Monday 29 December 2014

KIONGOZI MKUU WA AL- SHABAAB AKAMATWA SOMALIA


KIONGOZI MKUU WA AL- SHABAAB AKAMATWA SOMALIA




Wanamgambo wa kundi la Al shabaab.
Maafisa nchini Somali wamesema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali.
Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo amesema  Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupata taarifa za siri dhidi ya kiongozi huyo.
Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi. Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Alshabaab upande wa Amniyat.
Kundi la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.

NDEGE YAPOTEA NA ABIRIA 162







NDEGE YAPOTEA NA ABIRIA 162







Ndege inayopendelewa hasa kutokana na kuwa na   bei ya nafuu,AirAsia imepoteza mawasiliano na wataalamu wa anga na jopo la waokoaji wakijitaidi kuitafuta kujua wapi ilipo ndege hiyo iliyokuwa imebeba idadi kubwa abiria kutoka nchi mbalimbali kama Indonesia 157,Singapore 1,Malasia 1 na Wakorea 3 huku kukiwa na watoto 16 na Mjamzito kwenye kundi la Abiria waliopotea.Ndege hiyo A320-200 yenye abiria 162 ilitarajiwa kutua Singapore saa 8.30 asubuhi ya leo tarehe 28.12.2014.

Sunday 28 December 2014

PROPERTIES FOR SALE

 HOUSE FOR SALE: 3 BED ROOMS ALL ENSUITE KITCHEN, SITTING ROOM AND STORE, FENCED, LOCATED AT KIJITONYAMA, PRICE IS  TSH. 250 MIL ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).
 HOUSE FOR SALE: LOCATED AT SINZA PALESTINA, 3 BED ROOMS, SITTING ROOM,KITCHEN, FENCED AND CAR PARKING. PRICE IS TSH. 200 MIL       
SCHOOL FOR SALE: LULE SECONDARY SCHOOL,  7 HECOR AREA. LOCATED AT KIMARA SUKA, PRICE IS TSH. 1 BILL ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).
PLOTS FOR SALE: LOCATED AT BUNJU, 3800 SQM SIZE, PRICE IS TSH. 50 MILL AND ANOTHER ONE  ALSO LO CATED AT BUNJU, 1400 SQM SIZE, PRICE IS TSH. 45 MILL. ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

Tuesday 23 December 2014

CHELSEA YAUA , YAZIDI KUKAA KILELENI MWA LIGI

CHELSEA YAUA , YAZIDI KUKAA KILELENI MWA LIGI

 Wachezaji wa chelsea wakishangilia goli baada ya kuifunga timu ya stock city kwenye uwanja wao wa nyumbani katika mchezo ambao ulifanyika usiku wakuamkia leo . Ushindi huo unaifanya chelsea kuendelea kushika nafasi ya juu huku wakiwaacha man city kwa pointi tatu.













     

REAL MADRID MABINGWA WA DUNIA 2014

REAL MADRID MABINGWA WA DUNIA 2014



Klabu ya Real Madrid imeshinda taji lao la nne mwaka 2014 baada ya kuwashinda mabingwa wa Marekani Kusini kutoka Argentina San Lorenzo katika fainali la za kilabu bingwa duniani zilizochezwa nchini Morrocco.
Mabingwa hao wa kombe la klabu bingwa barani ulaya,Copa Del Rey na mabingwa wa Super Cup barani Ulaya walianza kufunga kupitia kichwa cha Sergio Ramos.
Makosa ya mlinda lango wa Lorenzo yaliihakikisha ushindi Real madrid baada ya Gareth Bale kuongeza bao la pili.
Real madrid hawakutatizwa na mabingwa hao wa Marekani kusini na hivyobasi kuongeza rekodi yao ya ushindi katika mecho zote kufikia 22.
Ushindi huo pia ni wa kwanza wa klabu hiyo Bernabeu.

Monday 22 December 2014

WAZIRI ANNA TIBAIJUKA ATENGULIWA RASMI NAFASI YAKE

WAZIRI ANNA TIBAIJUKA ATENGULIWA RASMI NAFASI YAKE



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anna Tibaijuka ametenguliwa rasmi nafasi yake ya Uwaziri na Rais Jakaya Kikwete leo tarehe 22.12.2014 kwenye mkutano aliouandaa na wazee wa jiji la Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Sunday 21 December 2014

MANCHESTER CITY 3-0 CRYSTAL PALACE

MANCHESTER CITY 3-0 CRYSTAL PALACE


Magoli yaliyofungwa kwenye kipindi cha pili na David Silva(49′,61′) na Yaya Toure kwenye dakika ya 81 yamezima kabisa ndoto ya ushindi kwa vijana hao wa Crystal Palace kwenye uwanja wa Etihad Stadium.
Kwa ushindi huu wa Manchester City kunaifanya kuongeza nafasi ya kutetea taji la ligi kuu ya Uingereza kwa kuzidi kuwasogelea karibu vinara Chelsea.Ushindi wa Manchester City unawafanya wawe na pointi 39 sawa na Chelsea ambayo ina mchezo mmoja mkononi.

