Monday 22 June 2015

Kombe la FIFA kwa wanawake,Cameroon yatupwa nje

Kombe la FIFA kwa wanawake,Cameroon yatupwa nje

Tarehe June 22, 2015
Mechi  kombe la FIFA la dunia kwa  wanawake zapamba moto.
Mechi kombe la FIFA la dunia kwa wanawake zapamba moto.
Mechi  kombe la FIFA la dunia kwa  wanawake zinazoendelea nchini Canada ambapo michezo ya hatua ya mtoano ya 16 bora inafanyika kwa sasa huku mwakilishi pekee kutoka Barani Afrika Cameroon  akitolewa.
Aidha, Katika michezo iliyochezwa mwishoni mwa juma wawakilishi pekee wa Afrika waliosalia katika fainali hizo Cameroon wamesukumizwa nje baada ya kula mweleka wa goli moja kwa bila dhidi ya China, huku Australia, Ufaransa na wenyeji wa Canada wakiungana na China kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.
Bao pekee lililofungwa dakika ya 80 ya mchezo na Kyah simon limetosha kuwapa ushindi wa goli moja kwa BILA kinadada wa AutsraliA dhidi ya brazil na kuwavusha katika hatua ya robo fainali.
Katika matokeo mengine nyota wa ufaransa, marie laure delie alifunga magoli Mawili huku bao lingine likifungwa na elo die thomis na kuwapa ufaransa ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya korea kusini na hivyo kufuzu kwa hatua ya robo fainali.
Wenyeji Canada nao wamepata ushindi wa goli Moja kwa bila dhidi ya Switzeland na kufuzu hatua ya robo fainali.
Leo inachezwa michezo mingine miwili kuwania kufuzu kwa hatua hiyo ya robo fainali ambapo bingwa wa zamani wa dunia  Norway wakiwa na ukame wa miaka 20 wa taji hilo wanachuana na England.

Sheikh Mkuu wa Tanzania apatikana

Sheikh Mkuu wa Tanzania apatikana

Tarehe June 22, 2015
Sheikh Aboubakar Zuberi.
Sheikh Aboubakar Zuberi.
Baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA) asubuhi ya leo lamteua Sheikh Aboubakar Zuberi kuwa Mufti mpya wa muda.
Hatua ya uteuzi huo inafuatia kifo cha aliyekuwa Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Issa Shaaban Bin Simba aliyefariki kutokana na  shinikizo la damu na kisukari katika Hospitali ya TMJ na kuzikwa mkoani Shinyanga wiki iliyopita.
Sheikh Zuber atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (siku 90) kuelekea katika uchaguzi wa kumpata atakayerithi nafasi hiyo kwa mamlaka kamili.

Serikali yakana kumtorosha Rais wa Sudani

Serikali yakana kumtorosha Rais wa Sudani

Tarehe June 22, 2015
Rais Omar el Bashir akiwa nchini Afrika kusini kwa mkutano wa viongozi wa Afrika.
Rais Omar el Bashir akiwa nchini Afrika kusini kwa mkutano wa viongozi wa Afrika.
Serikali ya Afrika Kusini imekana ripoti kwamba mawaziri wake walipanga njama ya kumtorosha rais wa Sudan Omar El Bashir wiki iliopita.
Katika tukio hilo nusura rais huyo akamatwe kufuatia agizo la mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita dhidi yake kutokana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Mahakama ya Afrika Kusini ilimuagiza Bashir kusalia nchini humo huku ikijadiliana kuhusu iwapo agizo hilo litekelezwe. Lakini kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wake bwana Bashir aliondoka nchini Afrika Kusini na kurudi nyumbani.
Rais huyo wa Sudan alikuwa nchini Afrika Kusini kwa mkutano wa viongozi wa bara Afrika na kwamba serikali ilikuwa inajua kwamba ilihitajika kumkamata kwa kuwa mwanachama wa ICC.
Kwa mujibu wa  gazeti la Sunday Times nchini Afrika Kusini limenukuu duru za serikali kwamba katika mkutano wa mawaziri ilikubalika kwamba Afrika Kusini itamlinda hata iwapo italazimika kukiuka uamuzi wa mahakama na kukiuka katiba.
Katika taarifa yake,serikali imekana kwamba kulikuwa na mkutano wa siri na kwamba itaipatia mahakama hiyo maelezo kuhusu vile Bashir alivyoondoka nchini humo.
Mahakama kuu imeipatia serikali ya taifa hilo hadi alhamisi kubaini ni vipi aliruhusiwa kuondoka.

