Saturday 27 February 2016

Uchaguzi Wa Meya Dar Wakumbwa Na Vurugu

Uchaguzi Wa Meya Dar Wakumbwa Na Vurugu

Tarehe February 27, 2016
Baadhi ya Polisi katika Ukumbi huo wa uchaguzi wa Meya.
Baadhi ya Polisi katika Ukumbi huo wa uchaguzi wa Meya.
Uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam umeahirishwa tena leo kufuatia kuibuka kwa vurugu kubwa wakati tangazo la kuahirishwa uchaguzi huo lilipotolewa.
Chanzo  cha vurugu hizo  Katika ukumbi huo wa Karimjee kinadaiwa kuwa ni mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi  kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani.
Suala hilo limewakasirisha madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia.
Wakati UKAWA  wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo  wenyewe, Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini, jambo lilowachukiza tena na kuibua vurugu ndani ya ukumbi.
Uchaguzi huo leo umeahirishwa kwa mara ya nne huku kukiwa na dalili ya figisu figisu inayoedelea kuwamisha uchaguzi huo.
Jeshi la Polisi likituliza vurugu katika uchaguzi wa Meya wa Dar.
Jeshi la Polisi likituliza vurugu katika uchaguzi wa Meya wa Dar.
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Karimjee jijini Dares salaam leo.
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Karimjee jijini Dares salaam leo.

Gianini Infantino Ndiye Rais Mpya FIFA

Gianini Infantino Ndiye Rais Mpya FIFA

Tarehe February 27, 2016
Gianini Infantino
Gianini Infantino
Gianni Infantino ameshinda katika uchaguzi wa  kuchagua Rais atakaye ongoza shirikisho la mpira wa miguu dunia FIFA.
Infantino amempiga boa mpinzani wake mkubwa Sheikh Salman al-Khalifa,Infantino ameibuka na ushindi wa Kura 115 dhidi ya Sheikh Salman aliyepata 88.

Ndugu Kolo Toure Na Yaya Toure Kuchuana Jumapili

Ndugu Kolo Toure Na Yaya Toure Kuchuana Jumapili

Tarehe February 26, 2016
Yaya Toure (kushoto) akiwa na ndugu yake Kolo Toure
Yaya Toure (kushoto) akiwa na ndugu yake Kolo Toure
Kolo Toure anatarijia kukutana na ndugu yake Yaya Toure katika moja ya mchezo wa fainali ya kombe la ligi ya Uingereza watakapo kutana Liverpool na Manchester City siku ya jumapili katika uwanja wa Wembley.
Lakini katika hali nyingine beki wa  Liverpool Kolo Toure anasema kuwa atatumia kila njia kuhakikisha kuwa nduguye hapati bao.
”Ananijua mie kwamba naweza kutumia kila njia kumzuia asifunge bao”,alisema Kolo Toure ambaye ni ndugu mkubwa wa Yaya Toure.

Tuesday 23 February 2016

Barcelona Yaigaragaza Arsenal 2-0, Messi Atupia Zote

Barcelona Yaigaragaza Arsenal 2-0, Messi Atupia Zote

Tarehe February 24, 2016
dee511dd-b890-4a33-b8f2-b4d7914dd56b
Hata pale walipocheza kwa ukamilifu, ilikuwa ngumu sana kuendana na Barcelona. Japokuwa Arsenal ilicheza kwa utulivu na nidhamu ya hali ya juu ni kama vile Barcelona walikuwa wanacheza peke yao.
1456259021282_lc_galleryImage_Arsenal_v_Barcelona_Champ
Muda si mrefu upepo usiozuilika ulitokea pale ambapo Neymar, Suarez na Messi waliungana na kuichanachana vipande Arsenal mpaka kuipatia timu yao bao la kwanza dakika ya 26 kipindi cha pili.
Punde si punde Messi akatupia bao la pili baada ya kupiga penati kwa staili yake ya mar azote ambapo kipa wa Arsenal, Peter Cech hakuwa na la kufanya zaidi ya kurudi kwenye nyavu na kuokota mpira.
1456263034581_lc_galleryImage_SPT_GCK_230216_Football_U
1456258724949_lc_galleryImage_Arsenal_v_Barcelona_Champ
1456263061565_lc_galleryImage_Arsenal_v_Barcelona_Champ
1456262621786_lc_galleryImage_LONDON_ENGLAND_FEBRUARY_2
c82a10a5-1b80-4b13-8983-7813ad7e14aa
fc9c14bc-a975-4fa6-830a-bd61660f76cd

