Friday 23 January 2015

Uchawi Kumbe sio Simba na Yanga tu katika Soccer hadi majuu!!

Uchawi Kumbe sio Simba na Yanga tu katika Soccer hadi majuu!!


Shabiki mmoja ambaye alijitokeza katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Mbeya City na Ashanti United kunako uwanja wa Chamazi alikuwa akionekana katika mavazi ambayo yanatafasiri ya imani ya kishirikina.
Shabiki mmoja ambaye alijitokeza katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya Mbeya City na Ashanti United kunako uwanja wa Chamazi alikuwa akionekana katika mavazi ambayo yanatafasiri ya imani ya kishirikina.
Wakati dunia ya sasa katika Soccer ikiamini kuwa ni mchezo wa Kisayansi, akili nyingi na nguvu kidogo, Mtandao huu wa HIVI SASA.CO.TZ umethibitisha kuwa Uchawi katika mchezo huu sio Tanzania tu, kumbe ni karibia Mataifa yote ya Afrika wachezaji wanaamini katika Imani za kishirikina.
Nimekuwa nikifatilia na kudadisi chini kwa chini juu ya Imani hii ya kishirikina kama inanafasi katika Soccer na kubaini kuwa kunabaadhi ya wachezaji, timu na Mataifa makubwa ya Afrika wanaendekeza maswala mazima ya kishirikina katika mchezo wa Mpira wa miguu.
Kama utakuwa na kumbukumbu nzuri, Mwaka jana, Machi 30 2014, Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, CECAFA Challenge Cup na wawakirishi wa Tanzania katika michuano mbalimbali ya Kimataifa, Dar es salaam Young Africans (Yanga SC), Ilijikuta ikiingia kwenye kashfa ya Imani ya Kishirikina, walipokuwa wakicheza na Mgambo JKT, kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kiungo wa klabu hiyo Hassan Dilunga, kunako dakika ya 10 ya mchezo Yanga ikiwa nyuma kwa bao 1-0, alimfata muamuzi wa kati wa mchezo huo na kumtaka amkague Mshambuliaji wa Mgambo JKT, Mohammed Neto akidai kuwa ameficha hirizi katika Bukta yake, Kitu ambacho kilipelekea mchezo huo kusimama kwa muda na hatimaye Neto kutolewa nje baada ya kukataa kukaguliwa uwanjani, Mwisho wa siku Yanga ilifungwa 2-1.
Katika hari ambayo iliwaacha hoi wapenda Soccer Tanzania, wakioni ni Ujinga uliokisiri, Ni pale tuliposhuhudia picha zikionyesha Wachezaji wa Ndanda FC, kutoka Mtwara, wakikatiza Uchi wa mnyama polini kwa imani za kishirikina ili waweze kupata ushindi katika moja ya michezo ya Ligi kuu ya Vodacom Bara (VPL).
Martine Tangazi ni Mtanzania ambaye anacheza mpira nchini Qatar, akiwa chini ya uangalizi wa kituo cha kufundisha na kukuza vipaji vya mchezo huo, Aspire Academy (Centre of Excellence), Yeye anasema kuwa haamini katika Uchawi licha ya imani hiyo kutawala katika vichwa vya wachezaji hasa Waafrika ambao ndio wanaongoza kwa kufanyiana ‘ndumba’ miujiza.
Chipukizi huyo (Tangazi) anasema kuwa asilimia kubwa ya Wachezaji wa Kiafrika waliopo katika Academy ya Aspire anayoichezea yeye, wanatoka katika mataifa ya Magharibi mwa Afrika, lakini ndio wanaoongoza kwa imani za kishirikina kwani kila kitu wanaamini katika imani hiyo ambayo Mwenyezi Mungu anaipinga kwa nguvu zote.
“Hapana kaka mimi siamini katika hilo, ubora wangu na Mungu ndio siraha yangu kubwa, Nisikudanganye, Wachezaji wengi wa hapa wanaimani hiyo tena kwa kiwango kikubwa sana” Amesema Tangazi alipokuwa akifanya mazungumzo na mwandishi wetu akiwa Qatar kwa njia ya Skype.
“Amini ninayokwambia, Wanaoongoza kwa imani za Kishirikina hapa ni watu kutoka nchi za Magharibi,Mbona Tanzania cha Mtoto kwa hawa Jamaa, Huu ni mji wa Waarabu kwahiyo wazawa wao wanamuomba sana Mungu ni watu wa Dua muda wote, Ila Waafrika sisi ndio tunaimani hizo” Amesema Tangazi.

clouds stream