Wakristo,Waislamu wahimizwa upendo

Wakristo,Waislamu wahimizwa upendo

Tarehe June 22, 2015
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili Mzee Ally Hassan Mwinyi amewataka waislam hapa nchini kuepuka shari,chuki na uadui baina yao na waumini wengine wasio kuwa waislam na badala yake wapende kuwa na amani,utulivu na mshikamano ambao umetufikisha hapa kuanzia nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961.
Aidha, Mzee Mwinyi amesema hayo kwenye ghafla ya ufunguzi wa msikiti mpya wa masjid Suhaib Ruumi uliojengwa kilimani Hewa Wilayani Nachingwea kwa msaada wa Taasisi ya Al-Hikima Education Centre ya jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi Mwinyi amesema  kuwa msikiti ni sehemu ya ibada na kupata mafundisho ya mwenyezi mungu na siyo vinginevyo hivyo  aislamu waache falaka badala yake wakae pamoja na kufanya ibada kwa pamoja kwa ajili ya mwenyezi mungu na pia kulinda amani na utulivu tulionao.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya mkoa wa lindi na wilaya ya Nachingwea akiwemo waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe ambae nae alitoa shukrani kwa niaba ya wananchi na waislam wa Nachingwea.

Urais 2015: Mwandosya ‘amtisha’ lowassa

Urais 2015: Mwandosya ‘amtisha’ lowassa

Tarehe June 22, 2015
Profesa Mark Mwandosya akizungumza na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya.
Profesa Mark Mwandosya akizungumza na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Maalumu, Profesa Mark Mwandosya amemtaka Mbunge wa Monduli Edward Lowassa asisite kumuunga mkono kama walivyofanya watangaza nia wengine ili mambo yaishe mapema.
Mwandosya alisema hayo  mwishoni mwa wiki wilayani Mbozi alipokuwa akizungumza na wanaCCM waliomdhamini katika mbio zake za urais, pamoja na wanachama wengine waliojitokeza katika Ofisi za CCM.
Nimesikia Membe amesema hapa Mbeya asipopitishwa yeye basi atamuunga mkono Profesa Mwandosya, nikasikia tena na Waziri Mkuu akisema hata kama asipopitishwa yeye atafarijika kama Profesa Mwandosya atakuwa mgombea, nikasikia tena na Wassira naye kupitia kwa mtu wake wa karibu ataniunga mkono, sasa namuomba mwenzangu naye Edward au maarufu kama Edo naye aseme Profesa ndiyo wangu, ili kazi iishe na tuipunguzie kazi Halmashauri Kuu,” alisema Profesa
Katika mkutano huo alisema  amefarijika kusikia anaungwa mkono na wagombea wenzake ambao ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe pamoja na kupata taarifa za Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira naye kusema anamuunga mkono.
Kufuatia kuungwa mkono na watangaza nia hao watatu  anamuomba pia Lowassa naye kumuunga mkono ili kuipunguzia kazi Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM).

Lowassa: ’ Hakuna wa kukata jina langu CCM’

Lowassa: ’ Hakuna wa kukata jina langu CCM’

Tarehe June 22, 2015
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na  wanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza na wanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiondoka kwenye viwanja vya CCM Mkoa wa Ruvuma.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiondoka kwenye viwanja vya CCM Mkoa wa Ruvuma.
Mbunge wa Monduli  Edward Lowassa amesema kuwa hatarajii  jina lake kukatwa
katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM) vitakavyoketi julai kumteua mwanasiasa atakaye peperusha bendeara ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais mwezi oktoba mwaka 2015.
Akizungumza mara baada ya kuwasili mkoani Ruvuma Lowassa amesema  anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.
“Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu”. alisema Lowassa.
Akiwa mkoani Ruvuma Lowassa amepata wadhamini ambao ni wanaCCM zaidi ya elfu 52.

Monday 15 June 2015

Matokeo ya mechi zote za jana kufuzu mataifa ya Afrka 2017

Matokeo ya mechi zote za jana kufuzu mataifa ya Afrka 2017

Tarehe June 15, 2015
arton10069

Licha ya kufanya mazoezi karibu wiki nchini Ethiopia timu ya taifa ya Tanzania imeendelea kufanya vibaya kuliko timu zote za ukanda wa Afrika mashariki baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya mafarao wa Misri, huku Kenya ikitoka sare na Congo, na Rwanda ikishinda. Matokeo mengine ya kushtua ni ushindi wa Ghana wa 7-1 dhidi ya Mauritius.
Togo 2 – 1 Liberia
DR Congo 2 – 1 Madagascar
Congo 1 – 1 Kenya
Egypt 3 – 0 Tanzania
Mozambique 0 – 1 Rwanda
Ghana 7 – 1 Mauritius
Sudan 1 – 0 Sierra Leone
Ethiopia 2 – 1 Lesotho
Niger 1 – 0 Namibia
Cameroon 1 – 0 Mauritania
Gabon 0 – 0 Ivory Coast