Kazimoto Aomba Msaada Wa Wakili

Kazimoto Aomba Msaada Wa Wakili

Tarehe February 23, 2016
Mwinyi Kazimoto
Mwinyi Kazimoto
Kesi ya shambulio la kudhuru mwili inayomkabili kiungo wa Simba, Mwinyi Kazimoto, imeanza kusikilizwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Shinyanga na kuomba msaada wa wakili.
Kazimoto ameshitakiwa kwa kosa la kumshambulia mwandishi wa habari  wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Mwanahiba Richard na kesi yake ilianza kusikilizwa jana.
Akisomewa shitaka hilo,  Mwanasheria  wa Serikali, Upendo  Shemkole, alisema mshtakiwa  alitenda  kosa hilo Februari  10, mwaka huu  katika Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga,   muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi na timu yake ya Simba.
Hata hivyo, mshitakiwa  huyo alikana  shitaka hilo na kuiomba  mahakama  kumpatia mwezi  mmoja ili atafute wakili  wa  utetezi  wake,  ombi  ambalo  lilikubaliwa.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama  hiyo, Rahim  Mushi,  anayesikiliza  kesi  hiyo,  alisema  kesi  imeahirishwa  hadi  Machi  21  mwaka huu,  itakaposikilizwa tena, ili kutoa fursa  kwa mshitakiwa  kupeleka  wakili wake.
Jumla ya mashahidi sita wanatarajiwa  kutoa  ushahidi  mahakamani hapo katika  kesi hiyo,  ambapo  pia alipewa  dhamana ya Sh  500,000.

Mchezaji ‘Amlima’ Refa Kadi Nyekundu Nchini Uturuki

Mchezaji ‘Amlima’ Refa Kadi Nyekundu Nchini Uturuki

Tarehe February 23, 2016
Salih Dursun akimuonesha refa kadi nyekundu
Salih Dursun akimuonesha refa kadi nyekundu
Mchezaji wa klabu ya Trabzonspor, Salih Dursun, ametolewa nje ya uwanja kwa kumuonyesha mwamuzi kadi nyekundu wakati wa mechi waliyofungwa mabao 2-1 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Tukio hilo lilitokea dakika ya 86 ya mchezo baada ya mwamuzi Denis Bitnel kumuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Luis Cavanda kwa kufanya madhambi ndani ya eneo la hatari.
Wachezaji wa Trabzospor walimzingira mwamuzi kupinga kadi hiyo.
Ni wakati huo ambapo Dursun alimnyang’anya refa kadi nyekundu aliyokuwa nayo na kumuonyesha kadi hiyo hatua ambayo ilipelekea na yeye kufukuzwa uwanjani.
Klabu hiyo ilisalia na wachezaji tisa uwanjani.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuingia katika mizozo na waamuzi, kwani Novemba mwaka jana mwenyekiti wao Ibrahim Haciosmanoglu alifungiwa siku 280 baada ya kuwafungia waamuzi wanne uwanjani kwa kushindwa kutoa penati kwa timu hiyo.

