Monday 27 July 2015

HOUSE FOR SALE



A HOUSE FOR SALE: Located at Goba few meters from main road,it has 3 bed rooms one being a master bed room, sitting room,dinning room,kitchen
, it has enough compound 1200 sqm, PRICE is TSH. 8O million ( negotiable ), contact us at 0652314181 for more details.

Rais Obama atua nchini Ethiopia


Rais Obama atua nchini Ethiopia



Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili nchini Ethiopia.
 Raisi Barack Obama akipokelewa na rais wa Ethiopia.
Rais Obama akipokea shada.
Rais Barack Obama wa Marekani hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya nchi za Afrika.
Ni mara yake ya kwanza tangu aongoze taifa la Marekani akiwa raisi kuhutubia wanachama hamsini na mbili wa umoja wa Afrika katika makao makuu yake yaliyoko Addis ababa. Mazungumzo yao yakiwa yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita za wenyewe kwa wenyewe sudan ya kusini.
Raisi Obama,aliwasili nchini Ethiopia akiwa anatokea mjini Nairobi ambako aliwaambia wakenya kuwa amna kikomo cha kile wanachokihitaji na kusisitiza kwa kutoa angalizo katika athari za ukabila na rushwa. Tamaduni mbaya kama unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za kulazimishwa ,tohara kwa watoto wa kike na kutopeleka watoto shuleni.

Matukio katika picha: Rais Obama alipowasili nchini Kenya

Matukio katika picha: Rais Obama alipowasili nchini Kenya



Rais wa Marekani Barack Obama akiwasili nchini Kenya.
Rais Barack Obama wa Marekani amewsili nchini Kenya na kupokelewa na mwenyejinwake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta   kwenye uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Akiwa nchini Kenya Rais Obama atafungua mkutano wa Kimataifa  wa kibiashara, Ugaidi na haki za binadamu  unaofanyika nchini humo kabla ya kuendelea na ziara yake nchini Ethiopia
Endelea kuwa nasi tutakujulisha kila kinacho endelea katika ziara ya Rais Obama nchini Kenya.
Rais Obama akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuwasili nchini Kenya.
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa na bibi yake Mama Sarah Obama kushoto na dada yake Auma Obama katika chakula cha jioni na wanandugu wa familia ya Obama nchini Kenya.
Ndege ya Marekani iliyombeba Rais Barack obama.
Rais Barack Obama wa Marekani akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Nkurunziza ashinda kwa kishindo Urais Burundi

Nkurunziza ashinda kwa kishindo Urais Burundi



Rais Nkurunziza ashinda.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ameshinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo, kwa kupata asilimia 69.41 ya kura zote zilizopigwa Jumanne wiki hii.
Taarifa zilizotolewa na AFP jana jioni, zilieleza kuwa Tume ya Uchaguzi ya Burundi, imetoa matokeo hayo yaliyoonesha kuwa amepata ushindi katika awamu ya kwanza ya upigaji kura.
Kwa matokeo hayo, Nkurunziza amewashinda wagombea wanane walioshiriki katika uchaguzi huo na hivyo kupata fursa ya kuongoza nchi hiyo kwa awamu ya tatu, baada ya kushiriki katika uchaguzi wa kidemokrasia mara mbili.

Tuesday 21 July 2015

KAGAME CUP 2015: Al-Khartoum 5 Telecom 0

KAGAME CUP 2015: Al-Khartoum 5 Telecom 0

Tarehe July 20, 2015
Wachezajin wa Khartoum ya Sudani wakishangilia baada ya kuifunga TELECOM ya Uganda
Ikiwa leo ni siku ya 3 tangu ufunguzi wa michuano ya Cecafa kuanza huku mchezo wa ufunguzi ukiwaacha Yanga akipata kichapo dhidi ya Gor Mahia. mechi ya mchana leo imeikutanisha timu ya Telecom ya Djibout na Al-Khartoum ya Sudan ambayo imeishia kwa timu ya Khartoum kupata ushindi wa mabao 5-0, huku magoli yakifungwa na Salah Bilal (22′ & 38), la tatu likifungwa na Ousmaila Baba kwenye dakika ya 66 ya mchezo.

Pele afanyiwa upasuaji tena


Pele afanyiwa upasuaji tena


Tarehe July 20, 2015
Mwnasoka mkongwe wa Brazil, Pele
Mchezaji mkongwe wa Brazil, Pele amelazimika kurejea tena hospitali kwa matibabu ikiwa ni miezi miwili imepita tangu afanyiwe upasuaji katika kibofu cha haja ndogo.
Vyombo vya habari vya Brazil vimesema Pele (74) alikuwa na maumivu ya misuli na amefanyiwa upasuaji mgongoni katika hospitali ya Albert Einstein, huko Sao Paulo.
Pele, ambaye ametwaa mara tatu kombe la dunia, alikuwa akitibiwa maambukizi ya mfumo wa haja ndogo miezi nane iliyopita baada ya kutolewa mawe kwenye figo yake.

