanzibar mwaka jana.

“Mgogoro huu wa CUF ni muendelezo wa hujuma zinazohusiana na kuzima harakati za kudai haki Zanzibar, ndio maana Lipumba analindwa na vyombo vya dola kuuendeleza mgogoro huu ili CUF ishindwe fuatilia mgogoro wa uchaguzi Zanzibar na kwamba wakubwa waonekane hawakukosea,” ameongeza.

Kauli ya Maalim inakuja wakati kukiwa bado na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF kuanzia ngazi ya kata hadi taifa, ambapo viongozi waandamizi wa chama hicho ambao ni Katibu Mkuu Maalim Seif Hamad na aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyefutwa uanachama wameendelea kusigana na kupelekea kufunguliwa kwa kesi mahakamani dhidi ya Lipumba, Msajili wa Vyama vya Siasa na wengine.

Hivi karibuni Lipumba akiwa katika mkutano wake wa ndani na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji ya CUF wilaya ya Temeke, alidai kuwa Maalim na wafuasi wake wanapanga mikakati ya kukiuza chama na kwamba anahonga baadhi ya viongozi wa CUF kuanzia kata ili wamkatae kwa madai kuwa yeye ni kikwazo kwa Maalim kukiuza chama hicho.

Rais Wa Zambia,Chad Uso Kwa Uso Na Rais Magufuli

Rais John Pombe Mafgufuli akimpokea mgeni wake Edgar Lungu uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Rais John Pombe Mafgufuli akimpokea mgeni wake Edgar Lungu uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kiserikali ya siku 3 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais Lungu amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini humo pamoja na wananchi.

Akiwa uwanjani hapo Rais Lungu amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Rais Lungu ataendelea na ziara yake ambapo pamoja na kutembelea miradi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia ikiwemo TAZARA na TAZAMA, atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, atashuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia na jioni atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili yake Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno naye amewasili nchini Tanzania kwa ziara kikazi ya siku 2. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais Idriss Deby Itno akiwa na Mkewe Mama Hinda Deby amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na wananchi.

Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Rais Idriss Deby Itno Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mwili Wa Fidel Castro Kuchomwa Moto, Majivu Kuzungushwa Kwa Wananchi

Fidel Castro Enzi ya uhai wake.
Fidel Castro Enzi ya uhai wake.

Cuba inaadhimisha siku tisa za maombolezo kufuatia kufariki kwa Fidel Castro, anayejulikana kwa siasa zake za kimapinduzi, aliyetawala taifa hilo kwa miongo kadhaa na ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 90.

Mwili wake, utachomwa hadi kuwa majivu kama alivyotaka, katika sherehe ya kibinafsi, ambapo majivu yake yatazungushwa katika msafara maalumu kote nchini kabla ya kuzikwa katika Makaburi ya Mji wa Santiago Desemba tarehe nne.

Akiwa kiongozi mwenye mrengo wa kushoto na mwanamapinduzi msifiwa, alipendwa na kuchukiwa na watu mbalimbali kote duniani.

Lowassa Atoa Neno Kwa Waliomtakia Kifo

Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa.
Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa.

Aliyekuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ametoa kauli hiyo Mjini Mbinga Mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani.

Pasipo kutaja jina la mtu, Lowassa amesema Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.”

Amesema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.

“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa, bado mlinipigia kura nyingi ila Mungu ndiye hupanga yote,” amesema.

Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu wa Zamani amewataka wanachama wa Chadema kuendelea kuwa na ujasiri na kudumisha umoja kwa kuendelea kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.

Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza juu ya watu ambao walihoji kuhusu mwenendo wa afya yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Friday 25 November 2016

Steven Gerrard astaafu soka

Steven Gerrard astaafu soka

Steven Gerrard astaafu soka

Aliyekuwa nahodha wa Liverpool na timu ya Uingereza Steven Gerrard amestaafu na kukamilisha miaka 19 ya kucheza soka.