Muhongo Ataka Matumizi Ya Teknolojia Ya Kisasa Katika Utafiti Wa Mafuta, Gesi

Muhongo Ataka Matumizi Ya Teknolojia Ya Kisasa Katika Utafiti Wa Mafuta, Gesi

Tarehe February 23, 2016
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko  kutoka kampuni  ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameyataka makampuni yanayojishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini kuongeza kasi ya utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili sekta ya  gesi na mafuta iweze kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo alipokutana na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger yenye makazi  yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili  utendaji kazi wa  kampuni hiyo.
Kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilihusisha watendaji kutoka Wizara hiyo pamoja na  taasisi zake  likiwemo  Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) na Mamlaka  ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Alisema  Tanzania kwa sasa ina utajiri mkubwa wa  rasilimali ya  gesi ambayo  itachochea katika  ukuaji wa uchumi wa nchi  kupitia umeme wa uhakika utakaotumika katika viwanda na kuongeza  ajira kwa  vijana wa kitanzania.
Aliendelea kusema kuwa ili  sekta ya gesi na mafuta iweze kuwa na mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi, Tanzania inahitaji wawekezaji  watakaowekeza kwa kasi kwa kutumia  teknolojia ya kisasa.
Alisisitiza kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na mwekezaji  yeyote mwenye nia ya kuwekeza kwenye sekta ya gesi na mafuta kwa kutumia  teknolojia ya kisasa.

Nkurunzinza Akubali Mazungumzo Na Wapinzani

Nkurunzinza Akubali Mazungumzo Na Wapinzani

Tarehe February 23, 2016
Rais wa BurundI, Pierre Nkurunzinza (kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon (kulia).
Rais wa BurundI, Pierre Nkurunzinza (kushoto) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon (kulia).
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amekubali kufanya mazungumzo na upinzani ili kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea katika nchi hiyo.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki-moon amesema kuwa rais Nkurunziza ameitikia mwito wa mazungumzo ya upatanishi yanayolenga kumaliza miezi 10 ya mzozo wa kisiasa.
Ban Ki-Moon ambaye yuko mjini Bujumbura katika ziara maalum amesema kuwa rais huyo pia amekubali kuwaachilia huru wafungwa 2000 huku mamia ya watu wameuawa katika makabiliano baina ya vyombo vya dola na wafuasi wa upinzani.
Machafuko yalianza mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania awamu ya 3 ya urais katika uchaguzi mkuu.
Wapinzani wake walidai kuwa rais huyo alikuwa anakiuka katiba ya nchi inayomtaka kiongozi asitawale kwa zaidi ya vipindi viwili.
Nkurunziza naye anashikilia kuwa hakuchaguliwa wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wake uliofuatia mazungumzo ya kusitisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu lakini mbili na nusu wametorokea mataifa jirani.

Rais Kenyatta Atumbua Jipu, Amsimamisha Kazi Jaji

Rais Kenyatta Atumbua Jipu, Amsimamisha Kazi Jaji

Tarehe February 23, 2016
Jaji Philip Tunoi
Jaji Philip Tunoi
Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji wa Mahakama ya juu aliyetuhumiwa kuchukua hongo katika kesi kuhusu kuchaguliwa kwa gavana wa Nairobi.
Rais Kenyatta amemsimamisha kazi Jaji Phillip Tunoi na akateua jopo la kuchunguza madai dhidi yake, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama.
Jaji adaiwa kupokea rushwa ya $2m Kenya
Jopo la kumchunguza Jaji huyo litaongozwa na Jaji Sharad Rao ambaye ndiye mwenyekiti wa Bodi ya Kuwachunguza Majaji na Mahakimu.
Wanachama wengine wa jopo hilo ni Jaji Roselyn Korir, Jaji Mstaafu Jonathan Havelock, Judith Guserwa, James Kaberere Gachoka, Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha.
Jaji Tunoi amekanusha madai dhidi yake.

Saturday 20 February 2016

Museveni Ashinda Urais Uganda

Museveni Ashinda Urais Uganda

Tarehe February 20, 2016
Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Museveni ametangazwa mshindi licha ya kwamba kuna vituo ambavyo bado matokeo hayajatangazwa.
Kwa mujibu wa Dkt Kiggundu amesema matokeo ya vituo hivyo hayawezi kubadilisha mambo.