Wilishere agonga 2 England wakipiku Slovenia 3 – 2, Euro 2016

Wilishere agonga 2 England wakipiku Slovenia 3 – 2, Euro 2016

Tarehe June 15, 2015
Wilshere-Rooney
Wayne Rooney (kushoto) na Jack Wilshere (kulia) wachezaji wa timu ya Taifa ya England walioifungia dhidi ya Slovenia kufuzu Euro 2016 mjini Ljubljana Juni 14.
Huku Slovenia na England wakiwa wametoshana nguvu, Wayne Rooney, nahodha wa timu ya Taifa ya England ndiye aliyetengenisha pande hizo dakika ya 86.
Slovenia ndiyo iliyoanza kufunga katika uwanja wa Milivoje Novakovic dakika ya 37 na kuiweka mbele nchi yake mbele ya mashabiki wa nyumbani, ushindi uliodumu kipindi chote cha kwanza na dakika 11 za mwanzo za kipindi cha pili.
Dakika ya 57, Jack Wilshere aliisawazishia England. Ilikiwa tena Wilshere aliyeiweka mbele England kwa bao la pili akisaidiwa na Adam Lallana dakika ya 73.
Katika pambanohili la piga nikupige, ushindi wa 2 – 1 wa England ulidumu kwa takribani dakika 10 kabla ya Nejc Pecnik kuzamisha mpira wavuni kwa kichwa akilishwa na Bojan Jokic. Dakika ni ya 84, mabao Slovenia 2 – England 2.
Lakini siku ilikuwa ya England, maana dakika ya 86, Rooney aliiweka timu yake mbele kwa bao la tatu, ushindi uliodumu hadi mwisho. Kipenga cha mwisho kinapulizwa, Slovenia 2 – England 3.

Mafarao waichakaza Stars 3 – 0

Mafarao waichakaza Stars 3 – 0

Tarehe June 15, 2015
Taifa Stars
Taifa Stars
Timu ya Taifa ya Tanzania, leo wamefungwa na mafarao.
Taifa Stars iliyokwenda Misri kuwava Mafarao hao imejikuta pabaya tangu kipindi cha kwanza ilipokuswa koswa huku mabao mawili waliokuwa wamefungwa yakikataliwa. Bao la kwanza la Misri lingekuwa lile lililokuwa limefungwa na Ahmed Hegazi dakika ya nne lakini likakatiliwa kwa kuwa Offside.
Stars pia walikoswa dakika ya 26 baada ya bao kukataliwa kwa madhambi yaliyofanywa na mafarao kwenye mlinda mlango.
Kipindi cha kwanza kiliisha bila pande zote kuandika bao.
Kipindi cha pili, mafarao walirudi na hasira na kutawala mpira. Juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 60 kwa Rami Rabia kuwafungia bao la kwanza.
Ndani ya dakika 10 Stars walijikuta wakifungwa mabao matatu, hawakuweza kurudi. Bao la mafarao la pili lilifungwa dakika ya 64 na Baseem Morsi, huku la tatu likifungwa dakika ya 70 na Mohamed Salah.
Mechi ya leo iliyochezwa katika kiwanja cha Borg El Arab ilikuwa ni ya kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Afrika mwaka 2017 kwa kundi G.
Michuano hiyo itaendelea mwezi wa Septemba Stars watakapokaribisha Nigeria huku Misri ikicheza ugenini dhidi ya Chad.

Kampuni ya kutengeneza silaha yatangaza kufilisika

Kampuni ya kutengeneza silaha yatangaza kufilisika

Tarehe June 15, 2015
_83626902_83626901

Kampuni ya kutengeneza silaha ya Colt yenye makazi yake huko Connecticut nchini Marekani imeamua kujisalimisha kwa kujaza jarada la kutangaza kufilisika kutokana na madeni makubwa wanayodaiwa huku  kampuni  ikiendelea na mipango mingine ya biashara huku ikiwa kwenye wakati wa maboresho. Kampuni hiyo ilipoteza muelekea baada ya kukosa zabuni ya kusambaza silaha mwaka 2013.
Kampuni ya Colt kupitia kwa kiongozi wake inasema wako wazi kufanya biashara kama itatokea ila wanachokifanya kwa sasa ni kuboresha zaidi biashara yake.