MAREKANI ‘ YAITUHUMU ’ KOREA KASKAZINI KUFADHILI UGAIDI

MAREKANI ‘ YAITUHUMU ’ KOREA KASKAZINI KUFADHILI UGAIDI


Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.
Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala wake utafanya hivyo baada ya kuilaumu nchi hiyo kufanya uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.
Amesema mara tu mchakato wao huo utakapokamilika, watajibu mashambulizi hayo. Korea kaskazini imeziita tuhuma hizo zilizotolewa na Marekani dhidi yake kuwa ni za uzushi.
Korea kaskazini ilikuwa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, kabla ya kuondolewa wakati wa utawala wa Rais George Bush wa Marekani mwaka 2008.

RAIS KIKWETE KUAMUA SAKATA LA ESCROW LEO ?

RAIS KIKWETE KUAMUA SAKATA LA ESCROW LEO ?



Rais Jakaya Kikwete leo anatarajia kulihutubia Taifa  ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti yanayoligusa taifa hilo ikiwemo sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha, Rais Kikwete  huenda atatumia siku ya leo kutaja hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka vyama mbalimbali vya upinzani pamoja na nchi wahisani   wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Miongoni mwa maazimio ya bunge, yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hiyo na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.
Watendaji  wa serikalini wanaodaiwa kuhusika kwa kutowajibika suala lililopelekea upotevu wa mabilioni ya fedha ambazo ni za umma ni Mwanasheria mkuu wa serikali,Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Waziri ardhi, nyumba na maendeleo ya Makazi.
Akaunti ya Escrow ilianzishwa katika Benki Kuu ya Tanzania ili kuhifadhi fedha, baada ya kuibuka kwa mvutano kati ya Shirika la Umeme la Tanzania, Tanesco na kampuni ya kufua umeme ya IPTL kuhusu ongezeko la mtaji wa uwekezaji, huku TANESCO ikilalamika kuwa gharama za kununua umeme kutoka kampuni ya IPTL zilizokuwa kubwa. Fedha hizo zingeendelea kutunzwa katika Akaunti hiyo hadi wakati ambapo suluhisho la mvutano wa wabia hao lingepatikana.

Thursday 18 December 2014

97.23% WAFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA TANZANIA

97.23% WAFAULU KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA TANZANIA


Matokeo ya wanafunzi wa Darasa la saba kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 nchini Tanzania yametoka huku ongezeko la ufaulu likiwa juu baada ya watoto 438, 960 kati ya 451,392 kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Matokeo hayo yametangazwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mh. Kassim Majaliwa, mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa osifi za TAMISEMI, jijini Dar es salaam.
Mh. Majaliwa, amesema kuwa, Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani, kwa matokeo hayo yanaonesha kuwa, alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 243 na kwa wasichana 240 kati ya alama 250.
“Waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali kwa awamu ya kwanza” Amesema Mh. Majaliwa.
Kwa upande mwingine Mh. Majaliwa, amewaagiza wazazi, walezi, wadau wa elimu na halmashauri zote kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza hapo mapema mwakani.

RAIS KIKWETE KUMALIZA SAKATA LA ESCROW LEO ?

RAIS KIKWETE KUMALIZA SAKATA LA ESCROW LEO ?


Rais Jakaya Kikwete.Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete leo atalihutubia taifa la Tanzania ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti  ikiwemo  sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo  kisiasa na kijamii wanasema kuwa  huenda  Rais Kikwete atatumia hotuba hiyo kutangaza hatua  atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow.
Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya raia na wapinzani wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Sakata la Akaunti ya Escrow liliibuliwa bungeni na mmoja wa wabunge wa bunge la Tanzania, David Kafulila na kusababisha mjadala mkali na kuamua Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kupewa jukumu la kuchunguza kashfa hiyo.
Kamati hiyo ilikuja na maazimio manane kuhusu taarifa ya ukaguzi maalum kuhusiana na miamala iliyofanyika katika akaunti ya Escrow ya Tegeta pamoja na umiliki wa kampuni ya IPTL.
Miongoni mwa maazimio ya bunge yaliwataja baadhi ya wanasiasa, mwanasheria mkuu, maafisa waandamizi wa serikali, majaji, wakuu wa taasisi za umma, viongozi wa dini, mawakili wa kujitegemea na watu binafsi kuhusika katika kashfa hiyo na hivyo kuagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.