Gerrard mwenye umri wa miaka 36 aliichezea Liverpool mara 710 na kushinda mataji manane makuu ,lakini akajiunga na klabu ya LA Galaxy ya ligi ya MLS nchini Marekani mwaka 2015.

Kiungo huyo wa kati ni mchezaji wa nne kuichezea mara nyingi Uingereza baada ya kucheza mara 144 mbali na kuwa nahodha wa timu hiyo ya taifa katika mashindano matatu kati ya sita aliyoshiriki.

''Ni bahati kubwa kushiriki katika michuano mingi wakati nilipokuwa nikisakata kandanda'',alisema Gerrard

"Nimekuwa na muda mzuri na nashkuru kwa wakati wote wa muda wangu katika timu ya Liverpool ,Uingereza na LA Galaxy.Nilifanikisha ndoto yangu ya utotoni kwa kuichezea Liverpool''.

Picha: Moto mkubwa watishia Israel

Mawaziri walumbana uteuzi wa mgombea urais Ufaransa

Francois Fillon, hakujarajiwa kushinda awamu ya kwanza ya kura zilizopigwa

Francois Fillon, hakutarajiwa kushinda awamu ya kwanza ya kura zilizopigwa

Mawaziri wakuu wastaafu wawili nchini Ufaransa walilumbana katika mdaalo wa Televisheni baada ya uteuzi wa mgombea wa urais wa mrengwa wa kulia wa chama cha Pepublican.

Francois Fillon, hakujarajiwa kushinda awamu ya kwanza ya kura zilizopigwa na kumlalamikia Alan Juppe kwa kuonyesha misimamo yake ya kale.

Bwana Juppe amesema kuwa mipango ya mpinzani wake ikiwemo suala la kupunguzwa kwa bajeti ilikuwa mibaya.

Mwakilishi kutoka Paris anasema atakayeteuliwa katika chama cha Republican pamoja na mgawanyiko wa uongozi wa chama cha Socialist atambambana na kiongozi Marine Le Pen wa mrengwa wa kulia katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mei mwakani.

Viongozi Colombia watia saini makubaliano ya amani

Rais Santos (kushoto) na kiongozi wa kundi la waasi Timochenko wakipeana mkono

Rais Santos (kushoto) na kiongozi wa kundi la waasi Timochenko wakipeana mkono

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos na kiongozi wa kundi la FARC Rodrigo Lodono maarufu kama Timochenko, wametia saini makubaliano ya amani huko Bogota ambapo inatarajiwa itamaliza malumbano yaliyodumu kwa takribani nusu karne.

Makubaliano ya kwanza yalipingwa mwezi uliopita kwa kura za maoni.

Wapinzani walipinga na kusema kwamba mkataba huo ulikuwa hauna manufaa kwao.

Wiki ijayo makubaliano yatawasilishwa bungeni kwa uchambuzi zaidi ambapo muungano wa serikali unawingi wa viti.

Upinzani unaongozwa na Alvaro Uribe aliyekuwa Rais ambapo wataongoza maandamano wakishinikiza kuwepo kwa kura za maoni kwa mara ya pili kuhusiana na mkataba huo.

Viongozi Colombia watia saini makubaliano ya amani

Rais Santos (kushoto) na kiongozi wa kundi la waasi Timochenko wakipeana mkono

Rais Santos (kushoto) na kiongozi wa kundi la waasi Timochenko wakipeana mkono

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos na kiongozi wa kundi la FARC Rodrigo Lodono maarufu kama Timochenko, wametia saini makubaliano ya amani huko Bogota ambapo inatarajiwa itamaliza malumbano yaliyodumu kwa takribani nusu karne.

Makubaliano ya kwanza yalipingwa mwezi uliopita kwa kura za maoni.

Wapinzani walipinga na kusema kwamba mkataba huo ulikuwa hauna manufaa kwao.