Mafuriko Georgia, hofu yatanda wanyama wakali waranda mitaani

Mafuriko Georgia, hofu yatanda wanyama wakali waranda mitaani

Tarehe June 15, 2015
518884300-Zoo-Animals-Escape-in-Georgia-Floods
Mafuriko katika mji mkuu wa Georgia yameua watu 12 huku hatari zaidi ikiwa ni wanyama wakali kama Simba, nyani chui  na mbwa mwitu kutoroka kwenye zoo walikokuwa wameifadhiwa na kuingia mtaani huku polisi wakiwaomba wananchi kukaa ndani huku wakifanya jitiahada za kuwawinda wanyama hao.
Hofu ilizidi kutanda kwenye mji huo wenye idadi ya watu milioni 1.1 baada ya mafuriko hao kuacha idadi kubwa ya watu wakiwa hawana makazi na wanyama wakali kama mbwa mwitu na wengine wakili wakiwa bado hawajakatwa hivyo kuzua hofu kubwa ya kudhuru binadamu kutokana kuwa na njaa.
Tukio hili licha ya kukutwa miili ya wafanyakazi 3 wa zoo hiyo ila mkurugenzi wa Zoo amesema anasikitika sana kuona moja ya kivutio kikubwa kwenye zoo hiyo simba mdogo mweupe kwa jina la Shumba kupigwa risasi.
Maafisa bado wanajitaidi kuwasaka wanyama hao waliotoroka kwa kutumia helikopta wanaamini watarudisha mji huo kwenye hali ya amani kwa wakazi wake.

Museveni apata mpinzani wa kipekee

Museveni apata mpinzani wa kipekee

Tarehe June 15, 2015
Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kushoto) akiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM, Bw Amama Mbabazi. Bw Mbabazi ametangaza kuwa atagombea kukiwakilisha NRM kwenye uchaguzi mkuu ingawa chama hicho kilishatangaza rasmi kuwa Museveni ndiye mgombea pekee na atakiwakilisha
Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kushoto) akiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM, Bw Amama Mbabazi. Bw Mbabazi ametangaza kuwa atagombea kukiwakilisha NRM kwenye uchaguzi mkuu ingawa chama hicho kilishatangaza rasmi kuwa Museveni ndiye mgombea pekee na atakiwakilisha
Rais Yoweri Museveni amekuwa madarakani kwa karibu miaka 30 toka alipotwaa madaraka mwaka 1986. Katika kipindi hiki chote amekumbana na wapinzani wa aina tofauti tafouti.Amekumbana na wapinzani wa kijeshi (waasi), amekumbana na upinzani ndani ya chama na serikali yake na wale wa siasa wa vyama vya upinzani.
Mmoja wa wapinzani ambao amekumbana nao na ambao wameonekana kumuhenyesha kweli ni yule aliyekuwa mtu wake wa karibu sana kiasi cha kuwa daktari wake walipokuwa wakipagania madaraka, Kanali Mstaafu Kizza Besigye.
Baada ya Museveni kutwaa madaraka, Besigye alikuwa mmoja wa kundi lililokuwa na madaraka katika jeshi na kwenye duru za Utawala.
Lakini mwaka 2001 Besigye alitangaza kumpinga Museveni upinzani ambao hadi sasa pande zote, waganda na Ulimwengu unaukumbuka. Kwa mara mbili mfululizo, mwaka 2006 na 2011 pande hizo mbili zilimenyana katika uchaguzi mkuu, na mara zote Besigye akitangaza kuwa alikuwa ameshinda isipokuwa Museveni aliiba kura.
Katika vinyanganyiro hivyo kulijitokeza sura ya serikali kutumia nguvu sana kumdhibiti Besigye na wakati mmoja Besigye ‘alikimbilia’ uhamishoni nje ya Uganda akirudi baada ya muda. Besigye amekamatwa mara kadha na kuswekwa ndani; moja ya operesheni za kumkamata zinazokumbukwa mno ni ile yeye na abiria waliokuwa kwenye gari lake walipomwagiwa pilipili kwenye gari yake na akaburuzwa hadi kwenye gari la wanausalama, vitendo vilivopelekea akimbizwe hospitali Nairobi kwa matibabu.
Wapinzani na wapenzi wa Museveni wote wameongezeka toka mwaka 2001, lakini hapajawepo mpinzani mwenye nguvu na ushawishi ndani ya chama chake kama, Bw. Amama Mbabazi, mwanasiasa mkongwe na swaiba wa Museveni kwa miaka mingi akishika nyadhifa tofauti Serikalini mara ya mwisho akiwa Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa Chama tawala cha Museveni cha NRM.
Amama Mbabazi akitangaza nia
Amama Mbabazi akitangaza nia
Bw Mbabazi ni tofauti kwa sababu amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa atachuana na Museveni kukiwakilisha chama chao kama Mgombea wa Urais, huku kamati ya chama hicho ikiwa tayari imeshatangaza kuwa Museveni hatokuwa na mpinzani kwenye chama hicho.
Ni takribani miezi 8 sasa toka Mbabazi ayenguliwe kutoka kwenye nyadhifa yake ya Waziri Mkuu, kuenguliwa kuliosemekana kutokana na ‘njama za wazi’ za kutaka na kujipanga kuwa Rais wa Uganda.
Katika kipindi hicho chote, kumekuwepo na sauti za chini chini kuwa Mbabazi angeligombea Urais lakini yeye mwenyewe alikuwa hajasema wazi wazi. Lakini sasa kaweka bayana kuwa atachuana na Museveni kwanza ndani ya chama, na akiibuka kidedea atagombea Urais wa nchi ya Uganda.
Makamanda wawili wameshavaa magwanda, maswali matano muhimu ni je,
1. nani ataibuka kidedea?
2.Nini hatma ya atakayepoteza katika hawa wawili?
3. Nini hatma ya chama cha NRM?
4. Museveni, anayesifika kwa mbinu za kisiasa na vita, ataweza kuvuka kwenye uchaguzi 2016?
5. Je baada ya miaka 30 ya Museveni, Uganda imekomaa kiusalama, kidomkrasia na utawala kuweza kuhimili mitikisiko ya sasa?