REAL MADRID WAMUWINDA DE GEA

REAL MADRID WAMUWINDA DE GEA



Real Madrid wako tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili mlinda mlango David De Gea toka klabu ya Man United usajili huu utavunja rekodi ya uhamisho iliyowekwa na kipa Gianluigi Buffon aliehamia Juventus toka Parma, Huku kukiwa na taarifa De Gea anafuraha kubaki na kikosi cha Manchester United na atasaini mkataba mpya hivi karibuni.
Timu ya Liverpool imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Guillermo Ochoa toka klabu ya Malaga kwa dau la £3milion ili kuwa mbadala wa Simon Mignolet ambae ameporomoka kiwango msimu huu.
Crystal Palace wanafanya mpango kumsajili kwa mkopo beki Ashley Cole mwenye miaka 33 toka klabu ya As Roma ya Itali.
Manchester United na Manchester City wako tayari kutoa dau la £20milion ili kuweza kumtwaa kiungo Ivan Rakitic wa klabu ya Barcelona.
Bosi wa Real Sociedad David Moyes anaimani ya kumpata kwa mkopo mshambuliaji Adnan Januzaj mwenye miaka 19, Januzaj alingara sana enzi za utawala wa kocha Moyes akiwa na Man United.
Meneja wa Sunderland Gus Poyet anataka kuongeza makali ya safu yake ya ushambulaji kwa kumsajili mshambuliaji Danny Ings toka klabu Burnley.
Tottenham wako tayari kuwaachia washambuliaji wake Emmanuel Adebayor na Roberto Soldado ili kupata pesa itakayotumika kumsajili mshambuliaji wa Fc Porto Jackson Martinez.

FIFA ‘YAAMURU’ SIMBA ILIPWE DOLA 300,000 ZA OKWI

FIFA ‘YAAMURU’ SIMBA ILIPWE DOLA 300,000 ZA OKWI



Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA, limeiamuru klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia kuilipa Simba SC , Dola za kimarekani 300,000 kufuatia ushindi wa kesi ya madai dhidi ya Mshambuliaji Emanuel Okwi.
Simba waliishitaki klabu hiyo kunako Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) baada ya Watunisia hao kukataa kuwalipa Simba pesa za uhamisho wa mchezaji Emanuel Okwi, alipouzwa kutoka Simba kwenda Etoile Du Sahel.
FIFA imeamuru Etoile kuwalipa Simba kiasi hicho ambacho ni zaidi ya Tsh. Milioni 500 za Kitanzania ikiwa ni pamoja na fidia, Awali waligoma wakisema kuwa walikumbwa na ukata wa fedha baada ya kuanza migogoro na Mchezaji huyo pale walipo taka kumkata mshahara alipochelewa kurudi kambini akitokea Uganda alipokwenda kuchezea timu ya Taifa.
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa FIFA, ilitoa ruhusa Okwi atafute timu ya kuchezea ili asipoteze kiwango chake, ambapo alirudi Uganda kucheza katika klabu yake ya zamani SC Villa lakini hakuchukua muda akauzwa Yanga SC ya Jijini Dar es salaam, hata hivyo hakukaa sana aliamua kutimkia kunako klabu yake ya Simba na kupewa mkataba wa miezi 6.
Kwa sasa Okwi yupo kwenye mkataba mpya na Simba baada ya jana kusaini mkataba wa miaka 2 kuwatumikia mabigwa hao  wa zamani wa VPL.

Breaking News… Bunge Afrika Mashariki lamvua spika madaraka yake

Breaking News… Bunge Afrika Mashariki lamvua spika madaraka yake


Zziwa
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki kabla ya kubwagwa leo Bi.Margaret Nantongo Zziwa.
Na Mahmoud Ahmad Arusha
BUNGE  la nchi za jumuia ya Afrika Mashariki,lenye makao yake mjini Arusha, limemvua madaraka ya Uspika wa bunge hilo Margaret Nantongo Zziwa, kutoka nchini Uganda.
Uamuzi huo umefanywa  leo katika kikao cha bunge hilo ambapo Spika huyo alipigiwa kura 36 za kutokuwa na Imani nae,  kura 2 zimeharika kura moja haikueleweka  hivyo kukosa sifa ya kuendelea na wadhifa huo.
Kwa mujibu wa kanuni ya 32 ya bunge la jumuia hiyo ya Afrika Mashariki inatakiwa theluthi mbili ya wabunge sawa na kura 30 kumung’oa Spika.
Sababu za kuondolewa madarakani ni kushindwa kutimiza majukumu kama Spika, matumizi mabaya ya kiti hicho kwa kuwapendelea ndugu ambao wameajiriwa ndani ya bunge hilo .
 Sababu nyingine anadaiwa kuwa na kauli mbaya dhidi ya wabunge na wafanyakazi wa bunge hilo, mume wake kuingilia shughuli za utendaji wa bunge kinyume na taratibu.
DSC_0228
Mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili Spika wa EALA, Mh. Frederic Ngenzebuhoro akisoma ripoti ya kamati yake iliyopelekea spika huyo kuong’olewa.
Wametoa saa 48 kwa wabunge wa Uganda,kujaza fomu kwa ajili ya kuomba nafasi hiyo ya Spika, kwa kuwa bado ni zamu ya Uganda kukalia kiti hicho.
 Maazimio hayo yamesomwa na Frederic Ngenzebuhoro, ambae ni mbunge wabunge hilo, pia ni mwenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Spika huyo.
 Ngezabuhilo,amesema tuhuma zote dhidi ya Spika huyo zimethibitika  hivyo wabunge kwa kauli moja wameamua kupiga kura ya kutokuwa na imani na Spika huyo .
Wakati wa maamuzi hayo spika hakuwepo bungeni huku  mwanasheria wake, Gety Tumwebaze ,kutoka Uganda,amesema spika anapinga kikao hicho, ni batili na maamuzi yatakayotolewa hawatayakubali kwa kuwa yapo nje ya taratibu za bunge hilo.
DSC_0263
Mheshimiwa Hafsa Moss akichangia mjadala wa kamati uliopewa kuchunguza tuhuma mbalimbali zinazomkabili spika huyo.
DSC_0317
Mh. Mukasa Mbidde akishiriki zoezi la upigaji kura lililopelekea kung’olewa kwa spika huyo.