Hofu yatanda Uchaguzi wa Rais Burundi

Hofu yatanda Uchaguzi wa Rais Burundi

Tarehe July 21, 2015
Vurugu nchini Burundi.
Hofu imetanda nchini Burundi kufuatia kutokea ufyatulianaji wa risasi na milipuko usiku kucha nchini Burundi, usiku wa kuamkia uchaguzi wa rais uliozua utata.
Vurugu  hizo zinafuatia wananci kupinga  Rais Nkurunziza kuwania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.
Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi. Maeneo mengine risasi hizo zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo. Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Kwa mujibu wa mshauri wa kisasa wa rais, amesema haya ni mashambulio yanayofanywa na ‘magaidi’ wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi
Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuzwa.

Monday 20 July 2015

BREAKING NEWS: Majambazi 5 mauaji ya Stakishari wakamatwa

 BREAKING NEWS: Majambazi 5 mauaji ya Stakishari wakamatwa
TAREHE 20 JULY


Jeshi la Polisi kanda ya Dar es Salaam chini ya Suleiman Kova imeyakamata majambazi 5 maeneo ya Mbagara yakiwa na fedha kiasi cha milioni 170 pamoja na bunduki 16 miongoni mwao ni zile zilizoibiwa kwenye kituo cha polisi Stakishari kilichopo Ukonga.






Sunday 19 July 2015

ZAIDI YAO MUSIC TOUR. Usikose kuuzulia burudani kutoka kwa wasanii wa bongo fleva mjini Dodoma, 1 August 2015

Baadhi ya wa sanii watakao kuwepo  kuwarusha wana Dodoma wakiongozwa na Yamoto band, Weusi, Belle9, Mo music, Samir, Baraka da prince, Mr brue, Nas B pamoja na Barnaba. Kuanzia saa nne asubuhi mpaka utakapo choka we mwenyewe, 1 / 8 / 2015, Kiingilio ni TSH 5000/=. USIKOSE.

Urais CCM wapamba Moto

Urais CCM wapamba Moto

Tarehe July 19, 2015

Mgombea Urais CCM akiwasili jijini Mwanza.
Urais umepamba moto CCM ambapo  chama hicho kimeanza mchakato wa kumtambulisha mgombea wake wa urais Dkt. John Pombe Magufuli aliyechaguliwa hivi karibuni.
Mgombea huyo jana amepokelewa  na umati wa wananchi alipowasili mkoani Mwanza  na baadae kuwahutubia wananchi  hao ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.
Aidha, mgombea  huyo alitambulishwa jijini Dar es salaam  siku ya jumanne  wiki  iliyopita amejizolea umaarufu kutokana na utendaji wake. Wanananchi mbalimbali jijini Dar es salaam wamekipongeza chama hicho kwa uteuzi huo.


Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM akiwasili kwenye ofisi za CCM mkoa wa Mwanza tayari kwa kuwasalimu wananchi na kujitambulisha.

Msafara wa mgombea Urais CCM jijini Mwanza.

Madiwani 20, Wenyeviti 6 kwa Lowassa, watua Chadema

Madiwani 20, Wenyeviti 6 kwa Lowassa, watua Chadema

Tarehe July 19, 2015
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa.
Madiwani 20 wa Chama  Cha Mapinduzi  CCM  katika Jimbo la Monduli, wamejiunga na Chadema kufuatia Mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa jina lake kukatwa  wakati akiomba ridhaa ya kugombea urais kupitia chama hicho.
Akizungumza jana katika mkutano wa hadhara kiongozi wa Madiwani hao, Julius Kalanga kutoka Kata ya Lepurko ambaye pia alikabidhi  kadi  yake  na  za wenzake 19 wa CCM kwa viongozi wa Chadema huku wakisisitiza kuwa wamefanya uamuzi  mgumu ambao Lowassa amekuwa akiusema mara kwa mara katika safari yake ya siasa.
Madiwani waliohama  kutoka chama cha Mapinduzi kwenda Chadema
Madiwani waliohama chama ni Kalanga mwenyewe, Edward Lenanu, Bazir Siamini, Sigur Olekibinti, Loti Yamat, Goodluck Lerunya, Pashet Sengurumi, Yase Runja, Gidion Kimongishu, Dora Kipuyo, Mary Morindat, Sara Lomayan na Halima Lusinde.
Kata ya Engaruka, Engutoto, Esilalei, Loksale, Majengo, Makuyuni, Meserani, Nalalani, Lemooti, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mferejini, Mswakini, Mto wa Mbu, Migungani, Selela, Sepeko na Lashaini.
Dotto Mlacha, Hawa Nyambiry, Alex Kamanda, Sion Kapela, Maria Lemta, Onesmo Naikoyo, Shaban Adam, Enditosidai Naikulo na Elifuraha Simon.
Wengine ni Dinna Solomon, Loti Naparana, Jocy Laizer, Edward Mathayo, Piniel Loning’o, Napir Mukare, Inot Leringa, Kalaine Lowassa, Maria Mepukori, Mary Stivin na Edward Kone.
Katika hatua nyingine, tangia kukatwa jina lake Mbunge huyo hajazungumza jambo lolote ambapo alitaka kuzungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam hata hivyo mkutano huo uli ahirishwa kwa madai kwamba amechelewa kuwasili jijini Dar es salaam akitokea mkoani Dodoma.