IGP Atangaza Operesheni Kamata Bodaboda

IGP Atangaza Operesheni Kamata Bodaboda

Tarehe February 20, 2016
nspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu.
Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Ernest Mangu amewaagiza makamanda wa polisi nchini kuendesha operesheni kali ya kuwachukulia hatua za kisheria waendesha bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani.
Akizungumza na wakuu wa polisi, IGP Mangu alisema makosa yatakayosababisha waendesha bodaboda kukamatwa ni pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu na kutokuvaa kofia ngumu.
Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za barabarani, lakini sasa mwisho wao umefika kwani jeshi la polisi halitavumilia vitendo vyao tena.
IGP Mangu amesisitiza pia jeshi la polisi kuwakamata waendesha bodaboda wenye makosa tu bila uonevu.

Rwanda Wamfagilia Raisi Magufuli

Rwanda Wamfagilia Raisi Magufuli

Tarehe February 20, 2016
Magufuli+Photo
Raisi wa Tanzania, John Pombe Magufuli
Wafanyabiashara wa Rwanda wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Raisi John Magufuli katika bandari ya Dar es salaam kwa kuimarisha ufanisi wa bandari na kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi jirani.
Hayo yameelezwa na waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa afrika mashariki,kikanda na kimataifa, balozi Agustine Mahiga alipotua nchini akitokea Kigali, Rwanda.
Balozi Mahiga alisema wafanyabiashara hao wamesema tangu raisi Magufuli aanze kuchukua hatua hizo, mizigo yao imekua salama zaidi na wamefanikiwa kuipata kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mizigo mingi ilikua ikipotea.
Alisema pia raisi wa nchi hiyo, Paul Kagame amemhakikishia kuwa ataendelea kushawishi wafanyabiashara wake kutumia bandari ya Dar es salaam ili kukuza uhusiano wa kibiashara uliopo.

Waziri Mkuu Abaini ‘Madudu’ Bandari Ya Tanga

Waziri Mkuu Abaini ‘Madudu’ Bandari Ya Tanga

Tarehe February 20, 2016
Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016.
Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo leo (Jumamosi) saa 6 mchana.
Majaliwa  aliwasili Tanga jana mchana ili kushiriki mazishi ya baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga, aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani kurejea Dar es Salaam.
Baada ya kufika Bandarini hapo, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini  na akataka apelekwe mahali tishari tatu za bandari hiyo zilipo.
Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat  (meli ndogo).
“Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo ni kwa nini mlinunua tishari tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe  (self propelled) “
“Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya Serikali kwa kukodisha tishari kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?” alihoji Waziri Mkuu.
“Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishari lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa,” aliongeza.
Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishari hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam.
“Pia wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana,” alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.
Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali.
Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali.

Ridhiwani Kikwete Atoa Vitabu 3438 Kwa Shule Chalinze

Ridhiwani Kikwete Atoa Vitabu 3438 Kwa Shule Chalinze

Tarehe February 19, 2016
riziwani1
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikabidhi vitabu kwa afisa elimu wa wilaya ya Chalinze
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete leo amekabidhi vitabu 3438 vya shule za Msingi 105 na sekondari 17 vyenye thamani ya shilingi milioni 68,760,000.
riziwani2
Mbunge Ridhiwani Kikwete akitoa neno baada ya kukabidhi vitabu hivyo leo katika shule ya msingi Mdaula.
riziwani3
Mratibu wa Taasisi ya kulea Village, Bwana Kombo akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitabu hivyo.
riziwani4