Samweli Sitta kurudisha fomu ya Urais leo

Samweli Sitta kurudisha fomu ya Urais leo

Tarehe June 15, 2015
Samweli Sitta akionesha fomu ya kugombea urais mara katika ukumbi wa NEC makao makuu Dodoma.
Samweli Sitta akionesha fomu ya kugombea urais mara katika ukumbi wa NEC makao makuu Dodoma.
Waziri wa uchukuzi Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Samuel Sitta anatarajia kurejesha fomu mara baada ya kupata wadhamini katika mikoa 15 ya Bara na Zanzibar ambao ni 450.
Samweli Sitta alichukua fomu ya kugombea urais juni 5 mwaka huu huku akiomba ridhaa ya kupta miaka mitano tu  aweze kuwashughulikia ipasavyo mafisadi na kumaliza kabisa tatizo la ufisadi  unao onekana kukwamisha maendeleo ya ya  nchi Hivisasa.
Kwa upande wa vipaumbele vyake  ni;
(i) Kuulinda muungano
(ii)  Kumalizia mchakato wa katiba Pendekezwa
(iii)  Kumaliza kabisa suala la Rushwa na ufisadi
(iv) Kuleta mahusiano mazuri kati ya  Wafanyabiashara na Serikali
(v) Kuimarisha Chama kiuchumi.

Mapigano makali yaibuka Kenya, Al shabaab 13 wauawa

Mapigano makali yaibuka Kenya, Al shabaab 13 wauawa

Tarehe June 15, 2015
Baadhi ya wanamgambo wa Al shabaab.
Baadhi ya wanamgambo wa Al shabaab.
Wapiganaji 13 wa Alshabaab wameuawa baada yao kushambulia kituo cha kijeshi cha Baure kilichoko eneo la Lamu katika pwani ya Kenya.
Msemaji wa jeshi la Kenya kanali David Obonyo ameithibitishia kuwa wapiganaji hao walivamia kambi hiyo ya kijeshi mwendo wa 5:45 alfajiri ya jana lakini wakazidiwa nguvu kabla hawajaingia ndani ya kambi hiyo.
Aidha amethibitisha kuwa wanajeshi wawili wa Kenya waliokuwa wakishika doria waliuawa katika shambulizi hilo.
Kanali Obonyo alisema kuwa wawili kati ya wale waliouawa ni wenye asili ya kizungu. Hakuna aliyepatikana hai japo washambuliaji wengine wa Al Shabaab wanasemekana kutorokea katika msitu mkubwa wa Bony ambapo wanajeshi wanawafwata.

Migiro ajitosa kuchukua fomu ya Urais leo

Migiro ajitosa kuchukua fomu ya Urais leo

Tarehe June 15, 2015
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro.
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Asha-Rose Migiro leo anatarajia kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) majira ya saa tisa mchana akifuatiwa na  kada mwingine wa chama  hicho Salum Marupu.
Aidha,  Migiro, atakuwa mwanamke wa nne kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo ya juu ya kuiongoza nchi kwa miaka mitano ijayo wakiwemo Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani, Amina Salum Ally.
Mwingine  ni aliyekuwa Mbunge wa Iringa na pia alishakuwa Naibu Waziri wa Fedha, Monica Mbega, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela.