Wednesday 17 December 2014

MAREKANI, CUBA KUMALIZA UHASAMA WA MIAKA MINGI ?


MAREKANI, CUBA KUMALIZA UHASAMA WA MIAKA MINGI ?



Nchi za  Marekani na Cuba zimetangaza kukomesha uhasama wa miaka hamsini na kufungua mwanya wa mazungumzo ya kidiplomasia ili kurejesha uhusiano kati yao.
Akitoa tangazo hilo la kihistoria Rais Barrack Obama, amesema kuwa mfumo wa Marekani wa kuitenga Cuba, umeshindwa.
Rais wa Cuba Raúl Castro, ameiomba Marekani kuvunjilia mbali vikwazo vya miaka mitano vya kiuchumi dhidi ya Nchi yake, ambayo anasema vimeiletea nchi hiyo madhara makubwa.
Kuondolewa kwa vikwazo hivyo vitahitaji kupitishwa na Bunge la Congress la Marekani, ambalo linaongozwa na wanachama wengi wa chama pinzani cha Republican. Wengi wao wanapinga ulegezaji kamba kwa vikwazo.

Tuesday 9 December 2014

SAKATA LA ESCROW LATUA KWA RAIS KIKWETE


SAKATA LA ESCROW LATUA KWA RAIS KIKWETE


Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete amepokea rasmi ripoti pamoja na ushauri wa Bunge kuhusiana na sakata zima la akaunti ya Tegeta Escrow. Hatua hiyo inafuatia kuanza kazi rami siku ya jumatatu desemba 8, 2014 baada ya kuimarika afya yake kufuatia upasuaji wa tezi dume  mwezi mmoja uliopita nchini Marekani.
Kwa mujibu wa kurugezi ya mawasiliano ikulu  imesema kwamba Rais kikwete amelekeza kuwa ripoti ya CAG iwekwe hadharani ili kila mwananchi ajue kilichosemwa na kupendekezwa  na mdhibiti wa mkuu wa Hesabu za serikali.
Amesisitiza kuwa ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi pamoja na mitandao ya kijamii ili kila mtanzania aweze kuisoma na kuielewa.
Kwa upande mwingine kufutia kupokea ripoti hiyo rais kikwete anatarajia kuitolea maamuzi baada ya wiki moja kuanzia wiki hii.

AMKENI!, Jinsi ya Kuacha Kugombana

AMKENI! 

 MSAADA KWA AJILI YA FAMILIA | NDOA

Jinsi ya Kuacha Kugombana

TATIZO

Je, wewe na mwenzi wako mnashindwa kuzungumzia mambo kwa utulivu? Je, kila mara una wasiwasi kwa sababu hujui ikiwa jambo lolote utakalosema au kufanya litamkasirisha mwenzi wako na hivyo kusababisha ugomvi mkubwa?
Kama hali iko hivyo, uwe na uhakika kwamba hali hiyo inaweza kuboreshwa. Lakini kwanza unahitaji kujua sababu inayofanya wewe na mwenzi wako mgombane mara nyingi.

KWA NINI HILI HUTUKIA

Kutoelewana.

Mwanamke mmoja anayeitwa Jillian * akiri hivi: “Nyakati nyingine mimi humwambia mume wangu jambo fulani lakini nashindwa kulisema kama nilivyokusudia. Au ninakuwa na uhakika kwamba nilimwambia jambo fulani, kumbe niliota eti nilimwambia. Hilo limewahi kutokea!”

Kuwa na maoni tofauti.

Hata iwe wewe na mwenzi wako mnapatana kadiri gani, maoni yenu kuhusu mambo fulani yatatofautiana. Kwa nini? Kwa sababu hakuna watu wawili wanaofanana kabisa—jambo hilo linaweza kufanya ndoa iwe yenye kupendeza au iwe na matatizo. Kwa wenzi wengi, jambo hilo linaleta matatizo katika ndoa.

Kuiga mfano mbaya wa wazazi.