Wiki ijayo makubaliano yatawasilishwa bungeni kwa uchambuzi zaidi ambapo muungano wa serikali unawingi wa viti.

Upinzani unaongozwa na Alvaro Uribe aliyekuwa Rais ambapo wataongoza maandamano wakishinikiza kuwepo kwa kura za maoni kwa mara ya pili kuhusiana na mkataba huo.

Wednesday 23 November 2016

Uefa: Man City yatinga hatua ya mtoano kwa mara ya nne mfululizo

David Silva akiifungia City goli

David Silva akiifungia City goli

Mchezaji kiungo David silva ameithibitishia klabu ya Manchester City kuingia hatua ya mtoano kwa mara nne mfululizo kwa kutoka sare ya goli 1-1 dhidi ya Borussia Monchengladbach.

Mchezo huo uliokuwa wa vuta nikutute ulishuhudia kila timu ikimaliza na wachezaji 10 kiungo Lars Stindl akilimwa kadi nyekundu dakika ya 51 kabla ya Fernandinho wa man city kuzawadiwa kadi nyekundu dakika ya 63.

Kocha wa timu ya Manchester City Pep Guardiola amesema amefurahishwa na kiwango cha timu yake na kuongeza kuwa kwa matokeo waliyoyayapata moja kwa moja wameepuka kupangiwa na Bayern Munich

Matokeo ya michezo mingine

Besiktas 3-3 Benfica

FC Rostov 3-2 Bayern Mun

Arsenal 2-2 Paris St G

PFC Ludogorets Razgrad 0 -0 Basel

Napoli 0 -0 Dynamo Kiev

Borussia Mönchengladbach 1-1 Manchester City F.C.

Celtic 0-2 Barcelona

Atlético Madrid 2-0 PSV Eindhoven

Polisi Wampiga Risasi Mwanafunzi

bastola

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Gerezani, Shakil Sures amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kujeruhiwa kwa risasi na polisi kwenye mazingira ya kutatanisha.

Tukio hilo linadaiwa kutokea siku ya Jumatatu eneo la Fire, Upanga licha ya watu kusikia milio ya risasi, kushuhudia polisi wakipita na kumuona kijana huyo akiwa tayari kajeruhiwa, lakini hakuna mwenye maelezo sahihi kuhusu nini kilitokea hadi askari hao wakachukua hatua hiyo.

Baadhi ya watu waliokuwepo eneo la tukio Fire, Upanga siku ya Jumatatu walidai kuwaona askari waliokuwa eneo hilo wakirusha risasi, bila kujua walikuwa wakipambana na nani.

Mmoja wa mashuhuda, Athumani Simba alidai walidhani ni majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi, baada ya kuona gari la polisi likipita eneo hilo.

“Niliwaona askari wawili wakielekea eneo la Fire huku wakipiga risasi, ghafla nilimuona mwanafunzi akilia huku akiwa ameshika mguu wake akiomba msaada,” alisema Simba.

Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha amesema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo jioni ya Jumatatu na kwamba jeraha lake linaendelea vizuri.

“Tumempokea mwanafunzi Shakil juzi jioni na kidonda chake kimesafishwa na kinaendelea vizuri,” amesema Aligaesha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Hamduni Salum amesema upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea. Hata hivyo, hakueleza mazingira ya tukio lenyewe yalivyokuwa.

“Tunawashikilia askari polisi wawili waliokuwa zamu siku hiyo ya tukio, upelelezi unaendelea ili kuangalia kwa nini walitumia nguvu kubwa kiasi hicho,” amesema Kamanda Salum.

Serikali Kula Sahani Moja Na Waajiri Wanaonyanyasa Wafanyakazi


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Serikali imesema kuwa haitawavumilia waajiri ambao hawatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na amewaonya waache tabia hiyo mara moja.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Amesema kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 kinaelekeza aina mbalimbali za mikataba inayotakiwa kutumika kuajiri wafanyakazi.