Urais 2015: ACT-Wazalendo yavunja ukimya Tarehe June 15, 2015

Urais 2015: ACT-Wazalendo yavunja ukimya

Tarehe June 15, 2015
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.
Chama cha ACT-Wazalendo kimetangaza rasmi kuwa mgombea urais kupitia chama hicho atajulikana agosti 10 mwaka huu.
Kwa mujibu wa    kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, wakati akihutubia wananchi  mjini Geita  hivi karibuni  amesma Halmashauri kuu ya chama hicho iliyokutana juzi mjini Tabora imepitisha ratiba kamili ya kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi mbali mbali za chama hicho kuanzia Julai mosi.
Alisema kuanzia Julai mosi mpaka Julai 17 itakuwa ni siku ya kuchukua fomu kwa ngazi ya udiwani kwa ada ya Sh 10,000, Julai 1-26 kwa ngazi ya Ubunge na uwakilishi na ada yake ni Sh 20,000 na kwa ngazi ya urais ni kuanzia Julai 1-26 na ada yake ni Sh 100,000.
Aliongeza kuwa vikao vya ngazi mbali mbali ya uteuzi vitaanza Julai 27 mpaka siku ya mwisho ya Agosti 10 wakati mkutano mkuu wa Chama utakapopitisha jina la mgombea Urais.
Akizungumza sifa za mtu anayetaka kuwa Rais amesema   ni pamoja na mwombaji kuwa ni mtu anayeonesha kuyaelewa matatizo ya Tanzania ya sasa na ya muda mrefu,  mwenye maono mapana juu ya maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya kizazi kijacho,
Sifa nyingine ni awe na upeo mpana kuhusu masuala ya Afrika na ulimwengu katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni, kijiografia na kijamii.

Tuesday 9 June 2015

PROPERTIES FOR SALE


 HOUSE FOR SALE: A house for sale located at Mbezi Beach Africana,it 2 floor, bed rooms, kitchen, sitting room, dinning room and enough space for car parking, area of 1500 sqm, its PRICE is TSH. 480 million. ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

 HOUSE FOR SALE: A house for sale located at Mbezi Goba, it has  3 bed rooms, sitting room,kitchen and dinning room, its PRICE is TSH. 47 million ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).
CARS FRO SALE: 3 Toyota vitz for sale: each one costs TSH 5 million ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

Membe akanusha undugu na Kikwete

Membe akanusha undugu na Kikwete

Tarehe June 9, 2015
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, amekanusha uvumi ambao umekuwa ukienezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa yeye na  Rais Jakaya Kikwete ni ndugu wa damu.
Amedai kuwa japo watu wanadai kuwa wanafanana kwa sura ni kweli lakini hawana uhusiano wowote wa kibaiolojia kwani hata watu wengine hutokea pia wakafanana lakini wakawa sio ndugu.
Mhe. Membe alikanusha uvumi huo Mjini Dodoma, wakati akichukua fomu za kuwania urais kwa tiketi ya CCM, ambapo pamoja na mambo mengine alisema ataimarisha viwanda vidogo na vya kati.

PROPERTIES FOR SALE


 HOUSE FOR SALE: A house for sale located at Mbezi Beach Africana,it 2 floor, bed rooms, kitchen, sitting room, dinning room and enough space for car parking, area of 1500 sqm, its PRICE is TSH. 480 million. ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

 HOUSE FOR SALE: A house for sale located at Mbezi Goba, it has  3 bed rooms, sitting room,kitchen and dinning room, its PRICE is TSH. 47 million ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).
CARS FRO SALE: 3 Toyota vitz for sale: each one costs TSH 5 million. ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

Monday 8 June 2015

HOUSES FOR SALE



 HOUSE FOR SALE: A house for sale, located at Bunju A, it has 3 bed rooms one being a master       bed room, sitting room, kitchen and dinning room.It has enough space for 2 cars packing, it is  500 meters from Bagamoyo road, its PRICE is TSH 35 million ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

HOUSE FOR SALE: A house for sale, located at Bunju A, 500 meters from Bagamoya road, it has 2 bed rooms, sitting room and a toilet, it is  TSH 20 million as PRICE. ( CONTACTS:0652314181, EMAIL:aramakurias@yahoo.com, rocklandrealestate1@gmail.com).

Sunday 7 June 2015

Serena atwaa taji lingine French Open

Tarehe June 8, 2015
Mchezaji wa tenisi Serena Williams akiwa na kombe lake baada ya kushinda mashindano ya French Open
Mchezaji wa tenisi Serena Williams akiwa na kombe lake baada ya kushinda mashindano ya French Open
Mwanadada mchezaji wa mpira wa tenisi, Serena William, ameshinda tena taji la French Open licha ya kuwa na hali sio nzuri baada ya kusumbuliwa na mafua katika mchezo uliomalizika jana.
Serena, alifanikiwa kumshinda mpinzani wake Lucie Safarova, katika fainali hizo baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ambapo amekuwa ni mchezaji wa tatu kushinda mataji 20 peke yake.