Mwanamke anayeitwa Rachel anasema: “Wazazi wangu waligombana mara nyingi na walitupiana maneno yasiyo na heshima. Kwa hiyo nilipoolewa nilizungumza na mume wangu kwa njia ileile ambayo mama yangu alizungumza na baba yangu. Sikuwa nimejifunza jinsi ya kuonyesha heshima.”

Kiini cha tatizo.

Mara nyingi, kiini cha ugomvi mkali si tukio lililouchochea. Kwa mfano, ugomvi unaoanza na maneno “Sikuzote wewe huchelewa!” huenda usimaanishe eti mtu anahitaji kufuata wakati, bali huenda mwenzi mmoja akahisi kwamba mwenzake hamjali.
Hata sababu iwe nini, ugomvi wa mara kwa mara unaweza  kuathiri vibaya afya yenu na hata unaweza kuongoza kwenye talaka hatimaye. Basi, mnawezaje kuzuia ugomvi?

MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA

Njia nzuri ya kuzuia magombano ni kutambua visababishi visivyoonekana wazi vinavyouchochea. Wakati ambapo mambo yametulia, wewe na mwenzi wako jaribuni zoezi lifuatalo.
1. Kila mmoja wenu aandike kwenye karatasi jambo lililofanya mgombane hivi karibuni. Kwa mfano, mume anaweza kuandika hivi, “Ulishinda siku nzima na rafiki zako na hukunipigia simu kuniambia ulikuwa wapi.” Mke anaweza kuandika hivi, “Ulikasirika kwa sababu nilishinda na rafiki zangu.”
2. Mkiwa na mtazamo unaofaa, zungumzieni mambo yafuatayo: Je, jambo hilo lilikuwa zito sana? Je, jambo hilo lingeweza kuachiliwa? Katika visa fulani, ili kudumisha amani, inaweza kuwa bora kukubali kwamba mna maoni tofauti na kufunika mambo kwa upendo.—Kanuni ya Biblia: Methali 17:9.
Ikiwa wewe na mwenzi wako mnaona kwamba jambo hilo lilikuwa dogo, kila mmoja aombe msamaha, kisha mwache kulizungumzia au hata kulifikiria.—Kanuni ya Biblia: Wakolosai 3:13, 14.
Ikiwa jambo hilo linaonekana kuwa zito sana kwa mmoja wenu au ninyi wote wawili, chukueni hatua inayofuata.
3. Andika jinsi ulivyohisi wakati mlipogombana, na mwenzi wako
pia
afanye vivyo hivyo. Kwa mfano, mume anaweza kuandika hivi, “Nilihisi kwamba unapendelea kuwa na rafiki zako kuliko kuwa nami.” Mke anaweza kuandika hivi, “Nilihisi kwamba unanitendea kama mtoto ambaye anapaswa kumwarifu baba yake kila wakati mahali alipo.”
4. Mbadilishane karatasi zenu, na kila mmoja asome maelezo ya mwenzake. Mlipokuwa mkigombana, ni nini hasa kilichokuwa kikimhangaisha mwenzi wako? Zungumzeni jinsi kila mmoja wenu angeshughulika na tatizo hilo bila ugomvi.—Kanuni ya Biblia: Methali 29:11.
5. Zungumzieni mambo ambayo mmejifunza kupitia zoezi hili. Mnaweza kutumiaje yale mliyojifunza kusuluhisha au kuzuia ugomvi usitokee wakati ujao?

Monday 8 December 2014

MESSI APIGA ‘HAT TRICK’ BARCELONA IKIUA MTU 5-1,KOCHA LIVERPOOL: HATUWEZI KUMTEGEMEA GERARD ,MTIBWA SUGAR WAPELEKA MSIBA MSIMBAZI, WAIGONGA SIMBA 4-2


MESSI APIGA ‘HAT TRICK’ BARCELONA IKIUA MTU 5-1




Mshambuliaji Raia wa Argentina, Lionel Messi, Jana ameongoza safu ya ushambuliaji kunako klabu yake ya Barcelona na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Espanyol, Huku nyota huyo aking’ara kwa kutupia bao 3, Hat Trick.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa ndani ya Uwanja wa Camp Nou, Espanyol ndio walianza kupata goli kupitia kwa Sergio Garcia dakika ya 13 kabla ya Messi kusawazisha bao hilo dakika ya 45 na kufanya timu hizo zienda kupumzika zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kwa mara ya pili Messi akawarudisha kati wenzake kwa kufunga bao la 2 dakika ya 50, zilipita dakika 3 tu, Pique akaiandikia Barcelona bao la tatu kunako dakika ya 53.
Pedro naye hakuwa nyuma katika mchezo huo kwani kunako dakika ya 77 aliiandikia timu yake bao 4 kabla ya Lionel Messi kumaliza kazi kwa kupachika bao la 5 kwa timu yake huku kwake likiwa ni bao la 3 dakika 81.