“Kisheria mwajiri anao wajibu wa kuhakikisha kila mtumishi wake ana mkataba wa kazi kwa maandishi,” amesema.

Kuhusu wafanyakazi kuwekwa ndani kiholela, kunyanyaswa, kushushwa vyeo na kusimamishwa kazi na wanasiasa, Waziri Mkuu amesema Serikali chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea kuzingatia utawala wa sheria na kanuni za utawala bora ili kuhakikisha kuwa haki za wafanyakazi zinalindwa ipasavyo.

“Kimsingi watumishi wanasimamiwa na mamlaka za kinidhamu na sheria mbalimbali ambazo hazina budi kuangaliwa kwa pamoja kabla ya kuchukua hatua. Ninawaagiza viongozi wenzagu wa kisiasa na walioko katika wizara na taasisi zote za Serikali, mikoani, wilayani, kwenye idara za Serikali na Halmashauri wazingatie utawala wa sheria wakati wa kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu wajibu na haki za wafanyakazi,” ameongeza.

Wafuasi wa Trump wakerwa na uamuzi kuhusu Clinton

Hillary Clinton na Donald Trump.


Wafuasi wahafidhina wa rais mteule wa Marekani Donald Trump wamelalamikia uamuzi wa kiongozi huyo wa kutofuatilia uchunguzi mpya kuhusu kashfa ya barua pepe iliyomkabili mpinzani wake Hillary Clinton.

Maafisa wake walitangaza Jumanne kwamba hatafuatilia ahadi yake ya kuhakikisha Bi Clinton anafungwa jela.

Bw Trump baadaye alifafanua na kusema hatua kama hiyo inaweza kuzua migawanyiko zaidi.

FBI walimuondolea Bi Clinton makosa lakini wafuasi wa Bw Trump walikuwa wakiimba "lock her up" (mfunge jela) kwenye mikutano yake ya kampeni.

Wafuasi wahafidhina sasa wanasema hatua hiyo ya Bw Trump ni "usaliti" na kwamba amevunja ahadi yake.

Tovuti ya Redstate.com imesema hatua ya Bw Trump kutomteua mwendesha mashtaka maalum wa kufuatilia tuhuma hizo dhidi ya Bi Clinton, kama alivyokuwa ameahidi, itafichua "ukweli kwamba yeye ni mtu aliyejidai kuwa wakati wa kampeni".

Tovuti ya mrengo wa kulia ya Breitbart News Network, moja ya tovuti za habari zinazomuunga mkono sana Bw Trump pia ilishutumu hatua hiyo na kusema ni "ahadi iliyovunjwa".


Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Ann Coulter, ambaye ni mhafidhina, aliandika kwenye Twitter: "Whoa! Nilidhani tulimchagua @realDonaldTrump kuwa rais. Tulimfanya FBI, & DOJ? Kazi yake ni kuwateua, si kufanya kazi yao."

Kisha, alifuatiliza kwa ujumbe mwingine: "Hakuna rais anayefaa kuwa akiwazuia wachunguzi kufanya kazi yao. #EqualUnderLaw (Wote sawa mbele ya sheria)"

Shirika la kisheria linaloegemea sasa za mrengo wa kulia la Judicial Watch lilisema huo ni usaliti kwa Wamarekani kuhusu "ahadi yake kwa Wamarekani ya kuondoa maji yote kutoka kwa 'kinamasi' cha ufisadi uliokithiri Washington".

Mfuasi wa Trump
Wafuasi wa Bw Trump kwenye kampeni walifurahia ahadi yake ya kufunga Clinton


Wakati wa kampeni, Bw Trump alisema mpinzani wake alikuwa mtu mwovu sana na kuapa kwamba angehakikisha kesi zinafunguliwa dhidi yake.

Alimweleza kama mgombea mfisadi zaidi kuwahi kuwania urais nchini Marekani.