Urais 2015: Membe awatisha watangaza nia CCM

Urais 2015: Membe awatisha watangaza nia CCM

Tarehe June 8, 2015
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiusalimia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe  pamoja na mke wake  wakiusalimia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amewatisha wasaka urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi wakati akitangaza nia ya kugombea urais Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa kufuatia wananchi wengi kuhudhuria katika mkutano wake suala linalo ashiria kukubalika na watanzania.
Akizungumza na mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya CCM Mkoa wa Lindi jana Membe ametamba kuipeleka nchi katika uchumi wa viwanda unaobebwa na kilimo na kuahidi kujenga serikali ya waadilifu.
Amesema kabla ya kuchukua uamuzi wa kufikiria urais alijipima na kuona anatosha kwa nafasi hiyo, pia baada ya kuwaangalia wagombea wenzake wote anaamini yeye ndiye mwenye sifa za kustahili kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Tanzania.
Amesisitiza  kuwa uadilifu wake ni wa kuzaliwa, uwajibikaji usio wa kawaida na ndiyo sababu kila uchaguzi wananchi wa Jimbo lake la Mtama wamekuwa wakimchagua kwa idadi kubwa ya kura.
Kwa  upande wa uzoefu amesema ana uzoefu mkubwa baada ya kuwa Ofisa usalama wa Taifa kuanzia mwaka 1978, Ofisa Ubalozi,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Naibu Waziri wa Nishati, Waziri wa Mambo ya Nje kuanzia Desemba mwaka 2006 hadi sasa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiusalimia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwasalimia wananchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiusalimia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiusalimia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana.

China yaitaja ajali Meli ya Yangtz kuwa mbaya zaidi

China yaitaja ajali Meli ya Yangtz kuwa mbaya zaidi

Tarehe June 8, 2015
Meli iliozama katika mto Yangtse nchini China
Meli iliozama katika mto Yangtse nchini China
Msemaji wa serikali nchini China anasema kuwa karibu watu 400 wanahofiwa kuaga dunia wakati feri ilipozama kwenye mto Yangtze siku ya jumatatu. Ajali hiyo inaripotiwa kuwa mbaya zaidi nchini humo tangu miaka 60 iliyopita
Idadi hiyo imeongezeka kwa haraka baada ya makundi ya uokoaji kusaka vyumba vya feri hiyo. Kwa sasa meli hiyo imendolewa majini kwa kutumia mitambo mikubwa.
Jumla ya watu 456 walikuwa ndani ya feri hiyo wakati ilipokumbwa na dhoruba ambapo ni watu 14 tu walioripotiwa kuponea ajali hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambi rambi rais wa China kufuatia vifo vya watu wengi kwenye ajali hiyo.

Kigwangalla awataka Wazee wawapishe vijana Urais 2015

Kigwangalla awataka Wazee wawapishe vijana Urais 2015

Tarehe June 8, 2015
Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dk,Hamisi Kigwangalla.
Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dk,Hamisi Kigwangalla.
Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dk,Hamisi Kigwangalla amewataka wazee wakae  pembeni  na  kusistiza kuwa  huu ni wakati wa vijana kuliongoza taifa hili na ameahidi kuwa iwapo atapitishwa na chama chake na akashinda atahakikisha kila Mtanzania anakuwa na bima ya afya.
Akihutubia wananchi wa Jimbo la Nzega mjini Nzega, Dk Kigwangalla alisema wengine wote waliobaki sio wazoefu wa kufanya kazi Ikulu bali ni wazoefu wa shughuli nyingine.
Amesema ni wakati wa watu ambao hawajaingia serikali kushika wadhifa wa urais kwani uzoefu umeonesha kuwa marais ambao huwa wameshafanya kazi serikalini huwa wanaharibiwa na mfumo na hivyo kutofanya vizuri. “Umefika wakati wa kuwa na rais ambaye hajafanya kazi serikalini, wazee watupishe sasa ni wakati wa sisi vijana,” alisema Dk Kigwangala.
Hakuna uzoefu katika nafasi ya urais bali wenye uzoefu huo wapo wanne ambao tayari wamekwisha pitia nafasi hiyo na kukaa kwenye jengo la Ikulu ambao aliwataja kuwa Baba wa Taifa Mwl, Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa na Rais Jakaya kikwete.
Amesema kuwa wote wanaowania nafasi hiyo akiwepo yeye mwenyewe wanauzoefu tofauti tofauti katika masuala mbalimbali, huku akiwabeza wenye uzoefu wa ubadhilifu wa mali za umma ikiwemo Rushwa na ufisadi hali ambayo akiteuliwa na kushinda nafasi hiyo atapambana navyo.
Akizungumzia vipaumbele vyake  amesema    atahakikisha ndani ya mwaka mmoja, Watanzania wote watakuwa na Bima ya Afya watakao lipiwa na Serikali pamoja na kuwajari watumishi wa Idara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili waweze kutoa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.
Amesema katika kuboresha suala la Elimu kwa watanzania kama atashika nafasi hiyo anatamanai Elimu yote kuanzia Awari,msingi na sekondari bure kwa kuwa atahakikisha nchi inakuwa na uchumi imara kwa kupunguza matumizi ya serikali,safari,posho na ukubwa serikali.
Kwa upande wa   kukuza uchumi kwa wakulima, wafanya Biashara wadogowadogo na viwanda anatamani kuanzisha mfuko wa kukopesha wananchi kwa kuwekeza Bill 500 kwa mwaka pamoja na kuboresha kitengo cha ustawi wa jamii katika Halmashauri kwa ajili ya kuelimisha,kuwaunganisha kwenye vikundi vya kudhaminiana na kuratibu shughugili zao.