KOCHA LIVERPOOL: HATUWEZI KUMTEGEMEA GERARD




Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Brenda Rodgers amewaonya wachezaji wake kwa kusema kuwa hawatakiwi kumtegemea nahodha wa timu hiyo Steven Gerrard kila mechi.
Rodgers amesema kuwa wachezaji hao wanafaa kuziba pengo la nahodha huyo bila wasiwasi wakati ambapo hayupo katika timu.
Gerrard mwenye umri wa miaka 34 alipumzishwa kwa mara ya pili mfululizo katika mechi ya nyumbani iliyokamilika bila kwa bila.
Licha ya kiungo huyo wa kati kuchezeshwa kunako dakika ya 67 hakuweza kubadilisha mambo uwanjani Anfield.
”Hatuwezi kila mara kumtegemea, haiwezekani kwamba kila mechi yeye ndiye atakayesababisha mchezo mzuri ama mabao”,alisema Rodgers.

MTIBWA SUGAR WAPELEKA MSIBA MSIMBAZI, WAIGONGA SIMBA 4-2




Klabu ya Simba leo imeambulia kipigo cha bao 4-2 kutoka kwa vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara Mtibwa Sugar kutoka Manungu, Tuliani, Morogoro katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es salaam.
Katika mchezo huo Simba ndio walianza kupata bao kupitia kwa Said Demla kipindi cha kwanza lakini halikuchukua muda mrefu Mshambuliaji Mussa Hassan Mgosi akaisawazishia Mtibwa katika dakika ya 28.
Katika kipindi cha pili Mtibwa waliongeza kupeleka msiba Msimbazi baada ya Mohammed Ibrahim kuiandikia timu yake bao la pili dakika ya 51 na dakika ya 53, kabla ya Ame Ally kufunga la nne dakika ya 78.
Dakika ya 89 mshambuliaji Amisi Tambwe alifunga bao la pili kwa Simba kwa mkwaju wa penati nakufanya matokeo yawe 4-2.
Mchezo huo kwa Simba ilikuwa ni kipimo katika kuelekea mchezo wa Nani mtani jembe hapo Desemba 13 wiki kesho, huku wakiwa wametoka kutoa sare ya 0-0 na Express ya Uganda juzi kunako uwanja wa Taifa.

KESI YA SHEIKH PONDA KUSIKILIZWA LEO,RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA TANZANIA,ZITTO KUIBUA KASHFA KUBWA ZAIDI YA ESCROW 2015

KESI YA SHEIKH PONDA KUSIKILIZWA LEO


Kesi ya Sheikh Ponda inasikilizwa asubuhi hii mkoani Morogor. Sheikh Ponda anakabiliwa na kesi ya  uchochezi   iliyotokea  Mkoani Morogoro.
Hatua hiyo inafuatia mara baada  ya  kuachiwa  huru kutokana na  kesi  ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self  iliyokuwa inamkabili jijini Dar es salaam. Katika kesi hiyo  Mahakama ilijiridhisha   kuwa  Sheikh Ponda hakuwa na  hatia.

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO YA WAKUU WA MIKOA TANZANIA



Wakuu wa mikoa takribani 6 nchini Tanzania wamehamishwa vituo vya kazi huku mkuu wa mkoa 1 mmoja mpya akiongezeka katika safu ya wakuu wa mikoa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Katibu mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kwamba  Rais Kikwete amemteua mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani  Arusha Bw. Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha.
Wakuu wamikoa wengine waliohamisha vituo vya kazi ni Bw. Elaston  Mbwilo  kutoka mkoa wa  Manyara  kwenda mkoa wa Simiyu. Bw. Mbilo anachukua nafasi ya Paschal Mabiti aliyepewa likizo kutokana na ugonjwa. Bw.Joel Nkanga Bendera amehamishiwa mkoani Manyara akitokea mkoa wa Mororgoro. Dkt Rajabu M. Rutengwe anayehamishiwa mkoa wa Morogoro kutoka mkoani Tanga.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa wengine ni Bw. Magagula  Saidi  Magagula kutoka mkoa wa Lindi kwenda mkoa wa Tanga. Mwantumu  Bakari  Mahiza anakwenda  mkoani  Lindi akitokea mkoani Pwani pamoja na Mhandisi Evarist B. Ndikilo  anakwenda  mkoani Pwani kutoka mkoa wa Arusha.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa mpya Bw Ntibenda ataapiwa leo Ikulu jijini Dares salaam ambapo wakuu wa mikoa wengine watabakia katika vituo vyao vya kazi.