Tume Ya Vyuo Vikuu Yafuta Matawi Ya St. Joseph

Tume Ya Vyuo Vikuu Yafuta Matawi Ya St. Joseph

Tarehe February 19, 2016
Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU
Kaimu mtendaji wa TCU, profesa Yunus Mgaya
Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufuta vibali vilivyoanzisha vyuo vikuu vishiriki vya sayansi ya kilimo na teknolojia na chuo kikuu kishiriki cha teknolojia ya habari tawi la songea vinavyoendeshwa na chuo kikuu cha mtakatifu Joseph (St.Joseph) baada ya kukiuka taratibu za uendeshaji.
Kaimu mtendaji wa TCU, profesa Yunus Mgaya amesema mara kwa mara tume yake imekua ikikitaka chuo kikuu cha Mt. Josefu kutoa elimu inayokidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na TCU katika kampusi za Songea lakini kimekua kikikiuka maagizo hayo.
“Tume imejiridhisha kuwa vyuo hivyo havitoi elimu nzuri na wanaoathirika zaidi na elimu hiyo ni wanafunzi ndio maana tumeamua kufuta kabisa vibali vilivyoanzisha vyuo hivyo,” alisema.
Vilevile TCU imeidhinisha uhamisho wa wanafunzi wote 2,046 waliokuwa wanasoma chuoni hapo kwa gharama za chuo cha Mt. Joseph.
Profesa Mgaya amewaarifu wanafunzi wanaosoma katika vyuo hivyo kuwa watahamishiwa katika vyuo vingine ambavyo vinatoa programu sawa na zilizokuwa zinatolewa vyuoni huko.

Wednesday 17 February 2016

Mchezaji Amuua Mwamuzi Baada Ya Kulambwa ‘Red Card’

Mchezaji Amuua Mwamuzi Baada Ya Kulambwa ‘Red Card’

Tarehe February 17, 2016
160217103805-red-card-ref-hand-exlarge-169
Mwamuzi mmoja nchini Agentina amepoteza maisha baada ya kuuawa na mchezaji aliyemtoa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la CNN, Cesar Flores, alikuwa akichezesha pambano mjini Cordoba, takriban kilomita 700 Kaskazini Magharibi mwa Mji Mkubwa wa Buenos Aires, pale ambapo alimwonyesha mchezaji ambaye hakuwa na silaha kadi nyekundu.
Baadae mchezaji huyo alichukua bastola ndani ya begi lake na kurudi uwanjani na kumpiga mara tatu mwamuzi huyo mwenye miaka 48, katika maeneo ya shingo, kichwa na kifua.
“Yote yalitokea wakati wa mechi,” chanzo cha polisi kilisema.
“Hatujui nini kilitokea kwa mwamuzi, lakini mchezaji alikuwa na hasira na kwenda kuchukua silaha yake na kumuua mwamuzi,” kilizidi kusema chanzo hicho.
Mtuhumiwa bado yupo mtaani na hajakamatwa.
Katika tukio hilo, mchezaji mwingine alijeruhiwa vibaya sana lakini inaaminika kuwa majeraha yake hayatatishia uhai wake.
Amerika ya Kusini imekuwa ikikumbwa na visa vya kutisha katika viwanja vya soka ambapo mwaka jana mwamuzi mmoja nchini Brazil alimnyooshea bastola mchezaji aliyemdhihaki, na mwaka 2013 mchezaji mmoja alichomwa kisu na mwamuzi baada ya kuzuka vurugu. Mwamuzi huyo baadaye alitekwa nyara na mashabiki ambao walienda kumtesa vibaya kabla ya kupigwa mawe hadi kufa.

Cavan Aimaliza Chelsea Akitokea Benchi,PSG -2 Vs Chelsea -1

Cavan Aimaliza Chelsea Akitokea Benchi,PSG -2 Vs Chelsea -1

Tarehe February 17, 2016
Edinson Cavan
Edinson Cavan
Chelsea imeshindwa kuwika jijini Paris walipokwenda kuivaa Paris Saint Germain kwa kukubali kufungwa magoli mawili kwa moja katikamchezo wao wa klabu bingwa ya dunia uliomalizika hivi punde.
Zlatan Ibrahimovic aliipatia PSG goli la kwanza baada ya kupiga mkwaju wa adhabu dakika ya 39 baada ya Obi Mikel kufanya madhambi.
Dakika ya 45 Obi Mikel aliipatia Chelsea goli la kusawazisha na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa zimefungana 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku PSG wakimtumia sana Di Maria kumlisha mipira Ibrahimovic ,Edinson Cavan aliingia kama mchezaji wa akiba na kuifungia PSG goli la ushindi dakika ya 78.
Na mpaka mpira unamalizika PSG walikuwa mbele kwa magoli 2-1.