Lakini tangu uchaguzi kumalizika, alionekana kuanza kulegeza msimamo.

Wiki moja iliyopita, alisema familia ya Clinton ni ya "watu wema".

Kisha, Jumanne asubuhi, msemaji wake Kellyanne Conway alisema hakutakuwa na uchunguzi zaidi kuhusu barua pepe za Bi Clinton ili kumpa nafasi ya "kupona".

Saa chache baadaye, Bw Trump mwenyewe aliambia New York Times kwamba uchunguzi mpya haujafutiliwa kabisa lakini hakuna uwezekano mkubwa wa hilo kufanyika kwani litazua migawanyiko zaidi.

"Nataka kusonga mbele. Sitaki kurudi nyuma. Sitaku kuumiza familia ya Clinton, sitaki kamwe."

Kwenye mahojiano na New York Time, Bw Trump pia alijitenga na kundi la watu wanaotetea ubabe wa watu weupe (Wazungu) ambao walipiga saluti za Nazi wakisherehekea ushindi wake mjini Washington Jumamosi.

Pia, alisema:

  • Shemeji yake Jared Kushner, mfanyabiashara wa nyumba na makao ambaye hana ujuzi katika demokrasia, anaweza kusaidia kupatikana kwa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina, alisema. Bw Kushner ni mumewe Ivanka, bintiye Bw Trump na ni Myahudi.

  • Marekani haifai kuwa "mjenzi wa mataifa" duniani, alisema.

  • Viongozi wa Republican Paul Ryan na Mitch McConnell "wanampenda tena, alisema

  • Anaweza kuendesha biashara zake na nchi pia, bila kuwa na mgongano wa maslahi

  • Kuna uhusiano fulani kati ya shughuli za kibinadamu na mabadiliko ya tabia nchi

Bw Trump ataapishwa 20 Januari, 2017.

Tuesday 22 November 2016

UEFA: Leicester City wang'ara mbele ya Club Brugge

Leicester iliutawala vyema mchezo huo

Leicester iliutawala vyema mchezo huo

Leicester city wamepata ushindi maridhawa wakati wa muendelezo wa ligi ya mabigwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya club Brugge.
Leicester wanahitaji alama moja tu kutinga hatua ya mtoano.
Leicester hawajapoteza mchezo wowote ligi ya mabingwa Ulaya
Leicester hawajapoteza mchezo wowote ligi ya mabingwa Ulaya
Mchezaji Shinji Okazaki alimaliza vyema kazi ya Christian Fuchs na kuandika goli la kwanza kwa kikosi hicho kinachonolewa na Muitaliano Claudio Ranieri.
Riyad Mahrez akaongeza goli la pili kwa penati murua ikiwa ni goli lake la nne ndani ya ligi ya mabigwa baada ya Marc Albrighton kuangushwa ndani ya eneo la hatari.
Leicester city hawashikiki katika ligi ya mabingwa Ulaya huku wakiwa wanaboronga EPL.

Dotmund wanakuwa timu ya nne kufunga magoli nane katika mchezo mmoja
Dotmund wanakuwa timu ya nne kufunga magoli nane katika mchezo mmoja

Matokeo ya michezo mingine

Monaco 2-1 Tottenham
Borussia Dortmund 8-4 Legia Warsaw
Sporting 1- 2 Real Madrid
CSKA Moscow 1- 1 Bayer 04 Leverkusen
FC Copenhagen 0-0 FC Porto
Dinamo Zagreb 0-1 Olympique Lyonnais
Sevilla 1- 2 Juventus

Samatta Aenguliwa Tuzo Mwanasoka Bora Africa, 5 Watakaomenyana Hawa Hapa

Mshanmbuliaji wa klabu ya TP Mazembe na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta
Mshambuliaji wa klabu ya Genk ya Ubelgiji na timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya wachezaji watano watakaowania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika 2016, na kumuengua nyota na straika wa Tanzania, Mbwana Samatta aliyekuwemo katika orodha ya awali ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ya heshima kubwa Afrika.