ZITTO KUIBUA KASHFA KUBWA ZAIDI YA ESCROW 2015



Sakata lingine litakalohusu kashfa nne kubwa zaidi ya ESCROW  kuibuka  mwakani kufuatia kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC)  kukamilisha ufisadi uliofanyika katika akaunti ya Escrow. Katika sakata hilo Bunge limetaka serikali kuwawajibisha  Mawaziri pamoja na watendaji wa serikali na kuendeleza uchunguzi kwa waliopata mgao wa fedha ambazo ni zaidi ya bilioni 306.
Kwa mujibu wa Mwenyikiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe amesema kwamba  kamati  yake  itatumia  mwezi desemba na januari mwakani  kupitia ripoti nne ambazo zina maslahi kwa Taifa.
Akinzungumzia kashfa hizo, Zitto amesema kuwa kashifa hizo ni za utoaji vibali vya kuagiza sukari na kuingiza  sukari  nchini,  ripoti  nyingine  ni uchunguzi wa ubinafsishaji wa Benki ya NBC, ripoti maalumu ya Bandari  pamoja  na  mikataba ya gesi.
Sakata la utoaji wa Vibali vya sukari,  imebainika kuwa  ufisadi wake ni mkubwa kuliko hata sakata la ESCROW lilionekana kuteka hisia za watanzania kwa takribani wiki moja. Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya sukari nchini Tanzania  kutangaza kuwa wana mpango  wa kuvifunga viwanda  vya sukari kutokana na kuviendesha kwa hasara kwa kuwa kuna ushindani mkubwa wa  soko la sukari  kutokana na kuruhusu wafanyabiashara kuingiza kutoka nje ya nchi.

Monday 1 December 2014

Je, Unahisi Mungu Yuko Karibu na Wewe?

MNARA WA MLINZI DESEMBA 2014

 

HABARI KUU | UNAWEZA KUMKARIBIA MUNGU

Je, Unahisi Mungu Yuko Karibu na Wewe?


“Kuwa na uhusiano mzuri na Mungu kunakufanya uhisi usalama, utulivu, na amani. Unahisi kwamba Mungu anakutakia mema siku zote.”—CHRISTOPHER, MWANAMUME KIJANA NCHINI GHANA.
“Mungu hukuona unapoteseka, naye anakupenda kuliko unavyoweza kuwazia.” —HANNAH, MSICHANA MWENYE UMRI WA MIAKA 13, ALASKA, MAREKANI.
“Inafariji na kufurahisha sana kutambua kwamba una uhusiano mzuri na Mungu!”—GINA, MWANAMKE KUTOKA JAMAIKA MWENYE UMRI WA MIAKA 40 HIVI.
Watu wengi huhisi kama Christopher, Hannah, na Gina. Wanaamini kwamba Mungu ni rafiki yao. Vipi wewe? Je, unahisi kwamba uko karibu na Mungu? Au, je, unataka kumkaribia au kuboresha uhusiano wako na Mungu? Huenda ukajiuliza hivi: ‘Inawezekanaje mwanadamu awe na uhusiano mzuri na Mungu Mweza-Yote? Ikiwa inawezekana, jinsi gani?’

INAWEZEKANA KUMKARIBIA MUNGU

Biblia inasema kwamba inawezekana kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Pia inasema kwamba Mungu alimwita Abrahamu, aliyekuwa Mwebrania ‘rafiki yake.’ (Isaya 41:8) Pia kumbuka mwaliko unaotolewa kwenye andiko la Yakobo 4:8: “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” Kwa hiyo, ni wazi kwamba inawezekana kuwa na uhusiano mzuri au urafiki na Mungu. Lakini kwa sababu hatuwezi kumwona Mungu, inawezekanaje ‘kumkaribia’ na kuwa na uhusiano mzuri pamoja naye?
Ili kupata jibu la swali hilo, fikiria jinsi urafiki kati ya wanadamu unavyositawishwa. Kwa kawaida, watu hujuana majina na kisha kuanzisha urafiki. Halafu, kadiri wanavyoendelea kuwasiliana ndivyo urafiki wao unavyositawi. Urafiki wao huzidi kuimarika wanapoendelea kutendeana mambo mema. Ndivyo ilivyo pia tunapotaka kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Acheni tuchunguze jinsi ya kufanya hivyo.

Tuesday 25 November 2014

HOUSES FOR SALE



House for sale:Amoderm house for sale it is a South African brick made ( interlocking bricks )  house, with 3 spacious master bed rooms for sale. LOCATION: Boko kwa mwamba, SIZE: Block fence zqm 420, TITTLE: 3 years ( no loan, smart ), PRICE: tsh. 125 mill ( semifinished ) and tsh. 150 mill (finished).Morgage acceptable



House for sale: 5 bed rooms house located near Kinyerezi catholic church. Has spascious 5 bed rooms, kithcen, dinning / sitting room, SIZE: 400 sqm , no titttle, PRICE: tsh.120 mill ( negotiable )




HOUSE FOR SALE: A house with huge compound full of trees, located at Kibamba ccm, near Kibamba primary school, 1750 sqm ( two plots ) . PRICE: tsh. 170 mill, tittle 99 years also it has home morgage loan in bank.
HOUSE FOR SALE: we have a new 3 bed rooms house at Kinyerezi ( Tabata ) for sale, have a block fence, no tittle. PRICE: tsh. 60 mill
HOUSE FOR SALE: Stone buiding for sale located at Sinza kijiweni, 3 apartment semi finished, 250 sqm with title, price; tsh. 800 mill (negotiable).
HOUSE FOR SALE: A house located at Mbezi Msigani, 4 bed rooms, kitchen,sitting or dinning room has a title deed, price:tsh 50 mil (installment allowed).