Raia Wa India Afukuzwa Kazi Kwa Kuwaita Watanzania ‘Nyani’

Raia Wa India Afukuzwa Kazi Kwa Kuwaita Watanzania ‘Nyani’

Tarehe February 17, 2016
ramada
Raia wa India, Dennis Smith ameachishwa kazi katika Hoteli ya Ramada, Dar es Salaam kwa madai ya kuwatukana wafanyakazi wa kitanzania wa ngazi za chini kwa kuwaita nyani.
Smith, ambaye ni meneja wa chakula na vinywaji wa hoteli hiyo, aliwatukana na kuwadhalilisha wafanyakazi hao siku ya Sikukuu ya Wapendanao akiwatuhumu kushindwa kuandaa meza vizuri.
Kutokana na udhalilishaji huo, wafanyakazi wa hoteli hiyo jana waligoma wakishinikiza meneja huyo asimamishwe kazi au wao waache kazi.
Meneja Rasilimaliwatu wa hoteli hiyo, Sebastian Nchimbi alisema tayari Smith ameachishwa kazi kutokana na tukio hilo kwani tabia ya unyanyasaji ya mfanyakazi huyo imekua sugu.
Mwakilishi wa wafanyakazi hotelini hapo, Mathew Misalaba alisema licha ya uongozi wa hoteli kumsimamisha kazi Smith, wamelipeleka suala hilo polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

Trump Hatakuwa Rais Wa Marekani-Obama

Trump Hatakuwa Rais Wa Marekani-Obama

Tarehe February 17, 2016
Barack Obama, Donald Trump
Barack Obama, Donald Trump
Rais Barack Obama amesema anaamini mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani. Amesema kazi hiyo ni “kazi kubwa”.
“Ninaendelea kuamini kwamba Bwana Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Rais Obama.
Trump, mfanyabiashara tajiri sana kutoka New York, anaongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa chama cha Republican.
Tayari ameshinda uchaguzi wa mchujo jimbo moja, na anaongoza kwenye kura za maoni jimbo la South Carolina, ambako wafuasi wa Republicans watashiriki uchaguzi wa mchujo Jumamosi.
Akiongea wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za kusini mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California, rais aliulizwa na mwanahabari kumhusu Trump.
Watu hawatampigia kura, alisema Rais Obama, kwa sababu “wanajua kuwa rais ni kazi kubwa”.
“(Kazi hii ) Si kama kuzungumza katika kipindi cha runinga, si matangazo au mauzo ya bidhaa, ni kazi ngumu. Si kazi ya kushawishi watu na kufanya utakalo ndipo utokee kwenye vichwa vya habari siku fulani.”
Hatahivyo Trump amemjibu Obama na kudai kuwa ni kama kusifiwa iwapo utakosolewa na rais ambaye ameharibu sana nchi.
Mwanasiasa huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.

Magufuli Arejesha Jeshi Bandarini

Magufuli Arejesha Jeshi Bandarini

Tarehe February 17, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.
Raisi John Magufuli ameamuru Jeshi la Polisi kurudi bandarini na kufanya kazi za ulinzi wa bandari pamoja na mita za kupimia mafuta.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza maamuzi hayo ya Rais jijini Dar es Salaam na kusema huo ni utekelezaji wa kile Rais Magufuli alichokisema mwaka jana wakati akitumbua majipu bandarini.
“Kama wananchi ambavyo watakumbuka, huko nyuma kulikuwa na Kitengo cha Polisi Bandarini ambacho kilikuwa kinasaidia ulinzi bandarini, lakini ikafika mahali ambapo Mamlaka ya Bandari ikafikiri wanaweza kuwa na ulinzi wa kwao, sasa Rais ameamua Polisi warudi bandarini na kufanya kazi za ulinzi kama walivyokuwa wanafanya zamani,” alisema Balozi Sefue.
Tayari Jeshi la Polisi limeshatekeleza agizo hilo la Rais na askari Polisi sasa wanafanya kazi ya ulinzi katika Bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine zote nchini.
Balozi Sefue pia alisema polisi watawajibika katika ulinzi wa mita za kupimia mafuta zilizopo bandarini hapo, ambako hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alienda na akamsimamisha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo, Magdalena Chuwa.

clouds stream