Ongwen ‘akiri ‘ kuwa mwanajeshi wa LRA Mahakama ya ICC


Kiongozi mmoja wa kundi la waasi nchini Uganda, Dominic Ongwen.
Kiongozi mmoja wa kundi la waasi nchini Uganda, Dominic Ongwen.
Mahakama yA ICC.
Mahakama yA ICC.
Kiongozi mmoja wa kundi la waasi nchini Uganda, Dominic Ongwen, amekuwa mwanachama wa kwanza wa kundi la Lord’s Resistance Army LRA, kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC.
Wakati wa kusikizwa kwa kesi yake huko The Hague leo , Bwana Ongwen amethibitisha kuwa ndiye yeye  huku akijieleza kuwa ni mwanajeshi wa zamani wa kundi la LRA.
Kiongozi huyo  anakabiliwa  na  makosa  ya uhalifu  dhidi  ya  binadamu na makosa mengine ya kivita, ikiwemo mauaji  pamoja  na utumwa.
Awali mwezi huu alikuwa amezuiliwa nchini  Afrika  ya  kati, miaka  kumi  tangu  ICC  ilipotoa ilani ya kumkamata.