Wednesday 1 July 2015

Argentina yafanya mauaji yaipiga Paraguay 6-1,Di Maria apiga mbili Copa America

Argentina yafanya mauaji yaipiga Paraguay 6-1,Di Maria apiga mbili Copa America



 Angel di Maria
Winga Timu ya Taifa ya Argentina na Klabu ya Manchester United ya Wingereza,Angel di Maria.
Timu ya Taifa ya Argentina imetinga kwa kishindo hatua ya fainali ya Copa America baada ya
kuitandika Paraguay kipigo cha mbwa mwizi cha magoi 6-1 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa
usiku wa kuamkia leo.
Mabao ya Argentina yamefungwa na Marcos Rojo (15), Javier Pastore (27), Angel Di Maria (47, 53),
Sergio Aguero (80) na Gonzalo Higuain (83), huku goli la kufutia machozi kwa Paraguay likifungwa
na Lucas Barrios (43).

Urais 2015: Watia nia 9 warudisha fomu

Urais 2015: Watia nia 9 warudisha fomu


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhavi fomu za kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini DOdoma Jana.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhavi fomu za kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini DOdoma Jana.
Wanasiasa 9 wamerejesha fomu za kuomba ridhaa kuteuliwa kuwa rais makao makuu ya CCM mkoani Dodoma. Wanasiasa hao  ni  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,  Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Bernad Membe na Balozi Mahiga.
Wengine ni  Joseph Chaggama, Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Monica Mbega, Amosi Siyantemi, Dk Mwele Malecela, pamoja na   Waziri wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe.
Baada ya kurudisha fomu hizo wanasiasa hao watasubiri vikao vya uteuzi vitakavyofanyika mapema  mwazoni mwa mwezi julai.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na chama hicho inaonesha kuwa  vikao vya uchujaji vitakuwa kama ifuatvyo,
Kamati ya usalama na Maadili Zanzibar 4/7/2015
Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya Taifa 5/7/2015
Kamati ya Usalama na Maadili Taifa 8/7/ 2015
Kamati ya Halmashauri kuu ya Taifa 9/7/2015
Halmashauri kuu ya Taifa 10/7/2015
Mkutano mkuu wa Taifa 11-12/7/2015

Mgogoro wa Kiuchumi Ugiriki wafikia pabaya

Mgogoro wa Kiuchumi Ugiriki wafikia pabaya


Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Christine Lagarde.
Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Christine Lagarde.
Ugiriki imeshindwa kutekeleza muda uliowekwa kulipa deni la Shirika la Fedha Duniani, IMF la euro bilioni 1.6, saa chache baada ya mawaziri wa umoja wa nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro kukataa kuongeza muda wa kulipa deni hilo ili kunusuru uchumi wa Ugiriki.
Ugiriki ni nchi ya kwanza iliyoendelea kushindwa mkopo wa IMF katika muda uliopangwa na sasa ni rasmi inakabiliwa na malimbikizo ya deni hilo.
Kuna wasiwasi kwamba hali hii itaiweka Ugiriki katika hatari ya kuondoka katika umoja wa nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya euro.
IMF imethibitisha kwamba Ugiriki imeshindwa kulipa deni lake muda mfupi baada ya kumalizika kwa muda uliokuwa umepangwa jana, Jumanne.
“Tumeiarifu Bodi ya Wakurugenzi kwamba Ugiriki kwa sasa iko katika malimbikizo ya deni na itaweza kupata fedha kutoka IMF, mara itakapolipa malimbikizo, amesema msemaji wa IMF Gerry Rice.
Kwa kumalizika kwa muda wa kulipa deni la umoja wa nchi za euro, Ugiriki haitapata mabilioni ya fedha za euro na imeshindwa kutekeleza muda uliopangwa kulipa deni la IMF.