Sunday 23 November 2014

WENGER ALIA NA MABEKI KIPIGO CHA MAN U

WENGER ALIA NA MABEKI KIPIGO CHA MAN U


Kocha wa arsenal Arsene Wenger amewalaumu walinzi wa timu hiyo kufuatia ushindi wa manchester United.
Kocha wa arsenal Arsene Wenger amewalaumu walinzi wa timu hiyo kufuatia ushindi wa manchester United.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene wenger amesema kuwa safu ya ulinzi ya Arsenal ni hafifu baada ya kushindwa 2-1 na Manchester United katika uwanja wa Emirates.
Arsenal walipatikana wakiwa wazi katika safu ya nyuma walipojaribu kutafuta bao la kukomboa baada ya Kieran Gibs kujifunga.
Wenger amesema kuwa kwa sasa safu hiyo ya ulinzi haina uzoefu wa kutosha kuweza kusoma mechi.
Katika mechi hiyo Arsenal walifanya mashambulizi 23 katika lango la Manchester United.
Wenger aliongezea ”ni mechi tuliotawala kwa asilimia 80 na hatujatawala mechi kama hivo kwa mda mrefu”.
”Mwisho wa mechi hatukuwa imara katika safu ya Ulinzi na tulifanya makosa ambayo walichukua fursa na kutuadhibu”.

SAKATA LA ESCROW: WALIOGAWANA FEDHA ZA UMMA KUJULIKANA WIKI HII


SAKATA LA ESCROW: WALIOGAWANA FEDHA ZA UMMA KUJULIKANA WIKI HII



Wabunge kujadili wizi mabilioni ya fedha za umma wiki hii mjini Dodoma.
Wabunge kujadili wizi mabilioni ya fedha za umma wiki hii mjini Dodoma.
Sakata la wizi wa mabilioni ya fedha za umma katika akaunti ya Escrow watuhumiwa wote kujulikana wiki hii siku ya jumatano na Alhamisi. Katika siku hizo Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania linatarajia kujadili ripoti ya escrow.
Hivi sasa  Wabunge wa kila vyama wamekuwa wakikutana kuweka misimamo yao kuhusu namna watakavyoshiriki kujadili ripoti hiyo ili kuokoa mabilioni ya fedha za wananchi zilizoibwa na watendaji wa serikalini na hatimaye kugawana.
Aidha,  katika Kikao cha Kamati ya Uongozi  wa Bunge  kilichofanyika jana asubuhi kilikubaliana suala hilo la escrow lijadiliwe kwa siku mbili badala ya moja  kama  iliyokuwa imepangwa awali.
Kwa upande mwingine   kambi Rasmi ya Upinzan Bungeni, imeibuka na madai kwamba  vigogo wanaotuhumiwa  kugawana fedha  za Escrow   wamenyofoa   baadhi ya karatasi zenye majina yao  ili kuficha  ushaidi  ambapo  wameandaa   propaganda ya kuwahadaa wananchi kuwa ripoti hiyo haijakamilika.
Naye Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia ametaja kurasa zilizonyofolewa katika ripoti hiyo kuwa ni zilizobeba mambo ya msingi ambazo ni ukurasa wa 57, 58 na 59.
Watanzania wanausubiri kwa hamu kubwa mjadala huo utakaorindima wiki hii ili kuwafahamu walioiba fedha za umma na kugawana huku mambo ya msingi kama ujenzi wa shule, madawa hospitalini yakikwama kutokana na tamaa ya watu wachache wasio wazalendo.

KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI


KENYA: MAUAJI WATU 28 YAHUSISHWA NA VITA YA KIDINI



Mauaji yaliyotokea nchini Kenya yadaiwa kuwa ya kulipiza kisasi.
Mauaji yaliyotokea nchini Kenya yadaiwa kuwa ya kulipiza kisasi.
Mshauri wa ngazi ya juu wa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji ya watu 28 waliokuwa wakisafiri kwenye basi moja yalilenga kusababisha vita vya kidini nchini kenya.
Aidha.Bw Abdikadir Mohammed alitoa wito kwa wakenya kutoka imani zote kuungana pamoja dhidi ya kile alichokitaja kuwa vitendo vya uhalifu.
Katika tukio la mauaji ya  watu 28 ambapo  wapiganaji  wa kundi la Al-Shabaab waliwapiga risasi wasafiri  ambao  hawangeweza   kukariri Koran.
Al Shabaab ilisema kuwa shambulizi hilo lilikuwa la kulipiza kisasi mauji ya hivi majuzi ya waislamu yaliofanywa na wanajeshi wa Kenya kwenye mji wa pwani ya Mombasa.
Serikali ya Kenya imesema kuwa imeanza kuwatambua waliotekeleza mauaji hayo na itawafikisha mbele ya sheria hivi karibuni.

clouds stream