Tuesday 2 June 2015

Meli yazama nchini China, abiria 400 hawajulikani walipo

Meli yazama nchini China, abiria 400 hawajulikani walipo

Tarehe June 2, 2015
Vikosi vya uokoaji tayari vikielekea eneo la tukio.
Vikosi vya uokoaji tayari vikielekea eneo la tukio.
Boti za kijeshi kwa ajili ya kutoa msaada.
Boti za kijeshi kwa ajili ya kutoa msaada.
Meli ikiwa imebeba zaidi ya watu 450 imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali katika Mto Yangtze kusini mwa  nchi ya China.
Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua watu wanane wameokolewa mpaka sasa na kazi inaendelea ya kuwaokoa abiria wengine.
Waziri Mkuu Li Keqiang anaelekea katika eneo la tukio hivisasa kuangalia namna ya kuwaokoa abiria waliokuwa wanasafiri katika meli hiyo huku  kazi ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika kaunti ya Jianli katika jimbo la Hubei.
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi ilipozama. Meli hiyo, Dongfangzhixing au Nyota ya Mashariki ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Nahodha na mhandisi mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamekaririwa wakisema kuwa meli ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka. Waliokuwa katika meli hiyo wengi wao walikuwa watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 wakiwa katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Shanghai.
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la serikali ya China, meli hiyo inamilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze.

Prof. Muhongo, Ngeleja, Kamani kutangaza nia leo

Prof. Muhongo, Ngeleja, Kamani kutangaza nia leo

Tarehe June 2, 2015
Prof.Sospeter  Muhongo,Williaum Ngeleja,  Dk. Titus Kamani  nao wanatarajia kutangaz nia kugombea urais leo.
Prof.Sospeter Muhongo,Williaum Ngeleja, Dk. Titus Kamani nao wanatarajia kutangaz nia kugombea urais leo.
Mbio za urais kupitia kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi imezidi kushika kasi huku Wanasiasa  mbalimbali  kutoka chama cha Mapinduzi wakijitokeza kutangaza nia pamoja na kuweka vipaumbele vyao endepo watachaguliwa kuwakilisha   chama chao kuiongoza nchi.
Aidha, wanasiasa wanaotarajia kutangaza nia leo ni Mbunge wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja pamoja, Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani  na  aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na chama cha Mapinduzi CCM imebainisha kuwa wanasiasa wanaotaka kuwania urais watachukua fomu makao makuu ya chama hicho yaliyopo mkoani Dodoma ifikapo juni 3 siku ya jumatano wiki hii.

Urais 2015: Makongoro Nyerere atangaza kuwang’oa mafisadi Tarehe June 2, 2015

Urais 2015: Makongoro Nyerere atangaza kuwang’oa mafisadi

Tarehe June 2, 2015
Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere akitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM, katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama jana.
Mbunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere akitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM, katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mwitongo, Butiama jana.
Makongoro Nyerere akivishwa na wazee mgolole baada ya kutangaza nia ya nia ya kugombea urais kupitia CCM.
Makongoro Nyerere akivishwa na wazee mgolole baada ya kutangaza nia ya nia ya kugombea urais kupitia CCM.
Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere naye ametangaza nia    ya kuwania urais kijijini kwao Mwitongo wilayani Butiama jana.
Akizungumza na Wananchi Makongoro, amesema anatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo kutokana na kukerwa sana na rushwa, kwa kuwa  inasababisha Watanzania wengi kupoteza haki zao.
Pia Makongoro amesema anatambua kuwa kuna makundi ndani ya CCM. Akipata   nafasi ya urais na baadaye  kuwa mwenyekiti wa CCM atayamaliza na wote tutabaki kitu kimoja.
Amesisitiza kuwa ataboresha hali ya majeshi ya Tanzania, pamoja na wanafunzi elimu ya juu kupata mikopo kwa wakati.
Amesisitiza kuwa Rais Kikwete, amefanya kazi nzuri katika kipindi cha uongozi wake, lakini kuna watu wanamhujumu ili aonekane hafanyi kazi.
Makongoro anakuwa mwanasiasa wa tano kutangaza nia ya kutaka kuwania urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, wengine ni Luanga Mpina,Edward Lowassa, Steven Wassira, Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu huku wengine wakijitokeza tena leo.

clouds stream