Ndege ya Jeshi yaangukia nyumba, watu 100 wafariki dunia


Ndege ya Jeshi yaangukia nyumba, watu 100 wafariki dunia


Nyumba na maduka yaliharibiwa katika ajali hiyo.
Nyumba na maduka yaliharibiwa katika ajali hiyo.
Ndege ya kijeshi yaua watu 30 Indonesia .
Ndege ya kijeshi yaua watu 30 Indonesia.
Takriban watu 100 wamefariki  baada ya ndege ya uchukuzi wa kijeshi ya Indonesia kuanguka mapema leo katika maeneo yenye makazi ya watu huko Medan Sumatra.
Maafisa wa kijeshi wanasema kuwa tayari miili 49 imepatikana katika eneo la ajali. Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules 130 ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 ilipoanguka. Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambayo iliangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Picha za runinga na kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.

Uhaba wa mafuta nchini wachukua sura mpya Bungeni

Uhaba wa mafuta nchini wachukua sura mpya Bungeni


Naibu wazii wa Nishati na Madini Charles Mwijage .
Naibu wazii wa Nishati na Madini Charles Mwijage .
Serikali imesema kwamba  akiba ya Mafuta ya Petrol nchini Tanzania inatoshelea hadi siku 40.Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa madai  kutokea uhaba wa mafuta siku kadhaa zijazo.
Akijibu hoja  ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyeomba Bunge hilo kujadili hoja hiyo kwa njia ya dharula kwa kuwa linamaslahi kwa uchumi wa  taifa Naibu wazii wa Nishati na Madini Charles Mwijage amesema mafuta yapo na kuna meli  zipo nje maji  marefu zinakuja nchini zikiwa na shehena ya mafuta.
Amewahakikishia wananchi kuwa nchi haiwezi kuapata tatizo la uhaba wa mafuta huku akisisitiza kuwa  kwa kushirikiana  na TCRA  wanawatafuta waliosambaza taarifa hizo.
Naye Naibu waziri wa Fedha Adam Malima amesema serikali itahakikisha kuwa wananchi wanapata  huduma  ya mafuta   kama  kwaida.

Urais 2015: Lowassa afunga mahesabu ya Wadhamini Morogoro

Urais 2015: Lowassa afunga mahesabu ya Wadhamini Morogoro

Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Milonge, akionyesha fomu zenye orodha ya majina ya wanachama wa ccm,104,03  waliomdhamini kugombea urais, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Milonge, akionyesha fomu zenye orodha ya majina ya wanachama wa ccm,104,03 waliomdhamini kugombea urais, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa akitoa shukrani katika kuhitimisha Mkoa wa mwisho wa kupokea orodha ya majina ya wadhamini.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa akitoa shukrani katika kuhitimisha Mkoa wa mwisho wa kupokea orodha ya majina ya wadhamini.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amehitimisha safari ya kusaka wadhamini katika mikoa 15 ya Tanzania bara na mitatu ya visiwani Zanzibar.
Akiwa Mkoani Morogoro Lowassa amepata wanaccm 104,038 waliojitokeza kumdhamini katika safari yake ya matumaini aliyoa ianza mara baada ya kutangaza nia ya kugombea urais uwanja wa sheikh Abeid Karume  jijini Arusha may 29 maka huu.
Lowassa pamoja na watia nia wengine CCM wanatakiwa kurejesha fomu za urais makao ya Makuu ya CCM mkoani Dodoma  wiki hii huku mwisho wa kurejesha fomu hizo  ikiwa ni julai 3,2015.
Baada ya kurejesha fomu watasubiri matokeo ya mchujo utaofanywa na kamatia Kuu CCM itakayoketi na kuanza zoezi a uchujaji.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na chama hicho inaonesha kuwa  vikao vya uchujaji vitakuwa kama ifuatvyo,
Kamati ya usalama na Maadili Zanzibar 4/7/2015
Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya Taifa 5/7/2015
Kamati ya Usalama na Maadili Taifa 8/7/ 2015
Kamati ya Halmashauri kuu ya Taifa 9/7/2015
Halmashauri kuu ya Taifa 10/7/2015
Mkutano mkuu wa Taifa 11-12/7/2015

Ghana yaanza kupaa Kimataifa, yazindua gari lake

Ghana yaanza kupaa Kimataifa, yazindua gari lake


Baadhi ya Magari yanayotengenezwa nchini Ghana.
Baadhi ya Magari yanayotengenezwa nchini Ghana.
Gari la Kantanka kutokana nchini Ghana.
Gari la Kantanka kutokana nchini Ghana.
Mafundi wa magari hayo.
Mafundi wa magari hayo.
Nchi ya Ghana imefungua njia kwa nchi  nyingine barani Afrika kufuatia kuanza utengenezaji wa magari aina ya Kantanka ambayo ni pamoja na lile  aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.
Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo. Babaake ni m’bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini. Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.
Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kwa mujibu wa mmoaja wa raia nchini humo amesema  watu wanapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni imara.

clouds stream