Wachezaji watano ambao sasa watamenyana kuisaka tuzo hiyo ni pamoja na Emerick Aubameyang kutoka nchini Gabon na anayekipiga katika klabu ya Borrusia Dortmund, Sadio Mane kutoka Senegal na anayekipiga katika klabu ya Liverpool, na Riyadh Mahrez kutoka Algeria na anyekinukisha katika klabu ya Leicester City.

Wengine ni pamoja na Mohamed Salah kutoka Misri na anayeichezea klabu ya Roma ya Italia na wa mwisho ni Islam Slimani kutoka Algeria na anayeichezea klabu ya Leicester City.

Trump abadili msimamo wake kuhusu barua pepe za Clinton

Clinton na Trump

Clinton na Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump hatoanzisha uchunguzi mwengine kuhusu barua pepe za Hillary Clinton ili kumsaidia ''kujiuguza'',msemaji wake amesema.

Mshauri mkuu wa Trump, Kellyanne Conway amesema kuwa Trump hatotekeleza ahadi yake ya kumteua mwendesha mashtaka ili kumchunguza aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Hillary Clinton.

Bw. Trump alitishia kumfunga jela Bi Clinton na katika mikutano yake wafuasi wake walimuungan mkono kwa kusema ''mfunge jela!''

Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani James Comey alimuondolea makosa bi Clinton.

Bi Conway alimwambia mtangazaji wa kipindi cha alfajiri cha MSNBC Joe Scarborough:Nadhani wakati rais mteule ambaye pia ni kiongozi wa chama chenu sasa ,Joe, anasema kabla hajaapishwa hapendelei kumfungulia mashtaka ,ni ujumbe mzito sana kwa wanachama.

''Na nadhani Hillary Clinton anafaa kujua kwamba raia wengi wa Marekani hawamuamini ,lakini Donald Trump anaweza kumsaidia kujiuguza,basi pengine kwamba hilo ni jambo zuri'',aliongezea.

RONALDO AMPIGA BAO GWIJI DI STEFANO KWA KUFUNGA DHIDI YA ATLETICO


Cristiano Ronaldo alifunga mabao matatu yaani hat trick wakati Real Madrid ikiiangusha Atletico Madrid nyumbani kwake Vicente Calderon jijini Madrid na hiyo ikawa ni hat trick ya 39 katika maisha ya soka ya Ronaldo.

Lakini kitu kikubwa kabisa kwa kwa Ronaldo ni kwamba, amefanikiwa kuivuka rekodi ya gwiji la Madrid, Alfred di Stefano katika ufungaji wa mabao katika derby ya timu hizo kubwa za jiji la Madrid, pia nchini Hispania.


Di Stefano alikuwa amefunga mabao 17 wakati akiichezea Madrid dhidi ya Atletico lakini Ronaldo aliyekuwa anashika nafasi ya tatu, hat trick yake imemfanya kufikisha mabao 18.

Sunday 20 November 2016

WENGER, MOURINHO BADO HAKIJAELEWEKA, HIVI NDIVYO WALIVYOPEANA MKONO BAADA YA GAME

Unaweza kusema hawa wazee wana lao jambo. Jose Mourinho na Arsene Wenger wanaonekana kweli hawaivi chungu kimoja.

Baada ya mechi ya Ligi Kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Arsenal, makocha hao walipeana mkono kwa staili ambayo inaonyesha ilimradi.

Mara baada ya mechi walikutana na kupeana mkono kama sehemu ya kutimiza wajibu lakini hakuna aliyemtazama mwenzake usoni wala kuzungumza.

 
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1, Arsenal wakisawazisha mwishoni kupitia Mfaransa Olvier Giroud aliyeingia kipindi cha pili.




clouds stream